Special message to Mama Janeth Magufuli

Special message to Mama Janeth Magufuli

Nyie mlikuwa mnamsifu na kumuabudu ndio maana mliishi kwà amani
Magufuli hakuwahi kusema kuwa aliwateka au kukataa kuwa hakuwateka, hivyo tunajaribu kuangalia ni watu gani waliyokuwa wanatekwa na sababu gani hadi wakawa wanatekwa? Mfano humu JF wapo watu ambao wanasema walikuwa wanaishi kwa mashaka ya kutekwa na Magufuli ila tupo wengine ambao hatukuwa tukiishi na hayo mashaka, ndio maana nauliza ni watu gani ambao ndio walikuwa wanatekwa au sababu zipi zilikuwa zinafanya uweze kutekwa?
M
 
Tumuweke Mo kundi la matajiri,Roma kundi la wasanii.
Je, katika miaka mitano ya Magufuli walitekwa matajiri wangapi na wasanii wangapi?
 
Huyu Mama kwa muonekano ni muungwana,mtu wa Mungu na Mvumilivu ingawa kiuhalisia simfahamu.

But katika hili Watanzania tupunguze unafiki, Mateso ya Jiwe yalimpata kila mtu nadhani hata huyu Mama ndiyo maana ukimuangalia muonekano wake umebadilika,kwa wanaotizama mbali yule mtu alikuwa anaingiza Taifa kwenye Crisis kubwa kama ile ya Nyerere miaka ya 90.

Alikuwa na Mema yake ila he was not a Good Leader at all kwasababu alikosa maamuzi ya hekima na busara,na pia hakuweza kuangalia Capacity ya nchi kuhandle Consenquences za Maamuzi yake hasa kwa miaka ya mbele.
 
Acha uchochezi na uchongqnishi mleta mada. Hakuna aliyemnanga jiwe leo. Hayo ni mawazo yako tu.

Hebu mtaje mtu aliyemtaja jiwe kwa jina lake. Vinginevyo ni uzushi na uzandiki tu unaojaribu kuueneza.
Makamba senior alimtaja
 
Huyu Mama kwa muonekano ni muungwana,mtu wa Mungu na Mvumilivu ingawa kiuhalisia simfahamu.

But katika hili Watanzania tupunguze unafiki, Mateso ya Jiwe yalimpata kila mtu nadhani hata huyu Mama ndiyo maana ukimuangalia muonekano wake umebadilika,kwa wanaotizama mbali yule mtu alikuwa anaingiza Taifa kwenye Crisis kubwa kama ile ya Nyerere miaka ya 90.

Alikuwa na Mema yake ila he was not a Good Leader at all kwasababu alikosa maamuzi ya hekima na busara,na pia hakuweza kuangalia Capacity ya nchi kuhandle Consenquences za Maamuzi yake hasa kwa miaka ya mbele.
Mema yake yalikuwa ni yapi kwenye uongozi wake?
 
Habari mama,

Pole sana kwa msiba wa mumeo!, alikuwa great leader na wananchi wengi wanamkumbuka kwa utumishi wake ingawa ulikuwa mfupi kuliko kiongozi yeyote aliyetawala nchi yetu.

Hiyo Pole niliyotoa ni ya kawaida kwasisi binadamu maana wote tumefiwa wapendwa wetu lakini lengo kuu ni Pole kwa unayosikia na kuona kejeli na kubagazwa kwa marehemu mume wako hadharani bila woga tena kwa mambo mengine yasiyo msingi.

Sikia mama, mume wako alitimiza wajibu wake bila kujali pale alipokosea lakini wewe u hai ubavu wake ukisikia maneno magumu sana. Pengine unalazimika kuwatia moyo watoto lakini wewe mwenyewe umebeba mzigo mzito.

Imagine hata leo maneno yaliyotamkwa mbele yako! Tushukuru mama Samia walau kutuliza moyo wako baada ya maneno magumu leo lakini sio rahisi.

Endelea kuvumilia malimwengu, endelea kuipenda Tanzania! Jipe moyo kama Bikira Maria alivyojipa moyo alivyoshuhudia mwanae akiteswa na kufa msalabani!

Endelea kujipa moyo kama Bikira Maria alivyovumilia hata waliomtenda ubaya Yesu walipoeneza uzushi dhidi yake kuwa wanafunzi wake wamemwiba hakufufuka. Haikuwa rahisi ila moja ya tunu tunayojifunza juu ya Bikira Maria mara nyingi ni yote aliyaweka moyoni!

Kasome utenzi wa Bikira Maria Luka 1: 46-55 Ukutie nguvu. All shall be well 🙏
Kuna clip moja ya mwezi September imemuonyesha mjane wa Magufuli, Mama Janet akiwa anacheza mapambio na wana gospel music wengine. Alionekana amenawiri, mwenye furaha na mtu huru. Hakika sijawahi kumuona akiwa na appearance ile wakati mumewe yuko Ikulu.

Hata kwenye mkutano wa CCM alikuwa ni mwenye furaha. Nyie wenye agenda ya legacy ya Magufuli msimsemee Mama Janet, Watanzania tunaiona furaha yake
 
Magufuli hakuwahi kusema kuwa aliwateka au kukataa kuwa hakuwateka, hivyo tunajaribu kuangalia ni watu gani waliyokuwa wanatekwa na sababu gani hadi wakawa wanatekwa? Mfano humu JF wapo watu ambao wanasema walikuwa wanaishi kwa mashaka ya kutekwa na Magufuli ila tupo wengine ambao hatukuwa tukiishi na hayo mashaka, ndio maana nauliza ni watu gani ambao ndio walikuwa wanatekwa au sababu zipi zilikuwa zinafanya uweze kutekwa?
Kwa nini hutaki kutumia akili hata kidogo, kwani utekaji ni sheria, kanuni au taratibu hadi atangaze hadharani kuwa anawateka?
Hiyo ni kazi ya watetezi wake mueleze kwa nini aliwareka. Mimi kama mtanzania ambae natagemea serikali iwalinde raia wake nashangazwa kuona wanatekwa wanashambuliwa hata kuuliwa na serikali ikiwa mshukiwa mkuu.
Kabla yake na baada yake mbona hatukuwahi kusikia utekaji na matumizi mabaya ya mamlaka, kuonyesha huna afya ya akili unaniuliza kwa nini aliwateka.
Nasisitiza kutetea upumbavu lazima uwe mpumbavu kuuzidi
 
Kwani Dr Ulimboka alijisikiaje aliposikia kwamba watu wazuri hawafi halafu akatajwa Kikwete kuwa ni katika watu wazuri?
Ukizungumzia suala la hisia kila mtu ana zake ndio maana watu walimwaga machozi katika msiba wa Magufuli na kila mtu alimuelezea Magufuli kwa aina yake.
Hapa mimi siko katika agenda ya kutetea yeyote kama wewe, nionyeshe mahala popote nilipoterea serikali za CCM zilizopita au zilizopo ?
Uovu wa Magufuli unasemwa kama vile uovu wa Kikwete na hata wa Samia unavyosemwa, ila wajinga kazi wanayo ya kutetea maovu
 
Hiyo Pole niliyotoa ni ya kawaida kwasisi binadamu maana wote tumefiwa wapendwa wetu lakini lengo kuu ni Pole kwa unayosikia na kuona kejeli na kubagazwa kwa marehemu mume wako hadharani bila woga tena kwa mambo mengine yasiyo msingi.

Sikia mama, mume wako alitimiza wajibu wake bila kujali pale alipokosea lakini wewe u hai ubavu wake ukisikia maneno magumu sana. Pengine unalazimika kuwatia moyo watoto lakini wewe mwenyewe umebeba mzigo mzito.
Kwenye kile kikao cha wahuni nilitamani kupata fursa ya kumnongoneza mjane aondoke kwenye kikao ili wajimwage zaidi
 
Kwa nini hutaki kutumia akili hata kidogo, kwani utekaji ni sheria, kanuni au taratibu hadi atangaze hadharani kuwa anawateka?
Hiyo ni kazi ya watetezi wake mueleze kwa nini aliwareka. Mimi kama mtanzania ambae natagemea serikali iwalinde raia wake nashangazwa kuona wanatekwa wanashambuliwa hata kuuliwa na serikali ikiwa mshukiwa mkuu.
Kabla yake na baada yake mbona hatukuwahi kusikia utekaji na matumizi mabaya ya mamlaka, kuonyesha huna afya ya akili unaniuliza kwa nini aliwateka.
Nasisitiza kutetea upumbavu lazima uwe mpumbavu kuuzidi
Wewe unaeleza kama kitu ambacho kimethibitika vile kwamba Magufuli ndio muhusika.
 
Hapa mimi siko katika agenda ya kutetea yeyote kama wewe, nionyeshe mahala popote nilipoterea serikali za CCM zilizopita au zilizopo ?
Uovu wa Magufuli unasemwa kama vile uovu wa Kikwete na hata wa Samia unavyosemwa, ila wajinga kazi wanayo ya kutetea maovu
Haumini kwenye kutofautiana mitazamo na ndio maana unataka watu wote tuwe na mitazamo sawa kuhusu Magufuli na hilo ndio linafanya uone mie natetea maovu.
 
Hakuna sehemu yeyote umeonyesha kukereheka na kuumizwa na matendo yake ya kikatili, hili siyo suala la mtazamo bali ukatili juu ya ubinadamu. Na kama hutatizwi na haki za binadamu na kuthamini uhai wao basi you are worse kuliko muuaji mwendazake
 
Wewe unaeleza kama kitu ambacho kimethibitika vile kwamba Magufuli ndio muhusika.
Kama yeye hakuhusika ni nani aliyekamatwa kuhusika na matendo haya wakati wa utawala wake?
Aliyemuua Akwilina aliwajibishwa?
Waliomshambulia Lissu walikamatwa?
Nikikuita mpumbavu siyo kama nakosea nina hakika na upumbavu wako, tetea maslahi mapana ya jamii unayoishi siyo ya mtu.
Naona baada ya spana hata avatar yako umebadilisha picha ya muuaji kweli wewe chizi
 
Kipindi hiki walipotea wengi pia: hatukuwasikia kwakuwa kundi lenye viherrehere na kidomodomoi ndilo lilikuwa in action
Tuonyeshe waliopotea ni kina nani kwa mfano hizo habari zenu za Chato ziwekeni wazi tulinganishe na huyu muuaji.
Na wanaokosoa siyo kundi la walio madarakani hivi sasa, ni kada mbali mbali waliokutana na ushetani wa mwendazake.
 
Hakuna sehemu yeyote umeonyesha kukereheka na kuumizwa na matendo yake ya kikatili, hili siyo suala la mtazamo bali ukatili juu ya ubinadamu. Na kama hutatizwi na haki za binadamu na kuthamini uhai wao basi you are worse kuliko muuaji mwendazake
Bado unaendelea kuonesha kutokuamini kwenye kutofautiana mitazamo, hapa tunajadiliana kila mmoja ana mtazamo tofauti na mwenzie ila wewe unasema et sioneshi kukereka na hayo madai ya ukatili wa Magufuli. Kimsingi unachosema ni kwamba sikubaliani na wewe.
 
Back
Top Bottom