Special message to Mama Janeth Magufuli

Special message to Mama Janeth Magufuli

Hebu tuwe realistic, tusijaribu kubadilisha ukweli wa kilichosemwa na Mzee Makamba, hapo hakuna siasa wala chochote kingine.

Kwa hiyo video uliyoiweka hapo juu, nimemsikia kwa kinywa chake akitamka; "watu wazuri hawafi" huyu amekosea, aambiwe ukweli, asitetewe akazidi kuharibika, mnamponza.

Ndio maana Samia ameomba radhi kwa hiyo kauli yake, kuonesha mzee alikosea.

..mimi nimesikiliza kwa kirefu zaidi kabla na baada ya hayo maneno yanayokukwaza.

..Ni kweli Mzee Makamba amekosea.

..Lakini ni makosa na nia mbaya kwa baadhi yetu kudai Mzee Makamba alimlenga Magufuli.

..Jambo lingine ni kwamba Rais Ssh aliomba radhi na kuliweka sawa suala hili.
 
Pamoja na mapungufu ya marehemu kama wanadamu wengine lakini mzee Makamba ameongea kama mtu aliyerukwa na akili.......
 
..Mzee Makamba hakuwa amemlenga yeyote yule aliyefariki.

..Pia tujiulize kwamba aliyefariki ndani ya Ccm ni Magufuli peke yake? Kwanini mtoa mada hakutaja wajane wengine kwa mfano mke wa marehemu Mzee Kawawa?

..Kwa maoni yangu Mzee Makamba alikosea aliposema kwamba Samia anaweza kufa. Na ktk jitihada za kurekebisha ndio akasema "watu wazuri hawafi..."

..Kama tungetaka kumchomeka Magufuli ktk suala hili, nafasi nzuri ni pale Mzee Makamba aliposema Samia anaweza kufa na Mungu akatuletea mwingine. Hiyo kwa maoni yangu ndio sehemu sahihi ya kumtuhumu amemsema Magufuli.

..Kwa maoni yangu haikuwa sahihi kumburuza Mama Janet Magufuli ktk suala hili. Tunatengeneza kitu ambacho hakipo. Pia nadhani wanaofanya hivyo hawana nia nzuri na yule mjane, nia yao ni vita vya kisiasa ndani ya Ccm.
Kwa hali ilivyo ya kisiasa hapa nchini na mahusiano ya marehemu na hawa walioshika hatamu kwa Sasa....na ukizingatia matamshi yaliyopita ya watu hao au waliokaribu na watu hao juu ya marehemu ni rahisi kuleta tafsiri hiyo katika lugha ya picha na mafumbo........Kwa kifupi mzee Makamba amewehuka kwa kauli haijalishi wajihi wa marehemu
 
Natumia makali0 kufikiria mkuu. Tena yenyewe hayana Malinda. Ili nikusaidie. Yameshakuwa sugu mpaka tembo ndio yanasikia.

Niambie kamanda Kuna jingine.


Yani wewe umeona uwanja tu mkuu.


Unajua gesi Ni yetu Ila tumeiuza halafu tunainunua. Yaani nakuja kwenu baba yako ananiuzia miti baadaye mkitaka mti inabidi mnunue hapo. Kimetumika kiungk gani kuwaza labda
Uwanja wewe unaona dogo? Unajua kwa nini mahakama imesema CAG Musa Assad alifukuzwa kazi kinyume cha sheria?
1.5 trillion jinga wewe
 
Kwa hali ilivyo ya kisiasa hapa nchini na mahusiano ya marehemu na hawa walioshika hatamu kwa Sasa....na ukizingatia matamshi yaliyopita ya watu hao au waliokaribu na watu hao juu ya marehemu ni rahisi kuleta tafsiri hiyo katika lugha ya picha na mafumbo........Kwa kifupi mzee Makamba amewehuka kwa kauli haijalishi wajihi wa marehemu

..Ccm wenyewe wanapenda kauli za Makamba.

..Wanapenda mipasho yake dhidi ya wapinzani.

..Wanapenda anavyotafsiri Misahafu hovyo-hovyo ili kuhalalisha hoja za kisiasa.

..Hakuna mkutano ambao Mzee Makamba hajatoa kauli ya kukera kwa Watanzania au kwa wale waliopokonywa uongozi ndani ya Ccm.

..Wakati wa Magufuli Mzee Makamba alidai wapinzani watabatizwa kwa moto.
 
..Ccm wenyewe wanapenda kauli za Makamba.

..Wanapenda mipasho yake dhidi ya wapinzani.

..Wanapenda anavyotafsiri Misahafu hovyo-hovyo ili kuhalalisha hoja za kisiasa.

..Hakuna mkutano ambao Mzee Makamba hajatoa kauli ya kukera kwa Watanzania au kwa wale waliopokonywa uongozi ndani ya Ccm.

..Wakati wa Magufuli Mzee Makamba alidai wapinzani watabatizwa kwa moto.
Ubinadamu unashamiri Kwa watu wema kufanya mema na kukemea mabaya ya watu wabaya...........

Wahenga wanasema mchuzi wa mbwa unatakiwa kunywewa ukiwa wa moto........

Kauli ya Makamba haikuwa ya kiungwana pamoja na kauli zote za nyuma
 
The truth is, Samia ameomba radhi kwa kauli aliyoitoa Mzee Makamba kwasababu alijua Makamba alikosea, hapa msijaribu kumtetea Mzee Makamba.

Kwa kinywa chake, hakutakiwa kutoa kauli ile ya "watu wazuri hawafi" kwenye mazingira tuliyopo, mbele ya Mama Janeth Magufuli, na Mama Mkapa, msikwepeshe huu ukweli kwa kujaribu kulipaka kosa mafuta, mwambieni ukweli huyo mzee abadilike.
Akili yako ndio ibadilike ianze kuona positively siyo negatively tu, wote tumeisikia dhamira yake mbaya inakutesa
 
Wewe ndio mwenye mahaba huyo mzee alimaanisha hatokufa atakuwepo 2025
Kwa hiyo kama ndio akachomekea wazuri huwa hawafi, ni sawa na kumaanisha kitu gani kwa waliokufa?

Punguzeni haya mahaba yenu, mnazidi kumuharibu huyo mzee.
M
 
Habari mama,

Pole sana kwa msiba wa mumeo!, alikuwa great leader na wananchi wengi wanamkumbuka kwa utumishi wake ingawa ulikuwa mfupi kuliko kiongozi yeyote aliyetawala nchi yetu.

Hiyo Pole niliyotoa ni ya kawaida kwasisi binadamu maana wote tumefiwa wapendwa wetu lakini lengo kuu ni Pole kwa unayosikia na kuona kejeli na kubagazwa kwa marehemu mume wako hadharani bila woga tena kwa mambo mengine yasiyo msingi.

Sikia mama, mume wako alitimiza wajibu wake bila kujali pale alipokosea lakini wewe u hai ubavu wake ukisikia maneno magumu sana. Pengine unalazimika kuwatia moyo watoto lakini wewe mwenyewe umebeba mzigo mzito.

Imagine hata leo maneno yaliyotamkwa mbele yako! Tushukuru mama Samia walau kutuliza moyo wako baada ya maneno magumu leo lakini sio rahisi.

Endelea kuvumilia malimwengu, endelea kuipenda Tanzania! Jipe moyo kama Bikira Maria alivyojipa moyo alivyoshuhudia mwanae akiteswa na kufa msalabani!

Endelea kujipa moyo kama Bikira Maria alivyovumilia hata waliomtenda ubaya Yesu walipoeneza uzushi dhidi yake kuwa wanafunzi wake wamemwiba hakufufuka. Haikuwa rahisi ila moja ya tunu tunayojifunza juu ya Bikira Maria mara nyingi ni yote aliyaweka moyoni!

Kasome utenzi wa Bikira Maria Luka 1: 46-55 Ukutie nguvu. All shall be well 🙏
Yeye mwenyewe alimchoka
 
Katika bara la Afrika Wanaojulikana Viongozi wazuri wanao watetea Wananchi wao walikuwa ni viongozi 5 tu Wa Kwanza Alikuwa Hayati Baba wa Taifa Mwalim Nyerere, Wa pili alikuwa Mzee Nelson Mandela ,Wa Tatu alikuwa ni Kiongozi wa Ghana Kwame Nkurumah, Wa Nne Alikuwa ni Kiongoz wa Libya Kanali Muammar Qaddafi na Wa Tano alikuwa Kiongozi wa Tanzania Doctor John Pombe Magufuli. Na Waliobakia ni Ma-Rais wa nchi tu wanachaguliwa na vyama vyao kuongoza nchi kwa muda malum na muda wao ukimalizika wanaondoka Madarakani wanakuja Ma-Rais wengine Tofauti na Kiongozi wananchi yeye anachaguliwa na Wananchi ili apate kuwaongoza Wananchi wake. Na hata kama akifa bado Kiongozi mzuri huwa anakumbukwa kwa wema wake juu ya Wananchi tofauti na Rais akifa watu hawakawii kumsahau.



 
Kwa kishindo kwa uchaguzi upi? Hayo maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura ndio unaongelea kushinda kwa kishindo?
Magufuli mwizi wa kura sijui alibaka uchaguzi hayupo kwahiyo ushindi nje nje hakuna wizi wa kura.
 
Azory aliisha lifanyia nini taifa hili au alikuwa na ugonvi hupi na Magufuli mpaka amuue? acheni siasa za maji taka,kila Mtu aliyekufa au kupata ajari kipindi cha Magufuli, Magufuli aliushishwa moja kwa moja,sasa huyo azory wapi na wapi na Magufuli?
Hao sio wazima. Kuna watu sio wanasiasa,sio wafanyabiashara,sio waandishi wa habari wala Magufuli hakuwa akiwajua ila et nao wanakwambia walikuwa wanaishi kwa hofu ya kutekwa na Magufuli.
 
Kama unapata wabunge na madiwani wengi, tena huku ukiwa unaibiwa, urais unaukosaje kwa mfano?
Nani sasa wa kukupa huo urais au kutangaza ushindi wa nafasi ya urais tofauti na mgombea wa ccm? Hapo ndio kwenye tatizo lenyewe na wala tatizo sio sanduku la kura, sasa wewe kwa sababu umeachiwa mgawane kwenye ubunge na udiwani ndio akili yako inakupa matumaini kwamba ipo siku wataamua tu na kumtangaza mshindi wa urais mgombea wa chama tofauti na ccm?

Magufuli kaonesha uwezo waliyonao chama tawala na kwambao huo ubunge na udiwani wameamua tu mgawane ili kubalance mambo japo siku zote wao ndio wenye nguvu huko bungeni.
 
Magufuli mwizi wa kura sijui alibaka uchaguzi hayupo kwahiyo ushindi nje nje hakuna wizi wa kura.

CCM haina uwezo tena wa kushinda bila wizi wa kura, na wala haitakaa ishinde tena kihalali bila wizi. Lakini Magufuli hakuwa mwizi wa kura, bali mporaji wa chaguzi zetu.
 
Back
Top Bottom