Special message to Mama Janeth Magufuli

Special message to Mama Janeth Magufuli

Nani sasa wa kukupa huo urais au kutangaza ushindi wa nafasi ya urais tofauti na mgombea wa ccm? Hapo ndio kwenye tatizo lenyewe na wala tatizo sio sanduku la kura, sasa wewe kwa sababu umeachiwa mgawane kwenye ubunge na udiwani ndio akili yako inakupa matumaini kwamba ipo siku wataamua tu na kumtangaza mshindi wa urais mgombea wa chama tofauti na ccm?

Magufuli kaonesha uwezo waliyonao chama tawala na kwambao huo ubunge na udiwani wameamua tu mgawane ili kubalance mambo japo siku zote wao ndio wenye nguvu huko bungeni.

Zamani ndio walikuwa na uwezo huo ila sio sasa. Wanaweza kufanya chochote watakacho ila sio kwa ridhaa ya wananchi tena. Kama kuingia madarakani ni kwa kulazimisha, iko siku hata hao vyombo vya dola wataona na wao wanaweza kukaa madarakani, kwani hata wanaokaa madarakani hawakai kwa kura za wananchi.
 
Acha uchochezi na uchongqnishi mleta mada. Hakuna aliyemnanga jiwe leo. Hayo ni mawazo yako tu.

Hebu mtaje mtu aliyemtaja jiwe kwa jina lake. Vinginevyo ni uzushi na uzandiki tu unaojaribu kuueneza.
Sexless
 
CCM haina uwezo tena wa kushinda bila wizi wa kura, na wala haitakaa ishinde tena kihalali bila wizi. Lakini Magufuli hakuwa mwizi wa kura, bali mporaji wa chaguzi zetu.
Ni kwa sababu tu wewe ulikuwa bado unaendelea kuita ni uchaguzi kilichokuwa kinaendelea na ndio maana unasema Magufuli alipora uchaguzi, uchaguzi wa kupangiwa kwamba urais ni wa ccm tu ila ubunge na udiwani ndio mgawane, sasa huo uchaguzi au utoto?
 
Ila jamaniiiii huyu mama anavumilia mengi, kama ni mm nisinge fika kwenye hvyo vikao, hata kama mumewe alikua na mapungufu ila sio kwa kusikia kauli hizi jamaniiiii 🥲
Kwa mara ya kwanza ndio naona viongozi wanapiga vijembe Hayati bila aibu. Akili za kipumbavu kabisa hizi. Rais anaongea maneno ya kejeri na wengine wanaiga.
 
Huyu mzee makamba ni mwendawazimu na soon maneno yake atayalipia kwa muumba. Soon atalipia kwa kauli zake. Mzee alikuwa na heshima sana miaka ya nyuma ila amekuwa na kauli za kipuuzi sana.
 
Mh. Makamba baba yake January kasema kuwa Kinana na Kikwete hawajafa maana watu wabaya huwa wanakufa akimaanisha Dkt Magufuli alikuwa mtu mbaya ndiyo maana alikufa, Mkapa alikufa kwa sababu alikuwa mtu mbaya, Mwl Nyerere alikufa kwa sbabau alikuwa mtu mbaya, Mzee Karume alikufa kwa sababu alikuwa mtu Mbaya, Horace Kolimba alikufa kwa sababu alikuwa mtu Mbaya …..
Du inchi iko kubaya sana
 
Mkuu unamanisha Magufuli alikuwa mfupi wa kimo kuliko Mkapa au Mwinyi? Au unamanisha ufupi UPI?
 
Ni kwa sababu tu wewe ulikuwa bado unaendelea kuita ni uchaguzi kilichokuwa kinaendelea na ndio maana unasema Magufuli alipora uchaguzi, uchaguzi wa kupangiwa kwamba urais ni wa ccm tu ila ubunge na udiwani ndio mgawane, sasa huo uchaguzi au utoto?

Usitake kupotosha, kwa trend ilivyokuwa inakwenda CCM kwa njia ya kura ilikuwa inakwenda kupoteza mpaka urais. Magufuli alivyoona hivyo na vile ni mpenda sifa za kishamba, akaanza kwa kupika idadi ya wapiga kura, kisha akapanga atangazwe kwa idadi gani ya kura. Kwajinsi uchaguzi ule ulivyokuwa wa kipuuzi, hata CCM waliona aibu kushangalia. CCM wanapenda kuiba, lakini kuwe na ushindani,na sio ule upuuzi aliofanya dhalimu.
 
Wewe unajichanganya kweli, hivi unataka kuniambia kabla ya Magufuli mlikuwa mnashindana na ccm kwenye sanduku la kura huku kukiwa na matumaini ya kumshinda ccm kupitia sanduku la kura?

Kwamba si kweli napotosha kuwa uchaguzi wa Tanzania ni kwamba nafasi ya urais ni ya ccm tu kisha ubunge na udiwani ndio wa kugawana?
 
Habari mama,

Pole sana kwa msiba wa mumeo!, alikuwa great leader na wananchi wengi wanamkumbuka kwa utumishi wake ingawa ulikuwa mfupi kuliko kiongozi yeyote aliyetawala nchi yetu.

Hiyo Pole niliyotoa ni ya kawaida kwasisi binadamu maana wote tumefiwa wapendwa wetu lakini lengo kuu ni Pole kwa unayosikia na kuona kejeli na kubagazwa kwa marehemu mume wako hadharani bila woga tena kwa mambo mengine yasiyo msingi.

Sikia mama, mume wako alitimiza wajibu wake bila kujali pale alipokosea lakini wewe u hai ubavu wake ukisikia maneno magumu sana. Pengine unalazimika kuwatia moyo watoto lakini wewe mwenyewe umebeba mzigo mzito.

Imagine hata leo maneno yaliyotamkwa mbele yako! Tushukuru mama Samia walau kutuliza moyo wako baada ya maneno magumu leo lakini sio rahisi.

Endelea kuvumilia malimwengu, endelea kuipenda Tanzania! Jipe moyo kama Bikira Maria alivyojipa moyo alivyoshuhudia mwanae akiteswa na kufa msalabani!

Endelea kujipa moyo kama Bikira Maria alivyovumilia hata waliomtenda ubaya Yesu walipoeneza uzushi dhidi yake kuwa wanafunzi wake wamemwiba hakufufuka. Haikuwa rahisi ila moja ya tunu tunayojifunza juu ya Bikira Maria mara nyingi ni yote aliyaweka moyoni!

Kasome utenzi wa Bikira Maria Luka 1: 46-55 Ukutie nguvu. All shall be well
Usimlinganishe masihi Kristo na binadamu.

Hekima na utulivu wa huyo mama, na magumu aliyoyapitia, walio karibu naye wanajua.

Ukatili wa mwenzi wake anautambua, na hawezi kuusahau. Yupo na mioyo ya wale waliodhulumiwa na marehemu.

"Nimemsamehe kwa yote aliyonitendea ila siwezi kumsamehe kuhusiana na kifo cha mtoto wangu" Tafakari hiyo kauli.

Alimpigia simu, mtoto anaumwa, amezidiwa. Jibu alilopewa, mimi ndiyo daktari? Na hapo, halali nyumbani kwa wiki nzima. Anakuja kutokea, mtoto hayupo Duniani.
 
Zamani ndio walikuwa na uwezo huo ila sio sasa. Wanaweza kufanya chochote watakacho ila sio kwa ridhaa ya wananchi tena. Kama kuingia madarakani ni kwa kulazimisha, iko siku hata hao vyombo vya dola wataona na wao wanaweza kukaa madarakani, kwani hata wanaokaa madarakani hawakai kwa kura za wananchi.
Zamani ipi unayokusudia wewe?
 
Wewe unajichanganya kweli, hivi unataka kuniambia kabla ya Magufuli mlikuwa mnashindana na ccm kwenye sanduku la kura huku kukiwa na matumaini ya kumshinda ccm kupitia sanduku la kura?

Kwamba si kweli napotosha kuwa uchaguzi wa Tanzania ni kwamba nafasi ya urais ni ya ccm tu kisha ubunge na udiwani ndio wa kugawana?

Narudia tena, usilete upotoshaji usio na tija. CCM waliendelea kuwa wezi wa kura, lakini bado walikuwa wanazidiwa na wapinzani. Na nafasi walizopata za ubunge, udiwani na hata kura za urais zilikuwa zinapanda kila uchaguzi. Na sio kwamba CCM walikuwa wanapanga iwe hivyo, ila walikuwa hawana jinsi kwani ndio uhalisia.

Dhalimu alipoingia kwakuwa alikuwa mpenda sifa, akaamua kunajisi uchaguzi ili aonekane kuwa alikuwa anakubalika sana, yeye na chama chake. Hiyo ndiyo sababu ya yeye kupika idadi ya wapiga kura, na kuagiza wagombea wa CCM watangazwe kwa shuruti. Ukweli huu uko wazi wala hauna kificho.
Zamani ipi unayokusudia wewe?
Kabla hajajiunga jamii forums.
 
Ila jamaniiiii huyu mama anavumilia mengi, kama ni mm nisinge fika kwenye hvyo vikao, hata kama mumewe alikua na mapungufu ila sio kwa kusikia kauli hizi jamaniiiii 🥲
....na wewe weka kidogo ya kwenye kikao japo kwa dondoo!
 
Narudia tena, usilete upotoshaji usio na tija. CCM waliendelea kuwa wezi wa kura, lakini bado walikuwa wanazidiwa na wapinzani. Na nafasi walizopata za ubunge, udiwani na hata kura za urais zilikuwa zinapanda kila uchaguzi. Na sio kwamba CCM walikuwa wanapanga iwe hivyo, ila walikuwa hawana jinsi kwani ndio uhalisia.

Dhalimu alipoingia kwakuwa alikuwa mpenda sifa, akaamua kunajisi uchaguzi ili aonekane kuwa alikuwa anakubalika sana, yeye na chama chake. Hiyo ndiyo sababu ya yeye kupika idadi ya wapiga kura, na kuagiza wagombea wa CCM watangazwe kwa shuruti. Ukweli huu uko wazi wala hauna kificho.

Kabla hajajiunga jamii forums.
Hivi tunaelewana kweli? Nakwambia hali ya uchaguzi ilivyo ni kwamba piga uwa lazima ccm ndio atangazwe mshindi wa nafasi ya urais kwa njia yeyote ile, na miaka yote kumekuwa na malalamiko hayo.
Prof. Assad alisema "watanzania wanashiriki kupiga kura ila hawashiriki uchaguzi" ila wewe bado ulikuwa unaamini kuna uwezekano wa siku kutangazwa mshindi wa urais asiye mgombea wa ccm, ndio nimekuuliza atatangazwa na nani huyo mshindi? Mpaka watu wanataka tume huru wanajua tatizo lilipo ila wewe mwezetu kumbe ulikuwa unaona ipo siku matokeo yatabadilika kwa mfumo huo huo wa uchaguzi jinsi ulivyo.
 
Hiyo Pole niliyotoa ni ya kawaida kwasisi binadamu maana wote tumefiwa wapendwa wetu lakini lengo kuu ni Pole kwa unayosikia na kuona kejeli na kubagazwa kwa marehemu mume wako hadharani bila woga tena kwa mambo mengine yasiyo msingi.
Nina mashaka makubwa na utashi wa baadhi ya wanachama wenzetu, ninadhani ipo haja kuwapima akili watu kabla ya kupewa platforms kuzungumza na public, madhara wanayoleta kwenye familia zetu hayana afya hata kidogo
 
Mzee Makamba kakosea sana...Bora aache wahuni WA mitandaoni kuropoka hayo sio yeye
Tatizo likianza usipolizuia, fahamu litaendelea. Marehemu alikuwa mropokaji mkubwa, na hakuna aliyemkemea. Alichokianzisha kinaendelea, tuendelee kushangilia.

Msaliti hatakiwi kuishi.

Kama hutaki kutoa hela tembea na mavi yako.

Watu wakiandamana kwenda kituo cha polisi, kwa nini msiwalaze chini?

Nimeona mama mmoja pale ameinua bango linasema hakuna maji, kamdai mume wako. Hapa mlichagua mbunge wa upinzani. Sipeleki maendeleo kwa wapinzani.

Kule Msumbiji nimeambiwa kuna watanzania wameuawa, wengine wamefungwa, wengine wamenyang'anywa malo zao. Naseme hivi, wakome kwenda kwenye nchi za watu.

Wakurugenzi, mshahara nikulipe mimi, gari nikupe mimi, halafu unamtangaza mpinzani ameshinda, una akili wewe?

Wanatakiwi wakiri makosa halafu walipe, watakaokataa kukiri, wabakie huko huko, waozee mahabusu.

Hivi mliwahi kukemea kauli hizi za kishetani? Hivi ukilinganisha kauli ya Makamba, na hizi hapa, zipi zenye athari mbaya?
 
Aaaamen.

Justice is coming,

God has remembered our nation, Tanzania.
Na kweli Mungu wetu analipenda Taifa hili. Ametutoa kwenye utawala wa shetani, akatuweka huru. Tuutumie uhuru wetu kwa hekima ili kuwa na Taifa bora. Tumepata uafadhali lakini hatujaufikia ukamilifu. Bado tupo gizani. Bado tuna katiba, Rais mfalme, chama dola, n.k.
 
Habari mama,

Pole sana kwa msiba wa mumeo!, alikuwa great leader na wananchi wengi wanamkumbuka kwa utumishi wake ingawa ulikuwa mfupi kuliko kiongozi yeyote aliyetawala nchi yetu.

Hiyo Pole niliyotoa ni ya kawaida kwasisi binadamu maana wote tumefiwa wapendwa wetu lakini lengo kuu ni Pole kwa unayosikia na kuona kejeli na kubagazwa kwa marehemu mume wako hadharani bila woga tena kwa mambo mengine yasiyo msingi.

Sikia mama, mume wako alitimiza wajibu wake bila kujali pale alipokosea lakini wewe u hai ubavu wake ukisikia maneno magumu sana. Pengine unalazimika kuwatia moyo watoto lakini wewe mwenyewe umebeba mzigo mzito.

Imagine hata leo maneno yaliyotamkwa mbele yako! Tushukuru mama Samia walau kutuliza moyo wako baada ya maneno magumu leo lakini sio rahisi.

Endelea kuvumilia malimwengu, endelea kuipenda Tanzania! Jipe moyo kama Bikira Maria alivyojipa moyo alivyoshuhudia mwanae akiteswa na kufa msalabani!

Endelea kujipa moyo kama Bikira Maria alivyovumilia hata waliomtenda ubaya Yesu walipoeneza uzushi dhidi yake kuwa wanafunzi wake wamemwiba hakufufuka. Haikuwa rahisi ila moja ya tunu tunayojifunza juu ya Bikira Maria mara nyingi ni yote aliyaweka moyoni!

Kasome utenzi wa Bikira Maria Luka 1: 46-55 Ukutie nguvu. All shall be well
Unaweza kukuta huyu mama sasa hivi ana amani kama Makamba!

Yule mtu wenu alikuwa katili sana. Mama huyu alikuwa ameteseka na kuvumilia mengi mno!

Sishangai Makamba kumchukia mtu yule...kwa jinsi alivyomdukua na kumdhalilisha. Huwezi ukawafanyia hivyo viongozi waandamizi wastaafu wa chama chako kwa kusema mapungufu yako wakiwa chumbani!

That man was evil!
 
Back
Top Bottom