Special kwa wadada wa mmu wenye mambo haya

Special kwa wadada wa mmu wenye mambo haya

Hii ni special kwa wadada wa kibongo hasa wale wenye vitambi, fanyeni mazoezi mchome hayo mafuta tumboni, hivi huwa mnajisikiaje kuwa na kitambi kama dume? mavitambi mengine mnajitakia, utakuta mdada asubuhi anaamkia michemsho, mitori, supu karibia nusu kilo ya nyama jamani kweli hapo kitambi utakiepuka? Mchana na jioni ni bia na nyama choma. Wengine hata kujizuia wanashindwa wanapokutana na bia za ofa, kwani lazima ukubali kula/kunywa kisa ofa?? Mwanamke shuti kuwa na self control bwana, jipimie kwa ajili ya mwili wako.

Wengine wanajisifia kwa kushinda bar, hivi hamjui kwamba ni aibu mwanamke kuwa paka la bar?unashindana na wanaume kunywa bila hata aibu? basi fanya mazoezi basi upunguze japo kitambi.

Ninajua mazoezi ni muhimu kwa wote wanawake kwa wanaume lakini wanawake wa miaka hii mmezidi vitambi vya bia.


Smile atakuja na thread yake baada ya kufanya research sasa hivi "Sifa za wanawake wenye vitambi kitandani".
 
Kumbe vitu kama hivi ndivyo vinakumaliza eeh!!! Najua una ugonjwa wa maeneo ya kifua 🙂🙂...Very good choice.



Michaela Pereira (huyo aliyeko kulia) wamuonaje? Mi naona yuko bomba kabisa. Ni zaftig.

o-MICHAELA-PEREIRA-CNN-GOOD-DAY-facebook.jpg
 
Last edited by a moderator:
Na mazoezi yanayozungumziwa si lazima ukimbie kilometre tano la hasha bali chakula unachokula kiwe sambamba na namna unavyoushughulisha mwili wako, sio hata kaumbali kadogo tu unapotakiwa kutembea mguu unapanda taxi kisha ukitoka hapo unaenda kugonga supu mkia wa kondoo na vikorombwezo kibao
 
topic nzuri sana
ila mimi nina swali,kuna mtu anajua pahali kuna yoga classes?hata zile za pregnant women
 
Habare ndio hiyo, janamke limevimbiana tu kama puto, kiuno hukioni, wala nyuma hapajulikani ni wapi.....badilisha mtindo wa ulaji wako usiharibu shepu yako.
 
Asante kwa kutupa ushauri bibie, nimeuchukulia vizuri kabisa ukizingatia kitambi sivifagilii pia. Unakuta mdada kabinuka kitambi mbele na nyuma baraka za allah.. mweeeh!!
 
Asante kwa kutupa ushauri bibie, nimeuchukulia vizuri kabisa ukizingatia kitambi sivifagilii pia. Unakuta mdada kabinuka kitambi mbele na nyuma baraka za allah.. mweeeh!!

apa una maanisha nini my dear BelindaJacob
 
Last edited by a moderator:
Post yako namba 11 imenimaliza, umeandika na kujijibu mwenyewe!

Wewe kweli unajuwa kutetea hoja yako.

Hahahaha nakuona kule siasa umejaa kweli, uwe unapita na huku, si unaona mambo ya kupunguza vitambi haya yanatufaa wote.
 
Unaonekana unakereka sana na miili ya wanawake wengine.
Source : choice of words (janamke)

Kila msomaji ana namna yake ya kuelewa mambo so uhuru ni wako, na una haki ya kuelewa vile utakavyo.
 
Back
Top Bottom