Binti Magufuli
JF-Expert Member
- Apr 2, 2011
- 7,479
- 5,161
Hii ni special kwa wadada wa kibongo hasa wale wenye vitambi, fanyeni mazoezi mchome hayo mafuta tumboni, hivi huwa mnajisikiaje kuwa na kitambi kama dume? mavitambi mengine mnajitakia, utakuta mdada asubuhi anaamkia michemsho, mitori, supu karibia nusu kilo ya nyama jamani kweli hapo kitambi utakiepuka? Mchana na jioni ni bia na nyama choma. Wengine hata kujizuia wanashindwa wanapokutana na bia za ofa, kwani lazima ukubali kula/kunywa kisa ofa?? Mwanamke shuti kuwa na self control bwana, jipimie kwa ajili ya mwili wako.
Wengine wanajisifia kwa kushinda bar, hivi hamjui kwamba ni aibu mwanamke kuwa paka la bar?unashindana na wanaume kunywa bila hata aibu? basi fanya mazoezi basi upunguze japo kitambi.
Ninajua mazoezi ni muhimu kwa wote wanawake kwa wanaume lakini wanawake wa miaka hii mmezidi vitambi vya bia.