Somo kutoka Ethiopia: taifa vitani mbioni kugawanyika, kisa kiongozi kukataa ushauri

Mambo yanaenda according na plan ya CIA..
Kwanza Ku control population kwa kuwapa njaa kubwa..
Sasa kuigawa nchi vipande
 
Watsup comrades,

Taifa la Ethiopia mbioni kugawanyika kama hali iliyopo isipodhibitiwa kwa hekima na busara sio miguvu tena.

Vita ni kati ya majeshi ya serikali ya shirikisho ya Ethiopia chini ya waziri mkuu Abiy Ahmed na vikosi vya chama cha TPLF - Tigray People Liberation Front, katika jimbo la kaskazini mwa Ethiopia linalopakana na Eritrea na Sudan

(Tukumbuke pia Ethiopia ilikuwa ktk vita ya karibu miongo miwili tangu 1993 na Eritrea ambayo ilikuwa ni sehemu ya Ethiopia, na waziri mkuu Abiy Ahmed mwaka 2019 alipata kuwa mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel kwa jinsi alivyofanikisha kuumaliza mgogoro huo wa muda mrefu kati ya Ethiopia na Eritrea)

Kiini cha mgogoro wa Tigray
kwa miaka mingi chama cha TPLF kime-enjoy maisha ya kuwa sehemu muhimu ya serikali ya shirikisho ya AdisAbaba - Ethiopia na kikiwa ni chama chenye nguvu miongoni mwa vyama vilivyounda serikali ya shirikisho ya Ethiopia.

Lakini ulipofika mwaka 2018 baada ya kuchaguliwa ndugu Abiy Ahmed kuwa waziri mkuu, ni alipata umaarufu na uungwaji mkono sana ktk harakati ya kupinga utawala uliokuwepo hivyo kwa uungwaji mkono sana akashinda na kuwa waziri mkuu.

Mara baada ya kuwa waziri mkuu Abiy Ahmed alitaka sana serikali ya shirikisho ya Ethiopia iwe na nguvu zaidi kuliko serikali na vyama vya majimbo hivyo alianza mchakato huo kwa kuunda chama kimoja kilichoitwa Property Party. Jambo hilo la kupunguza nguvu serikali za majimbo na kutaka vyama ku-surrender kwa chama cha Prosperity Party hakikuwafurahisha wazee wa kazi TPLF na hawakuunga mkono.

Hivyo ilipofika wakati wa uchaguzi mwaka jana 2020, waziri mkuu Abiy Ahmed aliahirisha uchaguzi ili kukabiliana na janga la corona, wazee wa kazi TPLF waligoma kuahirisha ktk jimbo lao la Tigray, wakafanya uchaguzi kama kawaida.

Abiy Ahmed na serikali yake waligoma kuutambua uchaguzi huo na uongozi uliochaguliwa na kukiona kitendo hicho kuwa ni dharau ama uasi kwa serikali ya shirikisho ya mjini AdisAbaba, hivyo aliamuru kuchukua hatua mbalimbali kama adhabu ili kuwashinikiza kutii msimamo wa serikali. Mojawapo ya hatua hizo ni kuzuia kupeleka fedha katika jimbo la Tigray kutoka serikali kuu na hatimaye kupeleka vikosi vya jeshi la ENDF - Ethiopia National Defence Forces kuwafunza adabu wazee wa kazi TPLF na kwa kuwapa onyo wakapiga facility moja ya TPLF.

(Ikumbukwe kwa kipindi chote cha vita kati ya Ethiopia na Eritrea ngome kuu ya kijeshi na kivita kwa upande wa Ethiopia ilikuwa ni Tigray na maeneo jirani kama Amhara, hivyo watu wa Tigray kuvizoea vita na pia makamanda wengi muhimu jeshini walikuwa watu wa Tigray, hata baada ya vita bado nguvu kubwa ya kijeshi ilibaki Tigray)

Kwahiyo lilipokuja suala la vita, watu wa Tigray halikuwachukua ugumu kujibu na hatimaye mapigano kuanza baada ya amri kamili ya Abiy Ahmed na ikichangiwa na hasira za TPLF kupunguzwa ushawishi wao ndani ya serikali ya shirikisho.

Je, ilikuwa ni lazima wapigane?
(kukataa ushauri kwa Abiy Ahmed ili kuwafunza adabu wazee wa kazi TPLF)

hakukuwa na ulazima wa kutumia mtutu wa bunduki maana TPLF waliomba mazungumzo kupitia umoja wa Africa lakini Abiy Ahmed alikataa kwa kujiamini na kutaka kutoa somo kwa kila atakayetaka kutunishiana misuli na serikali yake.
●UN pia walishauri njia za amani zitumike
●AU pia walishauri njia za amani zitumike
●na mataifa mengine pia walishauri njia za amani zitumike lakini mbabe Abiy Ahmed alikataa

The Ethiopian prime minister, who was awarded the Nobel Peace Prize in 2019, has rejected a request for peace talks as the conflict in Tigray deepens.
Tigray's leader, Debretsion Gebremichael, wrote to the African Union (AU) last week to request talks.
But PM Abiy Ahmed said in a tweet that there would be no dialogue "until our efforts to ascertain the rule of law are achieved".

Hali ilivyo sasa
mapigano yameendelea lakini vikosi vya serikali vimepunguzwa nguvu na kurudi nyuma kutoka katika maeneo waliyokuwa wanayashikilia. Na TPLF inazidi kuimarika hasa kwakuwa (inawatu) ndani ya jeshi la shirikisho na pia ina watu upande wa AdisAbaba hivyo inataarifa muhimu na pia baadhi ya majimbo taratibu yanaanza kufikiria upya jinsi ya kushirikiana na Abiy na mengine yanatoa support kwa TPLF.

Tayari Abiy Ahmed ameshaanza kuomba raia wajitolee kuiunga mkono serikali na jeshi ktk mapambano dhidi ya TPLF, uungwaji mkono anaotaka ni;

1. Vijana wenye uwezo na utayari kupigana front line kwaajili ya taifa lao wajitolee kujiunga na jeshi kupigana

2. Mchango muhimu wa kutoa taarifa muhimu kuhusu wapiganaji wa Tigray waliopo ktk maeneo yao ambao ni washirika muhimu wa TPLF kwa siri na ikumbukwe wengine wapo ndani ya jeshi kama wanajeshi wengine ni wafanyakazi na wafanyabiashara hivyo ni muhimu raia kutoa ushirikiano kama wana taarifa zozote

TPLF
kwasasa wamebadilisha madai na kutaka wananchi wa Tigray wapige kura ya kutoa maoni yao kama wanataka kujitawala au kuendelea kuwa sehemu ya Ethiopia. Na hili wanalitaka makusudi wakijua kuwa lazima matokeo yatakuwa ni kujitenga na kuanzisha taifa lao la Tigray.

Mwisho (somo)
vita hii kwanza inasikitisha sana kuona waafrika wenyewe wakipigana na mauaji, ubakaji, njaa watu kukimbia makazi yao ndani ya nchi yao kwa sababu za kisiasa zaidi.

Viongozi wetu wa Africa wawe makini ktk kufanya maamuzi yao na hasa kukubali ushauri wa wengine ilimradi ushauri huo unafaa kwa maslahi mapana ya taifa sio kutaka kuoneshana ubabe na kushikishana adabu kama ambavyo Abiy aliamini na kukusudia, leo anaanza kuomba wananchi wasaidie na mambo kuzidi kwenda kombo

Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki Africa
Asanteni
Ndio maaana kunachama Fulani hua kina pendekeza utawala wa majimbo na hayo ndio madhara yake
 
Ni wabishi wenye experience mmoja wa wanachama wao ni Tendros Gebreyesus mkuu wa WHO
Wako wengi Sana Tena sehemu nyeti huko duniani,wamejaribu kuwachomoa imeshindikana.

Ila PM analigawa Hilo Taifa kwa ukabila, kulikua na wanajeshi wa Ethiopia kabila wa tigray walioko kwny mission huko Sudan majuzi waliitwa na serikali ya Ethiopia kurudi nyumbani wamegoma kuondoka Sudan wakisema wakifika huk kwao wanajua Ni mwendo wa kushughulikiwa tu.
 
Mkuu somo lako zuri sana,na pia waafrika tuache hii tabia ya ubinafsi,ndio maana wengi wanaotemgwa wanatafuta uhuru wao wenyewe. Nakumbuka kuna tetesi pia TZ ilianza tabia hiyo ambayo mwishowe huwa mbaya.
 
Back
Top Bottom