Soma haya ujifunze bure katika maisha yako na uyazingatie

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
9,518
14,383
1. Punguza marafiki kwa sababu wapo marafiki ambao wanaweza kua vikwazo vya mafanikio yako na hauwezi kuwajua unapo kua nao na kuishi nao na kula nao unacheka nao na wengine unalala nao wengine hata unajinyima kula ili wale wao lakini ndo namba moja kwa kugeuka kujifanya rafiki huku wanakutafutia njia ya kukumaliza

2. Achana na washauri katika mafanikio yako Kila jambo unalo taka kulifanya katika maendeleo yako unatakiwa kutambua maendeleo ni vita na wala hayataki mshauri ukiingia vitani wewe pambana ushinde ukipenda kushauriwa kwa kila unalo taka kufanya katika maisha yako basi utakua unaishia kushauriwa tu na kila unalo panga kulifanya litakua linaishia njiani halitimii kwa sababu kila mtu atakuja na ushauri wake hapo ndipo unapo kwamisha malengo yako bila kutimiza

3. Kila unapo fanya jambo lolote linalohusu pesa na maendeleo yako kaa mbali na baadhi ya ndugu maana hakuna ndugu anapenda kua masikini halafu wewe uwe tajiri wakati yeye masikini kuna ndugu wanauana kwasababu ya mali na pesa hivyo Kuna baadhi ya ndugu wanaweza kua maadui katika mafanikio yako ndugu wakweli kwako n imama na baba yako tu katika mafanikio yako hata mtoto wako mpe njia nyingine za mafanikio lakini usimpe Siri za mafanikio yako wapo watoto wanaua wazazi wao ili warithi mali za wazazi wao hapo unatakiwa kujua maendeleo ni vita inayo piganwa na mtu yoyote katika hii dunia

4. Weka mbali mapenzi kwa muda unao pambana kutafuta pesa pesa na mapenzi vikikutana katika kichwa chako na akili zako vikatawala macho yako yataanza kuona vitamu na vizuri vingi Sana
 
1. Ukiwa na wengi ndo vizuri, lazima kuna baadhi watachochea maendeleo yako. Baadhi kati ya wengi ni zaidi kuliko baadhi kati ya wachache.

2. Sioni ubaya kwenye kusikiliza ushauri. Hata hivyo mshauri wa mwisho si wewe mwenyewe? Sikiliza tu unaweza pata kitu cha msingi kitakachokufungua macho sana.

Kama huelewi kitu unapuuza tu.

3. Kama ndugu hajawahi kukupa sababu ya kutokumuamini kwanini humuamini?

Ni ndugu tu ndo anaweza kukuua kisa hela? Wafanyakazi wako je? Kila mahali kuna watu.

4. Mapenzi ni moja ya mahitaji ya muhimu kwa binadamu, unataka watu wateseke kwa sonona?

5. Ni kwanini watu wanaogopa sana watu wenzao? Unaogopa kuumizwa? Sasa ni maisha gani hayo yana furaha tu hayana misukosuko? Ndo kuishi huko.
 
Kichwa cha habari unatuambia tusome haya bure tujifunze kwenye maisha yetu na tuyazingatie, Point namba 2 unatuambia tuachane na washauri (wewe mwenyewe ni mshauri)

Mbona unajikaanga na mafuta yako mwenyewe... Punguza sana ushauri, watu wana mipango yao tayari

Okay goodbye, na-log off
 
Lakini umechukua machache, najua sana kama una mipango yako lakini hiyo mipango unaitoa wapi ? Ni lazima Kuna vyanzo ndio vinavyokuwezesha kutengeneza mipango yako
 
1. Ukiwa na wengi ndo vizuri, lazima kuna baadhi watachochea maendeleo yako. Baadhi kati ya wengi ni zaidi kuliko baadhi kati ya wachache.

2. Sioni ubaya kwenye kusikiliza ushauri. Hata hivyo mshauri wa mwisho si wewe mwenyewe? Sikiliza tu unaweza pata kitu cha msingi kitakachokufungua macho sana.

Kama huelewi kitu unapuuza tu.

3. Kama ndugu hajawahi kukupa sababu ya kutokumuamini kwanini humuamini?

Ni ndugu tu ndo anaweza kukuua kisa hela? Wafanyakazi wako je? Kila mahali kuna watu.

4. Mapenzi ni moja ya mahitaji ya muhimu kwa binadamu, unataka watu wateseke kwa sonona?

5. Ni kwanini watu wanaogopa sana watu wenzao? Unaogopa kuumizwa? Sasa ni maisha gani hayo yana furaha tu hayana misukosuko? Ndo kuishi huko.
Mzee wa kuovatek
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom