DOKEZO Soko la Karume (Dar) kuna dalili za rushwa, TAKUKURU ije ikague mapato na matumizi ya makusanyo

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Kero yangu kubwa ambayo naomba jamii itambue ni kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ni kwamba Soko la Karume tunachanga michango mingi kama pesa ya usafi na ulinzi lakini hutujawahi ona mapato na matumizi ya pesa zetu zinaendaje.

Naomba kufikisha ujumbe huu kwa Serikali Kuu kupitia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuwa sisi kama Wadau wa Soko la Karume tunaona kuna mianya ya rushwa sana tu.

Hatuna sehemu ya kulalamika, tunaamini ujumbe huu kupitia JF utawafikia watu wengi na mamlaka zitachukua hatua kushughulikia malalamiko yetu, tunaoteseka ni sisi.
 
Unasemaje hamna sehemu ya kulalamika?

Watanzania nani katuroga?

Kuna Uongozi wa Soko, kuna viungozi wenu, kuna Mkuu wa Wilaya, Kuna Madiwani n.K

Mkishindwa gomeni siku mbili watawazingatia.
 
Back
Top Bottom