Daniel Mjema, Dodoma na Ramadhan Semtawa
"Simba ni mgonjwa, ana matatizo ya akili kichwani, namshauri apelekwe au aende Mirembe akapimwe akili na kupata matibabu kabla hajarudi Dares Salaam."
Mzee Malecela ambaye ni mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu na makamu mwenyekiti mstaafu wa CCM, alisema Simba atafanya kosa kama atarudi Dar es Salaam bila kwenda Mirembe kupima akili na kupata matibabu.
"Asirudi Dar es Salaam bila kupita Mirembe kupima akili, kwa maana atakuwa amepoteza fursa ya kujua matatizo aliyonayo kichwani kwake," alisisitiza.
"Kama Mheshimiwa Simba alikuwa na ushahidi wa tuhuma nzito kama hizo tangu mwaka 2005 kama ambavyo anataka Watanzania waamini, bado haiingii akilini ni kitu gani kilichomfanya asitoe taarifa hizo katika vyombo vya dola,†alihoji Kilango. Source - Mwananchi