Sofia Simba na Sakata la Mafisadi na Wapiganaji!

Sofia Simba na Sakata la Mafisadi na Wapiganaji!

Hoja hujibiwa kwa hoja.....Mzee Tingatinga na Mengi hawajapangua tuhuma zilizotolewa na Mama Simba. Badala yake wanakuja na lugha za vijiweni. Wote (Mama Simba, Mengi, Mama Kilango, Malecela) ni wachafu ila wanatofautiana wingi wa uchafu.

Tutasikia mengi mwaka huu.......wanasiasa tupeni raha...😀.....ingawa mwisho wake ni karaha kwetu!
 
Mkuu Junius,

Naona umechukua upande kwenye vita ya mahasimu wako - ccm
NO, Mkuu nilisema CCM wote mafisadi hata hao wanaojidai wapambanaji...sasa wamewekwa wazi wanabisha...wanabisha nini, bado nashikilia msimamo wangu kuwa CCM si chama safi...hao wanaitwa wapambanani akina Kilango na Mwakyembe wao pia wanabisha na ushahidi tumepata kauli kutoka kwa wana CCM wenyewe...
 
solomon acha kushindana na vichaa !!!tuwe na upeo wa mama kilango umu jf

Pdidy

Nilienda mirembe wakanipima akili zangu wakakuta nina IQ 19/200 chini ya kiwango cha chini cha mtu mzima ambacho ni 20 ya 200.

Hivyo ni kweli niko retarded, waliniuliza ni nani rafiki yangu wa karibu nikawajibu Solomon David, sasa huyu Solomon yeye huwa namshinda vitu vingi tu, sasa piga mahesabu anaweza kuwa na IQ kiasi gani

angalia range scale za IQ kwenye hii link

http://www.personality-and-aptitude-career-tests.com/iq-rating-scale.html

Kama kuna doctor yeyote unamfahamu tunahitaji msaada wako

Hivi leo siku gani? Jumanne?
 
Mama Simba amechagua vita ambayo hatashinda. Mwaka huu itabidi watafute mzimu wa nyerere kuwasaaidia.
 
Hoja hujibiwa kwa hoja.....Mzee Tingatinga na Mengi hawajapangua tuhuma zilizotolewa na Mama Simba. Badala yake wanakuja na lugha za vijiweni. Wote (Mama Simba, Mengi, Mama Kilango, Malecela) ni wachafu ila wanatofautiana wingi wa uchafu.

Tutasikia mengi mwaka huu.......wanasiasa tupeni raha...😀.....ingawa mwisho wake ni karaha kwetu!

hoja za mama simba ni zipi? mtoto akitoa viroja kwa nini ajibiwe kwa hoja?
 
pigo kali naona mnatapatapa,mara mnatafakari...jibuni hoja...kama anawazimu mngenyamaza kimya vinginevyo kimewachoma.

- Kichaa hufurahiwa na vichaa wengine wala sio siri! Ndio maana Mwalimu alikuwa hamjibu Idd Amin, maana wote wangeishia Mirembe!

- By the way, vipi Kiwira na Meremeta? Bwa! ha!

Respect.


FMEs!
 
NO, Mkuu nilisema CCM wote mafisadi hata hao wanaojidai wapambanaji...sasa wamewekwa wazi wanabisha...wanabisha nini, bado nashikilia msimamo wangu kuwa CCM si chama safi...hao wanaitwa wapambanani akina Kilango na Mwakyembe wao pia wanabisha na ushahidi tumepata kauli kutoka kwa wana CCM wenyewe...

Je msimamo wako ni kuwa alichosema mama simba ni ukweli?
 
- Hapana ndugu yangu nipo sometimes sipo, lakini wiki yote hii nimekuwepo na bado nipi mpaka mwisho wa wiki, ngoja tuvine hapa JF ngoma ya wachawi, sujakuona ndugu yangu vipi upo?

Respect.

FMEs!
Mie nipo kama sipo lakini nipo, si unajua maisha mkulu...pirika pirika...nikipataga wasaa, huwa nakuja hapa kijiweni kupata habari....
 
Vichaa hawa kila siku wakiachiwa wataendelea kuwafanya watanzania wote kuwa ni mazezeta. Wanaendelea kuuza nchi na wakiulizwa wao wanaleta ukichaa. Mwaka huu watabanwa tu hapa hapa.
 
- Hawa vichaa ni wengi sana maana mtumzima anapoandika, anajiuliza na kujijibu huku akijipa thanks, hakika hiyo inatakiwa kuwa safari ya Miremebe, au?

Respect.

FMEs!
 
- Kichaa hufurahiwa na vichaa wengine wala sio siri! Ndio maana Mwalimu alikuwa hamjibu Idd Amin, maana wote wangeishia Mirembe!

- By the way, vipi Kiwira na Meremeta? Bwa! ha!

Respect.

FMEs!
Mkuu majibu ya Mwalimu kwa Idd Amin yalikuwa ni damu kwa damu...nani alikuwa kichaa kati yao...aliyemaliza ugomvi kwa shari au aliyeanza shari bila ya ugomvi?
Ya kiwira na Meremeta mwenyewe yupo kikaangoni...tunataka haya ya uswahiba na mafisadi...inasomeka vipi...yaani unamkana shetani na huku ukicheza ngoma yake...hapo vipi mkuu?
 
- Kichaa hufurahiwa na vichaa wengine wala sio siri! Ndio maana Mwalimu alikuwa hamjibu Idd Amin, maana wote wangeishia Mirembe!

- By the way, vipi Kiwira na Meremeta? Bwa! ha!

Respect.


FMEs!

FMES ushaingia tena kwenye mtego wa kutetea CCM na wapiganaji wako?

Hivi kiwira, meremeta , na uchafu wote huu si ni hao hao CCM

CCM mnaanza kushindana waliokula sana na waliokula kidogo.

Msimsahau houseboy wenu(my very best friend) Solomon David! angalau fedha za chenji ya fegi atakuwa anatia mfukoni
 
- Hawa vichaa ni wengi sana maana mtumzima anapoandika, anajiuliza na kujijibu huku akijipa thanks, hakika hiyo inatakiwa kuwa safari ya Miremebe, au?

Respect.

FMEs!

Si ndio hapo sasa,

Kuna mwingine anajiita painstruth kasema kuwa alishafukuza wengi sana hapa jf wakati ana posts 8 tu. Yaani posts 8 zinatosha kufukuza watu wengi sana hapa JF?

Hawa hata sio vichaa, ni zaidi ya vichaa wa kawaida.
 
"Asirudi Dar es Salaam bila kupita Mirembe kupima akili, kwa maana atakuwa amepoteza fursa ya kujua matatizo aliyonayo kichwani kwake," alisisitiza.
Hii ni pamoja na Mwanakijiji
 
Mkuu majibu ya Mwalimu kwa Idd Amin yalikuwa ni damu kwa damu...nani alikuwa kichaa kati yao...aliyemaliza ugomvi kwa shari au aliyeanza shari bila ya ugomvi?
Ya kiwira na Meremeta mwenyewe yupo kikaangoni...tunataka haya ya uswahiba na mafisadi...inasomeka vipi...yaani unamkana shetani na huku ukicheza ngoma yake...hapo vipi mkuu?

wale wanaodhani kuwa wanaficha hisia zao za mapenzi yao kwa ccm wanaweza kuwa vichaa zaidi ya Idi Amini na Mwalimu combined.
 
- Tatizo siwezi kukujibu mtu mmoja na multiple IDs, kwa hiyo unaweza kuendelea nitajitahidi tu kukuelimisha inapobidi, pole sana mkuu!

- Halafu maneno ya kuwakwepa vichaa ni mazito sana na yanahitaji kuzingatiwa maana sio siri na humu tunao pia!

Respect.


FMEs!
 
FMES ushaingia tena kwenye mtego wa kutetea CCM na wapiganaji wako?

Hivi kiwira, meremeta , na uchafu wote huu si ni hao hao CCM

CCM mnaanza kushindana waliokula sana na waliokula kidogo.

Msimsahau houseboy wenu(my very best friend) Solomon David! angalau fedha za chenji ya fegi atakuwa anatia mfukoni

So far umefukuza wangapi?

Record yako si mchezo - posts 8 tu umefukuza wengi hapa JF. Nategemea mwisho wa siku leo utakuwa umefukuza wanachama 50.
 
Je msimamo wako ni kuwa alichosema mama simba ni ukweli?
Mama Simba proved me right kuwa CCM wote ni mafisadi hakuna mwenye uwezo wa kujidai kumnyooshea vidole mwenzake, zaidi ni ishara kuwa akina Kilango walikuwa wakiwazubaisha tu watanzania wakati wao wenyewe vidole vinajielekeza kwao...Mkuu lisemwalo lipo...maana Kilango anakiri kuwa madai hayo yapo muda mrefu na anamshangaa mama simba kwa nini hakuchukuwa hatuwa huku akisahau kuwa alisaidiwa yasifike mbali katika ile "kulindana lindana" na "usimwambie mtu".
 
MALUMBANO makali yameendelea kuitikisa Kamati ya rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi baada ya makombora ya juzi kuelekezwa kwa Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango na mumewe, mzee John Malecela.

Kamati hiyo imekuwa ikipokea mashambulizi makali baina ya wabunge ambao wanaonekana kuwa vinara wa vita dhidi ya ufisadi na wale ambao wanaona kuwa vita hiyo inawalenga, kiasi cha kurushiana tuhuma nzito zilizo na mwelekeo wa kuchafuana.

Baada ya kulipuana Jumanne, juzi ilikuwa zamu ya Mama Kilango na mumewe Malecela wakati Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Simba alipotoa tuhuma nzito akidai kuwa wawili hao pia wamekula fedha za ufisadi.

Habari kutoka vyanzo vyetu zilieleza kuwa Simba alidiriki kudai kuwa hata harusi ya makamu huyo wa zamani wa CCM na Kilango ilifadhiliwa na mtuhumiwa wa ufisadi, Jeetu Patel.

Patel kwa sasa ana kesi katika Mahakama ya Kisutu akituhumiwa kuiibia Benki Kuu (BoT) kwa kuchota takribani Sh11 bilioni kutoka katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA).

Akijieleza kwenye kamati hiyo, Simba alimtuhumu Malecela, ambaye aliwahi kuwa waziri mkuu katika serikali ya awamu ya kwanza, kuwa wakati akiwania kuteuliwa kugombea urais kwa tiketi ya CCM mwaka 2005, Jeetu Patel alimpa Sh200 milioni kwa ajili ya kampeni zake.

Malecela, ambaye wakati huo alikuwa makamu mwenyekiti wa CCM, aliondolewa mapema kwenye mbio za urais, ikiwa ni mara ya pili baada ya kuenguliwa tena mapema mwaka 1995.

Waziri huyo mwenye dhamana ya utawala bora akiwa na taasisi nyeti kama Takukuru na Idara ya Usalama wa Taifa, alizidi kurusha makombora kwa wanandoa hao, akisema Mama Kilango ni mnafiki na sio msafi kiasi cha kuwanyooshea wengine vidole wakati harusi na kampeni zake za ubunge zilifadhiliwa na mtuhumiwa huyo wa ufisadi.

Habari zinasema kuwa Mama Simba alikuwa akizungumza kwa kujiamini na kwa ujasiri na kumtuhumu Mama Kilango kuwa kelele zake zote zinatokana na nongwa ya "kuukosa U-first lady (kuwa mke wa rais)."

Alieleza kuwa kelele zote za mbunge huyo wa Same Mashariki zinatokana na chuki na uchu wa madaraka na si kweli kwamba ni mpinga ufisadi, kwa mujibu wa mtoaji habari wetu.

Lakini Patel, alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo za Waziri Simba kwamba alifadhili harusi ya Malecela na kampeni zake za urais, alionekana kustuka na kusema: "Haa...we nani kakwambia... Bwana ehee, mimi sijui lolote kuhusu hayo.

"Kwa sasa mimi najiangalia mwenyewe, nina matatizo yangu mengi nahangaika nayo."

Hata alipofafanuliwa kwamba, maneno hayo yalisemwa na Waziri Simba, alijibu: "Kama wao wamesema wenyewe huko, mimi sijui."

Naye Kilango alisema alishuhudia wakati wakati makombora hayo yakirushwa na kueleza kwamba anajiandaa kujibu mapigo.

Mbunge huyo machachari alisema anajua kwamba mambo yote yaliyosemwa, yanamlenga yeye na si mumewe Malecela.

"Mimi ni mwanasiasa... andikeni yote yaliyozungumzwa bila ya kuacha baadhi na siwezi kuwashtaki," alisema Kilango.

Mzee Malecela hakutaka kuzungumzia lolote kuhusu tuhuma hizo wakati alipoulizwa juu ya uhusiano wake na Patel na kama aliwahi kupokea kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kampeni.

"Ahaa... kijana naomba uniache nipumzike," alisema Malecela.

Mbali na mzee Malecela na mkewe, Waziri Simba pia alimgeukia mwenyekiti mtendaji wa IPP, Reginald Mengi akimtuhumu kuwa anaendesha vyombo vya habari vinavyoichafua CCM na serikali yake kwa maslahi yake binafsi.

Pia alimshambulia mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe na mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka, akiwatuhumu kuwa ni watu wenye njaa na kwamba, wanalipwa fedha kufanya kazi hiyo.

Waziri Simba alisema kuwa hata tuhuma dhidi ya mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge na mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, zimetokana na chuki binafsi.

Simba alisema kuwa uchunguzi wa kashfa ya rada ulishamalizika na Chenge akasafishwa na kuongeza kwamba hata uchunguzi wa Richmond umebaini kulikuwa hakuna rushwa, kwa mujibu wa mtoaji habari wetu.

Suala la Richmond liliibuka tena mbele ya kamati hiyo ya Mwinyi wakati mbunge wa Bukoba Vijijini, Nazir Karamagi alipolalamika kuwa ripoti ya kamati teule ya Bunge iliyoozwa Dk Mwakyembe haikumtendea haki.

habari hizo toka ndani ya kikao hicho zinaeleza kuwa Karamagi alisema ripoti ya Richmond ilionea baadhi ya watu na akapendekeza iundwe tume huru kupitia mchakato huo kuona kama wana makosa ili haki itendeke.

Mbunge huyo ambaye alijiuzulu uwaziri baada ya Lowassa kuachia wadhifa wake wa waziri mkuu kutokana na kashfa hiyo, alisema maamuzi yake kuhusu Richmond yalitokana na mapendekezo ya Bodi ya Tanesco.

Naye Dk Mwakyembe alijibu hoja iliyotolewa Jumanne na mbunge wa Ukonga, Dk Makongoro Mahanga aliyedai kuwa ripoti ya Richmond ni 'feki', akisema tatizo la Dk Mahanga ni uelewa mdogo.

Kuhusu hoja ya Karamagi, Dk Mwakyembe alisema malalamiko yake si sahihi kwa sababu yapo maeneo mengi ambayo Karamagi alishiriki na yako bayana hayahitaji mjadala.

Aliwatahadharisha Wabunge kuacha kudodosa sana ripoti ya Richmond kwani watazidi kumchafua Lowassa na kwamba wanaweza kufungwa kwa sababu upo ushahidi dhahiri.

Dk Mwakyembe aliwataka viongozi wa CCM wenye tuhuma kuiga mfano wa Mzee Mwinyi aliyejiuzulu baada ya mauaji yaliyofanywa na vyombo vya dola mkoani Shinyanga.

Akizungumza mbele ya kamati hiyo, kwa mujibu wa vyanzo vyetu, alimshambulia spika wa Bunge, Samuel Sitta akidai kuwa kama si mizengwe, suala la Richmond lingemalizwa kwa taratibu za kichama.

Habari hizo zinadai kuwa Chenge, aliyewahi kuwa mwanasheria mkuu wa serikali, alisema Lowassa alizungukwa na kwamba kulikuwa na njama za kummaliza ingawa hakusema njama hizo zilifanywa na nani.

Chenge aliitetea serikali ya awamu ya tatu kuhusu kuingia mikataba mibovu na kusisitiza hakukuwa na uzembe kwani mikataba yote ilipitiwa na kukubaliwa na Baraza la Mawaziri.

Hata hivyo, mbunge wa Muleba Kusini, Wilson Masilingi alisimama na kuomba kutoa taarifa na kumwomba Mzee Mwinyi na kamati yake wawabane wabunge wanaodai wanasema ukweli.

Masilingi alipinga maelezo ya Chenge kuhusu mikataba na kusisitiza kuwa maelezo yake yalijaa ushabiki na kusema Baraza la Mawaziri liliridhia mikataba kutokana na ushauri wake (Chenge).

Mbunge wa Kwela, Dk Chrisant Mzindakaya, ambaye aliwahi kupata umaarufu kwa kulipua kashfa, aliwataka wabunge wakubali matokeo kuhusu Ripoti ya Richmond ili taifa lisonge mbele badala ya malumbano yasiyokwisha.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, Mzindakaya aliwataka wabunge wafahamu kuwa ripoti hiyo ilishapitishwa na Bunge na haiwezi kurejeshwa ianze tena upya.

Naye Dk Mlingwa (Shinyanga Mjini), alisema mpasuko unaoinyemelea CCM unatokana na chama hicho kuacha misingi yake ya kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi na badala yake kinawakumbatia wafanyabiashara.

Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Emanuel Nchimbi alitumia nafasi yake kuomba maridhiano ya wabunge wa CCM, kujenga moyo wa kusameheana ili chama kisonge mbele.

Daniel Mjema,Dodoma
__________________
A wise man once told me, luck isn't some mystical

KWA HUU UPUUZI JAMANI NAHISI HATA RAIS WAKE ALIEMTEUA LAZIMA AWE ANA MATATIZO KAMA SI AKILI YA KISAIKOLOJIA
VIVA CHAMA CHA MAJAMBAZI
Wadau hii kamati itatoka kapa. Haitapata mafanikio yaliyokusudiwa, badala yake wabunge watavunjika vipande vipande mbele yao.
Alah kumbe bado makovu ya ugombea wa 2005 yanaendelea? Wakitoka huko wanatuambia sisi m wameshapatana na kuvunja kambi! kumbe uongo sio?
Ebu FMES na kibunango, leteni habari basi kumbe makundi bado yako kwenye chama chenu? Hizi ni habari toka Ikulu bwana tena kwa JK mwenyewe.
 
vichaa hawa kila siku wakiachiwa wataendelea kuwafanya watanzania wote kuwa ni mazezeta. Wanaendelea kuuza nchi na wakiulizwa wao wanaleta ukichaa. Mwaka huu watabanwa tu hapa hapa.

kabisa kaka na iwe hivi milele yote mwaka huu m'kijiji alisema yataibuka mengi tu ccm na bado
 
Back
Top Bottom