Sofia Simba na Sakata la Mafisadi na Wapiganaji!

Sofia Simba na Sakata la Mafisadi na Wapiganaji!

WAZIRI mkuu wa zamani, John Malecela jana alimshukia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Simba akisema kuwa tuhuma alizozitoa dhidi yake zinatokana na waziri huyo kuwa mgonjwa wa akili, huku mkewe ana Kilango, akimshangaa kwa kukalia tuhuma hizo kwa kipindi kirefu.

Mbali na wanandoa hao, mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi naye alipuuza tuhuma alizorushiwa na Waziri Simba akisema kuwa hawezi kubishana na mjinga.

Malecela, Kilango na Mengi ni miongoni mwa watu kadhaa walioshambuliwa na Waziri Simba Jumatano, akiwatuhumu wanandoa hao kuwa walichukua fedha za kifisadi wakati walipofanya harusi yao mjini Dodoma na katika kampeni za urais za mwaka 2005, huku akimtuhumu Mengi kuwa anatumia vyombo vyake vya habari kuichafua CCM na serikali yake kwa maslahi binafsi.

Wote watatu hawakuingia ndani kukanusha madai hayo ya Simba wala kutoa ufafanuzi, na badala yake Mengi na Malecela walimrushia maneno makali wakimwita kuwa ni mgonjwa wa akili, asiye na maadili, mropokaji na ambaye si msafi huku Kilango akisema kuwa bado anatafakari.

Malecela, ambaye alikuwa waziri mkuu na makamu wa kwanza wa rais (1990 hadi 1994), alidai kuwa Simba ni mgonjwa wa kichwa na akili hivyo anapaswa kupelekwa Hospitali ya Mirembe kabla ya kurudi Dar es Salaam baada ya bunge kuisha.

Hospitali ya Mirembe iliyo mjini Dodoma hujishughulisha zaidi na tiba ya watu wenye matatizo ya akili.

Kama ilivyokuwa kwa Kilango ambaye alidai juzi kuwa mashambulizi dhidi yake yanatokana na mumewe, Malecela naye jana alidai kushambuliwa kwake ni kutokana na mkewe Kilango kwamba ameona azungumze kwa kifupi kuhusu hali halisi ya akili ya Simba.

"Najua chanzo kikubwa ni mama (Kilango), yeye leo ametoa taarifa yake, lakini na mimi ninalo moja dogo la kusema kijana ambalo ni ushauri kwa Waziri Simba," alisema Malecela.

"Simba ni mgonjwa, ana matatizo ya akili kichwani, namshauri apelekwe au aende Mirembe akapimwe akili na kupata matibabu kabla hajarudi Dares Salaam."

Mzee Malecela ambaye ni mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu na makamu mwenyekiti mstaafu wa CCM, alisema Simba atafanya kosa kama atarudi Dar es Salaam bila kwenda Mirembe kupima akili na kupata matibabu.

"Asirudi Dar es Salaam bila kupita Mirembe kupima akili, kwa maana atakuwa amepoteza fursa ya kujua matatizo aliyonayo kichwani kwake," alisisitiza.

Kwa sasa Waziri Simba yuko Dodoma kuhudhuria vikao vya Bunge na alitoa kauli za kumshambulia Malecela, Kilango, Mengi na Mwakyembe kwenye mikutano inayoendelea baina ya wabunge wa CCM na Kamati ya Mwinyi ya kutafuta chanzo cha kutoelewana ndani ya chama hicho.

Malecela, ambaye aliwahi kuteuliwa kuwa mmoja wa watu sita wenye busara katika nchi za Umoja wa Madola mwaka 1985, hakueleza kama ana ushahidi wa madai yake.

Hata hivyo, Simba aliwahi kuugua akiwa Afrika Kusini na baadaye Hindul Mandal akiwa anasumbuliwa na kizunguzungu na kutapika, ugonjwa ambao waziri huyo aliwakariri madaktari wakisema utapona taratibu.

Hata hivyo, alipoulizwa iwapo tuhuma za yeye kufadhiliwa na Patel katika harusi yake na kupewa kiasi hicho cha fedha Sh200 milioni za kampeni za Urais mwaka 2005, Malecela alisema tuhuma hizo zimetolewa na mgonjwa.

Naye mbunge wa Same Mashariki, Kilango alionyesha kushangazwa na tuhuma hizo na kumshangaa waziri huyo kukalia tuhuma nzito alizozitoa kwa muda mrefu bila kuzifikisha kwenye vyombo vya sheria.

Kilango na Malecela walituhumiwa na Simba Jumatano kuwa nao walichukua fedha za ufisadi, akidai kuwa harusi yao ilifadhiliwa na Jeetu Patel, ambaye ni mtuhumiwa wa ufisadi na hali kadhalika kampeni za urais za Malecela za mwaka 2005.

Katika tuhuma zake, Waziri Simba alidai kuwa Kilango ni mnafiki na si msafi kiasi cha kuwanyooshea wenzake vidole na kwamba kelele zake zote zimetokana na kukosa kuwa mke wa rais baada ya Malecela kuenguliwa mapema na CCM kwenye mchakato wa kumpaya mgombea wake.

Lakini jana, Kilango alisema hatakatishwa tamaa na tuhuma hizo nzito, ambazo alisema bado anazitafakari, ili kubaini kiini chake na sababu za kutolewa sasa katika kipindi ambacho vita dhidi ya ufisadi imepamba moto.

Kilango, ambaye mwaka huu alitunukiwa Tuzo ya Mwanamke Jasiri na serikali ya Marekani, alimshangaa Simba kukaa kimya na tuhuma hizo tangu 2005 wakati vyombo vya dola vipo.

"Kama Mheshimiwa Simba alikuwa na ushahidi wa tuhuma nzito kama hizo tangu mwaka 2005 kama ambavyo anataka Watanzania waamini, bado haiingii akilini ni kitu gani kilichomfanya asitoe taarifa hizo katika vyombo vya dola,” alihoji Kilango.

Kilango alifafanua kwamba Simba ni waziri mwenye dhamana ya utawala bora ambaye ana vyombo vya uchunguzi chini yake kama Takukuru, lakini akashangaa kutovitumia.

“Ni imani yangu kwamba, mheshimiwa Simba ambaye ni waziri katika Ofisi ya Rais atapimwa na wananchi kama malumbano anayoyaanzisha sasa yana chembe ya ukweli kiasi gani au ni kujaribu kuwahamisha Watanzania katika vita nzito dhidi ya ufisadi,” alisema.

Katika taarifa yake ya maandishi, Kilango alisema asingependa kuingia katika malumbano na waziri huyo kwa kuwa itawapa taabu Watanzania kutofautisha pumba na mchele.

Kauli ya Simba inaonekana kuibua mjadala mpya katika vita dhidi ya ufisadi katika kipindi hiki ambacho kimetawaliwa na malumbano makali baina ya wabunge wanaojinadi kuwa ni makamanda wa vita ya ufisadi na wale wanaodai kuchukulia vita hiyo kuwa ni ya kukichafua chama na serikali.

Malumbano hayo yamefikia kipindi ambacho wabunge wenyewe wameanza kuhoji maamuzi yao ya kukubaliana na ripoti ya kamati teule iliyochunguza kashfa ya mchakato wa utoaji wa zabuni ya uzalishaji umeme wa dharura kwa kampuni ya Richmond Development na kutaka uchunguzi mpya ufanyike ukihusisha tume huru.

Tayari mawaziri wawili, Dk Makongoro Mahanga na Simba wamejitokeza kumtetea Edward Lowassa ambaye aliachia wadhifa wake wa waziri mkuu kutokana na kutakiwa na ripoti hiyo kufanya maamuzi kwa kutumia busara yake kutokana na kashfa hiyo.

Hata mbunge wa Bariadi, Andrew Chenge, ambaye alijiuzulu uwaziri baada ya kutajwa kwenye kashfa ya ununuzi wa rada, naye amejikuta akipata watetezi, akiwemo Waziri Simba ambaye alielezea kuwa uchunguzi umeonyesha kuwa mwanasheria huyo mkuu wa zamani wa serikali hana hatia.

Nje ya Bunge, Mengi ndiye aliyeguswa zaidi na Waziri Simba na jana aliongea na waandishi wa habari kuhusu tuhuma hizo akisema: "Dont argue with a fool because people may not know the difference between you and the fool (usibishane na mjinga kwa sababu watu wanaweza kushindwa kufahamu tofauti yako na huyo mjinga)."

Hata hivyo, Mengi alisema wakati mwingine unalazimika kujibu hoja "unapoona mtu anapotosha mambo kwa makusudi" na akaeleza kuwa Waziri Simba si mtu msafi hivyo ni vema katika vita ya ufisadi inayoendelea akakaa kimya kuliko kujitokeza na kuropoka.

Mengi, ambaye amekuwa akionekana kuunga mkono kundi linalopambana na ufisadi, alimtaka Waziri Simba kutafuta ushauri kutoka taasisi za serikali, ikiwemo Idara ya Usalama wa Taifa, kabla hajazungumza.

Hata hivyo, Mengi hakutoa maelezo ya tuhuma kwamba amekuwa akitumia vyombo vyake vya habari kuendesha kampeni zinazoichafua CCM na serikali yake kwa maslahi yake binafsi na badala yake alielezea uanachama wake kwenye chama hicho tawala.

"Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikituhumiwa na baadhi ya viongozi wa CCM kwamba, mimi si mwanachama wa chama hicho na kwamba sitoi misaada ya hali na mali kwa chama," alisema Mengi katika mkutano wake na waandishi.

"Kwanza, kuhusu kuropoka kwamba sitoi misaada kwa CCM, hilo ni jambo linalozushwa na watu binafsi na kwa malengo binafsi. Viongozi wakuu wa CCM ambao ni waadilifu na wanaosimamia ukweli wanajua undani wa jambo hili. Siwezi kusema nasaidia nini CCM, kwa kuwa itakuwa ni kukidhalilisha chama changu.

"Pili, kuhusu uanachama wangu wa CCM, napenda kuwaambia kwamba mimi ni mwanachama wa CCM tangu tarehe 18 Aprili,1977 na kadi yangu ni na. B124595, iliyotolewa na tawi la Kisutu, wilaya ya Ilala, mkoa wa Dar es Salaam."

Katika mkutano huo, Mengi alitumia vielelezo kujibu tuhuma kwamba amejiunga na CCM hivi karibuni.

Mengi alisema anashangaa kauli za Waziri Simba na katibu wa CCM mkoani Dares Salaam, Shaaban Kilumbe kwamba, alipita matawi yote na kubaini hakuna sehemu ambako aliwahi kuwa mwanachama.

"Lakini wakati mwingine inawezekana hakuona kweli kwa sababu labda hajui kusoma... ni kitu kibaya sana kujaribu kuzungumzia mambo yanayohusu kusoma wakati hujui kusoma, labda Reginald kasoma John," alituhumu.

Aliongeza kwamba wanaosema CCM hakuna kiongozi msafi ni dhahiri wao ndiyo wameingia katika chama hicho hivi karibuni na kusisitiza: "Ningetoa ushauri waondoke na watuachie chama chetu kwa kuwa hawafahamu misingi imara ya CCM."
Tangu Kamati ya Mwinyi ianze kazi ya kuwahoji wabunge mjini Dodoma, kumekuwepo na kurushiana maneno ya kudhalilishana baina ya wabunge hao wa chama tawala, kwa ufisadi na kupokea fedha zinazotokana na ufisadi.
 
We need this kind of things and information safi sana..polepole tutajua nani "ana akili" hata busara katika kundi hili kubwa la viongozo wetu wa zamani na CCM what a chance?? kumbe hata JM wapo kwa mipasho lol.
 
wewe mtaje Mungu wako, mimi nitaleta picha ya mama yake kavaa hijab.

1 Kings 19: 11 ...

Then He said, "Go out, and stand on the mountain before the Lord." And behold, the Lord passed by, and a great and strong wind tore into the mountains and broke the rocks in pieces before the Lord, but the Lord was not in the wind; and after the wind an earthquake, but the Lord was not in the earthquake; and after the earthquake a fire, but the Lord was not in the fire; and after the fire a still small voice.

Okay,

Leta picha ya "mama" yake huyu MUNGU kama unayo. Na ukimaliza ujieleze ni kwa nini ulitumbua pesa za madawati ya wanafunzi wa mtakuja.
 
Tayari mawaziri wawili, ""Dk Makongoro Mahanga"" na Simba

EMBU TUTAKE RADHI YALIOANDIKWA RED...WAMESHAVULIWA HAWA U DK WAO FWEKI.....NDIO MAANA WANAONGEA PUMBA
 
Yaani naisoma hii habari siku ya tatu leo na wala haina hayo maneno yaliyoombwa na takriban kila msomaji....Muheshimiwa kasemaje?? Nimeona mahala fulani kumesemwa watu wataanza kusoma magazetini Ijumaa, sasa kumbe hii ilikuwa ni promo ya magazeti tu?? Haya bwana, ngoja niende maskani nikasome hayo magazeti nieone kama kweli kuna mtu kathubutu kusema maneno ya closed door meetings...
 
Alivyoumbuliwa na RA kwamba familia yake ilikwapua hela za wawekezaji mwenyewe alikiri kwamba wawekezaji walichotewa hela zao kinyume na urtaratibu wa kampuni na baada ya kugundua hilo alilala mbele (resign). hakusema alipiga kelele dhidi ya ufisadi kwa sababu beneficiaries walikuwa familia yake na marafiki. Sasa huyu ni mpiganaji?

Mengi aliumbuliwa na RA, lini hapo?

Huyu ni the same RA wa richmond, Kagoda, EPA, Dowans, etc?

Angalia video ya majibu yake dhidi ya mashambulizi ya RA.

Mzee mengi 'mpenda vita' kama daily News wangeoongopa kwamba hesabu zao (NICOL) zilikuwa chafu unadhani anagekaa kimya?

Walichosema dailynews kilihitaji majibu gani? kama ambayo nasubiria toka kwako kuhusu pesa za madawati ya mtakuja?
 
Ha ha ha,

Unashindwa nini kuisema hapa kama ipo?



Kama vile na wewe ulivyopambana na mama roza muuza maandazi na ukapata jiko la mkaa (sina uthibitisho kwenye hili but nitasema tu anyway)?



Nani asiyejua nguvu zako zinatoka kwa Salum Abdalah (hapa sina uthibitisho ila nitamwaga udaku tu kwa vile hii ni JF)?



Ha ha ha, kawavurugia ulaji - EPA, Dowans, richmond, buzwagi, na IPTL kwa hiyo sasa hafai kusikilizwa (objectivity is rather said than formed?] ?
Duh km uwezo wako wa kufikiri ndio huo, then sina sababu ya kuendelea kujadiliana na ww. Lazima ww ni kilaza.
 
Tayari mawaziri wawili, ""Dk Makongoro Mahanga"" na Simba

EMBU TUTAKE RADHI YALIOANDIKWA RED...WAMESHAVULIWA HAWA U DK WAO FWEKI.....NDIO MAANA WANAONGEA PUMBA

Si ndio hapo sasa, Wanaendelea kumuita makongoro kuwa ni Dr wakati ni .... ehnnn .... what was that name? ....... mhhhh
 
Haya bwana, ngoja niende maskani nikasome hayo magazeti nieone kama kweli kuna mtu kathubutu kusema maneno ya

closed door meetings...

CLOSED DOOR MKIWA NDANI NDUGU MKITOKA INAGEUKA ""MIPASHO"" BEST

MMECHOKA MWAKA HUU MMEFULIA NA BADO YANAFUNUKA ZAIDI YA HAYA
 
Sofia anajua anachokifanya, kumbuka sofia kikwete,lowasa na rostam ni kundi moja hilo.
Sofia ni opportunists,njia zake za kusurvive huwa ni kujipendekeza,Sofia kama unasoma huu ujumbe hukumbuki kwamba ni wewe ulikuwa tayari kuhonga ngono kwa mzee Malechela wakati ni waziri mkuu ili upate madaraka,Rafiki yako wa karibu sana akakukemea kwamba huyo ni sawa na baba yako(wengine hili hamwezi kulijua).
Nadhani ni wakati mwafaka wa kuanza kuwaweka wazi hawa wanaotuona watanzania ni mabwege.

- Aliposhindwa hapo kwa mzee akakimbilia kwa mzee Kitwana Kondo, na kuishia kupata ubunge wa viti maalum, sasa Rais ni swahiba wa Kitwana Kondo mama kapata uwaziri tena wa ofisi ya rais na usalama, only in Tanzania!

- Waziri wa usalama wa taifa, anajua tena kwa muda mrefu sana kwamba Jeetu Patel ni fisadi, amenyamaza kimyaa mpaka uje kamati ya Mwinyi isiyo na meno yoyote kisheria ndio anakuja kulia akitetea mafisadi wote nchini, only in Tanzania!

- Ni kweli kabisa kwamba huyu mama anahitaji kupitia Mirembe, kila anapokwenda serikalini ni vurugu tu na kugeuza siasa za taifa midudinko, hivi Rais wa sasa ni mtu wa namna gani? Hamuoni huyu kichaa? I mean tizama alivyomchafua mama Kahama kwenye UWT, tizama alivyomchafua Marehemu Mbatia, tizama alivyomchafua waziri Buriani hivi when enough is enough!

Respect.


FMEs!
 
"Pili, kuhusu uanachama wangu wa CCM, napenda kuwaambia kwamba mimi ni mwanachama wa CCM tangu tarehe 18 Aprili,1977 na kadi yangu ni na. B124595, iliyotolewa na tawi la Kisutu, wilaya ya Ilala, mkoa wa Dar es Salaam."

Hata mini nina kadi yangu ya CCM tangu 18 Aprili, 1977 na kadi yangu ni B124594 lakini sijailipia tangu mwaka 1977 na bado ni mwanachama wa CCM halali. Sina risiti za malipo ya ada kwa muda wa miaka 32 na badi ni mwanachama wa CCM.

Kwa mantiki ya Mengi kuwa na kadi ndiyo maana ya kuwa mwanachama. Ningependa ammalize Sophia Simba kwa kuzitoa risiti zake za malipo ya ada kwa muda hiyo miaka 32 au basi risiti za miaka mitano iliyopita angalau ili Sophia aumbuke zaidi amasivyo ataambiwa kadi yake aipeleke makumbusho ya taifa.
 
Huyu mama kazi imemshinda.......

Kazi inapomshinda mtu, aliyempa ile kazi anapaswa kulijua hilo mapema na kufanya necessary changes.

Mteuzi nae kilaza. Wafu wanazika wafu wenzao.....
 
Duh km uwezo wako wa kufikiri ndio huo, then sina sababu ya kuendelea kujadiliana na ww. Lazima ww ni kilaza.

Mhh shehe yahaya tayari umefanya utabiri na kujua uwezo wangu wa kufikiri na ukilaza wangu. Utabiri huu umepitia wapi - mogadishu au bahrain?
 
Mengi is trying to gain attention!

Serikali kwa makusudi inataka ku-divert attention kwenye cases za msingi ambazo zina ushahidi ulio wazi. Tatizo ni kwamba serikali imeshindwa kutoa majibu ama kuchukua hatua kwa watuhumiwa na sasa wanatufanya tuanze kujadili issue za jikoni ambazo hazina mashiko.

Mfano Mama wa Utawala Bora anasema Mama Kilango ana donge, mara sijui Mzee Malecela alifadhiliwa kwenye harusi yake na mafisadi, mara Mwakyembe ana siasa chafu.

Hivi kuna watu wenye siasa chafu kuwazidi wana mtandao. Si ajabu hata hizi tuhuma alizoleta Mama Simba ni mwendelezo wa siasa chafu za mtandao.

Dhambi ya kula mtu haiishi mpaka uwamalize ndugu zako wote, so CCM watamalizana wao kwa wao. JK aliingia kwa siasa chafu, na same siasa chafu ndiyo inamtesa na ameshindwa kudhibiti makundi ndani ya kundi lake la mtandao. No wonder Sitta yuko kivyake, EL na RA wako kivyao, na wengineo kibao wamekuwa-mute kwa kuwa hawataki kuonyesha wako wapi.
 
Kwani Zitto ni mungu kwa hiyo haandikwi. Wanaotaka Zitto asiandikwe ndio wako inferior kwa Zitto?



Hivi unadhani Zitto akitaka kuoa mwanaume, ataoa wanaompinga au wale wanaomtetea kama wewe?

teh teh teh



JF inaboa, mara ohhoo watu wanaongelea watu, wakati wewe huyoooo mbele mbele kumwongelea masanilo na mwafrika. Je wamekukataa hawa?

Unasikia raha sana sasa, kwa kujibu post! lakini ujumbe umeupata

au sio, kama unaweza kujibu post vizuri namna hii, hakika umepata ujumbe.

m'babe wa Jamii forums!

wenzako hatujali kujibiwa, tunajali wewe kuambiwa ukweli, na kama raha ushakosa, cha kufanya jirekebishe, utakosa pa kupumulia humu, wanaume tukiingia kazini

Huwa hatuandiki post humu, wewe hujagundua tu unaandika pumba kati ya post 32 una thanks 42, nyingi ya hizo za wale wapuuzi wenzako,
wenzako huwa wanavuta na kuconvince wengi, sio!

huyu jamaa, kaparamia gari kwa mbele kama mjomba wake alivyosema

yet unamtetea fisadi Mengi kuwa mwanaCCM damu!

Cretin!!
 
Hata mini nina kadi yangu ya CCM tangu 18 Aprili, 1977 na kadi yangu ni B124594 lakini sijailipia tangu mwaka 1977 na bado ni mwanachama wa CCM halali. Sina risiti za malipo ya ada kwa muda wa miaka 32 na badi ni mwanachama wa CCM.

Kwa mantiki ya Mengi kuwa na kadi ndiyo maana ya kuwa mwanachama. Ningependa ammalize Sophia Simba kwa kuzitoa risiti zake za malipo ya ada kwa muda hiyo miaka 32 au basi risiti za miaka mitano iliyopita angalau ili Sophia aumbuke zaidi amasivyo ataambiwa kadi yake aipeleke makumbusho ya taifa.

Mengi atammaliza mtu ambaye inabidi akapimwe akili? Huyu mama Simba hana chochote kitakachommaliza zaidi ya prescription ya dakitari wake wa akili kule Mirembe.
 
1 Kings 19: 11 ...

Then He said, "Go out, and stand on the mountain before the Lord." And behold, the Lord passed by, and a great and strong wind tore into the mountains and broke the rocks in pieces before the Lord, but the Lord was not in the wind; and after the wind an earthquake, but the Lord was not in the earthquake; and after the earthquake a fire, but the Lord was not in the fire; and after the fire a still small voice.

Okay,

Leta picha ya "mama" yake huyu MUNGU kama unayo. Na ukimaliza ujieleze ni kwa nini ulitumbua pesa za madawati ya wanafunzi wa mtakuja.

Nimesema taja jina la Mungu wako nikuletee picha ya mama yake, hukutimiza sharti la mimi nikuletee picha ya Mungu wako amevaa hijab!!
 
Unasikia raha sana sasa, kwa kujibu post! lakini ujumbe umeupata

au sio, kama unaweza kujibu post vizuri namna hii, hakika umepata ujumbe.

m'babe wa Jamii forums!

wenzako hatujali kujibiwa, tunajali wewe kuambiwa ukweli, na kama raha ushakosa, cha kufanya jirekebishe, utakosa pa kupumulia humu, wanaume tukiingia kazini

Cretin!!

Wanaume hao wanaokupumulia ni pamoja na Masanilo na Mwafrika au unataka wengine zaidi?
 
Back
Top Bottom