Sofia Simba na Sakata la Mafisadi na Wapiganaji!

Mkuu Sikonge mbona hujasema kuna wengine wanasimamia kweli maana wanaamini hiyo kweli itawaweka huru?Bila kusahau wengine wanaosukumwa na nguvu za uzalendo, chachu ya mabadiliko na kutaka kuiona Tanzania njema.

Mkuu AmaniGK,

Umenikumbusha kisa kimoja. Jamaa mmoja alifungwa jela na mkewe akaamua kumsaidia. Akaenda kutembea nje ya ndoa wakati mumewe yuko jela na akaenda kumwambia mumewe "maasi" aliyoyafanya. Mumewe kuja juu, akamwambia kafanya hivyo kwa mapenzi ya juu sana kwa mumewe. Na alipofanya tu kaamua kuja kuwambia kwa sababu "kweli itamuweka huru".

Yes, kuna kweli nyingi. Hata Lowassa ana kweli yake ambayo anaamini itamuweka huru. Rostam, Chenge, Hosea, Mengi, Sophia Simba...... wote wana kweli yao ambayo wanaamini "itatuweka huru".
 
Mzee Nyerere aliwahi kuwaambia kuwa, Chama legelege huzaa serikali legelege. Sasa kama CCM yenyewe hii watu wanaanza kushikiana viuno, kunyoosheana vidole na kusodoana wewe unategemea nini?.
 
JK yupo au chamani sio kinara?watu wanapasuana kwa maneneo then yatafuata matendo
 
....Yaani kuthibitisha yeye ni mwanachama wa CCM kunahitaji kuitisha press conference?

No man, sio suala hilo moja tu!
Lingine ni kuweka rekodi sawa, za mambo anayodai anazushiwa!
BTW, sioni ubaya kuthibitisha uanachama wake, provided katiba ya nchi inamruhusu kufanya hivyo!
 
NDANI YA KIKAO CHA CCM
Habari za uhakika zilizonifikia jana ni kwamba kikao hiki kilikuwa really heated, PM alianza ku-trigger moto pale alipomwambia Rostam kwamba ni liability kwenye CCM, kwamba Kagoda ni ya kwake, kwamba Rostam alichukua 46b/=za EPA, akatoa 4b/= CCM na anatumia balance kuchonganisha na kukigawa Chama.

Akasema CCM haitakufa, wao wataondoka na kuicha CCM; aliendelea kumwambia kuwa kelele zake kwamba Lowassa atakuwa President ni ndoto. He will never be. Baada ya hapo moto ulimgeukia Mtoto wa Kindengereko - Sophia.

Akaambiwa kwamba na yeye pia ni liability katika CCM. Uchaguzi wa umoja wao uligubikwa na vitendo vya rushwa, na aliyekupa hizo pesa ni Rostam, leo hii unakuja kuongea nonsense kwa lengo la kukigawa chama.

Mzee Pinda baada ya kuwasha moto, floor ikarudi kwa wapigana wengine; nikipata muda nitawapa details ya yaliyojili.
 
Nakubaliana na Kimbweka kwa kuiba tu watashinda kwa kishindo. Jamani mwaka huu hata uwenyekiti wa mitaa wameshinda sana, sana, kwa kuiba kura. Wapiga kura wanajiandikisha 400, matokeo yakija CCM wamepata kura 480, 500 uwiiiiii wizi mtupu.

Halafu hawa viongozi wanatuchanganya tuuuuu hawana lolote. Huyu Sophia Simba anasema ingemalizwa kichama, kwani masuala ya mikataba ni ya kichama??!! haya ni mambo ya watanzania woteee, nadhani huyu mama ana matatizo sana. Kama Patel kamchangia mchango wa harusi rafiki yake mahela kibao si alitaka mwenyewe Patel kuchanga. Patel na Malicela ni marafiki wa siku nyingi. Suala la michango ni la mtu binafsi alikopata mahela Malecela angejuaje?? Kila mtu huchangia michango kutokana na uwezo wake, mimi huwa sitoi zaidi ya shilingi 30,000/= ndiyo uwezo wangu. Na nikikupa hiyo 30,000 yangu wewe ni mtu wangu wa karibu sana. Kwa sababu ndiyo uwezo wangu. Lakini kuna watu wanachangia mpaka mamilioni ya mapesa kwenye harusi na komunio.
Sophia Simba mama unaniacha hoi, punguza uswahili, uko mdundiko sana, umekaa kishari shari sanaaaa. Nafasi ya kazi yako pia iko very sensitive so watch out.

Watanzania kazi tunayo.
Hawa viongozi wanakaa wanatumia pesa zetuu kwa mambo ya kijingaaaaa, TUNAHITAJI MAJI SAFI, BARABARA, UMEME, SHULE ZENYE WALIMU ZILIZO BORA, HOSPITAL NZURI, WAZEE WETU WAANGALIWE NA SERIKALI KAMA ZILIVYO NCHI ZILIZOENDELEA.
Kwa mwendo wa kuunda kamati kila siku hatutafika popote. Waliokosa wachukuliwe hatuwa wafungwe, wanyongwe, wafukuzwe kazi. PERIOD no more TUMEZ WIZI MTUPU
 


Mkuu ya kweli haya lakini?Endelea kutujuza mkuu.Nimefurahishwa sana na maelezo ya PM
 
Kuna msemo wa Kiingereza usemao " With leaders Like this (Sophia Simba) who needs enemies!" Na huyu ndiye kiongozi ambaye ana wadhifa wa kupambana na Rushwa, Dhuluma, na ufisadi!! Alafu tunasema serikali iko serious na vita hii?

Sophia Simba ni Simba kweli kweli maana Simba haamininiki wala kuzoeleka! Kwetu sisi ambao tuna undani kidogo sishangai kwa nini jana ameamka na kumtetea Mhe. Chenge maana wakati kashfa ya "vijisenti" ilipoibuka Sophia Simba alikuwa waziri wa kwanza kumkejeli Chenge Bungeni akisema "labda kauza ngombe wake!" Matamshi yale yalimtia matatani na Mhe. Chenge na tangu hapo mahusiano yao hayakuwa mazuri. Juzi ilikuwa nafasi nzuri ya Sophia "kutubu" na kujitakasa. How cheap! Tunategemea nini kutoka kwa wanasiasa kama Sophia Simba? Samahani siwezi kuendela nasikia kichefuchefu!
 

Pinda ni leather weight sana kuweza kushindana na akina RA na Lowassa..to them he is just like a baby,maana yeye mwenyewe Pinda hajui alikuwaje kuwaje PM na hajui kama ataendelea kuwa PM..Kwa maneno rahisi Pinda hana influence ndani ya CCM,so maneno yake siyapi uzito wowote
 
Waziri Sophia Simba ni mfano wa kuigwa...yeye ameshachagua upande wa ku-upigania...wote sasa tunajua yuko upande wa Mafisadi na wala hamungunyi msimamo wake. Kwenye kikao amewataja kwa majina maadui zake...badala ya kuzunguka kwa kiswahili kingi.

Kila Mwanasiasa na wale wana jamii wanatakiwa waige mfano wa huyu Mama waseme wazi...wanasimama upande gani. Wananchi watajua wazi kwa makini kabisa kuwa wana pande mbili za kuchagua Mafisadi au Wapiganaji.

Hilo ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa letu. Watu vuguvugu wanafuata upepo ulipo hawatufai, wanatupotezea muda.

YY
 

Ila Mkuu ukumbuke kabla ya hiyo kweli kukuweka huru ni lazima Uifahamu Kweli.Ninavyotazama haya majibishano na malumbano bila kusahau taarabu na ngonjera zinazoendelea kwenye taifa letu kwa sasa, napata mawazo kuwa aidha hawa watu ni mojawapo ya Janja tu ya kuonekana kuwa wako karibu na watu wenye hali ngumu au watu wa chini ama ni msukumo tu wa kung'ang'ania vile walivyozoea kuwa navyo kwa maana ya uongozi na madaraka na mali. Haya majibishano yanasaidia tu kuhitimisha ule msemo wa zamani kuwa "Ukiona Zinduna basi ujue ambari iko nyuma"
 
Hadithi njoo utamu kolea,lete utamu huo tujionee.
 

Ni wazi unamjua Pinda wa magazetini na katika luninga akionyesha "unyenyekevu wake". Watch this game maana ni wazi sasa kazi imeanza rasmi...

By the way, Pinda was the PM to be hata kabla ya uchaguzi....
 

Zitto, mtanzania mwenzangu!
Haya hayana budi kutokea. Ni lazima yatokee, hizi ndio njia za kutokea laa sivyo umaskini utaongezeka kwa miaka mingine 100. Wote hawa sasa wanafaidi matunda ya ushenzi wao. Haiwezekani tena kufunga midomo wala kuziba masikio hadi pale mambo yatakapobadilika! Chamsingi sana ni kufikiria zaidi kuwa baada ya hapa tunaelekea wapi!

Mie nafurahika sana ninapoona yakiwafika (kuwa gunzo) Malecela, Sitta, Chenge, Lowasa, Kikwete, Mkapa, Mengi, Sofia, Mramba, Yona, Zitto, Mbowe, Maalim, Salim, Warioba, viongozi wa kanisa na misikiti pamoja na wengine wengi. Baada ya hapa, tutaweza kujenga misingi imara ya kitaifa na siyo ya kundi la wateule wachache. Walijua kuwa ukiwa ccm wewe utaendelea kubaki salama daima, badala ya kujua kuwa ukiwa mtanzania safi utabaki salama daima! NGOMA na iendelee kulia zaidi hadi ipasukie mbali, ili Watanzania wapate ahueni!
 

Kazi kwelikweli...

Ama kweli mungu anatupenda sana watanzania...
 
Amefanya kosa kubwa sana kujitetea kwa habari za magazeti wakati yaliyozungumzwa ndani ya kikao cha wabunge ni ya ndani na hata hayo magazeti hayatoi sources na kuandika kwa mujibu 'mtoa habari wetu'. Anawachingea wabunge wake ndani ya bunge.

Hapa look like you are right zito but kumbuka hii si enzi zile za baba wa taifa ambapo siri ni siri kweli..... sasa hivi some body can .......

Mwisho, ana mamlaka gani ya kusema Waziri Simba kabla ya kuongea kwenye vikao vya CCM awasiliane kwanza na Idara ya Usalama?

That is very clear Zitto badala ya kukurupuka anamkumbusha kwamba ange-verify hizo info zake kwa kuwatumia usalama wa taifa kwanza wapo chini yake
 

Mkuu....Maneno haya yalitamkwa na PETER KAYANZA MIZENGO PINDA? Ilikuwa nayeye akaamua kuita kijiko kijiko? Kama ni kweli, I like it!
 
...........Iacheni CCM ivunjike! Why holding it?

Sijui safari hii CCM watafikishana wapi maana sasa kumejitokeza makundi mahasimu matatu ambayo sidhani kama yata-reconcile kabla ya uchaguzi Mkuu.

Kundi la kwanza ni lile linalo jiita wapiganaji ambalo lina nia mbili. Kwanza kufanya juhudi zote kuiumbua serikali ili JK aonekane kuwa hafai kuongoza na pili kuwachafua baadhi ya wanachama wenzao ambao wana uwezo wa kifedha kwa kuibua mambo yao ya ufisadi. Ugomvi wao na JK ni kuwa baadhi yao wakati wa campaign walitegemea kupata vyeo vikubwa katika serikali baada ya uchaguzi, lakini wakaambulia chini ya matarajio yao na wengine waliwaunga mkono wagombea Urais walioshindwa. Wanaumizwa roho sana kuona watu ambao sio smart kama wao ndio wanatanua katika vyeo vya serikali kama uwaziri etc. Wengi wa wana CCM hawa ni wabunge wakiongozwa na Samuel Sitta. Hapa ndio utawakuta akina Mwakyembe, Selelii, Ole Sendeka , Ana Kilango etc. Kundi hili lina nguvu sana Bungeni lakini halina nguvu sana ndani ya CCM na linakumbana na upinzani mkubwa huko. Mfadhili mkubwa wa kundi hili ni mheshimiwa Mengi lakini kwa kuwa yuko peke yake uwezo wa kundi hili kifedha ni limited.

Kundi la pili ni wale wanaoitwa mafisadi ambao wana uwezo mkubwa kifedha na nguvu kubwa ndani ya CCM. Hawa wanawapinga sana kundi la kwanza lakini hawana uaminifu wa kweli kwa JK maana wanaona kuwa amewasaliti kwa kuacha kuwakingia kifua wanapopata matatizo au mashambulizi toka katika serikali yake au wapiganaji katika kundi la kwanza, wakati ni mbinu zao ndio zilimuingiza JK madarakani. Hawa pia wana nguvu Bungeni na uwezo wa kuwadhibiti wana CCM wengi kutokana na fedha zao. Hapa ndio utawakuta akina Lowassa, Rostam Aziz, Chenge etc. Uzito wa kundi hili ni kuwa wana wafadhili wengi kati yao na pia ufadhili wa wafanyabiashara wakubwa ambao nao wanapigwa vita na kundi la kwanza. Kwa hiyo hawa fedha kwao sio tatizo.

Kundi la tatu ni la wanachama waadilifu ambalo wao loyalty yao iko 100% kwa CCM na JK. Hawa hawana uwezo mkubwa wa fedha, lakini ni wengi sana katika grassroot ya CCM na baadhi yao pia wamo Bungeni. Hawa ni kama wazee wa CCM kama Mzee Mwinyi, vijana kama akina Nchimbi, Guninita etc. Kundi hili ndio core ya CCM na haliwaamini sana wanachama walio katika makundi hayo mawili ya awali kwa sababu yote hayana uaminifu wa moja kwa moja kwa CCM na JK. Kutokana na ukubwa wa kundi hili, hata kama moja ya yale makundi mawili ya kwanza yakimeguka hawa watabaki na majority kubwa tu. Kwa kuwa CCM haina fedha kama chama, wao huwategemea wafadhili wa kundi la pili kwa maslahi tu ili mambo yao yaende mbele.

Hali hiyo inajionyesha wazi kuwa hata makundi yote mawili, yaani la kwanza na la pili yakimeguka bado CCM itaendelea kusimama kwa hili kundi la tatu ingawa majority yake itapungua. Kwa vyovyote vile, kama wataojitoa wakiingia upinzani na hivyo kusababisha kupatikana kwa effective opposition, then nchi hii itakuwa imepiga hatua kubwa maana hii absolute majority ya CCM ndiyo inayoleta taabu sana kwa maendeleo ya nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…