Sofia Simba na Sakata la Mafisadi na Wapiganaji!

Sofia Simba na Sakata la Mafisadi na Wapiganaji!

Eidha Mengi smart kama anavyotaka watu wafikirie au washauri wake ni watu wa HOVYO HOVYO

Kwanza hii ni wrong move strategically...for obvious reasons

Pili huwezi kutafuta ligi na Sofia simba...period!!

Tatu anasema Sofia simba akatafute taarifa usalama wa Taifa lakini kasahau kuwa huyo huyo sofia simba ndiye waziri wa Usalama wa Taifa

Nnne: Mengi keshaingia kwenye huo mtego sasa i hope next time hatowaambia mawakili wake wazungumze kwa niaba yake...huyo mama keshaingia ulingoni na by the look of things naamini kuwa keshavaa gloves

Tano: Hiyo ya kubishana na mjinga ingebidi afafanue je mjinga ni nani hapo?


GT

you have nailed it

Kuna kipindi nilishawahi kusema kuna baadhi ya watu wanaweweseka kwa sasa..

So what is this? Yaani unaita wana habari kuelezea utumbo na ugomvi wako na wajinga? Can't believe this.. na kesho wahariri mtakaa na kuandika habari za udaku..

mie simo
 
Huyu Mengi kachanganyikiwa UTUMBO huu hata mtoto wa darasa la pili hawezi kuandika uchafu kama huu.
Hongera mama Simba Mwana Ashanti kumlima huyu Chakubimbi Mengi.
 
..hawawezi huyu mama ni spika ya jk......hamkuona alivyowanyamazisha waliotaka amtose baada ya kuonekana wazi ametumia cheo chake kupaka watu matope na kuwapiga..wakafikiri angeondolewa kugombea uwenyekiti uwt ...jk akajifanya haoni hasikii.....na siku ya uchaguzi akawaambia wabunge wamchague ......waachane na wazeee wasiosoma[janeth kahama]
wewe bwana kwa muda mrefu kila post mbili basi moja ni jk au familia yake kuishambulia.kulikoni?
una maana janet alikuwa na cv kali kuliko simba? Nakuuliza hivi jk alifanya nini?
 
GT

you have nailed it

Kuna kipindi nilishawahi kusema kuna baadho ya watu wanaweweseka kwa sasa..

so what is this?yaani unaita wana habari kuelezea utumbo na ugomvi wako na wajinga ?cant believe this..na kesho wahariri mtakaa na kuandika habari za udaku..

mie simo

labda Mengi anahitaji kununuliwa hiki kitabu:

184-1.jpg



watu wamemwekea ndoano na yeye kaingia

labda angefanya homework yake kujua who EXCTLY is Sofia Simba na how she fights her battles..regardless of her ideology
 
..hawawezi huyu mama ni spika ya JK......hamkuona alivyowanyamazisha waliotaka amtose baada ya kuonekana wazi ametumia cheo chake kupaka watu matope na kuwapiga..wakafikiri angeondolewa kugombea uwenyekiti UWT ...jk akajifanya haoni hasikii.....na siku ya uchaguzi akawaambia wabunge wamchague ......waachane na wazeee wasiosoma[janeth kahama]

ambaye ilibidi auze ile nyumba kwa harara ya dola laki 8!

mpaka leo sista J hajarecover
 
Uliyoyasema kwenye kamati ya mzee Mwinyi ni ya aibu kwa aliyekuteua na wale uliojaribu kuwatetea. Sitaki niyarudie lakini kwa heshima yote uliyobakia nayo your time is up ma'am. Thank you for your unforgetable diservice to our country. Tukiamka tusikie umejiuzulu na kuwa mfano wa utawala bora. Usisubiri uundiwe kamati.
Kwanini aondoke? kumpa ukweli Mengi ambaye ni mfadhili wa Chadema? kama wewe unaona hafai kwa vile kagusa maslahi yako.kwetu sisi anafaa.
Mengi achague moja kula Chadema.hawezi kula huku na huko wameshtuka.
 
Huu mkakati wa kuwafanya watu wote, wanasiasa wote waonekane wezi na mafisadi ni makakati wa wahalifu kuhalalisha UHALIFU ili ionekane kwamba uhalifu ni jambo la kawaida sawa na kula na kulala. Hapa sizungumzii CCM pekee, nazungumzia hata vyama vya upinzani. Haiwezekani kabisa na hatutafika kwa kupotosha mambo. Historia itatuhukumu.

Hebu tuangalieni historia ya vita ya UFISADI Tanzania na neno ufisadi limetokea wapi. Tutakuja kuona aibu kabisa hapo baadaye. Ni aibu tena aibu kubwa. Lazima jamani tutambue juhudi binafsi za watu katika vita ambayo sasa imeingia kuwa kama vita ya Somalia.
 
RMengi ameshakuwa na migongano na mawaziri wa Usalama wa Taifa (Utakumbuka Masilingi alimtishia) sasa SSimba. Kulikoniiiiii....
 
RMengi ameshakuwa na migongano na mawaziri wa Usalama wa Taifa (Utakumbuka Masilingi alimtishia) sasa SSimba. Kulikoniiiiii....

KULIKONI ni gazeti. Lakini jamani tuache kuzungumza kwa kejeli na vijembe kama vya kusutana. Tuzungumze hoja na kuacha kupindisha mambo.
 
labda Mengi anahitaji kununuliwa hiki kitabu:

184-1.jpg



watu wamemwekea ndoano na yeye kaingia

labda angefanya homework yake kujua who EXCTLY is Sofia Simba na how she fights her battles..regardless of her ideology
GT huwa unaniacha mbavu sina! Mengi anasoma kitabu hiki na kile cha how to win friends and influence people anakisoma nani? Au bado yule yule
 
Ama kweli ccm sasa imechoka, Waziri Simba ndiye anaye simamia utawala bora, vyombo muhimu vipo chini yake (Takukuru na Usalama wa Taifa) sasa kama amefika mahali pa kuona kuwa Jeetu Patel ni fisadi kwa kuchangia au 'kufadhili' harusi ya Anne Kilango anachelewa nini kumshughulikia kupitia vyombo hivyo tunavyovitegemea watanzania?

Kama kuchangia kampeni za uraisi ni tatizo wewe kama waziri mwenye dhamana ya kusimamia utawala bora unasubiri nini? Je una orodha ya wale wote waliomweka madarakani Mheshimiwa Rais kwa michango yao? Je wana kashfa yoyote ya ufisadi au la? Ni mpaka kamati ya Mzee Ruksa ikae ndio upate pa kuzungumzia?? kwanini usiwajibike maana huna faida na taifa hili.

Kama kweli kina Sendeka na wenzake wanaganga njaa kwanini
wasishughulikiwe na vyombo husika? Kwani nini cha ajabu kuweza kupata evidence ya kuganga kwao njaa ilhali vyombo vyote vya usalama na rushwa vipo chini yako?

Inavyoonekana sasa CCM imefika pabaya kwani wale wenye dhamana ya kutuongoza badala ya kufanya hivyo wanatafuta pa kuegemea.. sisi waongozwaji tuegemee wapi?? Haijalishi kiongozi anajifanya msafi kiasi gani kama kuna chembe ya ufisadi hatumtetei hata kidogo kwani tumechoshwa, anapaswa kuwajibika kama sio kuwajibishwa.

Ushauri wa bure kwako waziri Sophia Simbani ni huu.. majukumu yako kwa taifa hili ni kusimamia utawala bora, yote unayoyajua yaliyokwenda kinyume na dhana ya utawala bora wapaswa kuyafanyia kazi na kutoa taarifa kwa watawaliwa pia kuhakikisha unatumgoza vema kumalizia awamu hii ya kwanza ya Mheshimiwa Jakaya, vinginevyo kabidhi mikoba kuna wenye uwezo na uchungu na nchi hii.
 
Ghafla watu wameacha Kumnanga Sofia, haooooooo wenyewe wanaanza kumsafisha! ha ha ha! Patamu hapo!

Sifa zetu zileeeee! Jamaaa mshenzi kwelikweli! Wakimaanisha mambo yake Super! This is Tanzania Bwana!
 
Huyu Mengi kachanganyikiwa UTUMBO huu hata mtoto wa darasa la pili hawezi kuandika uchafu kama huu.
Hongera mama Simba Mwana Ashanti kumlima huyu Chakubimbi Mengi.

Ndugu yangu na wewe umezidi ushabiki! ukiambiwa uonyeshe uchafu hapo utaweza..
 
MALUMBANO makali yameendelea kuitikisa Kamati ya rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi baada ya makombora ya juzi kuelekezwa kwa Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango na mumewe, mzee John Malecela.

Kamati hiyo imekuwa ikipokea mashambulizi makali baina ya wabunge ambao wanaonekana kuwa vinara wa vita dhidi ya ufisadi na wale ambao wanaona kuwa vita hiyo inawalenga, kiasi cha kurushiana tuhuma nzito zilizo na mwelekeo wa kuchafuana.

Baada ya kulipuana Jumanne, juzi ilikuwa zamu ya Mama Kilango na mumewe Malecela wakati Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Simba alipotoa tuhuma nzito akidai kuwa wawili hao pia wamekula fedha za ufisadi.

Habari kutoka vyanzo vyetu zilieleza kuwa Simba alidiriki kudai kuwa hata harusi ya makamu huyo wa zamani wa CCM na Kilango ilifadhiliwa na mtuhumiwa wa ufisadi, Jeetu Patel.

Patel kwa sasa ana kesi katika Mahakama ya Kisutu akituhumiwa kuiibia Benki Kuu (BoT) kwa kuchota takribani Sh11 bilioni kutoka katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA).

Akijieleza kwenye kamati hiyo, Simba alimtuhumu Malecela, ambaye aliwahi kuwa waziri mkuu katika serikali ya awamu ya kwanza, kuwa wakati akiwania kuteuliwa kugombea urais kwa tiketi ya CCM mwaka 2005, Jeetu Patel alimpa Sh200 milioni kwa ajili ya kampeni zake.

Malecela, ambaye wakati huo alikuwa makamu mwenyekiti wa CCM, aliondolewa mapema kwenye mbio za urais, ikiwa ni mara ya pili baada ya kuenguliwa tena mapema mwaka 1995.

Waziri huyo mwenye dhamana ya utawala bora akiwa na taasisi nyeti kama Takukuru na Idara ya Usalama wa Taifa, alizidi kurusha makombora kwa wanandoa hao, akisema Mama Kilango ni mnafiki na sio msafi kiasi cha kuwanyooshea wengine vidole wakati harusi na kampeni zake za ubunge zilifadhiliwa na mtuhumiwa huyo wa ufisadi.

Habari zinasema kuwa Mama Simba alikuwa akizungumza kwa kujiamini na kwa ujasiri na kumtuhumu Mama Kilango kuwa kelele zake zote zinatokana na nongwa ya "kuukosa U-first lady (kuwa mke wa rais)."

Alieleza kuwa kelele zote za mbunge huyo wa Same Mashariki zinatokana na chuki na uchu wa madaraka na si kweli kwamba ni mpinga ufisadi, kwa mujibu wa mtoaji habari wetu.

Lakini Patel, alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo za Waziri Simba kwamba alifadhili harusi ya Malecela na kampeni zake za urais, alionekana kustuka na kusema: "Haa...we nani kakwambia... Bwana ehee, mimi sijui lolote kuhusu hayo.

"Kwa sasa mimi najiangalia mwenyewe, nina matatizo yangu mengi nahangaika nayo."

Hata alipofafanuliwa kwamba, maneno hayo yalisemwa na Waziri Simba, alijibu: "Kama wao wamesema wenyewe huko, mimi sijui."

Naye Kilango alisema alishuhudia wakati wakati makombora hayo yakirushwa na kueleza kwamba anajiandaa kujibu mapigo.

Mbunge huyo machachari alisema anajua kwamba mambo yote yaliyosemwa, yanamlenga yeye na si mumewe Malecela.

"Mimi ni mwanasiasa... andikeni yote yaliyozungumzwa bila ya kuacha baadhi na siwezi kuwashtaki," alisema Kilango.

Mzee Malecela hakutaka kuzungumzia lolote kuhusu tuhuma hizo wakati alipoulizwa juu ya uhusiano wake na Patel na kama aliwahi kupokea kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kampeni.

"Ahaa... kijana naomba uniache nipumzike," alisema Malecela.

Mbali na mzee Malecela na mkewe, Waziri Simba pia alimgeukia mwenyekiti mtendaji wa IPP, Reginald Mengi akimtuhumu kuwa anaendesha vyombo vya habari vinavyoichafua CCM na serikali yake kwa maslahi yake binafsi.

Pia alimshambulia mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe na mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka, akiwatuhumu kuwa ni watu wenye njaa na kwamba, wanalipwa fedha kufanya kazi hiyo.

Waziri Simba alisema kuwa hata tuhuma dhidi ya mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge na mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, zimetokana na chuki binafsi.

Simba alisema kuwa uchunguzi wa kashfa ya rada ulishamalizika na Chenge akasafishwa na kuongeza kwamba hata uchunguzi wa Richmond umebaini kulikuwa hakuna rushwa, kwa mujibu wa mtoaji habari wetu.

Suala la Richmond liliibuka tena mbele ya kamati hiyo ya Mwinyi wakati mbunge wa Bukoba Vijijini, Nazir Karamagi alipolalamika kuwa ripoti ya kamati teule ya Bunge iliyoozwa Dk Mwakyembe haikumtendea haki.

habari hizo toka ndani ya kikao hicho zinaeleza kuwa Karamagi alisema ripoti ya Richmond ilionea baadhi ya watu na akapendekeza iundwe tume huru kupitia mchakato huo kuona kama wana makosa ili haki itendeke.

Mbunge huyo ambaye alijiuzulu uwaziri baada ya Lowassa kuachia wadhifa wake wa waziri mkuu kutokana na kashfa hiyo, alisema maamuzi yake kuhusu Richmond yalitokana na mapendekezo ya Bodi ya Tanesco.

Naye Dk Mwakyembe alijibu hoja iliyotolewa Jumanne na mbunge wa Ukonga, Dk Makongoro Mahanga aliyedai kuwa ripoti ya Richmond ni 'feki', akisema tatizo la Dk Mahanga ni uelewa mdogo.

Kuhusu hoja ya Karamagi, Dk Mwakyembe alisema malalamiko yake si sahihi kwa sababu yapo maeneo mengi ambayo Karamagi alishiriki na yako bayana hayahitaji mjadala.

Aliwatahadharisha Wabunge kuacha kudodosa sana ripoti ya Richmond kwani watazidi kumchafua Lowassa na kwamba wanaweza kufungwa kwa sababu upo ushahidi dhahiri.

Dk Mwakyembe aliwataka viongozi wa CCM wenye tuhuma kuiga mfano wa Mzee Mwinyi aliyejiuzulu baada ya mauaji yaliyofanywa na vyombo vya dola mkoani Shinyanga.

Akizungumza mbele ya kamati hiyo, kwa mujibu wa vyanzo vyetu, alimshambulia spika wa Bunge, Samuel Sitta akidai kuwa kama si mizengwe, suala la Richmond lingemalizwa kwa taratibu za kichama.

Habari hizo zinadai kuwa Chenge, aliyewahi kuwa mwanasheria mkuu wa serikali, alisema Lowassa alizungukwa na kwamba kulikuwa na njama za kummaliza ingawa hakusema njama hizo zilifanywa na nani.

Chenge aliitetea serikali ya awamu ya tatu kuhusu kuingia mikataba mibovu na kusisitiza hakukuwa na uzembe kwani mikataba yote ilipitiwa na kukubaliwa na Baraza la Mawaziri.

Hata hivyo, mbunge wa Muleba Kusini, Wilson Masilingi alisimama na kuomba kutoa taarifa na kumwomba Mzee Mwinyi na kamati yake wawabane wabunge wanaodai wanasema ukweli.

Masilingi alipinga maelezo ya Chenge kuhusu mikataba na kusisitiza kuwa maelezo yake yalijaa ushabiki na kusema Baraza la Mawaziri liliridhia mikataba kutokana na ushauri wake (Chenge).

Mbunge wa Kwela, Dk Chrisant Mzindakaya, ambaye aliwahi kupata umaarufu kwa kulipua kashfa, aliwataka wabunge wakubali matokeo kuhusu Ripoti ya Richmond ili taifa lisonge mbele badala ya malumbano yasiyokwisha.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, Mzindakaya aliwataka wabunge wafahamu kuwa ripoti hiyo ilishapitishwa na Bunge na haiwezi kurejeshwa ianze tena upya.

Naye Dk Mlingwa (Shinyanga Mjini), alisema mpasuko unaoinyemelea CCM unatokana na chama hicho kuacha misingi yake ya kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi na badala yake kinawakumbatia wafanyabiashara.

Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Emanuel Nchimbi alitumia nafasi yake kuomba maridhiano ya wabunge wa CCM, kujenga moyo wa kusameheana ili chama kisonge mbele.


Daniel Mjema,Dodoma
 
Hakuna aliye msafi ndani ya CCM.

Mengi ni mwana CCM, sio msafi hata kidogo, hajui kuwa Sophia Simba katumwa na ikulu ambayo yeye Mengi anaiona safi

Mi nadhani Mengi hajui anapigana na nani
 
1968
Operation CHAOS — The CIA has been illegally spying on American citizens since 1959, but with Operation CHAOS, President Johnson dramatically boosts the effort. CIA agents go undercover as student radicals to spy on and disrupt campus organizations protesting the Vietnam War. They are searching for Russian instigators, which they never find. CHAOS will eventually spy on 7,000 individuals and 1,000 organizations.
 
Kiote kwa misingi ipi..kwa kuwa kasema malecela kapokea 200m kwa Jeatu?? Mengi is just another bogus and opportunist..hana la maana analoongea hapa

hata mimi la maana silioni. hawa wafanyabiashara wengi ni waizi hawana ufanyabiashara wowote na ndio maana wanakumbatiana na mafioso wenzao waliopo serikalini.
 
Hakuna aliye msafi ndani ya CCM.

Mengi ni mwana CCM, sio msafi hata kidogo, hajui kuwa Sophia Simba katumwa na ikulu ambayo yeye Mengi anaiona safi

Mi nadhani Mengi hajui anapigana na nani

Mengi sio hajui tuanapigana na nani pia hajui anachoongea .mi naona anaweweseka tu.Aliyemwambia yeye sio mwana CCM nani?
 
Back
Top Bottom