Mkutano wa CCM Dodoma ni Uthibitisho kuwa CCM ni Chama cha Mafisadi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkutano wa CCM Dodoma ni Uthibitisho kuwa CCM ni Chama cha Mafisadi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, Nov 6, 2009.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Nov 6, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,576
  Likes Received: 18,547
  Trophy Points: 280
  Kwanza natanguliza samahani kwa wale wa CCM wote na viongozi wake ambao ni safi hii haiwalengi hao individuals ila kinachoendelea sasa kwenye huu mkutano wa Tume ya Maridhiano ni uthibitisho tosha kuwa Chama chao wanachokiamini, sasa ni chama cha mafisadi!.

  Kimetiwa mfukoni na wenye pesa zao! Licha tuhuma nyingi za kupokea fedha za mafisadi, Mpandazoe nae kashusha nyingine katika kuwatetea wapiganaji na kumtetea Mzee Mengi kuwa alimpa Sofia Simba Milioni 5 alizotumia kuhonga kupata uenyekiti wa UWT.

  Pia nimegundua kumbe muuwaji wa Chadema Busanda ni Mzee Mengi, baada ya taarifa za CCM kugaragazwa vibaya Busanda, ni Mzee Mengi aliyeokoa jahazi kwa kutoa Milioni 1OO, zilizotumika kusambaza kilo mbili mbili za sukari kila kaya on election eve, kesho yake Chadema Chali!

  Tuhuma za fedha za Jeetu Patel kufadhili hili na lile ni nyingi tuu na hazina ubishi.Kuna wabunge walikuwa kimya kwa muda mrefu sana bungeni, mara ghafla wamekuwa outspoken na ziara zao za na Mzee kugawa milioni mia mia majimboni mwao.

  Hivi hamjiulizi hawa wafanya biashara na fedha zao wanazozamisha kwao zina lengo gani? Siku zote nia ya mfanya biashara ni kupata faida, sasa hawa wanainvest kwenye CCM ni faida gani wanaitegemea.

  Afadhali nia ya wenzetu wenye asili ya Asia lengo litakuwa ni kujipendekeza kwa CCM ili kulinda maslahi ya biashara zao, sasa hawa wazawa wanawezaji kweli kugawa milioni mia mia huku watoto wao kila siku wanalia njaa. Hakuna ubishi kuhusu nguvu ya fedha ya RA na influence yake ndani ya Chama.

  Nami nimefikia conclusion hii hii kuwa CCM ni Chama Cha Mafisadi na wasafi wachache!.
   
 2. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #2
  Nov 6, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Scandals zote hizi bado ulikuwa hujui kuwa CCM ni chama cha Mafisadi papa na nyangumi? Chama hiki na wanachama wake hawafai!!
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  Nov 6, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,576
  Likes Received: 18,547
  Trophy Points: 280
  Bulesi, usiwaingize wanachama wa kawaida, hawa hawana kosa lolote yaani ni innocent victims, viongozi ndio wanaowakumbatia mafisadi papa na nyangumi.

  Hata hili la wanachama wa CCM halinitatizi, kumbe wanatumia fedha hizi za ufisadi kufanya wanacho kifanya kwa waTanzania kwenye chaguzi. Mimi sina chama, wala sio mshabiki wa chama chochote, ila nashabikia kushamiri kwa demokrasia ya kweli yenye level playing ground.

  Nimeshuhudia kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la Busanda na Biharamulo, kwa hali ilivyo, thre was no way CCM ingeshinda, lakini matokeo ni CCM! tena sio kwa kuiba kura, bali wananchi wamewachagua. Leo ndio nimejua fedha zinatoka wapi, kumbe kwa interest ya CCM, papa na nyangumi ni kitu kimoja CCM ishinde.

  Tatizo ni kuwa papa na nyangumi, wote ni samaki na wote ni mafisadi, wengine kwa fedha chafu za wizi na magendo, wengine kwa fedha za mikopo na kukataa kulipa ila wote wezi, wote mafisadi na ndio wafadhili wa CCM mmoja akiishika CC na NEC mwingine akiwabeba wanaojiita wapigaji lakini wote lao maja kuhakikisha CCM inatawala milele.
   
 4. Pilato

  Pilato Member

  #4
  Nov 6, 2009
  Joined: May 29, 2008
  Messages: 60
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mmh kazi ipo..!!
   
 5. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #5
  Nov 6, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  samahani mkuu pasco,
  unamzungumzia mengi gani?
  mengi huyu huyu anajinadi anapiga vita ufisadi?
   
 6. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #6
  Nov 6, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  nambari wani...
   
 7. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #7
  Nov 6, 2009
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,668
  Likes Received: 21,901
  Trophy Points: 280
  Nakukubalia kabisa hawa ni nambari wani... Huoni yanayoendelea kule Dodoma? ni nambari wani katika Ufisadi, rushwa, umbea ,uzushi,mipasho na takataka zote. AIBU NAMBARI WANI!
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Nov 6, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,576
  Likes Received: 18,547
  Trophy Points: 280
  Ndiyo ni Mangi huyo huyo unayemfahamu, ila angalizo, yeye katoa fedha hizo milioni 100 kuokoa CCM Busanda at the dying minutes, uamuzi wa kununua kilo mbili za sukari na kuzisambaza ni wa CCM.

  Wazee wa CCM wote tulikaa nao hoteli moja tuu ya maana hapo Geita, wakiongozwa na Mzee wa kusafisha njia na mamaa shujaa, kumbe wote wanafadhiliwa na fedha huku za fisadi papa kule za fisadi nyangumi.

  Sio siri ndiye mfadhili mkuu wa kundi la makamanda wakiambatana nae majimboni mwao huku akimwaga milioni 100 mpaka 500 kwenye majimbo yao. Kuna watu kama Mpendazoe alikuwa mkimya mkimya siku zote, sasa analishwa maneno na yeye eti ni mtapikaji mzuri bungeni na ndiye alitoa data za ufadhili wa mzee kwa Chama.

  Ole Sendeka ni muongeaji mzuri, ndiye aliyempatia kitalu cha Tanzanite Mererani na kumvisha U legunan wa wazee wa Kimasai na kumbadili jina aitwe Ole-Mangi. Kwenye kesi yake na Ole Milya Mzee alikuwa Sambamba nae hadi mahakamani hata mawakili wa Sendeka wametolewa na kulipiwa na Mangi, huku waandishi wa vyombo vyake wakilia njaa. Kisa Ole Milya anafadhiliwa na fisadi papa kumng'oa Ole Sendeka Simanjoro.
   
 9. bullet

  bullet JF-Expert Member

  #9
  Nov 6, 2009
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 959
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Jamani hamjui msemo maarufu wa CCM kuwa Ina wenyewe, na wenyewe ndio sisi! Sasa jiulize wenyewe ndio akina nani? Wanachama wa kawaida wapo? Hapana ni wale wale papa na nyangumi. Tena bahati nzuri walijibatiza wenyewe
   
 10. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #10
  Nov 6, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hao wasafi ni kina nani?
   
 11. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #11
  Nov 6, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  nambari wani pia kwa kuiba kura!!
   
 12. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #12
  Nov 6, 2009
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Mnakumbuka usemi wa Waziri mkuu zero "alisema ukitaka mambo yako yakunyookee kuwa mwanachama wa CCM" usemi huu ni tata sana. Ndo maana hata mafisadi walitaka mambo yao yawanyookee ndo maana wakawa wanchama na wakatengeneza mtandao ambao umekuwa kiza kikubwa ndani na ccm na ndo maana wanahangaika kuuondoa. Kwa maana hiyo basi Mafisadi waishaipora ccm ya wakulima na wafanyakazi na kuwa ccm ya mafisadi. hebu fikiria ufisadi unaanzia kwa balozi wa nyumba kumi na kuendleea hadi juu.
   
 13. M

  Mchili JF-Expert Member

  #13
  Nov 6, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  CCM hakuna msafi, ni degree ya uchafu inatofautiana tu. Ila kwa vile ni wasanii wazuri, wengine unaweza ukajiaminisha kuwa ni wasafi kumbe ukisugua kidogo tu unakuta tope.
   
 14. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #14
  Nov 6, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Nimemuuliza mtoa mada. Na hii ni mara ya pili. Anaropoka ropoka tu! Hao wasafi ni nani? Au ni kuandika ilimradi uonekane umeandika?!
   
 15. m

  monie2009 Member

  #15
  Nov 6, 2009
  Joined: Jun 19, 2009
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani mimi i fail to understand, hivi ebu watanzania wenzangu nielimisheni kwenye hili, hivi ni akina nani hao wanaopigia kura ccm kila chaguzi na kuwaweka juu namna hii wakati kila mmoja wetu hapa naona anaelewa ufisadi wa ccm? Kwa kweli mimi huwa sipigi kura baada ya kupiga kipindi fulani nikitegemea mabadiliko lakini matokeo yake hali ikawa tofauti kabisa na mategemeo ya wengi. Mimi sielewi kabisa huyo mtu tena mlalahoi anayeinua mkono wake tena akiwa na uhuru wake kwenye chumba cha kupigia kura, halafu kwa hiari yake mwenyewe anamchagua mgombea wa ccm, sielewi labda watu tunatofautiana sana kwenye perception.
   
 16. M

  Magezi JF-Expert Member

  #16
  Nov 6, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Generally siasa za Tanzania bado ni changa. Tatizo la tanzania wala siyo siasa bali wizi wa mali ya umma kwa kisingizio cha kusaidia CCM. Na kinacho haribu nchi yetu ni watendaji wa vyombo vya dola kuwa makada wa CCM, ukiangalia walinzi wa ikulu, polisi, JWTZ viongozi wa vyombo hivi waote wana kadi za CCM mfukoni sasa hayo maendeleo tutayapataje??

  Huwezi kumkemea mwizi wa mali ya umma ili hali ni mwenzako na kila anapoiba anakupatia na wewe.
   
 17. M

  Magezi JF-Expert Member

  #17
  Nov 6, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  vijijini ndo hasa CCM wanaiba sana kura.......mijini watu wamekata tamaa ya siasa kwa hiyo wengi hatupigi kura. Kwa siasa za tanzania ukitaka kuingia kweli kwenye siasa na moyo wa dhati labda uwe mmoja wa mafisadi (CCM) kwa sababu zinakera sana.

  Kumbuka uchaguzi wa mwaka 2000 ambapo mzee momosa cheyo ktk kituo alicho pigia kura yeye na mkewe alipata kura sifuri, na CCM ikanyakua kura zote sasa ktk mazingira hayo ukiwa kweli umedhamiria unaweza kuanzisha vita ya msituni na hapo amani hakuna.
   
 18. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #18
  Nov 6, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,576
  Likes Received: 18,547
  Trophy Points: 280
  .
  Lets be realistic, tuwe wakweli jamani, haiwezekani CCM wakawa wachafu wote, hata Sodoma na Gomora alikuwepo Lutu, ndivyo vivye kwenye CCM, pamoja na kutiwa mkononi na mafisadi na kazi yake ni kuwasikiliza hao, miongoni mwao, wapo baadhi ambao ni safi, sio lazima kutaja majina, mmoja wa wasafi hawa ni kijana mdogo Nape na wengine wengi wapo.
   
 19. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #19
  Nov 6, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,576
  Likes Received: 18,547
  Trophy Points: 280
  Monie, Watanzania wa vijijini ndio walio wengi, wao hakuna lolote wajualo zaidi ya chama cha Nyerere, kwao CCM ndio baba, CCM ndio mama. Wapinzani hawajafika huko vijijini ndio maana umeshuhudia CCM ikijizolea viti vya ubwete mitaa kibao. Hivi hujiulizi kwa nini hawakusimamisha wagombea nchi nzima, hawakuambia ukweli, sababu ni kuwa havina ofisi tawi wala shina maeneo husika.

  Nimewahi kusema, na kusema na kusema sana kuwa watu wanaichagua CCM sio kwa sababu wanaipenda sana, bali hawana mbadala wa maana, ndio maana watu wamekuwa na matumainiu makubwa sana na Chadema na CUF pamoja na maroroso yao, lakini ndio the only altenative.
   
 20. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #20
  Nov 6, 2009
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135

  Ah!! Nina Hasira sana na Hiki Chama cha Mafisafi yaani Kodi zetu zote wamegawana Eti 2 kilo za Sugar unampa mtu kura yako then unaishi maisha ya Tabu sana Tunaitaji Mabadiliko na haya mabadiliko ni wewe uwaambuie wenzio. Huyu RA ana nini ndani ya maslam ya Taifa? Yaani najiuliza maswali nakosa jibu Je Huyu Mama anayewapaka wapinga Ufisadi ni kibaraka wa Richmonduli tunajua hilo ili kuwakashifu mwenzie. Na haya majina wanayojipa je tukiwaita watalaumu. ooops nimechoka Sasa tumechoka. Tunasema Ufisadi basi
   
Loading...