So Sad!...@SnowBall nawaageni hapa MMU..

Wanabodi heri ya mwaka mpya kwenu wote

Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuwepo hapa kwa muda mrefu kidogo...Lakini pia niwashukuru nyote kwa kunipokea. Tumeishi vizuri na mmekuwa msaada kwangu kwa kipindi nilichokuwepo hapa. Ila kwa sababu zilizo nje ya uwezo wangu sitakuwa na ninyi kama tulivyozoea. Kwa wale wenye simu yangu nadhani tutawasiliana huko..nitakuwa nje ya social networks kwa muda.
Binafsi ntawamiss sana ila imebidi.
Mwenyezi Mungu awabariki sana
Ndimi wenu mdogo SnowBall

karibu tena na ID yako mpya.
 
Heeee!
Pacha sikusomi mtoto wa mamake mie!
Hebu fanya mcontinuisho wa hii habari kwa haraka kidogo.
 
All the best babangu. Mungu atangulie kila jambo, mfanikiwe shambani na mjini. Mtunze mkeo na umthamini isije ikala kwako, na hivi huko uendako hautakuwa na washauri wa maana kama sie kwi kwi kwi. Mie sikupigii bwana, paw siku hizi ana wivu kama joka la mdimu
 
Mkuu karibu tena kijiweni kwetu...

Btw hata mimi nishaanza kuona dalili za kuiaga JF...
 
Mwenye busara husema kwaheri kwa wale walio wake kwa maana atarejea tena...!siwezi kua mbea ili nijue nn kisa maana bin Adam tuna sehem ya maisha ye2 ni siri NENDA mpwa ukirudi naamini utatukuta.
 
^^
Karibu tena, binafsi ntakukumbuka kwa walau kuchangia thread zetu wanachama wachanga jf tofauti na wengne ambao mpaka watazame join date ya memba ndio wachangie.
Kwa hilo ulitaka kumfikia muungwana watu8 Mr Rocky n.k
Karibu tena Mkuu
^^
 
Last edited by a moderator:
Binafsi huwa namkubali sana huyu mkuu, ni mmoja kati ya wanaMMU waliokuwa wanajua kujenga hoja, kujadili hoja na kujumuisha hoja...

Mtazamo na fikra zake hakika tutazikosa...

^^
Karibu tena, binafsi ntakukumbuka kwa walau kuchangia thread zetu wanachama wachanga jf tofauti na wengne ambao mpaka watazame join date ya memba ndio wachangie.
Kwa hilo ulitaka kumfikia muungwana watu8 Mr Rocky n.k
Karibu tena Mkuu
^^
 
Last edited by a moderator:
mmmh atakuwa kamfata ........... huyu si bure si ndo alikuwa nanii wake humu jamvini? ....maana nae aliaga japo alirudi ila sasa ndo jiii haonekani hata
au kuna jf mpya watu wnaelekea huko baada ya kuona huku kumejaa nn???? mmmhhhhh!!!!
 
Au mkuu shemeji anakubana anaona anaweza kuibiwa huku,teh teh maana jf kuna mambo ya kikubwa mengi.!
 
I hop kuna kheri ....basi Mwenyezi Mungu awe nawe na akufanyie wepesi katika shughuli na majukumu yako yote. U will be missed!
 
Mapi anakutakia safar njema. Uende na ikikupendeza urudi salama
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom