Miss Halima
Senior Member
- Aug 4, 2026
- 170
- 382
Ni muda gani unauchukua kujibu baada ya kuusoma au kusubiri majibu kutoka kwa mtu ambaye umemtumia ujumbe mfupi wa maneno (message)? Kwa upande wa mwigizaji Nia Long wa Marekani yeye aliwahi kusema kuwa akimtumia mtu ujumbe alafu ukachukua siku zima kujibiwa hatazungumza na huyo mtu tena kwa kile alichodai kuwa ni ishara kwamba yeye si kipaumbele.
Kauli hiyo iliibua mjadala mkubwa huku watumiaji wengine wa mitandao ya kijamii wakidai kuwa simu hazipaswi kuamua ustawi wa uhusiano kati ya mtu na mtu. Baadhi yao walisema wanaamini hupaswi kuweka ukomo kwa mtu kujibu sms zako na suala hilo halipaswi kufanywa lionekane kuwa ni tafsiri ya kiwango gani cha heshima kutokana na mambo mengi ambayo yanaweza kupelekea mtu kuchelewa kukujibu.