SIYO Jukumu la CHADEMA kuikosoa CCM ili ijisahihishe na kutawala Vizuri

Mh. Dr Slaa nikupengeze sana kwa kazi nzuri unayofanya. Nakunaliana na MM na kwa kuongezea naomba CDM muengeze efforts kwenye kuweka CCM UNDER THE SPOT-LIGHT kwa ahadi zake. Nimeomba hili kwenye post yangu nyingine naomba nirudie tena hapa kwamba CDM iweke BANGO kwenye office makao makuu -DSM na huko mikoani ya count down to 90 days tangu kujivua gamba. Hii itahamasisha wananchi wengi zaidi kufuatilia kwa karibu ahadi au propaganda za CCM.

mimi naamini kuwa CHADEMA sasa yahitaji michango ya wananchi ya hali na mali kwa kuwa sasa imedhihirika wazi kwamba CDM ina matakwa na nia kamili ya kuleta mabadilioko na maendeleo kwa watanznia walio kalia uchumi mkubwa katika nchi yao kwa miaka mingi bila kupata mafaniko

kutoa ni moyo usambe ni utajiri.... !
 
Kwa hiyo mwanakijiji unaadvocate political manipulation kwa wananchi.
Yaani serikali ikifanya jambo zuri, unataka chadema iseme au itende kinamna fulani hilo jambo lionekane ni baya au "halitoshi?".
Je itakuwaje pale chama tawala kitatenda kwa ufasaha mkubwa baadhi ya mambo yanayosimamiwa na kuaminiwa na chama pinzani ambayo ni ya maslahi kwa taifa?.

Hii hoja ya mwanakijiji inaniconvince tuamini kwamba siasa ni game fulani ya kumanipulate mass.
Kama chama tawala kinafanya kazi vizuri sana, halafu chama pinzani kikaja na hoja ambazo si bora kuliko za chama tawala, halafu kikaconvince mass kwamba hizo ni sera bora zaidi, hii ni suicidal kwa mass yenyewe na chama pinzani chenyewe.
Mimi ninadhani siasa hasa ile inayohusu misingi ya uchumi wa nchi haina budi kujengwa katika misingi ya kisayansi, kwa maana ya kweli za uchumi tunazozijua, na si katika propaganda za kilayman ili mradi tu ueneze fitna mass ikichukie chama tawala na kukiweka madarakani chama pinzani.

Hoja hii ya Mwanakijiji ina pungufu moja kubwa.
pungufu lenyewe ni kujaribu kuonyesha kwamba CHAMA CHA UPINZANI KINA JUKUMU LA KUJIANDAA KUSHIKA DOLA TU, WAKATI HUOHUO INAACHA JUKUMU LA CHAMA CHA UPINZANI KUCHANGIA KATIKA KUTOA MAWAZO MBADALA YA KUSAIDIA NCHI IEEDELEE.

Tatizo la hoja hii ya Mwanakijiji ni kwamba Inajaribu kukita misingi ya "Uchama kwanza", Taifa next. nitaeleza hii pointi.
(1)Chadema au chama fulani kushika dola ni Ishara ya kufaulu kwa Chama Hicho, kufaulu kwa wananchi kutakuja pale ambapo chama fulani kitaunda serikali itakayo deliver. haitamsaidia mwananchi yeyote iwapo CHADEMA Itatimiza lengo lake la kushika dola halafu ikafanya yaleyale kama ya CCM au ikafanya chini ya hapo. sasa je wanasiasa makini wanataka washike dola tu ndo wajione wana nafasi ya kutoa mchango wa Kusaidia Nchi?.

(2) Je ni vipi kama Kusaidia nchi kutajumuisha kutoa mawazo mazuri ambayo yakifanyiwa kazi kutasaidia Kuimprove maisha ya wananchi na hivyo wananchi kuona kwamba kumbe hata Wapinzani wana mawazo mazuri na hivyo wanafaa kupewa dola?.

kiufupi hoja ya mwanakijiji imejaribu kulificha jukumu moja la chama cha upinzani at the expense ya jukumu lingine. KIUFUPI CHAMA CHA UPINZANI KINA JUKUMU KUBWA MUHIMU SANA NALO NI NCHI NA WANANCHI KWANZA, NA KUTIMIZA JUKUMU HILI SI KUSHIKA DOLA PEKE YAKE, BALI INAWEZA KULITIMIZA KWA KUKOSOA NA KUPENDEKEZA NJIA MBADALA, LAKINI WAKATI HUO HUO KIKIJINADI NA KUJIPAMBANUA MBELE YA UMMA KWAMBA KINAWEZA KUSHIKA DOLA.
Kutokikosoa Chama Tawala ni Ubinafsi na Kutokukipa mawazo mbadala kwa ajili ya maslahi ya Umma ni uchoyo usiomithilika kwa wananchi, ni sawa na kuwaadhibu wananchi kwamba Madhali mmeninyima kura, basi na mimi siwaonesheni njia bora za kutatua tatizo kadha wa kadha

vyovyote itakavyokuwa mwana kijiji yuko sahihi. itakuwaje wapinzani wakitoa mawazo mbadala then chama tawala kikayafanyia kazi isivyo sahihi na hivyo kutozaa matunda tarajiwa? pia tumeona bunge hili kwamba cdm wanajitahidi kupresent vitu vya maana na matokeo yake au wanaznmewa na chama tawala au chama tawala wanapiia kura hoja zao na wanashinda kwa wingi wao. so, mwana kijiji yuko sahihi tu.
 
Fikiria kwa mfano, sualal la Mswada wa mapitio ya sheria ya Katiba Mpya umepingwa na CCM wameenda kuupitia tena. Guess watakuja na kupata credit nani? Siyo Chadema bali CCM! Ungeniuliza mimi ningesema wauache uende Bungeni upitishwe na wabunge wa CCM na Chadema waanze kampeni ya kuupinga na kupinga mchakato na kukataa kushiriki kwa sababu x,y. Ingekuwa ni showdown nzuri ya kisiasa.

Well jibu ambalo nitalipata ni kuwa "Katiba mpya ni suala la taifa zima na siyo suala la Chadema". na kwamba "ni suala la maslahi ya taifa". Well.. Katiba Mpya haikuwa ajenda ya CCM anyway! Ni bora watu wangesubiri hadi 2015 waiingize Chadema kusimamia mchakato wa Katiba Mpya kuliko kuitegemea CCM kuandaa mchakato mzuri wa kuelekea Katiba Mpya!

Think about it: HIvi kweli kuna mtu anategemea CCM itatengeneza mchakato ambao utasababisha uwepo wa Katiba ambayo inaweza kutumika kuiondolea nguvu yake au hata kuitoa CCM madarakani? Really?
 
Think about it: HIvi kweli kuna mtu anategemea CCM itatengeneza mchakato ambao utasababisha uwepo wa Katiba ambayo inaweza kutumika kuiondolea nguvu yake au hata kuitoa CCM madarakani? Really?

Si mimi! Haya majamaa ya CCM yana super majority bungeni. Nitashangaa sana endapo mwishowe yatapitisha katiba "mpya" ambayo inaweza baadaye kuja kutumika kuyaondoa hayo majamaa madarakani.
 
Mwanakijiji,

Bila katiba mpya ambayo ita trip off power of the president, wakuu wa mikoa/wilaya , kubadili mfumo mzima wa utawala na uundwaji wa tume huru ya uchaguzi bado itakuwa ni ndoto kuindoa ccm madarakani, hivyo hapa chadema must put all card on the table kuhakikisha ccm hawana pa kupumulia! nadhani katiba mpya na tume huru ya uchaguzi ndo road map ya kuiweka ccm bench hivyo hapa chadema wasilaze damu, hata maandamano ya juzi ilibidi yafanyike tu kama showdown ya nguvu ya umma! kuwachachafya watawala!

Mwanakijiji usiwape ccm credit wasizostahili kabisa, chadema imekwisha itetemesha ccm na uthibitisho wa hilo ni pale raisi wa nchi anapoanza kulalama kwenye vyombo vya habari, raisi anapofikia hatua ya kulalamikia chama cha upinzani maana yake amepigwa electric shock au amepigwa ganzi hawezi kufanya chochote, hana good options za kukabiriana na kishindo cha chadema.

Hivyo basi kwenye suala la katiba chadema need to put all card on table tena kwa kuwa karibu sana na wanaharakati, This is it, bila katiba mpya na tume huru ya uchaguzi basi hata ccm idhoofishwe vipi bado watajishindisha tu, tumeona yaliyotokea zanzibar kwenye uchaguzi wa Oct 2010. Hivyo tutapata katiba tunayoitaka sio kwa utashi wa ccm bali kwa utashi wa umma wa watanzani, na agenda hii ya katiba ni must win hata kwa mtutu wa bunduki.
 
Si mimi! Haya majamaa ya CCM yana super majority bungeni. Nitashangaa sana endapo mwishowe yatapitisha katiba "mpya" ambayo inaweza baadaye kuja kutumika kuyaondoa hayo majamaa madarakani.

NN.. mwanzoni na kwa muda mrefu nilikuwa naamini kuwa CCM inataka mabadiliko ya kweli. Uchaguzi wa mwaka jana ulinifundisha jambo moja wazi - hawana mpango wa kuleta mabadiliko yatakayosababisha kwa wao kuondolewa madarakani. Yaani, watengeneze sheria mbazo refa siyo wao, mpira siyo wao na uwanja na washiligaji wasiwe wao. Hiyo ni njozi. I got it. Mabadiliko ya kweli Tanzania yataletwa na chama kingine. CCM italeta mabadiliko yale tu ambayo yatasaidia kukiimarisha madarakani kwa miongo mingi ijayo.
 
CCM wanajua fika kwamba kinachowabakisha madarakani ni mfumo wa ovyo wa kisiasa na sio utashi wa wananchi. Katika hali ya kawaida, na kwa kuzingatia kwamba wana namba bungeni, watahakikisha katiba yeyote ijayo haiharibu mazingira yao kisiasa. Mimi binafsi nipo cynical and skeptical na zoezi zima la katiba mpya kusimamiwa na CCM. Mswada huu uliopo ni ushahidi mdogo tu kwamba inawezekana tutakapata katiba mpya lakini itakuwa ni mbovu kuliko hii iliyopo.

Mimi ninaamini kabisa kuwa pakiwepo juhudi zaidi, mshikamano zaidi na akili zaidi, CCM inashindika hata kwa mazingira haya tuliyo nayo. Mazingira ya kuishinda CCM ni mazuri kuliko yaliyokuwepo Kenya kuiondoa KANU. Lakini bado kuna kitu kinakosekana. Vyama vyetu vya upinzani bado vinategemea makosa ya CCM ili viweze kufanya siasa na kupata umaarufu. Ndio kusema CCM wangekuwa smart wakafanikiwa kuweka mambo yao sawa na kupata watu smart katika safu yao ya uongozi, upinzani ungeweza kupwaya ghafla.

Tunahitaji twende mbele zaidi. Ifike mahala watu waone kwamba CDM, kwa mfano, ni zaidi ya chama cha upinzani. Waone kwamba ni chama kinachosubiri kuunda serikali. Inabidi tuwafikishe wananchi mahala ambapo watakosa imani na CCM in totatilty kiasi kwamba hata wamuweke nani na hata waje na sera gani, bado wananchi washindwe kurudisha imani nao. Hatujawafikisha hapo bado. Ukiona watu wanaongelea kwa kusifia kwamba upinzani mzuri unaona wanavyochachafya CCM ujue bado. Lengo la upinzani sio kuichachafya CCM; ni kuiondoa madarakani ili upinzani wapate fursa ya kutekeleza dira, falsafa na sera zao. We are on the right track, but we need to work a bit harder especially in shaping and redirecting our people's attitudes!
 
Laiti Watanzania wengi zaidi wangekuwa na fikra kama zangu haya majamaa ya CCM yangekuwa yashawekwa benchi zamani sana. Manake bila hata katiba mpya bado nina imani tunaweza kuyashinda, tena kuyashinda vibaya sana.

Hii inawezekana tu pale ambapo watu wengi zaidi watayanyima kura zao na kupigia chama kikuu cha upinzani. Angalau kwa kufanya hivyo tutayaweka haya mamtu katika mazingira magumu sana ya kuchakachua kura. Hivi hebu fikiria, tukiyakataa katakata yatafanya nini?

Manake hata kama hayana chembe ya soni yakichakachua itakuwa dhahiri mno kiasi kwamba hata kipofu ataweza kuona. Na kwa kufanya hivyo ndo yatazidi kujichimbia kaburi na kupoteza kabisa uhalali wa kutawala na kuongeza kasi ya mabadiliko. Kila yatakapokuwa yanaenda watu wanayazomea na kuyaita majizi. Unafikiri yatakuwa na ujanja haya mamtu?

Usicheze na nguvu ya umma bana. Nchi ni yetu sisi wananchi na tukiyakataa haya mamtu hayatakuwa na ujanja wowote. Hayawezi kujilazimisha kututawala kama kweli hatutataka yatutawale!!

We just need to break that fear factor and once we do that these thugs will be history.
 
..Ifike mahala watu waone kwamba CDM, kwa mfano, ni zaidi ya chama cha upinzani. Waone kwamba ni chama kinachosubiri kuunda serikali. Inabidi tuwafikishe wananchi mahala ambapo watakosa imani na CCM in totatilty kiasi kwamba hata wamuweke nani na hata waje na sera gani, bado wananchi washindwe kurudisha imani nao. Hatujawafikisha hapo bado. Ukiona watu wanaongelea kwa kusifia kwamba upinzani mzuri unaona wanavyochachafya CCM ujue bado. Lengo la upinzani sio kuichachafya CCM; ni kuiondoa madarakani ili upinzani wapate fursa ya kutekeleza dira, falsafa na sera zao. We are on the right track, but we need to work a bit harder especially in shaping and redirecting our people's attitudes!

Imebidi nisimame kukupa standing ovation.. tatizo watu wengine ambao ni wapinzani na hata wapenzi wa upinzani wanajisikia vibaya kuona watu wanakosa imani na serikali ya CCM. Wanajisikia hatia. Na CCM inajua huu mchezo haichelewi kulia "wanapandikiza chuki dhidi ya serikali na dhidi ya chama". Na watu wanaanza kutoa maoni "hapana hatupandikizi chuki!"!!
 
Manake hata kama hayana chembe ya soni yakichakachua itakuwa dhahiri mno kiasi kwamba hata kipofu ataweza kuona. Na kwa kufanya hivyo ndo yatazidi kujichimbia kaburi na kupoteza kabisa uhalali wa kutawala na kuongeza kasi ya mabadiliko. Kila yatakapokuwa yanaenda watu wanayazomea na kuyaita majizi. Unafikiri yatakuwa na ujanja haya mamtu?

NN, tatizo ni kuwa ukianza kuwaamsha watu kuona ukweli wa ubovu wa CCM na wakaanza kuichukia CCM watu wanaokuona unapandikiza chuki. Si unaona maandamano kidogo tu yale watu wakaanza kuitwa "wahaini". Ndio maana kwenye hili nimeweka wazi kwanza wapinzani watambue kuwa hawatakiwi kuwa "wapinzani wa kudumu". Wapinzani wenyewe wakijua kuwa lengo lao ni kuidhoofisha seriklai na chama tawala - kwani ni lengo la chama tawala kudhoofisha upinzani - basi hakutakuwa na kuoneakana aibu.

NN ukisema "ikataeni CCM" watakuita "mchochezi"!
 
Mzee MM,
Kwa mara nyingine tena natoa shukran zangu za dhati kwa kipande ulichotoa kwani haswa ndio maana halisi ya Ushindani ndani ya siasa za vyama.

Labda nimkumbushe ndugu yetu alopingana nawe kwamba Upinzani au Opposition ndio neno na maana halisi ya ushindani huu ambao mwanzo wake ni tofauti za Itikadi baina ya vyama, na hizi itikadi tofauti huzaa tofauti za vipaumbele (sera) ktk ujenzi wa taifa ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Sasa ni maajabu ya Mungu kweli tukisema chama kimoja kinaweza kubariki chama kingine kifanikiwe kwa kufuata itikadi ambayo hawaiaminii au kupendekeza sera ambazo ndizo chanzo cha tofauti baina ya vyama viwili, laa sivyo sioni sababu ya kuwa na vyama vya Upinzani ikiwa wote wanakubaliana kimsingi.

Nimewahi kusema vyama vya siasa ni sawa na tofauti za kiimani ktk dini zetu, siku zote kila dini inaamini ukifuata ibada zake bila shaka utaiona pepo na hakika yote haya utayapata ktk mwongozo yaani misahafu yao inayokuelekeza ibada kamili zinazotakiwa kufuatwa ili kuipata hiyo pepo. Na katika siasa ni vile vile, kwanza inatanguliwa na imani (itikadi) kisha kuna ibada zake ambazo naweza kusema ni sera na hizi sera haziwezi kuwa sawa baina ya chama na chama kwa sababu ndio tofauti zenyewe.

Watu wengi wanachanganya sana tunapozungumzia sera, labda niwafahamishe kitu kimoja kwamba hata ktk dini tunaposema SALA ni lazima utakuta kila dini inaamini sala ni moja ya ibada kubwa ya kila muumini wa dini hiyo, lakini ni jinsi gani ibada hiyo ya sala inatakiwa kufanyika ndipo tofauti zinapokuja baina ya dini na dini na hivyo hivyo ktk vyama, sasa kinachoshangaza ni pale chama kimoja kinapojaribu kukishawishi chama kingine kifunge sala kama wao hali kutokubaliana kiimani ndiko kumezua tofauti ya sala (sera) baina yao.

Mimi nadhani watu wengi wanashindwa kuelewa siasa za vyama vingi zina malengo gani haswa badala yake wanafikria ni mkusanyiko wa viongozi wazuri ambao wana elimu ya juu na utashi sawa isipokuwa mmoja anakuwa mzembe kuliko mwingine. Laa.. Vyama vinashindana kiitikadi, vinafundisha mtazamo tofauti wa kiitikadi kufikia maendeleo.

Kwa mfano, hakuna dini yeyote duniani inapingana na Amri kumi za Mungu - hakuna, hata hao Baniani watakwambia kuua ni dhambi,kuiba ni dhambi, Unafiki na kadhalika. Na sisi wote tunaamini kwa uwezo wa akili zetu kutambua mabaya hata kabla ya dini hizi kuwepo ama kuja kwetu. Binafsi naamini dini zimekuja baada ya sisi wenyewe kupoteza mwelekeo hivyo kutukumbusha tuzo kubwa tulopewa na Mwenyezi Mungu yaani Akili, akili ya kutambua na kupembua mabaya yasiyostahiki kwetu binadamu kuyafanya.

Kwa hiyo CCM au Chadema wote hawa pamoja na Upinzani wao wanafahamu mabaya yasiyotakiwa, kukemea mabaya na kuongozana mwenzako ktk kutenda mema haina siasa za chama isipokuwa kumwelekeza mwenzio jinsi ya kuongoza hapo ndio sawa na kutaka kumtia maji muumini wa chama kingine hali hakubaliani na ibada (sera) zako.

Hivyo, ushindani upo ktk kudhoofishana kupinga mwelekeo na ibada za CCM ndilo jukumu kubwa la Chadema na vyama vya Upinzani kwani ndio kiini cha tofauti zao laa sivyo tungekuwa na chama kimoja tukatofautisha vichwa vya viongozi wetu. kama ilivyokuwa wakati wa Kambarage.

Lakini sivyo, tumeunda vyama vya kisiasa ili kuonyesha tofauti ya mwelekeo kufikia maendeleo, na kila chama kuwaonyesha wananchi ubora wa fikra zao ktk kukamilisha hata jambo moja tu, wakati huo huo kupinga njia nyinginezo kuwa haziwezi kutupeleka peponi bali zinatupeleka motoni, na hakika sasa hivi joto la jahanam tunalipata, hivyo Chadema wanayo kila sababu ya kuwadhoofisha CCM ambao bado wanakazania safari ya kutufikisha Jahanam..na huwezi kuirekebisha safari inayo kwenda Jahanam kwa kuomba dereva afungulie kiyoyozi ati kwa sababu joto limezidi. Au Wabunge wengine kulisukuma gari lilipokwama wakati wakijua fika dereva anakotupeleka siko..jamani hii sio kazi ya Upinzani hata kidogo..

Na sidhani kama ni Kazi ya Chadema kuwakosoa CCM kwa udereva wao hali wao ndio wameshika Usukani na sijui kama kuna dereva yeyote anayependa kukosolewa wakati akiendesha gari maana kila dereva hujiona anajua kuliko mwingine ingawa hajui mwisho au matokeo ya vitendo vyake..Mara zote hukubali makosa baada ya ajali kutokea..

Na hata kama CCM watagundua kwamba wanavyoendesha sivyo nakujaribu kufuata maelekezo ya Chadema, haiwezekani kuwa sawa kwani dereva wa gari ni mmoja akiamua kulipitisha ktk korongo atalipitisha hata kama utamkemea vipi na kibaya zaidi ni pale vyama vya Upinzani wanapojaribu kumshauri na kumwekeza CCM njia hali hiyo njia hawaifahamu isipokuwa CCM mwenyewe ambaye ndiye kawabeba abiria.

Kazi kubwa ya vyama vya Upinzani ni kuwadhoofisha Utawala.. Vipi?.. kuwambia wananchi - Jamani eeeh huyu jamaa anakotupeleka siko hata kidogo angalieni pori najangwa ndio linazidi kweli kuna mji huko mbele?. Pili yaonyesha kalewa (na madaraka), na hajui hata kuendesha na upo uwezekano kubwa tusifike huko anakotaka kutupeleka..jamani eeeh tusimamishe bus na tushuke mimi najua njia sio hii tumeiacha nyuma..kwa ridhaa yenu nipeni mimi usukani nitawafikisha ktk mji wa mkuu wa maisha bora kwa kila mwananchi.. Sasa dereva CCM atachukia na kutukana apendavyo lakini yote haya akijua abiria wakishuka hana safari tena.

Mimi naamini demokrasia sii utamaduni wa mtu mweusi hata kidogo, ila tutajifunza na itachukua karne nyingi kwa vizazi vyetu kuweza kujua nini hasa mbegu hii ya demokrasia ilipandwa ili tuvune kitu gani.. Leo hii tunafikiria demokrasia ni mfumo utakao tupa viongozi bora badala ya demokrasia kutupa itikadi tofauti zenye sera bora kulingana na Watu na Mazingira yetu wakati huo.
 
Mkandara, shukrani mkuu wangu. Umenikumbusha yaliyotokea Canada hivi karibuni sijui itakuwaje wakati wa uchaguzi lakini chama cha upinzani hakikuchelewa kurukia hoja ya kutumia madaraka vibaya kwa serikali iliyoko madarakani na hawakufanya hivyo ili serikali ya Harper. Na utaona hata kwenye matangazo yao ya kampeni wanashambulia sera za chama tawala ili kukifanya kionekane duni. Fikiria Chadema ikitoa tangazo linasema "CCM imeshindwa" na kutaja mambo kadha wa kadha.. mbona patachimbika Tanzania!
 
CCM wanajua fika kwamba kinachowabakisha madarakani ni mfumo wa ovyo wa kisiasa na sio utashi wa wananchi. Katika hali ya kawaida, na kwa kuzingatia kwamba wana namba bungeni, watahakikisha katiba yeyote ijayo haiharibu mazingira yao kisiasa. Mimi binafsi nipo cynical and skeptical na zoezi zima la katiba mpya kusimamiwa na CCM. Mswada huu uliopo ni ushahidi mdogo tu kwamba inawezekana tutakapata katiba mpya lakini itakuwa ni mbovu kuliko hii iliyopo.

Mimi ninaamini kabisa kuwa pakiwepo juhudi zaidi, mshikamano zaidi na akili zaidi, CCM inashindika hata kwa mazingira haya tuliyo nayo. Mazingira ya kuishinda CCM ni mazuri kuliko yaliyokuwepo Kenya kuiondoa KANU. Lakini bado kuna kitu kinakosekana. Vyama vyetu vya upinzani bado vinategemea makosa ya CCM ili viweze kufanya siasa na kupata umaarufu. Ndio kusema CCM wangekuwa smart wakafanikiwa kuweka mambo yao sawa na kupata watu smart katika safu yao ya uongozi, upinzani ungeweza kupwaya ghafla. Tunahitaji twende mbele zaidi. Ifike mahala watu waone kwamba CDM, kwa mfano, ni zaidi ya chama cha upinzani. Waone kwamba ni chama kinachosubiri kuunda serikali. Inabidi tuwafikishe wananchi mahala ambapo watakosa imani na CCM in totatilty kiasi kwamba hata wamuweke nani na hata waje na sera gani, bado wananchi washindwe kurudisha imani nao. Hatujawafikisha hapo bado. Ukiona watu wanaongelea kwa kusifia kwamba upinzani mzuri unaona wanavyochachafya CCM ujue bado. Lengo la upinzani sio kuichachafya CCM; ni kuiondoa madarakani ili upinzani wapate fursa ya kutekeleza dira, falsafa na sera zao. We are on the right track, but we need to work a bit harder especially in shaping and redirecting our people's attitudes!

Kongamano lile la UDASA ambalo wewe ulikuwa mratibu wake lilikuwa na malengo haya kwa mbali. Bahati mbaya kabisa ni kuwa wanaoipigia CCM kura hawahudhurii wala kushiriki kwa namna yoyote makongamano kama haya. Wakibahatika kushiriki mnawazomea. Mwisho wa siku mnaonekana wahuni!
 
Haya ndio mawazo ambayo nataka tuachane nayo; upinzani unapokosoa serikali au viongozi wake una lengo la kudhoofisha serikali hiyo ili ianguke kwenye uchaguzi ili wao wapinzani waje kusimamia sera zao za maendeleo na kuwaongoza wananchi kuelekea mafanikio. Lengo la upinzani siyo kuwa upinzani wa kudumu bali kuja kushika dola na kutekeleza sera zake. JIulize kama wapinzani watatoa sera mbadala na sera hizo nzuri za upinzani zikichukuliwa na chama tawala na kufanyiwa kazi upinzani utahitaji kushika dola kwa ajili gani? Wananchi watataka kuwapa dola wapinzani kwa sababu gani wakati sera zao zinatekelezwa na serikali iliyoko madarakani.?

Napendekeza wananchi wetu waanze kujua kuwa CHADEMA ni chama kinachotaka kutawala. CUF kilijua hili na kikahakikisha kinaidhohofisha serikali ya Zanzibar kiasi kwamba CCM walikuwa hawana jinsi isipokuwa kukubali kuwamegea kidogo keki ya kutawala kule Zanzibar.

Kwenye kauli yako ya mwisho ni kuwa ni jukumu la chama tawala kujikosoa na wanachama wake kuikosoa ijisahihishe isije ikakosolewa na chama cha upinzani na kuondolewa madarakani. Mpinzani wa kweli anataka kuona serikali inaboronga inafanya vibaya ili kumulilka udhaifu wa serikali hiyo na kuwafanya wananchi waangalie nje ya chama tawala na kutafuta chama kingine ambacho kitakidhi mahitaji yao.

Ahsantum kwa majibu yako murua na nimeshukuru sana japo kwa uchache umenielewa.Nilipo RED ndio kusudio langu kukufahamisha hilo. Lakini unapaswa kujua kuwa ku borrow sera za mwenzako au mpinzani wako sio kosa kisharia kwani kila chama kina nia ya kuchukua dola. Na ili uchukue Dola lazima ufanye mazuri kwa wananchi husika ndio maana huko Tanzania CCM imeamua kujivua Gamba ili irudishe imani kwa wananchi ili waweze kuiridhia tena kuendelea kutawala. usishangae sana kuona baadhi ya Sera za Chadema wakazitumia katika kurejesha imani hiyo.

Lakini awali ya yote naomba sana upunguze USHABIKI hususan unapojadili hoja nzito kama hii. Hakika fahamu kuwa ethics za uandishi zinakataa zaidi mwandishi kuwa shabiki wa kushabikia upande mmoja na kuuacha mwingine. Sasa kama nia na dhumuni la hii mada yako ni kutaka kuijuza jamii basi acha ushabiki na kama kuwajaza jazba na hamasa Chadema basi go on. Kwani jukumu la waandishi ni kuelimisha na kuhabarisha jamii yale yanayojili.

Sasa mimi kama mwandishi ambaye sikusudii kwa aina yoyote kupendelea upande wowote wa shilingi nazidi kukupinga. Kama nilivyobainisha hapo awali kuwa upinzani sio uadui na vile vile kila Chama kinaweka wazi Sera zake kwa jamii na kuzinadi kwa jamii husika bila kificho. Na ufahamu kuwa kazi za upinzani ni kuikosoa na kuleta mawazo mbadala kwa Serikali kwa nia na madhumuni ya kuchochea maendeleo ya jamii lakini wakati huo huo kikijinadi na kujinasibu kwa sera zake nzuri.

Siku zote upinzani utajinadi na kujinasibu kwa Sera zake kwa nia ya kudhoofisha Chama tawala na sera zake. lakini ikumbukwe sio dhambi kwa chama chochote kilicho makini ku borrow sera mbadala kwa upinzani kwa nia ile ile ya kuleta maendeleo ya jamii na kutaka kuendelea kubaki madarakani kama wanavyofanya vyama pinzani kutaka kuongoza dola.

Siku zote katika uongozi wapinzani wanakuwa na wazo mbadala tofauti na wazo la chama tawala ndio maana hata bungeni kunakuwa na bajeti mbili za Serikali yaani ile ya Serikali ya chama tawala na ile ya chama cha upinzani lakini zote zinakuwa na madhumuni ya kuchochea maendeleo kwa jamii.

Sasa nikirejea kwenye mada utaona kazi kuu ya upinzani ikiwa pamoja na kutaka kuongoza dola lakini pia kuikosoa Serikali iliyomadarakani kwa kuleta wazo mbadala na hata kuonyesha njia ya kutatua tatizo husika kwa urahisi zaidi ya vile chama na serikali tawala itavyofanya.Kwani upinzani sio uadui.
 
from kitila Mkumbo
CCM wanajua fika kwamba kinachowabakisha madarakani ni mfumo wa ovyo wa kisiasa na sio utashi wa wananchi. Katika hali ya kawaida, na kwa kuzingatia kwamba wana namba bungeni, watahakikisha katiba yeyote ijayo haiharibu mazingira yao kisiasa. Mimi binafsi nipo cynical and skeptical na zoezi zima la katiba mpya kusimamiwa na CCM. Mswada huu uliopo ni ushahidi mdogo tu kwamba inawezekana tutakapata katiba mpya lakini itakuwa ni mbovu kuliko hii iliyopo.

Mimi ninaamini kabisa kuwa pakiwepo juhudi zaidi, mshikamano zaidi na akili zaidi, CCM inashindika hata kwa mazingira haya tuliyo nayo. Mazingira ya kuishinda CCM ni mazuri kuliko yaliyokuwepo Kenya kuiondoa KANU. Lakini bado kuna kitu kinakosekana. Vyama vyetu vya upinzani bado vinategemea makosa ya CCM ili viweze kufanya siasa na kupata umaarufu. Ndio kusema CCM wangekuwa smart wakafanikiwa kuweka mambo yao sawa na kupata watu smart katika safu yao ya uongozi, upinzani ungeweza kupwaya ghafla. Tunahitaji twende mbele zaidi. Ifike mahala watu waone kwamba CDM, kwa mfano, ni zaidi ya chama cha upinzani. Waone kwamba ni chama kinachosubiri kuunda serikali. Inabidi tuwafikishe wananchi mahala ambapo watakosa imani na CCM in totatilty kiasi kwamba hata wamuweke nani na hata waje na sera gani, bado wananchi washindwe kurudisha imani nao. Hatujawafikisha hapo bado. Ukiona watu wanaongelea kwa kusifia kwamba upinzani mzuri unaona wanavyochachafya CCM ujue bado. Lengo la upinzani sio kuichachafya CCM; ni kuiondoa madarakani ili upinzani wapate fursa ya kutekeleza dira, falsafa na sera zao. We are on the right track, but we need to work a bit harder especially in shaping and redirecting our people's attitudes!

Nimevutiwa sana na maoni yako kwani yanayoa changamoto kubwa kwa jamii kufanya mabadiliko makubwa.

Kwa kuongezea ni lazima tufahamu kuwa kuna mbinu nyingi sana ambazo vyama au wanasiasa wanatumia katika kupata wanachama na wapiga kura hususan kipindi hiki ambapo elimu ya Uraia kwa jamii imeenea na kutambuliwa.

Zama zile au CCM na vyama karibu vyote walielekeza nguvu zao kwa wazee kwani hao ndio walikuwa wapiga kura wakuu na vijana walikuwa washabiki tu lakini sio wapiga kura. Chadema amegundua njia mbadala kwa kuwahamasisha Vijana kupenda uongozi na kupenda jamii na uzalendo wa nchi yao dhidi ya wabadhilifu na mafisadi kwa kuelewa kuwa hali ya maisha inazidi kuwa ngumu ni kwa sababu ya ufisadi. Sasa imewawekea bayana kazi ya kuleta maisha bora kwao ni kwa njia yya kisanduku cha kura.

Hii imeamsha moyo kwa vijana kuwa wapiga kura wazuri. mfano kwa mara ya Kwanza katika chaguzi za Tanzania tunaona vijana wengi walijitokeza kupiga kura kuliko wazee. Sasa hii ni ngao kubwa sana kwa Chadema kwani generation hii haijui enzi za ujamaa na kujitegemea au wakati wa chama kimoja na elimu ilikuwa bure n.k

Lazima tukubali mabadiliko yote ya utawala yapo mikononi mwa vijana kwani wao wana nguvu, moyo na hata hari ya kuhakikisha wanapata maisha bora na mustakabali mzuri kwa ustawi wao.

Nimependa sana maoni yako
 
CCM wanajua fika kwamba kinachowabakisha madarakani ni mfumo wa ovyo wa kisiasa na sio utashi wa wananchi. Katika hali ya kawaida, na kwa kuzingatia kwamba wana namba bungeni, watahakikisha katiba yeyote ijayo haiharibu mazingira yao kisiasa. Mimi binafsi nipo cynical and skeptical na zoezi zima la katiba mpya kusimamiwa na CCM. Mswada huu uliopo ni ushahidi mdogo tu kwamba inawezekana tutakapata katiba mpya lakini itakuwa ni mbovu kuliko hii iliyopo.

Mimi ninaamini kabisa kuwa pakiwepo juhudi zaidi, mshikamano zaidi na akili zaidi, CCM inashindika hata kwa mazingira haya tuliyo nayo. Mazingira ya kuishinda CCM ni mazuri kuliko yaliyokuwepo Kenya kuiondoa KANU. Lakini bado kuna kitu kinakosekana. Vyama vyetu vya upinzani bado vinategemea makosa ya CCM ili viweze kufanya siasa na kupata umaarufu. Ndio kusema CCM wangekuwa smart wakafanikiwa kuweka mambo yao sawa na kupata watu smart katika safu yao ya uongozi, upinzani ungeweza kupwaya ghafla.

Tunahitaji twende mbele zaidi. Ifike mahala watu waone kwamba CDM, kwa mfano, ni zaidi ya chama cha upinzani. Waone kwamba ni chama kinachosubiri kuunda serikali. Inabidi tuwafikishe wananchi mahala ambapo watakosa imani na CCM in totatilty kiasi kwamba hata wamuweke nani na hata waje na sera gani, bado wananchi washindwe kurudisha imani nao. Hatujawafikisha hapo bado. Ukiona watu wanaongelea kwa kusifia kwamba upinzani mzuri unaona wanavyochachafya CCM ujue bado. Lengo la upinzani sio kuichachafya CCM; ni kuiondoa madarakani ili upinzani wapate fursa ya kutekeleza dira, falsafa na sera zao. We are on the right track, but we need to work a bit harder especially in shaping and redirecting our people's attitudes!

Hivi Dr. Kitila kwenye siasa hakuna copy right? Kama official document ya kutawala ambazo zimepigiwa kura ni Ilani za uchaguzi then inakuaje CCM wana copy ilani ya uchaguzi ya chama kingine bila makubaliano? Hapo nani anahusika na kuwezesha kulinda rights za vyama kati ya msajili wa vyama na tume ya uchaguzi? Hata kama hakuna copy right lipelekeni hilo jambo kisiasa kwamba CCM ni wezi wa idea zenu na kwakua wao siyo original hawawezi kufanya vile inavyotakiwa. Find a way ya kuwafanya wananchi waamini kuwa CCM are incapable and can never come up with realistic development concepts ndiyo maana hata mswada wameuleta ukiwa completely flout kama alivyo sema prof Shivji si tu technical wise hata error za kawaida tu indicating these people are never serious in National development issues. Lazima mfanye siasa ki science muweze kuwaondolea CCM credibility mbele ya wapiga kura.
 
Nimesoma Mada hii, nimefarijika sana na mawazo amabayo yametolewa na pia nimefarijika jinsi amabvyo Dr Slaa amekuwa akichangia mada hii. mimi pia nimeelimishwa sana na mada hii na ninamuunga mkono ndugu MM kuwa chama cha upinzani sio kuwamulikia tochi chama tawala bali ni kuwawekea giza wasione mbele, halafu wakitumbukia kwenye shimo kirudi na kuwaeleza wananchi jinsi jamaa walivyoshindwa kuona njia na matokeo ya hilo ni wanachi kukipa dola na kuongoza nchi.

Kwa sasa CCM wamepoteza Dira ya kuongoza nafikiri hakuna asiyejua hilo hata wale wenye mioyo migumu ya kutokubali ukweli huwa wakikaa peke yao nafikiri huwa wanaumia moyoni ila ni mapenzi tu juu ya hicho chama ndio yanawafanya wasikubali ukweli au ni kwa maslahi binafsi ndio maana wamechagua kuwa vipofu na viziwi.

Dr Slaa tupo pamoja nanyi katika hii vita ngumu ya kumkomboa mwanchi anyekandamizwa wengine bila ya kujua kwa kua CCM iliwanyima elimu ya kuweza kuona kwamba nchi hii si lazima itawaliwe na CCM pekee au hakuna mtu aliyezaliwa kuja kuongoza nchi hii, na kwamba wao wanchi ndio wanaoweza kuamua nani atawale na nani asitawale, na wanachi wanayohaki ya kumuweka pembeni anayetawala kwa faida ya kundi la watu wachache na kuwaacha wananchi kwenye lindi la matatizo na jambo la kusikitisha na ambalo ni baya zaidi ni CCM kutawala kwa mabavu hata pale wananchi wanapoikataa. Kukataa kwa makusudi kuweka tume huru ya uchaguzi itakayo simamia maslahi ya wananchi.

CCM wamekuja na usemi wa kujivua gamba ili kurudisha imani ya wananchi lakini ndio wameharibu kabisa, sisi tunauliza mbona Magamba yanalenga katika uchaguzi wa 2015 badala ya kutekeleza ahadi zao!? na kama wamekubali kwamba kunamafisadi ndani ya CCM na hapo mwanzo walikataa hii inazihirisha kwamba wao ni chama cha Mafisadi na hawastahili kuongoza nchi hii kwa vyovyote vile.

CHAMA MAKINI NI CHENYE NDOTO YA KUTAWALA, CHADEMA NI CHAMA MAKINI.
 
Vyama ni kama organism haviwezi kubakia vimefungwa na fikra za zamani. Kutokana na mahitaji ya nyakati na watu katika zama zao vyama vinaweza kubadilisha. Vinginevyo, wakati wa kuanzishwa CCM ilikuwa ni chama c ha Kijamaa. Leo hii kimekuwa chama kikuu cha kibepari nchini japo mfumo na muundo wake ni wa kijamaa. Think about it. CCM inafuata itikadi gani?
Kwani hujasoma katiba ya CCM?
 
Mwanakijiji

Kudos comrade! Article nzuri sana hii.Ni kweli tuna tatizo kama Taifa.Upinzani katika harakati za kuiondoa CCM madarakani na katika kuhakikisha kuwa malengo yake baada ya kushika dola yanatimia kulingana na sera,ni lazima tujikite kwenye misingi na tu-focus on a national agenda for the next 50 years to come.
Tanzania as a country is less than the sum of its parts. The motivational ideas that we are stronger together, and that we must by all means retain the current constitutional/political arrangement is, I am afraid, extremely naive.

If Tanzania was a Multinational company (MNC), and there was very little prospect (as is currently the case with Tanzania) that its perilous situation could be turned around, many Shareholders or investors would clamor for a Core reassessment of direction. Of course, we are not a 'Corporate entity' and I recognize that we cannot reasonably take a Profit/Loss account perspective to a Nation’s affairs.

Nonetheless, I believe that to safeguard the country from being in this mess for another 50 years, we need to stop chesting-thumping about Tanzania being this, and that (It’s hilarious at some point), and instead start asking ourselves some critical, albeit difficult, questions about who we are, where we are going, how we have got it so wrong to date, and how best to arrive at our destiny so that we can preserve and handover a decent country to future Generations.

This process will, in my view, at least require a constitutional conference where we will put all the big questions on the table, and hopefully arrive at a new political/constitutional settlement. Although I doubt that a New Constitutional settlement will give us all that we need (given the various competing interests), it’s outcome should be a significant improvement on what we currently have.
Also and the most Important aspect, we need to embark on a massive project of reorientation of our people to be anchored around the values of honesty, respect, selflessness, belief in the greater good etc We probably all agree that the political class has ruined/is ruining our country, but we also know that our greatest problems transcend society. We need a hand-over-matter sort of blueprint to serve as a catalyst for relocating our lost moral compass, and not the current comical TV/Radio-based 'rebranding' project. Achieving the objectives of this monumental proposition which must start from our homes and pre-tertiary education system will not be easy, but I refuse to believe that it is too late to start.

Of course, a reorientation and a new political/constitutional settlement alone will not solve all of our problems, but will serve as a platform for changing a lot that is wrong with our country and for the realisation of our dream of a progressive democratic nation.
 
Back
Top Bottom