Uchaguzi wa Senegal na funzo kwa Demokrasia ya Tanzania

Mr RoundAbout

Member
Oct 6, 2023
70
85
Ni siku mbili sasa Senegal wamepata Rais wao mpya Tena wanauempenda kijana mbichi kama gimbi kutoka morogoro Mhe Faye.

Alikuwa katika selo za gereza kuu mjini Dacar kama mfungwa wa kisiasa chini ya uongozi uliopita ikiwa ni mpango wa Rais aliyetaka kujiongezea muda kuzima nguvu ya upinzani Ili kufanikisha nia yake OVU.

Nguvu ya UMMA na kelele za wenye Senegal zilisababisha mpango haramu wa Rais aliyekuwepo madarakani wa kujiongezea muda wa kutawala kushindwa na hatimaye uchaguzi ulitangazwa.

Faye aliachiwa siku 14 kabla ya uchaguzi ikiwa ni mwendelezo wa Serikali kuwanyima wapinzani mazingira ya kushinda kiti cha Urais, alifanya kampeni Kwa siku 10 tu na hatimaye ndiye Rais wa Senegal, amemwangusha waziri Mkuu wa serikali iyokuwepo ambae kimsingi alikuwa anapigiwa upatu na Rais alikuwa madarakani.

NINI TUNAJIFUNZA HAPA TANZANIA?

Chama Cha mipinduzi hapa Nchini kijitathmini katika mazingira yafuatayo;
1. Kukubalika kwake kunatokana na nguvu ya dola au mapenzi ya watanzania?

2. Ikitokea siku Tanzania imepata katiba mpya yenye kuheshimu misingi ya kidemokrasia, CCM itaendelea kutawala?

3. Mfumo wa uchaguzi wa Tanzania ni HURU?

Kama mazingira hayo matatu yanamchango katika kusaidia CCM iendelee kutawala basi ni wazi Viongozi wahakikishe kuwa hakuna mabadiliko yatakayotokea katika mambo hayo matatu Ili wao waendelee KUTAWALA.
 
Back
Top Bottom