Historia imejirudia, CCM imekuwa Mkoloni na CHADEMA Mdai Uhuru!

Desprospero

JF-Expert Member
Feb 1, 2023
887
2,201
Niliwahi kusikia kwa Mwalimu wangu kuwa historia ina tabia ya kujirudia na kwamba hakuna jipya chini ya jua.

Kwamba hata haya mavazi na fasheni zake si jambo jipya. Yaliwahi kuwepo kwa nyakati tofauti.

Kabla ya Uhuru wetu 1961 nchi ya Tanganyika (sasa Tanzania) ilitawaliwa na Serikali ya Mkoloni aliyetumia nguvu ya dola kutawala. Huo utawala wa wazungu ili uweze kusavaivu ulilindwa kwa nguvu za dola na mifumo yake. Hii ndio maana wenyeji waliunda chama TANU kupigania uhuru na haki ya watu wake.

Kama tunakumbuka Julius Nyerere alitajwa kama gaidi kwa kuwa alihamasisha vita dhidi ya wakoloni kupitia TANU. Watu ni wengi tu wanaume kwa wanawake waliuawa ama hadharani au kwa siri kwa kupotezwa. Watu weusi walijitoa kwa hali na mali kuunga mkono harakati za ukombozi.

Pamoja na madhila yote hawakukata tamaa japo Kuna baadhi hawakuamini kuwa iko siku moja nchi itakuwa huru na kujitawala kwa mujibu wa matakwa ya wananchi. Hatimaye siku Ikifika na Uhuru ukapatikana.

Moja ya sifa Kuu ya Serikali ya kikoloni ni kulindwa na dola-mfumo. Bila dola utawala wa Mzungu usingefika mbali maana upinzani (TANU) ulikuwa mkubwa sana.

Historia hii inajirudia mapema mno hata miaka 100 hatujafika. Safari hii yule aliyekuwa mpinzani (TANU/CCM) ndiye Mkoloni akiwa na sifa ile ile ya kulindwa na dola huku Chadema ikichukua nafasi ya TANU ya enzi hizo. Si tumeshuhudia Freeman Mbowe akiitwa gaidi? Si tumeshuhudia kina Dk. Slaa na Mwabukusi wakitaka kuuliwa kuwa ni magaidi. Ni wangapi wamepotezwa kwa kuunga mkono harakati za upinzani?

Tatizo au sheria ya historia ni kwamba upinzani haujawahi kushindwa miaka yote. Kwa karibu sana naona CCM ikianza kulegea miguu na shingo kama dalili za kusalimu amri. Haya mambo yanayopiganiwa na Chadema ni dalili za anguko.

USHAURI wangu kwa upinzani. Jiandaeni kisaikolojia kutangaza Uhuru. Jiandaeni kuongoza siyo kutawala. Kaeni kwa kujiamini kuunda Serikali msijefika Ikulu msijue cha kufanya. Andaeni wananchi kisaikolojia. Kinachofanywa na CCM kwa sasa ni kusomba rasilimali zao Ulaya. Nao wanajua fika muda wa kuwaachia upinzani nchi umewadia ndio maana unaona baadhi ya vigogo wao wakichangia kwa Siri mikutano ya Chadema.

Kama TANU iliungana na ASP na kuzaq CCM sioni ubaya wala haya Chadema nayo iliungana na ACT-Wazalendo kuunda Chama Cha Ukombozi (CCU). Ondoeni hofu na woga Kanani iko hatua chache sana kwa Sasa. Nawasilisha!
 
Umeandika uchafu ..... nahisi kinyaaa mwandishi ni tabulasa fulan la hovyo ....uhuru gani chadema inadai
 
Picha huwa hazidanganyi
fb_img_1680258242993-jpg.2572153
 
Back
Top Bottom