Nimeweka hoja ya ulinzi wa Rais kukuonyesha mantiki ya tofauti kati ya Rais wa nchi na wananchi mwingine.
Wewe unazungumzia istihaki. Unajua hata maana ya istihaki?
Kwangu kamwe istihaki haziwezi kumfanya binadamu mwingine awe na thamani kuliko binadamu wengine.
Yaani hapo unachosema ni sawa na kusema kuwa Diamond Platnumz ni tofauti na raia wengine kwa sababu kila hushangiliwa na mashabiki wake kila wamwonapo.
Unachekesha wewe.
Kusema wewe hauna tofauti na Rais wa nchi ni kuongea kwa kinadharia lakini kiuhalisia Rais wa nchi na wananchi wa kawaida wako tofauti.
Mimi ndo naongea kiuhalisia zaidi maana mahitaji yote yaliyo ya msingi kwa uhai wa binadamu hayatofautiani kisa tu huyu anafanya kazi hii na yule anafanya kazi ile.
Huyo Magu wako anaweza kuishi bila kula?
Hapana. Wewe unaongelea dhana ya kinadharia inayosema binadamu wote ni sawa lakini kiuhalisia binadamu wote siyo sawa.
Hapana. Wewe ndo nadhani hata hujaielewa vizuri hiyo dhana. Binadamu wote ni sawa haina maana ya kwamba kweli wote tuko sawa, la sivyo kusingekuwa na watu wafupi, warefu, wanene, weusi, wa kiume, wa kike, ma huntha, na kadhalika.
Hiyo dhana inahusiana na mambo ya kuheshimiana na kutendeana vyema pasipo kubagua wala kubaguana kwa kutumia vigezo bandia.
Rais kutokea miongoni mwa wananchi hakumfanyi awe ni sawa na wananchi wengine katika matendo na majukumu yake kama Rais.
Rais ni cheo tu. Cheo pamoja na istihaki zinazokuja na hicho cheo hakimfanyi awe tofauti na wananchi wengine. Naye ni mwananchi tu.
Matendo na majumu ya Rais ndiyo yanamfanya awe ni tofauti na wananchi wengine ndiyo maana hata Katiba ya Tanzania 1977 katika Sura ya Pili, Ibara ya 33(1-2) imebainisha ukweli kuhusu umuhimu wa Rais wa nchi.
Umuhimu wa cheo chake ama nafasi yake hakumfanyi awe tofauti. Naye ni mtu tu kama mimi na wewe.
Lazima uelewe kuwa kujiheshimu ni kuheshimiwa.
Huu ushauri nakushauri ungewapa huyo Magu wako na Mkapa.
Ninapoongelea Rais nina maana taasisi kwa ujumla wake.
Taasisi ni lidude au taasisi ni watu?
Rais Magufuli amevaa taasisi ya Urais na kutokana na taasisi hiyo, anatakiwa kisheria ajiheshimu.
Teh teh teh...sasa mbona hata hajiheshimu? Mtu anaropoka ropoka tu utadhani mlevi bana....
Hebu mtumie huo ushauri ajirudi bana.
Wewe mwananchi unaweza kuchagua kutojiheshimu na hakuna mtu au sheria inayokutaka kujiheshimu.
Kuna sheria inayotaka rais ajiheshimu?
Rais hawezi kuchagua kutojiheshimu na kama atataka kufanya hivyo basi inabidi aachie madaraka.
Kuna sheria inayomtaka hivyo?
Hii ndiyo tofauti ya msingi kati ya Rais wa nchi na mwananchi wingine.
Jaribu tena maana bado hujanionyesha tofauti aliyonayo Magufuli na wananchi wengine.