Siungi mkono Rais kutukanwa!

Siungi mkono Rais kutukanwa!

Lini wapinzani wa Bongo wamewahi kulipwa kwa siasa za kistaarabu?Huyu Lema kesho na keshokutwa atapigwa virungu kama sio mabomu ya machozi na nyie wafuasi wa CCM mnaomsifia leo hii ndio mtakuwa wa kwanza kumkejeli na kumdhihaki na hata huyo anaemtetea leo hii nae hatamsaidia kwa lolote.
Kwa hiyo unajaribu kusema aache ustaarabu na amewasaliti?
 
Sawa, lakini hata mimi sidhani kabisa kama hilo kosa linaendana na adhabu aliyopewa huyo kijana.

Angeniita mimi 'bwege' unadhani hata angekamatwa?

Au hata ningeenda kumfungulia mashitaka unadhani angepewa hiyo adhabu aliyopewa?
Very true .
 
Naunga mkono hoja ya Lema. Ni vyema tukashindana kwa hoja.
 
KIJANA ALIKOSEA KWELI AJIFUNZE KUJENGA HOJA ZA KISIASA

KWA UPANDE WA PILI ANGESAMEHEWA INGELETA PICHA YENYE KUVUTIA ZAIDI KULIKO IYO ADHABU YA KUWAFANYA WAOGOPE KUMZUNGUMZIA RAISI KWA MAMBO AMBAYO ANAKOSEA

.....
Kwani kijana amehukumiwa na sheria au Rais?Sheria ya mtando iko wazi ndio uliyo nshikisha adabu!
 
Je, ni haki pia Rais mstaafu kuwatukana Watanzania kwamba ni Wapumbavu na Malofa kisa tu hawaungi mkono chama chake na mgombea wake wa nafasi ya Urais? Mbona hakuchukuliwa hatua zozote hata kupewa onyo tu kwa kuwatukana Watanzania!?

Rais yeye ana haki ya kuwaita watoto wa wenzie '******' eh?
 
Kemea kwanza tendo linalofanywa na vijana na madiwani wenu. Kitendo cha kumchangia fedha mtuhumiwa kinatoa taswira mbaya kwa chama chenu japo wengine wanaona ni kitendo cha kishujaa lakini huwezi kuenzi ushujaa katika mambo ya kijinga.
Kijana hakuchangiwa pesa eti sababu kafanya vema kumtukana mkuu (japo yeye aliwahi kuitwa mpumbavu na lofa). Alichangiwa pesa ili asiende jela kwa miaka mi3 na aendelee kushiriki vema shughuli za maendeleo katika jamii.

Hata hivyo itoshe tu kusema si sawa kwa mtu yeyote kumtukana au kuwatukana watu wengine. Katika hili hakuna aliye juu ya sheria hata awe raisi au raisi msfaafu.

Niwashauri viongozi wetu wawe na subira na kutunza maneno ili wasiseme au kufanya yale yatakayowafanya watukanwe. Kwa nyongeza tu, kiongozi makini katika mfumo mzuri wa kidemokrasia ni yule anayeweza kupuuza mambo madogo madogo. Raisi mstaafu Jakaya M Kikwete ni mfano mzuri kwa sababu simfahamu mwingine aliyetukanwa kama yeye katika nchi hii.
 
Rais wa Marekani anaitwa majina mengi mabaya kuliko hilo la bwege...
Sheria hizi lengo ni kuleta hofu kwa ujumla kwa watu
wasiwe free kumkosoa....
Unajua tofauti kati ya kutukana na kukosoa?
 
Hii ni taswira ya kushuka kwa maadili ya vijana wetu...wakichekewa wataota mapembe...wapelekwe mahakamani tu...
Watumie mitandao responsibly...
Si utamaduni wetu kutukana wakubwa...awe rais au jirani...washikishwe adabu...hakuna namna...
 
" Ninafikiri ni vyema na muhimu tukaendelea kukosoana kwa njia mbali mbali, lakini kwa hakika kabisa siungi mkono rais kutukanwa kwa kejeli ambazo zina sura ya mizaha na sio mabadiliko , Rais kuitwa BWEGE ni kosa na utovu wa nidhamu .

Kosa hili halipaswi kutiwa moyo wala kuungwa mkono , lakini kumwambia Kijana huyu kuwa alikosea ni jambo muhimu zaidi na la busara "

Godbless Lema (Mp)
Mmh! Huyu ni wewe Mh Lemma? There some thing wrong here.Lakini kamanda pia ulipaswa kusema ni vipi huyu kijana alitakiwa kukanywa.Nahisi kina tatizo kati kati yako na diwani Nanyoro na Malissa si bure.
 
Hii ni taswira ya kushuka kwa maadili ya vijana wetu...wakichekewa wataota mapembe...wapelekwe mahakamani tu...
Watumie mitandao responsibly...
Si utamaduni wetu kutukana wakubwa...awe rais au jirani...washikishwe adabu...hakuna namna...
Halafu wengi wanafikiri wanafikiri huyo kijana fine aliyo pewa ilitoka mdomoni tuu kumbe hipo kwenye sheria ya mitandao!

Najua Lema ataonekana mbaya lakini leo kafanya wengi waliogopalo!
 
Kwani ni rahisi tu anayetukanwa nchi hii?? Kumwambia mtu amejinyea jukwaani sio tusi?? Wapinzani wanatukanwa mara ngapi nchi hii tena na wanasiasa wakubwa wa ccm,wananchi wanatukanwa mara ngapi nchi hii?? Hivi kilaza na bwege utofauti wake ni nini?? Kumtukana rais wala mtu yoyote yule siyo vyema,ila tuache unafki SIO KWA RAIS LIWE TUSI ILA KWA MWANANCHI,NA VIONGOZI WENGINE SIO TUSI.......
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ukiniita bwege nikakuita kilaza lipi neno la kuudhi na lipi la kufurahisha??
 
Hivi nikimuita huyo ndugu "mtakatifu" au "mfalme" au "dikteta" ni kosa pia!? Naomba kufahamishwa!?
 
Kwani ni rahisi tu anayetukanwa nchi hii?? Kumwambia mtu amejinyea jukwaani sio tusi?? Wapinzani wanatukanwa mara ngapi nchi hii tena na wanasiasa wakubwa wa ccm,wananchi wanatukanwa mara ngapi nchi hii?? Hivi ****** na bwege utofauti wake ni nini?? Kumtukana rais wala mtu yoyote yule siyo vyema,ila tuache unafki SIO KWA RAIS LIWE TUSI ILA KWA MWANANCHI,NA VIONGOZI WENGINE SIO TUSI.......
Ukitukanwa mahakama ipo...
Ni jukumu lako kwenda mahakamani...
Akitukanwa Rais wapo wa kumwendea mahakamani sababu ni Rais...
Vyeo vinaenda na privileges ...huwezi kujilinganisha na mwenye cheo...ni kutafuta BP tu...
 
Kwakweli Lema wewe pekee na Zitto ndio mna faa kuitwa makamanda maana mnafanya wengine wasio yaweza!

Kumekuwa na tabia ndani ya Chadema ya kuogopa kukosoana kwa kuhofia kufukuzwa lakini wewe umevunja ukimya!

Najua huko aliko Ephata na God listen wamechanganyikiwa maana wamefanya kitendo cha aibu na wewe hujawakwepesha umewambia na wamekuelewa!
 
Back
Top Bottom