Siungi mkono Rais kutukanwa!

Siungi mkono Rais kutukanwa!

"Ninafikiri ni vyema na muhimu tukaendelea kukosoana kwa njia mbali mbali, lakini kwa hakika kabisa siungi mkono rais kutukanwa kwa kejeli ambazo zina sura ya mizaha na sio mabadiliko, Rais kuitwa BWEGE ni kosa na utovu wa nidhamu.

Kosa hili halipaswi kutiwa moyo wala kuungwa mkono, lakini kumwambia Kijana huyu kuwa alikosea ni jambo muhimu zaidi na la busara"

Godbless Lema (Mp)

Bora umemtambua
 
Kemea kwanza tendo linalofanywa na vijana na madiwani wenu. Kitendo cha kumchangia fedha mtuhumiwa kinatoa taswira mbaya kwa chama chenu japo wengine wanaona ni kitendo cha kishujaa lakini huwezi kuenzi ushujaa katika mambo ya kijinga.

..kijana anapaswa kuchangiwa.

..kwasababu adhabu aliyopewa ni kubwa mno kulinganisha na kosa alililofanya.

..bora wangempa adhabu ya kupiga deki na kufyagia hospitali.
 
"Ninafikiri ni vyema na muhimu tukaendelea kukosoana kwa njia mbali mbali, lakini kwa hakika kabisa siungi mkono rais kutukanwa kwa kejeli ambazo zina sura ya mizaha na sio mabadiliko, Rais kuitwa BWEGE ni kosa na utovu wa nidhamu.

Kosa hili halipaswi kutiwa moyo wala kuungwa mkono, lakini kumwambia Kijana huyu kuwa alikosea ni jambo muhimu zaidi na la busara"

Godbless Lema (Mp)


Maadamu wewe umenena basi wafuasi wako wote pia watakuunga mkono, lkn maneno hayo hayo yangesemwa na Ole Sendeka sasa hivi hapa server ingejaa kwa matusi ya kumtukana na kutafuta sababu ya kuhalalisha hayo matusi dhidi ya Raisi wa JMTZ!
 
Lini wapinzani wa Bongo wamewahi kulipwa kwa siasa za kistaarabu?Huyu Lema kesho na keshokutwa anaweza kupigwa virungu kama sio mabomu ya machozi na nyie wafuasi wa CCM mnaomsifia leo hii ndio mtakuwa wa kwanza kumkejeli na kumdhihaki na hata huyo anaemtetea leo hii nae hatamsaidia kwa lolote.
ukifanya kizuri utasifiwa na ukiboronga pia utaadhibiwa, na hiyo si ndo kauli yenu? kwahyo wasifiwe tu?
 
Rais ana haki ya kuwatukana watoto wa Watanzania wenzie v.ilaza!? Haki hiyo kaitoa wapi? Rais mstaafu ana haki ya kuwatukana Watanzania kwamba ni Wapumbavu na Malofa!? Haki hiyo kaitoa wapi!?

Hii ni taswira ya kushuka kwa maadili ya vijana wetu...wakichekewa wataota mapembe...wapelekwe mahakamani tu...
Watumie mitandao responsibly...
Si utamaduni wetu kutukana wakubwa...awe rais au jirani...washikishwe adabu...hakuna namna...
 
Kuna clip moja inarushwa startv, Lema anasema, "Iwapo leo nitahamia ccm".

Mkuu lema sioni sababu ya we kuanzisha thredi, vinginevyo tutajie wanaounga mkono kutukanwa rais.

Ila michango ni kitu cha kawaida kama ilivyo kwa mawakili wa serikali kumtetea aliyemtukana rais au muuaji wa halaiki, sio kwamba wale mawakili wanaunga mkono, bali ni mambo ya court proceddings tu.
Wanao unga mkono wamejionesha kwa kutoa michango na waratibu wao!

Lema kahamua kujitenga na dhambi msimlazimishe!
 
kwa kiasi fulani u see, hujamfikia rais so huwez jifananisha nae, na kwa akili zako unahisi hiyo kodi yako anakula rais tu? hao wabunge wako wanalipwa na nn? lowasa wenu mpaka leo anakula kodi yako,

Kwa hiyo hoja yako nini hapo kwenye kodi yangu?
 
"Ninafikiri ni vyema na muhimu tukaendelea kukosoana kwa njia mbali mbali, lakini kwa hakika kabisa siungi mkono rais kutukanwa kwa kejeli ambazo zina sura ya mizaha na sio mabadiliko, Rais kuitwa BWEGE ni kosa na utovu wa nidhamu.

Kosa hili halipaswi kutiwa moyo wala kuungwa mkono, lakini kumwambia Kijana huyu kuwa alikosea ni jambo muhimu zaidi na la busara"

Godbless Lema (Mp)


Naona taratibu watu wameshaanza kujitenga na fisadi Lowasa, wameanza kugundua kwamba jamaa ni psychopath na hakuna anakowapeleka zaidi ya kuwatumia tu kwa ego zake!
 
Hoja ya Mh. Lema imesimamia kwenye sentensi hiyo ya mwisho.. Lema haungi mkono Rais kutukanwa kitu ambacho waungwana wengi tunaona ni sahihi lakini pia adhabu aliyopewa huyo dogo ni kubwa sana.. Angeadhibiwa tu kibusara kwa kupangiwa kusafisha labda kituo cha polisi kwa wiki moja au wiki kadhaa ingekuwa vyema kuliko kumpiga faini ya million 8... Anyway, serikali inatafuta pesa kwa njia yeyote awamu hii..
Adhabu za makosa ya kimitandao zilitungwa bungeni kupitia sheria za makosa ya kimitandao hivyo judge ana tekeleza sheria..siku nyingine judge anaweza kumpa kifungo cha mwaka hata mmoja!
 
Unawezaje kujilinganisha na rais wakati hata ujumbe wa mtaa huna,lazima utambue heshima anayopewa rais ni taasisi si kama mtu binafsi

urais gani wakati kapiga kanzu wenzio,ni siri yake moyoni anajuwa kilichofanyika
 
Mh. Lema tazama humu ndani wanaokupongeza ni kina nani...Mengine utachanganya na za kwako.

Kutukana mtu yeyote sio sawa, iwe kiongozi, rais au raia. Binadamu wote ni sawa iwe rais au raia hakuna aliyeko juu ya sheria. Hakuna mwenye mamlaka ya kutukana na kutukanwa either.

Tunachokipinga ni aina ya adhabu iliyotolewa haiendani na kosa lenyewe na ina leta tafsiri ya kidikteta ya kumtukuza rais kama Mungu. Hata Mungu anasemehe maisha yanaendelea. Miaka mitatu jela wakati kuna wezi wa mabilioni ya fedha wametuibia nchii hii wanatamba uraiani kwa mfano kina Mramba na Daniel Yona haikubaliki kabisa. Kiongozi sio Mungu ni binadamu ty kama binadamu wengine anayechaguliwa wakati mwingine na watu wajinga kabisa wasiojitambua kabisa!!..
 
Rais hana privilege yoyote ya kuwatukana Watanzania kwa tusi la namna yoyote ili iwe v.ilaza, Wapumbavu, Malofa au tusi lolote lile.

Ukitukanwa mahakama ipo...
Ni jukumu lako kwenda mahakamani...
Akitukanwa Rais wapo wa kumwendea mahakamani sababu ni Rais...
Vyeo vinaenda na privileges ...huwezi kujilinganisha na mwenye cheo...ni kutafuta BP tu...
 
Ha ha ha ha kumbe jpm unamtambua mlivyojifanya kususia uapishwaji

Nyie ni pasua kichwa
 
Adhabu za makosa ya kimitandao zilitungwa bungeni kupitia sheria za makosa ya kimitandao hivyo judge ana tekeleza sheria..siku nyingine judge anaweza kumpa kifungo cha mwaka hata mmoja!
Watu tunachokiongelea hapa ni double standards.. Matusi si mazuri kwa pande zote sio upande mmoja tu.. Kwahiyo na sisi tulioitwa malofa na wapumbavu tukiamua kujikusanya kupeleka shauri mahakamani Mr. Clean ataadhibiwa??

Wewe kama Mwanasheria naomba unijibu hilo..
 
Kemea kwanza tendo linalofanywa na vijana na madiwani wenu. Kitendo cha kumchangia fedha mtuhumiwa kinatoa taswira mbaya kwa chama chenu japo wengine wanaona ni kitendo cha kishujaa lakini huwezi kuenzi ushujaa katika mambo ya kijinga.

Kwa hiyo kama huyo diwan ni ndugu yake huyo jamaa aliyetukana hapaswi kumsaidia. Jiongeze Hata kidogo acha kukurupuka . Ni Kosa mtu kumsaidia Mume wa dada yake. Ulitaka amtenge
 
Ulinzi wa rais na hoja yangu vina uhusiano gani?
Nimeweka hoja ya ulinzi wa Rais kukuonyesha mantiki ya tofauti kati ya Rais wa nchi na wananchi mwingine.

Kusema wewe hauna tofauti na Rais wa nchi ni kuongea kwa kinadharia lakini kiuhalisia Rais wa nchi na wananchi wa kawaida wako tofauti.
Nope. Ni kinyume chake. Mi naongelea uhalisia wewe unaongelea ya kufikirika kama ilivyo kawaida yako.
Hapana. Wewe unaongelea dhana ya kinadharia inayosema binadamu wote ni sawa lakini kiuhalisia binadamu wote siyo sawa.
Hapana. Rais wa nchi anatokana miongoni mwa hao hao wananchi. Hatokei sayari nyingine kama Mushtara huko hadi awe tofauti na siye binadamu wengine.
Rais kutokea miongoni mwa wananchi hakumfanyi awe ni sawa na wananchi wengine katika matendo na majukumu yake kama Rais.

Matendo na majumu ya Rais ndiyo yanamfanya awe ni tofauti na wananchi wengine ndiyo maana hata Katiba ya Tanzania 1977 katika Sura ya Pili, Ibara ya 33(1-2) imebainisha ukweli kuhusu umuhimu wa Rais wa nchi.
Heshima ya rais lazima ilindwe....na heshima ya wengine haina ulazima wa kulindwa eh?
Lazima uelewe kuwa kujiheshimu ni kuheshimiwa.

Ninapoongelea Rais nina maana taasisi kwa ujumla wake.

Rais Magufuli amevaa taasisi ya Urais na kutokana na taasisi hiyo, anatakiwa kisheria ajiheshimu.

Wewe mwananchi unaweza kuchagua kutojiheshimu na hakuna mtu au sheria inayokutaka kujiheshimu.

Rais hawezi kuchagua kutojiheshimu na kama atataka kufanya hivyo basi inabidi aachie madaraka.

Hii ndiyo tofauti ya msingi kati ya Rais wa nchi na mwananchi wingine.
 
Back
Top Bottom