Siungi mkono Rais kutukanwa!

Godbless J Lema

Arusha MP
Sep 28, 2013
92
2,205
"Ninafikiri ni vyema na muhimu tukaendelea kukosoana kwa njia mbali mbali, lakini kwa hakika kabisa siungi mkono rais kutukanwa kwa kejeli ambazo zina sura ya mizaha na sio mabadiliko, Rais kuitwa BWEGE ni kosa na utovu wa nidhamu.

Kosa hili halipaswi kutiwa moyo wala kuungwa mkono, lakini kumwambia Kijana huyu kuwa alikosea ni jambo muhimu zaidi na la busara"

Godbless Lema (Mp)
 
Sawa, lakini hata mimi sidhani kabisa kama hilo kosa linaendana na adhabu aliyopewa huyo kijana.

Angeniita mimi 'bwege' unadhani hata angekamatwa?

Au hata ningeenda kumfungulia mashitaka unadhani angepewa hiyo adhabu aliyopewa?


Rais wa Marekani anaitwa majina mengi mabaya kuliko hilo la bwege...
Sheria hizi lengo ni kuleta hofu kwa ujumla kwa watu
wasiwe free kumkosoa....
 
" Ninafikiri ni vyema na muhimu tukaendelea kukosoana kwa njia mbali mbali , lakini kwa hakika kabisa siungi mkono Rais kutukanwa kwa kejeli ambazo zina sura ya mizaha na sio mabadiliko , Rais kuitwa BWEGE ni kosa na utovu wa nidhamu . Kosa hili halipaswi kutiwa moyo wala kuungwa mkono , lakini kumwambia Kijana huyu kuwa alikosea ni jambo muhimu zaidi na la busara " Godbless Lema (Mp)
mkuu ni kweli kumpeleka mahakamani yule Kijana haikuwa busara, atawapeleka mahakamani watu wangapi
 
Asante Lema,

Lakini mbona kama alichangiwa 4.5m za faini na viongozi wa chama chako mkoa, au mlimchangia baadae mkamwambia lakini kijana umekosea au ulinyamaza kimya.
 
Sawa, lakini hata mimi sidhani kabisa kama hilo kosa linaendana na adhabu aliyopewa huyo kijana.

Angeniita mimi 'bwege' unadhani hata angekamatwa?

Au hata ningeenda kumfungulia mashitaka unadhani angepewa hiyo adhabu aliyopewa?
Kwa hiyo unataka kujilinganisha na Rais wa nchi?

Gharama za kukutunza unataka kuzilinganisha na gharama za kumtunza Rais?
 
Ukiwa mwanasiasa kuwa na ujasiri wa kupokea yote na kuvumilia yote ndio sifa kuu ya viongozi shupavu, hakuna anaeunga mkono dhihaka dhidi ya rais au binadamu yeyote, lakni kinachopingwa ni adhabu na muamsho dhidi ya sheria mbovu ya mawasiliano ya mtandao...
hats wew jua kuwa hatukuungi mkono wew tunaunga mkono unachokisimamia, siku ukijichanganya tunakubwaga tu Kama wenzako..
 
Back
Top Bottom