Siungi mkono Rais kutukanwa!

Siungi mkono Rais kutukanwa!

Ni Kweli, Lakini Busara Ya Kumkanya Na Kumsaidia Ni Bora Zaidi Kuliko Kumwacha Akaozee Jela Wakati Inawezekana Kumrekebisha Mtaani.
Je, Huyo Hakuwa Mmoja Kati Ya Vijana Walioitwa Wapumbavu Kisa Wanataka Mabadiliko?
Kwa bongo mkubwa hakosolewi
 
Kemea kwanza tendo linalofanywa na vijana na madiwani wenu. Kitendo cha kumchangia fedha mtuhumiwa kinatoa taswira mbaya kwa chama chenu japo wengine wanaona ni kitendo cha kishujaa lakini huwezi kuenzi ushujaa katika mambo ya kijinga.
Mbona humwambii mwenyekiti wa ccm awakemee vijana wake wanao kesha wakiporomosha mitusi mitandaoni?
 
Siyo rais wa Marekani tu.

Hata wa Kenya tu hapo.

Achilia mbali akina David Cameron, Jacob Zuma, Francois Hollande na wengineo huko kwenye demokrasia kutushinda sisi.
Hapa demokrasia yetu ni kupandisha bendera za vyama vya siasa tu basi
 
Asante Lema,

Lakini mbona kama alichangiwa 4.5m za faini na viongozi wa chama chako mkoa, au mlimchangia baadae mkamwambia lakini kijana umekosea au ulinyamaza kimya.
Swali lako halina msaada.
 
"Ninafikiri ni vyema na muhimu tukaendelea kukosoana kwa njia mbali mbali, lakini kwa hakika kabisa siungi mkono rais kutukanwa kwa kejeli ambazo zina sura ya mizaha na sio mabadiliko, Rais kuitwa BWEGE ni kosa na utovu wa nidhamu.

Kosa hili halipaswi kutiwa moyo wala kuungwa mkono, lakini kumwambia Kijana huyu kuwa alikosea ni jambo muhimu zaidi na la busara"

Godbless Lema (Mp)
Sasa aona umeanza kupevuka na kuwa wise!
Endelea na msimamo huo.
 
Ulinzi wa rais na hoja yangu vina uhusiano gani?

Nope. Ni kinyume chake. Mi naongelea uhalisia wewe unaongelea ya kufikirika kama ilivyo kawaida yako.

Hapana. Rais wa nchi anatokana miongoni mwa hao hao wananchi. Hatokei sayari nyingine kama Mushtara huko hadi awe tofauti na siye binadamu wengine.

Heshima ya rais lazima ilindwe....na heshima ya wengine haina ulazima wa kulindwa eh?
Sio ashauli watu wavunje sheria kwa kungoa matairi ya magari yanayo kamatwa.
 
In This Country Hakna Ki2 Kama Freedom Of Speech,,,,kwa Sababu Yeye Kumuita Bwege Ni Maoni Na Maono Yake Kwani Mtu Akikuita Wewe Mpumbav Na Wakati Wewe Unajua Sio Mpumbav Si Inabaki Kuwa Opinion Yake Tu Unless Kwel Ni Bwege
 
Vyocyote utakavyotafsiri ila ukweli ni kwamba Lema amepingana na akina Malisa na Nanyaro waliochangisha hizo fedha. Usiweke tafsiri yako isiyoeleweka
Hivi wewe Lowassa unaemtukana kila siku hakuwa kiongozi?Hivi wewe unaweza kumwambia baba yako ameji.... kama ambayo umekuwa ukimdhalilisha huyu mzee hapa kila siku?Au ni kwasababu mods wanakulinda?
 
Sawa, lakini hata mimi sidhani kabisa kama hilo kosa linaendana na adhabu aliyopewa huyo kijana.

Angeniita mimi 'bwege' unadhani hata angekamatwa?

Au hata ningeenda kumfungulia mashitaka unadhani angepewa hiyo adhabu aliyopewa?
Dah!

Kuna kitu Kinaitwa Hekima na Busara,

Kuwa Mimi kama Kijana nikiwa nipo na vijana katika mazingira ya kawaida naweza kutumia Maneno yasiyo na sitaha ama Matusi lakini isionekane kama ni kosa kulingana na rika na uhusiano, lakini Maneno Kama Hayo Hayo ukimtolea Mtu Mzima asiye wa Rika yako na wala huna Uhusiano Wowote wa Karibu Kiutani, Ni kosa Kisheria.
 
"Ninafikiri ni vyema na muhimu tukaendelea kukosoana kwa njia mbali mbali, lakini kwa hakika kabisa siungi mkono rais kutukanwa kwa kejeli ambazo zina sura ya mizaha na sio mabadiliko, Rais kuitwa BWEGE ni kosa na utovu wa nidhamu.

Kosa hili halipaswi kutiwa moyo wala kuungwa mkono, lakini kumwambia Kijana huyu kuwa alikosea ni jambo muhimu zaidi na la busara"

Godbless Lema (Mp)
Hapo nakuunga mkono kwa 100%. Maneno ya busara sana, Mungu akubariki kijana.
 
Mhesh. Lema unafahamu suala hili limekuwa mjadala kutokana na mambo mawili; 1. Kwa bahati nzuri wakati kijana yule anatiwa hatiani kwa kosa la "kumwita Rais kuwa ni bwege" kule Arusha, kule Dodoma naibu spika wa Bunge alikuwa ametoka kumdhalilisha mbunge wa upinzani kwa kumwambia kuwa "aache ubwege wake". 2. Sheria ya mtandao imeibua maswali mengi mno mno!

Ni sawa, hata mimi siungi mkono Rais kuitwa "bwege", lakini tujiulize pia je, tunaunga mkono nani aitwe "bwege"? Kwamba rais wetu asiitwe bwege lakini wengine wana deserve kuitwa mabwege, siyo? Hivi tunawezaje kumwambia yule kijana kuwa alikosea, wakati inaonekana ni halali kwa ninyi wabunge wa upinzani kuitwa "mabwege"?

Tunalo tatizo kubwa katika jamii yetu, kwanza ya kuona kama vile viongozi hawakosei wakati ukweli viongozi hao ndio wamekuwa sehemu au bomba la kutiririsha ukiukwaji wa maadili katika jamii yetu. Huyu kijana ambaye leo mnamwambia alikosea, ndiye alishuhudia watanzania wenzake pale Jangwani wakitukanwa na mtu wa hadhi ya Rais kwamba ni wapumbavu kabisa kwa sababu tu wanaunga mkono siasa za upinzani.

Nakubaliana na wewe Mhesh. Lema tumwambie huyo kijana kwamba kumwita Rais kuwa ni "bwege" ni kosa kimaadili (ya hapa kwetu maana kwa wengine sio shida) achilia mbalia sheria hiyo ya hovyo ya makosa ya mtandao. Lakini viongozi wetu nao wafahamu kuwa wao pia wananayoyatenda na kuyatamka yanachochea vijana "kuwaita mabwege"!
Huu ukweli hata Lema anaujua ila basi tu.
 
Sawa, lakini hata mimi sidhani kabisa kama hilo kosa linaendana na adhabu aliyopewa huyo kijana.

Angeniita mimi 'bwege' unadhani hata angekamatwa?

Au hata ningeenda kumfungulia mashitaka unadhani angepewa hiyo adhabu aliyopewa?

Sasa we nani? Mpaka utiliwe umuhimu kuhivyo? Tuache siasa pasipo hitaji siasa. Mkuu wa nchi si shemeji yako
 
Dah!

Kuna kitu Kinaitwa Hekima na Busara,

Kuwa Mimi kama Kijana nikiwa nipo na vijana katika mazingira ya kawaida naweza kutumia Maneno yasiyo na sitaha ama Matusi lakini isionekane kama ni kosa kulingana na rika na uhusiano, lakini Maneno Kama Hayo Hayo ukimtolea Mtu Mzima asiye wa Rika yako na wala huna Uhusiano Wowote wa Karibu Kiutani, Ni kosa Kisheria.

Hekima na busara? Vilitumika hivyo ktk kuita watoto villaza?
 
Back
Top Bottom