Sitamani kuzaa mtoto wa kike

Sitamani kuzaa mtoto wa kike

Khaa!! Molembe! Mie nawasoma hapa wote hata siwaelewi!! Ni hatari sana dunia kuwa na wanaume wengi kuliko wanawake. Ili uwatendee wengine haki basi kila watoto 3 utakao wazaa 2 wawe wa kike. Mbona jinsia zenyewe siku hizi unachagua tu
Tuache ubinafsi
 
Kuna matukio mabinti wa siku hizi wanafanya mpaka nakosa hamu ya kuja kuwa na mtoto wa kike maana yanatia aibu na kichefuchefu, Fikria mzazi unakutana na picha ya binti yako akiwa uchi wa mnyama kwenye mitandao hivi utajisikiaje,

mzazi unatumia pesa nyingi kukapeleka kabinti kako shule mwisho wa siku anarudi akiwa na mimba mtaa mzima unakucheka, nawapenda sana watoto wa kike ila kuna visa nikiviona nachukia kuzaa mtoto wa kike maana wanaibisha sana.

Na wewe nae unazaa? au umekurupuka tu?
 
KikulachoChako

Haya nakutakia uzao mwema,mimba isikusumbue ili utakapojifungua kidume chako kiwe kishoga salama kama aliyekuzalisha.
 
Last edited by a moderator:
U better re think and come up na hoja ya msingi....

Tabia za watoto ni matunda ya malezi waliopata kwa walezi wao....

Unaweza kuzaa midume na ikawa mifurska vilevile
 
Tatizo ni kwamba wanaume wengi (na wanawake pia) wana focus zaidi in women's supposed weaknesses based on women's sexuality. Ukweli ni kwamba, on average, women are just as smart and capable in most (if not all) human endeavors in life, on the same foot as men if given a fair chance. Nimesoma na wasichana wa kihindi na kizungu wengi ambao walinizidi akili darasani, and end of the day nilibaki na misuli yangu tu ya kujivunia.
 
Molembe

Mawazo yako mabaya,omba msamaha kwa Mungu na omba akupatie watoto wa baraka.
 
Last edited by a moderator:
Nashukuru mungu kwa kunipa mtoto wa kike, ni baraka toka kwa mungu. Mtoto ni mtoto kikubwa kumlea kwenye misingi ya kumjua na kumpendeza mungu, unaeza zaa hiyo midume ikawa mashoga, teja, jambazi ili mradi tu tafran...msipende kukufuru!!
 
Ablessed

Hilo wanalisahau mazingira ya sasa ya malezi hakuna ya afadhali, mtoto wa jinsia fulani Mungu awasaidie tu watoto wetu.
 
Last edited by a moderator:
Duuh nimeshangaa sana baadhi ya maneno ya watu hapa eti mtoto wa kike ni laana basi muache kutuoa mana mtakuwa mnaoa Laana! kumbuken sote tumezaliwa na mama zetu ambao nao walikuwa watoto hao hao wakike,Je kwa hiyo mama zetu ni laana?? Haramu huzaa haramu yenyewe! kwa hiyo sote tu haramu usimnyooshee mtoto wa kike kidole.DAIMA KUMBUKA MTOTO UMLEAVYO NDIVYO AKUAVYO!!!
 
Hakuna baraka kubwa kama kuzaa watoto wa kike,kama wewe ni mzazi utakubaliana na mimi,watoto wa kike wana mapenzi ya dhati kwa wazazi wao,wana huruma wanajali haraka shida za wazazi. Malezi mema na zaidi mafundisho ya kumpenda Mungu,kuwa karibu nao sana wakiwa wadogo mpaka anakuwa
 
Bila wenzio kuzaa watoto wa kike huyo mwanamke unayetaka kuzaa naye mtoto wa kiume ungempata wapi? Ungezaa na mwanaume mwenzio? Kwa maana iliyo wazi ni kwamba hutaki wanawake wawepo.

Katika kizazi hiki ni Kazi ngumu sana kumlea mtoto wa kiume mpaka afikie kuwa mwanaume kuliko mtoto wa kike kufikia kuwa mwanamke. Ipi aibu kubwa kunyooshewa vidole kuwa yule ni baba wa yule binti anayetembea nusu uchi au yule ni baba ya yule kijana anayegawa nyuma
 
Back
Top Bottom