Sitaki habari za simba na yanga: Jiheshimu uheshimiwe

BICHWA KOMWE -

JF-Expert Member
Jul 21, 2022
4,749
10,310
Hivi huko Tanganyika huwa mnasoma somo la nidhamu mashuleni?

Umekutana na mtu, wala hamfahamiani kihivyo, hujui anapenda nini, hujui anavutiwa na nini, unakurupuka tu?

Nani aliwaambia kila mtu ni shabiki au mfuasi wa mpira?

Umekutana na mtu, wala havutiwi hata na mipira, unaanza kuleta mastori ya simba na yanga? Unaugua?

Ati oooh, hivi lile goli la jana la Mayele ulilionaje? Alipiga hat trick....blah blah....

Kwanza huyo Mayele mwenyewe ndio nani? Mimi hata simjui.

Nikikuhurumia sana ili usifadhaike nitajifanya tu kuitikia kwa kuguna mhhhh, mhhhh, yess, oooh yess... ndiwooooooooo.......

Nikikasirishwa na mastori yako ya mayele nakutimua au nakucharaza bakora.

Kabla ya kumrukia mtu hakikisha unajiridhisha kama hicho unachomwambia anakifurahia au kukipenda. Mjifunze kuelewa mipaka ya mazungumzo.

MY TAKE: Tupunguze ushamba na kurukia watu.
 
Mbona hamna hata ishu huko!

Halafu wafuasi wa mpira huwa wako kama mazombi! Wanaburuzana tu!

Na vile wanavyotaniaga nashindwa hata kuelewa dhana nzima ya ule utani wao! Halafu wanacheka eti!

Is it truly laughable? Atii ooh Yanga kapiga, ooh goli sijui nini, mara makolo.....Hata haichekeshi kabisa.

As a matter of fact hata huwa sielewi wanachozungumza. It is insensible!

Cc Nyani Ngabu tunaomba hekima zako hapa
 
Mchezo wa Mpira ni mzuri kwa watu wenye hela huko ulaya bongo Mimi huwa nawaona ni kama makanjanja we na umasikini wako huna hata uhakika wa kula Milo miwili kutwa kijiweni unajadili Mpira unachosikiliza radio ni Mpira unachoangalia ni Mpira gazeti limetoka la michezo tayari unalo

Ni jambo la kushangaza mtu anakufuata na kuniuliza matokeo vipi Jana ? Ulionaje like pira biriyani? wakati huo Mimi na mwaka sasa sijaangalia mpira

Umasikini na ushabiki wa Mpira utajikuta unaingia kwenye matatizo ya afya ya akili
 
Kwani Simba na Yanga ndo nini?

Simba najua Ni Mnyama na yanga najua ni yake mahindi mwaka 1992 kwenye 94 hivi kipindi cha Njaa tulikuwa tunyaita yale mahindi Ya njano mahindi ya yanga
😂😂😂 Eeeeeeehhhh

Kuna unga fulani pia ulikuwa unatoka marekani unagawiwa kwa wanafunzi mashuleni ulikuwa wa njano haswaaa wanauita YANGA. Juzi tu hapa. Miaka ya 2010. 😉😉

Dokta mwaka 1992 ulikuwa na miaka mingapi 😉😉😉😉
 
Back
Top Bottom