The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,495
- 2,043
Ndugu wanabodi naweza nisiekewke kirahisi kuhususiana na hii hoja yangu, lakini nimekaa na kutafakari mambo kadhaa:
Mijadala inayohusu mpira wa miguu hapa nchini imekuwa mingi na inachukua muda mwingi sana, ina wafuatiliaji wengi na wachangiaji wengi.
Na kwa kulifahamu hilo ndio maana zimeibuka media nyingi sana zinazojihusisha na mambo ya kuchambua na kuuzungumza mpira wa miguu.
Hata hivyo uchambuzi wote unakuwa na maana au kukolezwa na uwapo wa simba na yanga. Kwa maneno mengine ukifanya uchambuzi ama utangazaji wako kama hautazungumia simba ama yanga basi jua dhahiri mjadala wako utakudodea.
Wapenzi na mashabiki wa vilabu hivi huvizungumzia kwa hisia kali sana ni kana kwamba vinawasaidia kupata kipato chochote kumbe ni mapenzi tu.
Na ukitaka kushuhudia uchizi na nguvu ya hawa wapenzi wa hivi vilabu, basi patokee jambo wasilolitaka pale clabuni, yaani utawashuhudia wanafura kana kwamba mtu kaibiwa hela yake.
Yaani wana nguvu ya kumtoa yeyote na kumuweka yeyote wamtakaye ilimradi tu wafurahie wawe na cha kumnanga mtani.
Jambo hili lina athari hasi sana kwa vijana wetu kwani kwa kadri wanavyotumia muda mwingi kujadili mpira wanatengeneza ombwe kwenye mijadala inayohusu mustakabali wa taifa letu na changamoto zake.
Amini usiamini kusipokuwa na presha ya kutosha ya mijadala inayotoka kwa umma, watawala na viongozi wanabweteka hawaumizi vichwa juu ya namna bora ya kutatua changamoto za watu wao!
Maana kiongozi akfungua redio anasikia simba wanalia "mrudisheni chama" ikiisha hiyo atasikia tena "huyu mayele ni zaidi ya mesi"
Alafu watu wanabishania hayo tangu asubuhi jioni . Wengine wanaishia kupigana. Unadhani huyo kiongozi atapata tabu ya kuumiza kichwa juu ya vitu kupanda bei?
Kama hiyo haitoshi niliwahi kuwa na rafiki yangu Kutoka nchi ya Uganda alishangaa sana kuona muda wa kuongelea yanga na simba unavyotuchukulia akili nyingi na muda mrefu badala ya kujadili matatizo yetu.
Napendekeza kama ikiwezekana hivi vilabu vifutwe ili watu wajadili maendeleo na sio kutwa kucha kujadili mpira. Mahali popote kulipowahi Kutokea mageuzi yoyote, ni kwamba yale mageuzi yaliletwa na mijadala mingi ya umma.