Kuwatumia vibaya Diamond na Ali Kiba kwenye siasa za Simba na Yanga ''kutaua" soka la Tanzania

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
15,120
27,126
Inajulikana tangu enzi za Pontyo wa Pilato kwamba shabiki wa Yanga hawezi kuwa shabiki wa Simba and vice versa. Sio tu hivyo bali hadi kwenye kutakiana mafanikio na kuombeana njaa ndani ya uwanja.

Shabiki wa Simba hawezi kufurahia mafanikio ya ndani ya uwanja ya Yanga hata itokee nini.

Miaka ya nyuma wazee wetu walikuwa wanachukia hadi rangi za timu pinzani.

Mfano Mwameja Mohamed Mwameja (jina lake haitwi Mohamed Mwameja ila anaitwa Mwameja Mohamed Mwameja) anasimulia.

Baba angu ni shabiki wa Yanga lia lia kama tu ilivyo kwa mzee wangu mzee Hussein Daima( Baba mzazi wa Mohamed Hussein Machinga kule Mtwara)

Familia yetu inajulikana ni familia ya wanayanga watupu. Kuna kipindi nikiwa Simba Sport niliwahi kuhisiwa Nina mapenzi na Yanga hadi kutengwa kambini Zanzibar mwaka 92 baada ya mimi kusaini Yanga na Ken Mkapa na Kipese kusaini Simba. Sekeseke lilikuwa kubwa sana hadi Mzee Mwinyi akaingilia kati na kutumia busara ya kiutu uzima ambapo alisema Mimi nibaki Simba na Ken Mkapa abaki Yanga.

Sakata hilo lilikoleza uvumi kwamba Mimi Yanga. Kabla mzee Mwinyi hajaingilia kati kuna watu walitumwa kuja kunimwagia tindikali ila Mwenyezi Mungu alininusuru watu hao hawakunidhuru.

Maneno ya chinichini yalikuwa kwamba Mimi Mwameja Nina mapenzi na Yanga ila Simba nipo kikazi tu.

Sasa pale kwetu Tanga Mwakidila kulikuwa na mzee rafiki yake baba shabiki wa Simba lia lia.

Kuna siku huyu mzee alikuja nyumbani sasa akasikia kiu akanituma nimletee maji ya kunywa.

Pale nyumbani kwetu ilikuwa karibu kila.kitu ni kijani na njano hadi vikombe.

Nikachukua maji kwenye kikombe cha rangi ya njano nikampelekea yule Mzee. Mzee alifura kwa hasira. Pamoja na kwamba alikuwa na kiu lakini alinimwagia yale maji yote.

" umekosa adabu wewe mtoto unaweza vipi kuthubutu kunipa maji kwenye kikombe cha rangi cha njano"

Hivyo ndivyo ilivyo kuwa.

Back 2 Diamond na Ali Kiba.

Diamond anajulikana ni shabiki wa Simba, lakini ghafla tukasikia sijui amekuwa shabiki wa Yanga. Sijui kapewa hela sijui kashawishiwa na Hajj blah blah blah.

Juzi tena tukashuhudia kituko cha karne. Ali Kiba ambae anajulikana kama shabiki wa Yanga eti kahamia Simba kafanya na wimbo kabisa.

Kwenye interview anasema hawezi kushabiki timu ambayo imemtenga(kumtenga vipi? Kutompa show? Kumpa show Diamond? ama? )

If the answer is Yes how deep was ur bond with Young Africans for you to live the team just like that? (Wewe sio mchezaji wala muajiriwa. Ur just a mere fan)

MADHARA YAKE: Itawafanya vijana wadogo na watakao zaliwa baadae waone kumbe mtu kuhama Yanga kwenda Simba ni jambo la kawaida tu.

Ukitangukia stage hii, Itaua ushabiki na unazi wa Simba na Yanga ambao ndio roho ya mpira wa Tanzania.

Mpira utapoteza mvuto. Vijana watajihusisha na .mpira kwa ajili ya kubeti tu.

ATHARI ZIMEANZA KUONEKANA
Hivi kweli leo hii timu kongwe nchini kama Yanga na Simba haziwezi kujaza uwanja wa Mkapa mpaka ipigwe promo?

Mpaka watu wahamasishwe?

Miaka ya tisini hakukuwq na instagram wala Facebook wala twitter wala tiktok wala akukuwaga sijui na promo lakini viwanja vilikuwa vinajaa mapema tena kwenye mechi ambayo Yanga au Simba wanacheza na timu ya kawaida achilia mbali mechi ya Simba na Yanga au ya kimataifa.

Hivi kweli timu kongwe kama Simba ambayo ina mamilioni ya mashabiki Tanzania inastahili kweli kujitapa kuujaza uwanja wa mkapa? Kweli? Seriously kabisa? Ndio tumefikia hapo?

Uwanja ambao Mwamposa mtu mmoja aliujaza ukatapikq hadi nje.

Kwa kujivunia kujaza uwanja tumerudi nyuma kwa miaka sabini . Kwa ukubwa wa Yanga na Simba zinapaswa kuwa zimeshavuka hiyo stage ya kutamba kujaza uwanja..

Timu kama Azam au Tabora United zingejisifu kujaza uwanja ingeweza kueleweka lakini sio kwa Simba na Yanga.

TUNAPOELEKEA: kama huu upuuzi wa kuwaingiza wasanii kwenye siasa za Simba na Yanga asipokemewa tunapoelekea itakuwa ili Simba na Yanga zijaze inabidi mashabiki walipiwe tiketi kuingia uwanja ni, wachukuliwe kwenye magari kutoka matawinj kwao, wapelekwe na pombe au pilau za bure..
 
Naunga mkono hoja ni ushamba kuwatumia wasanii wa muziki au tasnia nyingine kama kigezo cha timu hizi kukubalika.

Shabiki wa ukweli hahami hata siku moja. Mimi nimekuwa shabiki wa Arsenal licha ya kuwa Arsenal imekuwa ikifanya vibaya kwenye EPL kwa miaka ishirini sasa sijawahi kufikiria kuhama na hiyo ni timu ya ughaibuni ambako sijawahi kufika sembuse timu ya hapa nyumbani.

Eti Diamond anasema amehama Simba kumfuata Haji Manara,huu ni ujinga kabisa.
 
Naunga mkono hoja ni ushamba kuwatumia wasanii wa muziki au tasnia nyingine kama kigezo cha timu hizi kukubalika. Shabiki wa ukweli hahami hata siku moja. Mimi nimekuwa shabiki wa Arsenal licha ya kuwa Arsenal imekuwa ikifanya vibaya kwenye EPL kwa miaka ishirini sasa sijawahi kufikiria kuhama na hiyo ni timu ya ughaibuni ambako sijawahi kufika sembuse timu ya hapa nyumbani. Eti Diamond anasema amehama Simba kumfuata Haji Manara,huu ni ujinga kabisa.
Sahihi kabisa mkuu
 
Inajulikana tangu enzi za Pontyo wa Pilato kwamba shabiki wa Yanga hawezi kuwa shabiki wa Simba and vice versa...
Hiyo miaka ya 90 unayosema Simba na Yanga zilikuwa zinajaza uwanja kulikuwa na uwanja wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 60,000?

Unasifia kujaza uwanja wa watu 8k!!??? Tukubali tukatae ila ukweli ni kuwa kizazi hiki kimeuheshimisha mpira wa bongo, hizo nyingine zitabaki kuwa ngojera tu.
 
Hiyo miaka ya 90 unayosema Simba na Yanga zilikuwa zinajaza uwanja kulikuwa na uwanja wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 60,000? Unasifia kujaza uwanja wa watu 8k!!??? Tukubali tukatae ila ukweli ni kuwa kizazi hiki kimeuheshimisha mpira wa bongo, hizo nyingine zitabaki kuwa ngojera tu.
Nilitaka nimjibu hivyo hvyo, eti anachukulia poa watu kufika 40k uwanjani, tuviwanja twa zamani wakiingia watu 15k tu tumejaa.
 
Hiyo miaka ya 90 unayosema Simba na Yanga zilikuwa zinajaza uwanja kulikuwa na uwanja wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 60,000? Unasifia kujaza uwanja wa watu 8k!!??? Tukubali tukatae ila ukweli ni kuwa kizazi hiki kimeuheshimisha mpira wa bongo, hizo nyingine zitabaki kuwa ngojera tu.

1. Uwanja wa taifa ( shamba la bibi)
2. Ccm kirumba mwanza.

3. Sokoine Mbeya.

vinaingiza watu wangapi mkuu
 
Siasa ndiyo zinaharibu mpira wa nchi hii. Hilo la wachezaji kuhama na sasa wasanii wa muziki, chimbuko lake ni mkono wa wanasiasa. Na mpira unatumika kama experiment, halafu mambo hayo hayo yanaenda kufanyika kwenye siasa.

Kuna dhana kuwa lazima hizi timu ziwe sawa, mmoja akionekana kumuacha mwenzie anapigwa pini. Sitashangaa kukuta Phiri anaandaliwa makazi huko Yanga tena na watu walioko ndani ya Simba.
 
Inajulikana tangu enzi za Pontyo wa Pilato kwamba shabiki wa Yanga hawezi kuwa shabiki wa Simba and vice versa.
Sio tu hivyo bali hadi kwenye kutakiana mafanikio na kuombeana njaa ndani ya uwanja.

Shabiki wa Simba hawezi kufurahia mafanikio ya ndani ya uwanja ya Yanga hata itokee nini.

Miaka ya nyuma wazee wetu walikuwa wanachukia hadi rangi za timu pinzani.

Mfano Mwameja Mohamed Mwameja ( jina lake haitwi Mohamed Mwameja ila anaitwa Mwameja Mohamed Mwameja) anasimulia.

Baba angu ni shabiki wa Yanga lia lia kama tu ilivyo kwa mzee wangu mzee Hussein Daima( Baba mzazi wa Mohamed Hussein Machinga kule Mtwara)

Familia yetu inajulikana ni familia ya wanayanga watupu. Kuna kipindi nikiwa Simba Sport niliwahi kuhisiwa Nina mapenzi na Yanga hadi kutengwa kambini Zanzibar mwaka 92 baada ya mimi kusaini Yanga na Ken Mkapa na Kipese kusaini Simba. Sekeseke lilikuwa kubwa sana hadi Mzee Mwinyi akaingilia kati na kutumia busara ya kiutu uzima ambapo alisema Mimi nibaki Simba na Ken Mkapa abaki Yanga.

Sakata hilo lilikoleza uvumi kwamba Mimi Yanga. Kabla mzee Mwinyi hajaingilia kati kuna watu walitumwa kuja na kwenye mechi ambayo Yanga au Simba wanacheza na timu ya kawaida achilia mbali mechi ya Simba na Yanga au ya kimataifa.

Hivi kweli timu kongwe kama Simba ambayo ina mamilioni ya mashabiki Tanzania inastahili kweli kujitapa kuujaza uwanja wa mkapa? Kweli? Seriously kabisa? Ndio tumefikia hapo?

Uwanja ambao Mwamposa mtu mmoja aliujaza ukatapikq hadi nje.

Kwa kujivunia kujaza uwanja tumerudi nyuma kwa miaka sabini . Kwa ukubwa wa Yanga na Simba zinapaswa kuwa zimeshavuka hiyo stage ya kutamba kujaza uwanja..

Timu kama Azam au Tabora United zingejisifu kujaza uwanja ingeweza kueleweka lakini sio kwa Simba na Yanga.

TUNAPOELEKEA : kama huu upuuzi wa kuwaingiza wasanii kwenye siasa za Simba na Yanga asipokemewa tunapoelekea itakuwa ili Simba na Yanga zijaze inabidi mashabiki walipiwe tiketi kuingia uwanja ni, wachukuliwe kwenye magari kutoka matawinj kwao, wapelekwe na pombe au pilau za bure..
 
So unabisha radio ya taifa haikutumika kupromote!? Mpaka hapo nimegundua unabishia vitu usivyo na ufahamu navyo!
Haikuwa promotion mkuu. Watu walikuwa wanaambiwa tu wiki ijayo kuna mechi ya Simba na Yanga. Hakukuwaga na blah blah blah sijui Msanii fulani atakuwepo etc
 
Back
Top Bottom