Wana Simba SC mlioshtushwa na Tetesi za Beki Onyango kwenda Yanga SC ina maana Mbinu hii ya Waandishi wa Habari na Mawakala hamuijui au?

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Huu sasa ni mwaka wa 15 hii Mbinu inatumiwa na Waandishi wa Habari za Michezo nchini na Mawakala wa Wachezaji wao na wakati mwingine Wote kwa pamoja hushirikiana ili kufikia Lengo Mama.

Ni kwamba kila unapofika muda wa Wachezaji Maarufu na wenye Umuhimu ndani ya Klabu husika ndiyo huwa muda wa Mavuno ya Pesa hasa kwa Waandishi wa Habari za Michezo ( hasa wa Magazeti ) na wale baadhi ya katika Redio na Runinga.

Mtindo huu Unaitwa 'Jambisha' ambapo Mchezaji husika akiona Mkataba wake umeisha au unaelekea kuisha na anataka Kuongeza Thamani yake katika Usajili mpya na Mshahara mkubwa kwa Timu yake huamua Kuwatafuta Waandishi wa Habari za Michezo ili mara kwa mara wawe Wanaandika kuwa anahamia Timu Pinzani / Hasimu ili Mabosi wa Klabu yake Washtuke, Waogope na haraka Wampandie Dau na wamuongezee Mkataba wenye Maslahi makubwa na manono.

Kinachofanyika hapa ni kwamba huyu Mwandishi wa Habari za Michezo akianza 'Kujambisha' na Lengo kufikiwa kwa Mchezaji Kusajiliwa tena na kwa Pesa zaidi basi 20% ya ambazo atapata atampa kwa Makubaliano ambayo huwa wanakuwa wanaingia na ambayo siyo ya Kusalitiana / Kudhulumiana.

Hivyo basi Mashabiki wa Simba SC hapa Mitandaoni Jamiiforums na Kwingineko acheni kupata Presha kusikia Beki Joash Onyango Mkataba wake unaelekea mwishoni na Yanga SC wanamnyatia Kumsajili kwani hata huyu Beki Onyango kwa sasa ameisha na ana Mapungufu makubwa ya Kimchezo ammayo mara nyingi huwa yanazibwa vyema na Mabeki wenzake akina Inonga, Kapombe, Tshabalala na hata Kiungo wa Ukabaji Mkude.

Tena kama kuna Mchezaji ambaye Simba SC wakisikia anataka Kuondoka au anaturingia wa Mfano wa huyu Joash Onyango nashauri upesi sana Waachane nae kwani licha ya Simba SC bado kuwa na Hazina ya Mabeki imara wa Kati mfano wa Pascal Serge Wawa na Kennedy Wilson Juma ila kuna Mabeki Wawili mmoja kutoka Congo DR ila anacheza PSL ( Ligi Kuu ya Afrika Kusini ) na mwingine anacheza Asec Mimosas FC ya Ivory Coast ambao wako katika Rada za Simba SC kwa sasa ambapo wote ni Mahiri na wana Uwezo wa juu ya Kumzidi huyu Beki anayedengua Mkenya Joash Onyango.

Na nawahakikishieni na hata wale mliobahatika kidogo Kucheza Mpira na mnaujua Mpira kwa Jicho la Kiufundi mtakubaliana nami kuwa Beki Joash Onyango akihamia Yanga SC kamwe hatopata Namba Kikosi cha Kwanza kwani hana hicho Kiwango cha kuwaweka Mkeka / Benchi Mabeki mahiri na ninaowakubali wa Yanga SC akina Dickson Job, Bakari Mwamnyeto na Yanick Bangala.

Binafsi nilivyosikia kuwa Beki Joash Onyango Kesho Simba SC ikicheza na Orlando Pirates FC hatocheza kutokana na kuwa na Kadi Tatu za Njano nilifurahi na kushukuru kwani kwa nilivyowaona Washambuliaji HATARI wa Orlando Pirates FC na wenye Kasi na Mbinu nyingi za Kushambulia na Madhaifu yake ( Beki Joash Onyango ) niliyoyaona katika Mechi kadhaa la Ligi Kuu ya NBC, ASFC na CAFCL na hii ya CAFCC kama angekuwepo Kesho Simba SC tungefungwa Goli nyingi na tungejuta hata Kumpanga / Kumchezesha kwani kwa sasa hatufai tena, imetosha na aachwe aende anakokutaka au huko Yanga SC akaizee Benchi.

Wiki hii umeamza 'Kujambishwa' na wana Habari za Michezo nchini Tanzania kuwa Beki Joash Onyango anaenda Yanga SC Msimu ukimalizika na Mimi sasa nawaandaa mapema tu kuanzia sasa 'Mtajambishwa' tena na Wanahabari wa Magazetini kuwa Khalid Aucho na Fiston Mayele wanahamia au wanatakiwa na Simba SC ili Wavune pakubwa kutoka kwa Matajiri wao GSM.

Acheni Shaka Onyango si pengo SSC!!!
 
km wachezaji na vongozi wataendela na dharau zao za kutomuamkia onyango basi watavuna walichopanda, lazima aende mahali atapoheshimiwa
 
Mbona na wewe umetumia mbinu ya muandishi wa habari. Babu onyango aonekane si lolote simba,


Lengo la muandishi kumpandisha thamani. Lengo lako kumshusha thamani.

Umesema Mwandishi analipwa na onyango. Wewe hujasema unalipwa na nani?
 
Ataenda kokote lakini siyo Yanga, Yanga siyo kambi ya wazee.
Uko sahihi kabisa. Kwa mtu mwenye akili timamu atagundua Yanga ya miaka hii inaamini katika uwekezaji wa wachezaji vijana! Na siyo wachezaji wazee.
 
Mwamnyeto ni mchezaji wa timu ya Taifa wakati Inanga hata timu ya kijiji hayupo
 
Back
Top Bottom