GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,542
- 108,877
Sijui jinsi mtakavyojitetea kwa hili Kwangu au hata kwa wengine waliokuwa na mtazamo kama Wangu ila kwa jinsi nilivyoona jana katika Kurasa mbalimbali za Watu wa Yanga kwa mtazamo wangu kwa Jicho dogo la Kibiashara naona kama vile litawaathiri pakubwa sana.
Bado sijazithibitisha na sitaki Kuziamini pia kuwa kuna Taarifa fulani fulani zinaanza Kuratibiwa za Kuwahamasisha Wapenzi na Mashabiki wa Simba SC wasiwe Wateja wa Kampuni ya Simu ya Tigo kwakuwa tu Mmiliki wake mpya kwa sasa Tajiri Rostam Aziz ni mwana Yanga SC Kindakindaki na Mmoja wa Wafadhili wakubwa tu wa Klabu hiyo.
Binafsi nadhani hata Rostam Aziz Mwenyewe asingeruhusu kuwa hapo ( kwa Kujulikana na kutajwa kama Mmiliki ) hasa kwa Maslahi ya Kibiashara na Kuzikwepa hizi Siasa zetu za Simba na Yanga hivyo basi badala yake angemuweka Mtu mwingine hapo ambaye kama Msimamizi na Yeye abakie tu kuwa Mmiliki na ikiwezekana azuie pia Kutajwa hivyo kwani Watanzania ( hasa Mashabiki wa hizi Klabu Kubwa Mbili nchini Tanzania ) tunajijua Wenyewe jinsi tulivyo na Nongwa ( Visununu ) vya kuhamishia Masuala ya Kimpira na kuyaleta katika Mambo ya Msingi ( Serious Issues ) hapa Bongo.
Leo GENTAMYCINE nitafurahi zaidi nikiona Wabobezi wakubwa wa Masuala ya Biashara na Masoko hapa JamiiForums wakija na Uchambuzi na Ufafanuzi wao ili nami pia nielimike kwani kwa jinsi ninavyoona sasa wana Yanga SC katika Kurasa zao mbalimbali za Kijamii wanavyotamba kuwa Mfadhili Wao Rostam Aziz kawa Mmiliki wa Kampuni ya Simu ya Tigo huku wakiwazodoa Watu ( Mashabiki ) wa Simba SC kama ( endapo ) Watu wa Tigo hawatalifanyia Kazi na kuliangalia Kiumakini kwa Afya ya Kibiashara linaweza kuja kuwa na Madhara makubwa Kwao kwa Siku za baadae.