Siri ya Kuuwawa Zitto - UWONGO

Siri ya Kuuwawa Zitto - UWONGO

Ukweli Zitto mm nakufagilia ile mbaya mdogo wangu. Niliisoma thread yako ya mkasa wa issue ya dini na kampeni zako kule vijijini jimboni kwako uliyoielekeza kwa speaker nikagundua kichwa yako iko vizuri. So man you call me at any time that we hav much to share anytime from now! Hope we need to talk! 0715314066
 
Nne, Nawashauri viongozi wenzangu wa CHADEMA na hasa wanachama tutumie muda wetu kujenga mshikamano ndani ya chama. Fitna, majungu, uongo, uzandiki nk kamwe havijengi chama. Chama chetu lazima kiwe mfano bora wa kuheshimu demokrasia na haki za binaadamu. Wananchi hawawezi kutoa dola kwa chama chenye mifarakano. Tusiruhusu kugawanywa kwa matakwa ya watu wachache. Tusimamie misingi ya kuanzishwa chama chetu.QUOTE]

Kiukweli nikisoma maandiko au kusikiliza maneno ya hawa vijana watatu wa Chadema (Zitto Kabwe, John Mnyika na Tundu Lissu) huwa napatwa na imani sana na future ya CHADEMA na Tanzania kwa ujumla. Yeyote kati yao anapoongea au kuandika hupati tabu kujua kwamba anachoongea ndicho anachoomanisha. Lakini nasikitika sana watanzania wanawa-underutilize vijana hawa. Kimsingi hawa si wanasiasa ni wana taaluma ya ukombozi wa hali za watanzania. Nami napenda kuongezea hapo aliposema Zitto, sio tu si wakati wa kuleta fitna, uzandiki chuki nk. ndani ya Chadema, bali pia si wakati wake kuleta hayo hata ndani ya jamii ya Watanzania; Wana JF tuwe jukwaa la kutokomeza haya hususan sintofahama na kubezana kwa masuala ya kidini ambayo leo hii yanatumiwa sana humu JF kutugawanya watanzania.
Inatosha kwa JF moderators kutoa ban completely kwa yeyote atakayepost/ au kuchangia chochote ambacho kina ishara ya kukashifu au kui-under value dini nyingine.
Vinginevyo tutazidi kutoa nafasi kwa mchwa wazidi kuitafuna Nchi aisey, kwani kwao mifarakano ya watanzania wao ni furaha.
 
Chanzo cha habari hiyo kwenye gazeti la Mtanzania ni Juliana Shonza, ambaye amekuwa kipenzi cha wana CCM kwa maneno anayozungumza kuhusu chadema

Juliana Shonza: hatutakuamini tena uyasemayo.
Kama uliwahi kumuamini pole sana, sitalajii mtu makini kama wewe mpaka leo hii ulikuwa unasikiliza porojo za kitchen party za Juliana Shonza na huyu Mwampamba.

Ila kwa sababu Chadema inaonesha hakuna wagongaji wazuri sasa CCM ndio amefika siku si nyingi kitumbo mtakiona kimeshajibu maana mpaka sasa nadhani Mtela atakuwa ameshanyanganywa huo Mrupo na vijana machachari wa UVCCM.
 
Aibu yao clouds FM. Kina Kibonde wanavyoshabikia huo umbeya mpaka unaamua kuzima redio. kesho sijui watasemaje?
 
Msalimie Mzee bwana sijui na mimi utanitukana manake ni salamu tu nimekuomba unifikishie
Nilijuaga JF wote ni ma Great Thinker kumbe tuna vilaza kibao sijui tutawasaidiaje ili tuwe tunajadili mambo kwa uhuru. hapa hatuko kuchambua ID tuko kuchambua maada acha ubongolala kama huna point jaribu nyingine mnachosha sana, haya kuanzia sasa nitalikana jina langu kisa ukiliona unaweweseka KILAZA - MBURULA wewe
 
Heshima ya Upande mmoja! Hapa Zitto utapongezwa kwakuwa tu 'umem-save' 'nabii' SLAA. Hawa hawa ndio wanaokuporomoshea matusi kila siku! Lengo lao wakutumie tu kama 'kile kifaa' kisha waku-dump! Sijui kama hulijui hili!

Wewe akili yako bado sana gamba limekuelemea. Fahamu kuwa cdm haiwezi kum-dump zito kwa kuwa ni mbunge halali aliyepigiwa kura na hao unaodhani watam-dump. Kama nyie magamba si wanafiki na mnampenda mbona mliweka mgombea wenu kwenye uchaguzi? Si mngemwacha zito "mnayempenda" apite bila kupingwa?
 
Matendo ya mtu mmoja yasifanyiwe propaganda kama ni malengo ya taasisi.

Nne, Nawashauri viongozi wenzangu wa CHADEMA na hasa wanachama tutumie muda wetu kujenga mshikamano ndani ya chama. Fitna, majungu, uongo, uzandiki nk kamwe havijengi chama. Chama chetu lazima kiwe mfano bora wa kuheshimu demokrasia na haki za binaadamu. Wananchi hawawezi kutoa dola kwa chama chenye mifarakano. Tusiruhusu kugawanywa kwa matakwa ya watu wachache. Tusimamie misingi ya kuanzishwa chama chetu.l

wenye akili zetu tumekusoma. naona mmeanza kujihami hata akitiwa hatiani muwe mmesepa.
cc kwa Mtela mwampamba, kilio cha usaliti.
 
Hili gazeti ningekuwa hata mtendaji wa kata tu ningekomaa lifungiwe.

Kwanza hawa mabindi na hawa wavulana ( maana inaonyesha hawajakuwa), wanastahili wafikishwe mahakamani kwa kula njama ya kuona maisha ya ZITO yanahatarishwa kwa sumu na kisha wakakaa kimya-Ujinga huu nyie mabinti na wavulana mliofukuzwa CDM mkome.
 
heko sana mkuu,umefanya jambo la busara sana kutokea na kusema ukweli.
Sasa naanza kuiona CDM mpya,yenye nguvu,mshikamano na umoja ikianza kujengwa kwa kasi kubwa sana, na kwa mtindo huu uliofanywa nawe kamanda, naomba wale wote wenye chuki binafsi dhidi ya mtu au kiongozi ndani ya CDM waweke pembeni chuki zao na tukijenge chama kwa ajili ya ukombozi wa kweli wa mtanzania. Ningependa kuona huu kuwa mwisho wa malumbano baina ya mtu na mtu ndani ya CDM. Mungu akubariki sana kamanda ZZK,Mungu ibariki CDM, Mungu wabariki watanzania waondokane na utawala dhalimu wa magamba.
 
Mkuu sijui kama ni ya Lwakatare ama ya Ben! All in all ni kwamba Zitto ni mwanasiasa aliyeiva. Na mwanasiasa kama huyu tusingetegemea kwamba aseme ni kweli kilichoandikwa kwenye gazeti. Huyo angekuwa ni mwansiasa uchwara. Nadhani asilimia kubwa ya watu hatukumwelewa Zitto watu wamekimbilia tu katika kanusho
Mara nyingi wanasiasa huwa hawaishii kukanusha tu,bali huiwasisitizia gazeti husika wakanushe la sivyo watawashitaki mahakamani.

Kukanusha ni hatua nzuri tu,however kuna mengine alishawahi kusema humu kuhusiana na issue ya "kutaka kuuwawa".

Kwa namna flani siasa za bongo ni kama mambo ya "abra kadabra","now you see it,now you dont"
 
Chama kilikuwa na muda wa kujiondoa kwenye matendo ya Lwakatare lakini kwa sasa ni vigumu kutofautisha kwa sababu CHADEMA kwa sasa kinatumia resources zake kumtetea mahakamani, kwa maana kuwa, matendo yake bila kujalisha kama mazuri au mabaya, yanaihusu CHADEMA.
Chadema imetoa msaada wa wanasheria ili kuhakikisha kuwa anatendewa haki.

Tusubiri kwanza ithibitike kuwa video ile ni authentic ndiyo tuwaulize kuhusu hatua za kuchukua.

Only if kama una nia nzuri na mageuzi nchini.
 
Zitto wewe sio mtu makini hata siku moja ,kwa uzi huu umekurupuka .Kila siku nasema Watanzania watakufahamu vyema kuwa wewe ni mtu wa aina gani . Sio kila tuhuma zinazokuhusu unatakiwa kuzijibu ,kukaa kimya pia ni busara . Usililolijua ni kama usiku wa giza ,bila kujua umeshajiingiza kwenye mtego wa malumbano na vijana walioaminika kuwa walikuwa wanashirikiana na wewe kwa mabaya ama mazuri pindi wakiwa CDM kabla hawajafukuzwa na kwenda CCM .

"Brother you're falling ",amini usiamini .Kuna uzi umeanzishwa humu muda si mrefu na Mwampamba (kama vile mods wameuondoa ) ila unazunguka kwa kasi twitter na Facebook .Hawa vijana wameanza kukuvua nguo jemedari ,chukua hatua stahiki . Kama ni kweli unayotuhumiwa ya kuihujumu CDM ni kweli rudi kwa Watanzania waombe radhi bado wanaimani kubwa sana na wewe . Ukiona wanakukingia kifua kwa kila baya unalorushiwa jua hawaamini wanaona kama vile ni chuki binafsi .Ila kama unajua na kuamini huna makosa endelea kupambana na kutunishiana misuli na hawa vijana .

Umeandika humfahamu Ben Saanane ,ila wameshaanza kukusuta kuhusu hilo .Huo ni mwanzo tutasikia mengi sana ,hao vijana kwa uzi huu wanaona kama vile unaanza kuwasaliti kwani wanajua wazi kuwa wameanguka ,hawatakubali waanguke peke yao .Utakuwa salama kama ni kweli hukushirikiana nao kwa jambo lolote lililopelekea kwa wao kufukuzwa CDM .Wanavidonda visivyotibika ,walichokiandika leo kupitia Mwampamba imenishangaza sana nanukuu "Ni maneno yanayoudhi na kutoka katika misingi ya kulindana" ,leo maneno yako yanawaudhi kwamba ugomvi wao sasa wanaugeuzia kwako na sio Dr.Slaa na Ben Saanane.Mbaya zaidi wanasema walikula kiapo kutokukuhusha na tuhuma zao iweje wewe unaanza kuwachokonoa ! Wanajitapa wanayo last card inayoweza kukupoteza "Blackmail "

Kila jambo lina mwanzo na mwisho ,baadhi ya mambo huishia pabaya .
I bet the movie has just began bro,you have given it out clearly to him....yetu macho na masikio.
 
Josephine Mushumbusi ID yake ni Josephine. Huyu Josephine03 ni mtu mwingine.
Are you sure of this,Kama zote ni zake je?mimi sioni Kama ni issue this is a free forum for great thinkers she is so free to use any Id na kuchangia atakavyo mahusiano yake hayawezi kumkataza kuchangia kma watu wengine wanavyodai.
 
Ni KInyume kwa sababu siku zote walikuwa wakimsimamia Zitto hili la kuamua kuconfess mbele ya umma limeshammaliza Zitto ni gharama kubwa sana kwake ameipata kujisafisha na kukaa nao mbali ni hapa kwa verified ID na unverified amekuwa akiwatetea leo hawezi kuwakana ,hawezi kuchomoka ,mwisho wa fitina ni fitina wahenga hawakutunga methali toka hewani walijua kweli

na wasiwasi sana na wewe,ni swala la muda tu,ngoja tusubiri.
wanaowatumia leo,hawatawatumia kesho
kwanini msifanye kazi halali,kuliko kutumika,hii si kazi halali.
 
Msalimie Mzee bwana sijui na mimi utanitukana manake ni salamu tu nimekuomba unifikishie

Ukikimbizana na kichaa aliyeiba nguo zako ukiwa unaoga.......................Utaumia sana lakini ndo imekuwa tena
 
Zitto: CHADEMA si pango la wauaji

• ASEMA HAAMINI KAMA DK. SLAA ANAWEZA KUMUUA

na Waandishi wetu




SIKU moja baada ya gazeti la Mtanzania kuandika habari likidai kuwa siri ya kumuua Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA) imefichuka, kiongozi huyo amejitokeza akisema ni uzushi.

Habari hiyo ilidai kuwa ilipangwa Zitto anyweshwe sumu hotelini na kumtaja Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa kuwa ndiye alimtuma kijana Ben Saanane kutimiza mkakati huo.

Hata hivyo, baadhi ya wachambuzi wa kisiasa walisema habari hiyo inayodai tukio hilo lilitokea Mei mwaka jana jijini Dar es Salaam, ilikuwa ni propaganda ya kuhamisha mjadala wa sakata la kuteswa na kuumizwa kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini (TEF), Absalom Kibanda.

Kibanda alitendewa unyama huo Machi 6 mwaka huu, lakini hadi leo vyombo vya dola vimeshindwa kuwakamata wahusika na badala yake yamekuwa yakiibuliwa matukio mbalimbali ili kupoteza ajenda hiyo inayoonesha udhaifu wa kiutendaji wa vyombo hivyo.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Zitto alisema habari hiyo imemletea usumbufu mkubwa kwani ndugu, jamaa, marafiki na wapiga kura wake wamejawa na wasiwasi kwamba anaweza kuuawa.

“Moja, sijawahi katika maisha yangu yote kukutana na mtu anayeitwa Ben Saanane na hivyo hicho kikao ambacho inasemekana nilikuwa naye na akajaribu kunipa sumu hakijawahi kutokea. Imetajwa Hoteli ya Lunch Time ambayo sio tu sijawahi kufika, pia hata siijui ipo wapi,” alisema.

Alifafanua kuwa haijawahi kutokea yeye kufanya kikao cha pamoja na Ben Saanane, Juliana Shonza na Mtela Mwampamba. Hivyo habari iliyoandikwa ni ya kufikirika.

“Pili, siamini kamwe kuwa Katibu Mkuu wa chama changu (Dk. Slaa) anaweza kupanga kuniua maana hana sababu ya kufanya hivyo. Napenda kurudia kusema kwamba mimi ninaamini kuwa kila nafsi itaonja mauti.

“Kila mtu atakufa. Kama nitakufa kwa kuuawa na mtu mwingine ndiyo itakuwa nimeandikiwa hivyo na Mungu. Ndiyo maana hata siku moja silalamiki kuhusu vitisho vya kuuawa. Kama kuna mtu anafikiria kuwa kumuua Zitto ndiyo furaha ya maisha yake atakuwa anajidanganya tu maana Zitto anaweza kufa kimwili, lakini mawazo, fikra na maono yake yataishi tu,” alisema.

Aliongeza kuwa haogopi kufa maana maisha aliyoyachagua ndiyo haya ambayo yamejaa vitisho, kwamba muhimu kwake ni kufanya kazi zake kwa bidii, uhodari na uaminifu.

“Tatu, nawashauri watu ambao wamehama CHADEMA na kuhamia vyama vingine watumie muda wao kujenga vyama vyao badala ya kila siku kuzungumzia masuala ya chama ambacho wao sio wanachama tena.

“Kama mtu kaamua kuhama CHADEMA anapoteza haki ya kujadili masuala ya CHADEMA, maana kama angekuwa anapenda kuyajadili asingehama. Naonya mtu yeyote ambaye anatumia jina langu ili kufanikisha malengo yake ya kisiasa,” alionya Zitto.

Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA (Bara), alisema chama hicho si pango la watesaji wala wauaji, kwamba kuna mwanachama wa chama kingine cha siasa anayedhani kuna mtu ndani ya CHADEMA anapanga mipango ovu aende kwenye vyombo vya sheria kumshtaki.

“Matendo ya mtu mmoja yasifanyiwe propaganda kama ni malengo ya taasisi. Nne, Nawashauri viongozi wa CHADEMA na hasa wanachama tutumie muda wetu kujenga mshikamano ndani ya chama. Fitna, majungu, uongo, uzandiki nk kamwe havijengi chama,” alisema.

Saanane ang’aka

Naye Saanane aliyedaiwa na gezeti hilo kuwa ndiye alikuwa ametumwa kumdhuru Zitto, alisema amesikitishwa jinsi lilivyoshiriki katika dhamira nzima ya kumchafua.

Akizungumza katika ofisi za Tanzania Daima jana, Saanane ambaye ni mjumbe wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) alisema kutokana na habari hiyo ameamua kukutana na wanasheria wake kuangalia hatua za kuchukua ili ukweli ubainike.

“Nasisitiza sijawahi kupanga kumuua mtu yeyote, sijawahi kutumwa kumuua Zitto Kabwe. Nimesikitishwa kuona chombo cha habari kikitumika kwa maslahi binafsi ya kuchafua watu kisiasa,” alisema.

Aliongeza kuwa mara zote alizokutana na Zitto, hawajawahi kufika katika Hoteli ya Lunch Time wakiwa pamoja kama ilivyoelezwa katika gazeti hilo.

Hayo ndo majibu ya Mhe Zitto na Saanane kwa hiyo tafadhalini chambueni matatizo yenu badala ya kupoteza lengo la kumpata aliempiga Kibanda
 
heshima ya upande mmoja! Hapa zitto utapongezwa kwakuwa tu 'umem-save' 'nabii' slaa. Hawa hawa ndio wanaokuporomoshea matusi kila siku! Lengo lao wakutumie tu kama 'kile kifaa' kisha waku-dump! Sijui kama hulijui hili!

omba assignment nyingine, kwa leo zzk amewatibulia...
 
Mh.zitto haya magazeti yetu na vyombo mbalimbali vya serekali vinaendeshwa na skendo/mawazo ya watu humu jamii forums
1)TCRA ilivifungia vyombo kadhaa vya habari baada ya thread kuanzishwa humu
2)gazeti hilo la mtanzania na magazeti mengine yanaendeshwa na habari wanazoziona huku
3)hata kukamatwa kwa lwakatare walipata hiyo clip hukuhuku jamii forums
Kwaiyo nadhani wasikupe shida sana na pili washauri wabadilike kama nchi inaendeshwa na mawazo ya watu hapa jf inasikitisha

Kikubwa mheshimiwa zitto nakushauri hama chadema na utengeneze chama chenye malengo ya kumkomboa mtanzania
Chadema imeshaoza sana .........Take this from me

Vipi unataka ahamie CCM nini?,kila siku mnaambiwa CDM sio mtu lakini vichwa vyenu vimejaa maji hamuelewi
 
Back
Top Bottom