Siri ya Kuuwawa Zitto - UWONGO

Siri ya Kuuwawa Zitto - UWONGO

Naushangaa sana uandishi wa habari wa wanahabari wengi wa Kitanzania!!!!
 
Hakuna sheria ya kuwafikisha mahakamani hawa waandishi uchwara? Kwa habari kama hizi waandishi wa habari wanaendelea kujiweka hatarini kutokana na habari zao zinazochanganisha watu. Hapa naona kama wanabahati sana kwani Zitto angekuwa mtesaji wa kung'oa meno na kucha, wangeipata habari yao!!!!..

Nampongeza Zitto kwa ujasiri wa kukanusha hili ila nashauri kama anaweza kuwachukulia hatua za kisheria afanye hivyo. Gazeti la Mwanahalisi lilifungiwa kutokana na sababu za "uchonganishi", sasa wao Mtanzania wanapatanisha au wanachonganisha?? Na kwa nini na wao wasichukuliwe hatua kwa kosa la uchonganishi???
 
Huu ndiyo mwisho wa shonza na mtela!! Sijui watatumia kete gani sasa!!?
 
kwa wanafalsafa na wataalamu wa fasihi, watabaini kuwa uzi wa zitto umejaa falsafa ya hali ya juu. anaonekana kukanusha lkn kwa undani anasema kuwa kama ni kweli basi itakua imeandikwa na Mungu.

kwa kusoma juujuu, zitto amemuokoa slaa na tope la ugaidi ambalo lilikua limeanza kumchafua. kisiasa ana sababu zake anazozijua zilizomfanya amuokoe mzee.

TAHADHARI KWA ZITTO
kamanda zitto ni kwa mara ya kwanza naona zaidi ya 90% ya wachangiaji wakikuunga mkono! wamekuunga mkono kwa asilimia kubwa KWA SABABU UMEMUOKOA SLAA. habari ya leo ya gazeti la mtanzania ni kubwa sana! weka maanani kuwa una maadui wengi chamani
 
Nimependa ulivyoandika lkn tahadhari inafaa usipewe sumu then ukasema wacha niinywe Mungu atanilinda! Utaangamia ohoooo!
 
Zitto anapendwa sana na watu, akiwa mgombea wa kiti cha urais kwa kupitia CHADEMA, CCM tutakuwa na wakati mgumu sana.

Haimaanishi hivyo hata siku moja, Watu tunapenda CDM na Viongozi wake wake wote usikurupuke mkuu
 
kwa wanafalsafa na wataalamu wa fasihi, watabaini kuwa uzi wa zitto umejaa falsafa ya hali ya juu. anaonekana kukanusha lkn kwa undani anasema kuwa kama ni kweli basi itakua imeandikwa na Mungu.

kwa kusoma juujuu, zitto amemuokoa slaa na tope la ugaidi ambalo lilikua limeanza kumchafua. kisiasa ana sababu zake anazozijua zilizomfanya amuokoe mzee.

TAHADHARI KWA ZITTO
kamanda zitto ni kwa mara ya kwanza naona zaidi ya 90% ya wachangiaji wakikuunga mkono! wamekuunga mkono kwa asilimia kubwa KWA SABABU UMEMUOKOA SLAA. habari ya leo ya gazeti la mtanzania ni kubwa sana! weka maanani kuwa una maadui wengi chamani

Ni wewe wasema
 
Naipenda chadema kwa sababu ina watu makini mno akiwemo zitto . Mhariri wa mtanzania lazima atakuwa anajiona kama amejisaidia nguoni
 
Zitto wewe sio mtu makini hata siku moja ,kwa uzi huu umekurupuka .Kila siku nasema Watanzania watakufahamu vyema kuwa wewe ni mtu wa aina gani . Sio kila tuhuma zinazokuhusu unatakiwa kuzijibu ,kukaa kimya pia ni busara . Usililolijua ni kama usiku wa giza ,bila kujua umeshajiingiza kwenye mtego wa malumbano na vijana walioaminika kuwa walikuwa wanashirikiana na wewe kwa mabaya ama mazuri pindi wakiwa CDM kabla hawajafukuzwa na kwenda CCM .

"Brother you're falling ",amini usiamini .Kuna uzi umeanzishwa humu muda si mrefu na Mwampamba (kama vile mods wameuondoa ) ila unazunguka kwa kasi twitter na Facebook .Hawa vijana wameanza kukuvua nguo jemedari ,chukua hatua stahiki . Kama ni kweli unayotuhumiwa ya kuihujumu CDM ni kweli rudi kwa Watanzania waombe radhi bado wanaimani kubwa sana na wewe . Ukiona wanakukingia kifua kwa kila baya unalorushiwa jua hawaamini wanaona kama vile ni chuki binafsi .Ila kama unajua na kuamini huna makosa endelea kupambana na kutunishiana misuli na hawa vijana .

Umeandika humfahamu Ben Saanane ,ila wameshaanza kukusuta kuhusu hilo .Huo ni mwanzo tutasikia mengi sana ,hao vijana kwa uzi huu wanaona kama vile unaanza kuwasaliti kwani wanajua wazi kuwa wameanguka ,hawatakubali waanguke peke yao .Utakuwa salama kama ni kweli hukushirikiana nao kwa jambo lolote lililopelekea kwa wao kufukuzwa CDM .Wanavidonda visivyotibika ,walichokiandika leo kupitia Mwampamba imenishangaza sana nanukuu "Ni maneno yanayoudhi na kutoka katika misingi ya kulindana" ,leo maneno yako yanawaudhi kwamba ugomvi wao sasa wanaugeuzia kwako na sio Dr.Slaa na Ben Saanane.Mbaya zaidi wanasema walikula kiapo kutokukuhusha na tuhuma zao iweje wewe unaanza kuwachokonoa ! Wanajitapa wanayo last card inayoweza kukupoteza "Blackmail "

Kila jambo lina mwanzo na mwisho ,baadhi ya mambo huishia pabaya .
 
Mh.zitto haya magazeti yetu na vyombo mbalimbali vya serekali vinaendeshwa na skendo/mawazo ya watu humu jamii forums
1)TCRA ilivifungia vyombo kadhaa vya habari baada ya thread kuanzishwa humu
2)gazeti hilo la mtanzania na magazeti mengine yanaendeshwa na habari wanazoziona huku
3)hata kukamatwa kwa lwakatare walipata hiyo clip hukuhuku jamii forums
Kwaiyo nadhani wasikupe shida sana na pili washauri wabadilike kama nchi inaendeshwa na mawazo ya watu hapa jf inasikitisha

Kikubwa mheshimiwa zitto nakushauri hama chadema na utengeneze chama chenye malengo ya kumkomboa mtanzania
Chadema imeshaoza sana .........Take this from me

wewe nae wakumshauri zito! au unajishadua tu kuwa unamshauri ahame chama,,,,mm nadhani wewe ndo unahitaji ushauri wa zito
 
Ninachofahamu ni kuwa serikali ya masalia iliyokuwa inaongozwa na ZZK ilipinduliwa na Ben Saanane kama ambavyo Serikali ya JK ilivyopinduliwa na RICHMOND/DOWANS ya Rostam. Kama ambavyo haiingii akilini JK anaposema hamfahamu Rostam ndivyo hivyohivyo haiingii akilini ZZK anaposema hamfahamu aliyepindua kikundi chake cha Masalia.
nadhani mnachokitafuta kitakuja tu,ila msiwe wa kwanza kuja JF na kuanza kupiga kelee,maana watanzania tumewazoea
utasikia ooooooooooooooooooh timu yetu kwa sasa safi inashinda tu haina wakongwe wengi,likitokea la kutokea ,utasikia ohhhhhhhhhhhhhhhhhh tumehujumiwa timu yetu wakonge wachache,vijana wengi,huwa hamueleweki nini mnataka,tupo JF tunawasubiri kwa hamu wazee wa kulamba matapishi
 
HUU NDIYO UHURU WA MAWAZO,
SIKU ZOTE NAAMINI GAZETI LA MTANZANIA HALIWEZI KUANDIKA HABARI ZA KWELI KWA SABABU KUANZISHWA KWAKE HAKUKUWA NA CHEMBECHEMBE ZA UKWELI:bange:
 
Huyo ni mdogo wangu kwani mimi nina miaka zaidi ya 60 na yeye anakadiriwa kuwa na miaka 39 and I am used to calling a spade a spade labda wewe mtoto wako akipata cheo anabadilika jina na kuitwa kaka yako. Hiyo ni nidhamu ya kwenu. Kwetu mdogo wako ni mdogo wako bila kujali cheo, pesa au kitu kingine chochote. Nashindwa kujadili sana kwa kuwa sielewi upeo wako lakini dalili zinaonyesha kuwa upeo wako ni mdogo kwa kuwa upo ushaihidi wa kiutafiti kuwa wasiokuwa na kitu kichwani huwaona wenzao wenye nazo kama ndiyo hamnazo kumbe ni kinyume chake. Wasio na staha hata maneno ya staha huona kama ni matusi. Nikubaliane na wewe kuwa unazo akili zinazokutosha wewe kwa mambo yako.
kumuita dogo....nk.... sidhani kama kichwani kwako pamekaa vizuri
 
MWAKALINGA y.r katika watu walisema ukweli nakuunga mkono. Zitto bado anamtihani mzito sana na ndipo atakapogundua kuwa mtaji wa siasa ni nguvu ya umma na siyo kikundi cha watu wachache wanaoweza kuhadaa umma kwa muda.

Naamini hadaa haiwezi kudumu. Katika saga hili la Beni,Zitto na waliokuwa Masalia tutasikia mengi sana ambayo kama ulivyomuasa yanaweza kumuweka Zitto uchi!
 
Last edited by a moderator:
Hongera ZZK na uongozi mzima wa cdm, mmeonyesha ukomavu na pia mmeiepusha cdm na mtego wa siasa za kitoto, ambao mbele ungetengenezewa filamu tata, Bavicha iwaonye vijana wake ie,Ben kuwa na kiasi/kuchagua linapokuja suala la kumuongelea kiongozi wako hadharani...pia heche na sugu wachunge 'uhuru' wao hapa dom (desert) wasijetengenezewa kashfa, kila kiongozi wa cdm awe makini na kuitafakari kauli ya JK "Tutashambulia til 2015"...BAVICHA iwekeze na ivune ktk m4c hasa vijijini,makombe ya mbuzi,mashindano ya ngom nk..CDM INAWEZA, Amina.
 
Kauli kama hizi zisizo na kupulizia upepo kidonda ndio tunazitaka... Hongera kwa maelezo yako na ombi langu kwenu CDM na wanasiasa vijana achane siasa za kizamani za fitina na kuchafuana ni siasa za magumashi na watoto wa vijiweni wanaoganga njaa.. Take politics as proffessional na mtuonyeshe tofauti..
Hivi hakuna maadili ya kuwa mwanasiasa au kiongozi maana hawa wanasiasa wengi vijana wanafuata upuuzi ule ule uliofanywa na wachwara na vilaza wa siasa, sioni tofauti... wa siasa za maji taka..

Waone kama akina Nape na Kaka yake Mgulu na Hao vyanzo vya habari Mwampamba, Lukosi, Shoziii.. aibuuu wako kwenye chama kikubwa barani afrika na chenye historia na misingi ya maana but the way they talk, their action, hawaitendei haki CCM. U should learn from senior CCM leader and ur own our brother Zitto, simsifii ila kwa hili na kusimamia anachokiamini amewacha mbali sanaa.

Hawa watu tusipowambia ukweli tutakuja kupata viongozi wanazi na vilaza sanaa baadaye maana system yetu ilivyo usishangae siku moja ukasikia kati ya hawa wachumia tumbo wamepewa uongozi serikali.. Na ndio maana vijana vilaza wachumia tumbo wanaingia kwenye vyama vya upinzani ili wapate umaarufu utakao wasidia kuhongwa nafasi za uchumia tumbo CCM... hAWA SIO WANASIASA NI VIBARAKA.. WASHAONA DILI MJINI AJIRA NGUMU NA WANATAKA WASUKUME VOGUE NA MAGARI MAZURI MAZURIII..
 
Zitto wewe sio mtu makini hata siku moja ,kwa uzi huu umekurupuka .Kila siku nasema Watanzania watakufahamu vyema kuwa wewe ni mtu wa aina gani . Sio kila tuhuma zinazokuhusu unatakiwa kuzijibu ,kukaa kimya pia ni busara . Usililolijua ni kama usiku wa giza ,bila kujua umeshajiingiza kwenye mtego wa malumbano na vijana walioaminika kuwa walikuwa wanashirikiana na wewe kwa mabaya ama mazuri pindi wakiwa CDM kabla hawajafukuzwa na kwenda CCM .

"Brother you're falling ",amini usiamini .Kuna uzi umeanzishwa humu muda si mrefu na Mwampamba (kama vile mods wameuondoa ) ila unazunguka kwa kasi twitter na Facebook .Hawa vijana wameanza kukuvua nguo jemedari ,chukua hatua stahiki . Kama ni kweli unayotuhumiwa ya kuihujumu CDM ni kweli rudi kwa Watanzania waombe radhi bado wanaimani kubwa sana na wewe . Ukiona wanakukingia kifua kwa kila baya unalorushiwa jua hawaamini wanaona kama vile ni chuki binafsi .Ila kama unajua na kuamini huna makosa endelea kupambana na kutunishiana misuli na hawa vijana .

Umeandika humfahamu Ben Saanane ,ila wameshaanza kukusuta kuhusu hilo .Huo ni mwanzo tutasikia mengi sana ,hao vijana kwa uzi huu wanaona kama vile unaanza kuwasaliti kwani wanajua wazi kuwa wameanguka ,hawatakubali waanguke peke yao .Utakuwa salama kama ni kweli hukushirikiana nao kwa jambo lolote lililopelekea kwa wao kufukuzwa CDM .Wanavidonda visivyotibika ,walichokiandika leo kupitia Mwampamba imenishangaza sana nanukuu "Ni maneno yanayoudhi na kutoka katika misingi ya kulindana" ,leo maneno yako yanawaudhi kwamba ugomvi wao sasa wanaugeuzia kwako na sio Dr.Slaa na Ben Saanane.

Kila jambo lina mwanzo na mwisho ,baadhi ya mambo huishia pabaya .

mwampamba ni msaliti,,,mwampamba sio level ya ziti kisiasa,,,,mwampamba anamtumkia kafiri ccm ili apate riziki yake,,,,mwampamba sio msemaji wa zito wala chadema,,,mwampamba hawezi kumtishia zito kwa stori za kupika eti atazidi kusema kadri atakavyo hitajika! ha ha ha mwambie hiyo ni danganya toto anawadanganya magamba ili azidi kuwalia mihela yao kwa hidaya zake ila kwa vile mjinga ndo waliwalo ngoja aendelee kuwalia
 
Mimi nitakuwa wa mwisho kukuamini kutokana na kauli zako zenye utata juu ya chama chako na viongozi wake wa juu. Wewe umekuwa ukimsifia JK kuliko viongozi wa chama. Mawasiliano yako na UWT na matukio mbalimbali ya kuihujumu Chadema yananifanya nisite kukuamini. Kama unatubu dhambi sasa basi fanya hivyo kwa dhati bila kurudi nyuma na kama unatuhadaa Watanzania wa sasa si wajinga watakukana.
 
Back
Top Bottom