Siri ya Kuuwawa Zitto - UWONGO

Siri ya Kuuwawa Zitto - UWONGO

At a time like this ,this is important and crucial message. It is only for intellectual pple like u. Ahsante sana u r my role model in whom i hav never lost my trust.wabeja sana
 
Gazeti la mtanzania linatuka kama toilet paper nimelisomna leo ni habari za cahdema chadema tena zinajirudia rudia kwa agle tofauti tofauti
 
Hiyo kauli ya Zitto inaonesha kuwa kuna mfarakano ndani ya CHADEMA. Kwa vile wewe ni mfuatiliaji wa posts za humu JF utakuwa shuhuda kwamba wengi wa machadema anapozungumzwa Zitto huwa wanamsema vibaya ikiwa ni pamoja na kumtukana. Cha ajabu sijawahi kusikia kiongozi nwingine wa CHADEMA akimtetea Zitto.

Pitia pitia majina ya wachangiaji leo, kuna baadhi ya wanachadema maarufu hawamo kwa ID zao kwa kuogopa aibu!

Yuwapi Mwita Maranya?

amebaki lwesye shardcole kaonyesha ushabiki
 
Hivi habari za kina Wema sepetu,Diamond na wapumbavu wengne zmekwisha..mana hawa waandish ndo habari wanazozijua.
 
Wewe unaweza ukawa zaidi ya muongo. How did you calculate your 6%, I thought it is 0%?

Halafu turudi hapa:

Viongozi wa CHADEMA si wa kweli?
Wewe ndio kilaza namba moja,unamtetea huyo aliyehongwa suti nne kilimanjaro???Mpaka sasa ni miaka 8 amefikisha 6% ya ahadi zake utamwitaje????Refer kuna uzi ulikuwa hapa jamvini jana(anayeweza kumwekea huyu kilaza bocho huo uzi msaada pliz)
 
Katika gazeti la Mtanzania toleo na. 7269 la Jumatano Machi 27, 2013 kuna habari yenye kichwa chenye maneno ‘SIRI YA KUUWAWA ZITTO YAFICHUKA’ na vichwa vidogo ‘yadaiwa ilipangwa anyweshwe sumu hotelini’ dk. Slaa atajwa kumtuma Saanane kummaliza’. Habari hii imeniletea usumbufu mkubwa kwani ndugu, jamaa, marafiki na wapiga kura wangu, wamejazwa na wasiwasi mkubwa sana kwamba ninaweza kuuwawa.

Napenda kusema yafuatayo:

Moja, sijawahi katika maisha yangu yote kukutana na mtu anayeitwa Ben Saanane na hivyo hicho kikao ambacho inasemekana nilikuwa naye na akajaribu kunipa sumu hakijawahi kutokea. Imetajwa Hoteli ya Lunch Time ambayo sio tu sijawahi kufika, pia hata siijui ipo wapi. Haijawahi kutokea mimi kufanya kikao cha pamoja na Ben Saanane, Juliana Shonza na Mtela Mwampamba. Hivyo habari iliyoandikwa ni ya kufikirika na hivyo naomba mwandishi ahakikishe kuwa vyanzo vyake vya habari vimempa habari sahihi.

Pili, Siamini kamwe kuwa Katibu Mkuu wa chama changu anaweza kupanga kuniua maana hana sababu ya kufanya hivyo. Napenda kurudia kusema kwamba mimi ninaamini kuwa kila nafsi itaonja mauti. Kila mtu atakufa. Kama nitakufa kwa kuuwawa na mtu mwingine ndio itakuwa nimeandikiwa hivyo na Mungu. Ndio maana hata siku moja silalamiki kuhusu vitisho vya kuuwawa nk. Kama kuna mtu anafikiria kuwa kumuua Zitto ndio furaha ya maisha yake atakuwa anajidanganya tu maana Zitto anaweza kufa kimwili lakini mawazo, fikra na maono ya Zitto yataishi tu. Siogopi kufa maana maisha niliyoyachagua ndio haya ambayo yamejaa vitisho. Muhimu kwangu ni kufanya kazi zangu kwa bidii, uhodari na uaminifu. Siku zote nitasimamia ukweli bila kujali uchungu wa ukweli huo.

Tatu, nawashauri watu ambao wamehama CHADEMA na kuhamia vyama vingine watumie muda wao kujenga vyama vyao badala ya kila siku kuzungumzia masuala ya chama ambacho wao sio wanachama tena. Kama mtu kaamua kuhama CHADEMA anapoteza haki ya kujadili masuala ya CHADEMA maana kama angekuwa anapenda kuyajadili asingehama. Naonya mtu yeyote ambaye anatumia jina langu ili kufanikisha malengo yake ya kisiasa. CHADEMA sio pango la watesaji wala wauaji. Kama kuna mwanachama wa chama kingine cha siasa anayedhani kuna mtu ndani ya CHADEMA anapanga mipango ovu aende kwenye vyombo vya sheria kumshtaki. Matendo ya mtu mmoja yasifanyiwe propaganda kama ni malengo ya taasisi.

Nne, Nawashauri viongozi wenzangu wa CHADEMA na hasa wanachama tutumie muda wetu kujenga mshikamano ndani ya chama. Fitna, majungu, uongo, uzandiki nk kamwe havijengi chama. Chama chetu lazima kiwe mfano bora wa kuheshimu demokrasia na haki za binaadamu. Wananchi hawawezi kutoa dola kwa chama chenye mifarakano. Tusiruhusu kugawanywa kwa matakwa ya watu wachache. Tusimamie misingi ya kuanzishwa chama chetu.


=============


Thread inayoongelea kilichoandikwa na Mtanzania hii hapa - https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ajwa-kumtuma-ben-saanane-kummaliza-zitto.html

Ni kama nimeku-overunderstand hapo kwenye red, au ni uelewa wangu mdogo
 
Kama kweli kauli yako ni ya dhati achana na usaliti kwa chama chako maana hata ukibisha vipi wewe ni mfadhili wa iliyokuwa hujama ya chama kwa masalia hivyo kama unatubu fanya hivyo kwa dhati kabisa. Kama utajifanya kichwa ngumu Watanzania wa sasa si wajinga na hao unaowatumikia wanaweza kukusaliti vilevile ukimaliza kazi yao au ukishindwa kuikamilisha.
 
bora hata umetufafanulia...mana nilishaanza kupoteza iman na chadema
 
kama uliwasoma hao wote vizuri wala hulikuwa huna haja ya kufikiri hivi kwani wao wote walikuwa wanataka kuonesha kuwa hizi habari za sumu ni uzushi wa wakina Mwampamba! Na ndio maana saanane alitaka wahojiwe ili ukweli ujulikane lakini hakuna haja tena maana muhusika mkuu amekanusha hizo tuhumu na kuziita uongo!

Naona hapo umejaribu kumuelewa tofauti josephine lakini alikuwa anasimamia kwenye ukweli kuwa huu ni uzushi na kweli ndugu yetu zitto ametueleza mwenyewe na sioni haja ya kukuza mambo haya kiasi hiki!
Mkuu naomba tukubali kutokubaliana.
Hiyo thread ilikuwa mahsusi kuhusu tuhuma za Lwakatare kuhusiana na kesi ya ujasusi ambapo Ben Saanane alijaribu kutaka hao aliowataja wakahojiwe na polisi.

Yaani una maana Josephine alikuwa anasema Mh. Zitto ni mzushi, labda sikuelewi vizuri, kwa sababu huo ujumbe wa kwanza alikuwa anamwabis Ben kuwa, wale wati aliowataja ndiyo wame-engineer sarakasi la Lwakatare.
 
piga, ua, garagaza.... kamanda na kiongozi wangu ni zitoooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo
 
This is very good Zito, umeanza kukomaa, I like it very much. Umenikuna dogo. Big up
 
ban saanane ni kirusi hatari pale chdm.
afukuzweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Aibu ya Mwigulu, aibu ya zoka(tiss) aibu ya masalia, aibu ya waandishi wachumia tumbo, aibu ya sisiem.
Big up mheshimiwa Zitto, tuko pamoja na makamanda wote watetea ukombozi wa mnyonge wa tanzania. Tutawatii makamanda wote na tutasimama kuwatetea kwa lolote na kwa wakati wowote.
VIVA CHADEMA MKOMBOZI WA KUTOKA KWA PILI. YAANI BAADA YA KUTOKA KWA KWANZA MIKONONI MWA MKOLONI MWEUPE, TAIFA TUNAHITAJI KUTOKA KWA PILI MIKONONI MWA MKOLONI MWEUSI CICIEM.
.
 
Back
Top Bottom