Siri ya Kuuwawa Zitto - UWONGO

Siri ya Kuuwawa Zitto - UWONGO

LOGIC
wapo wale wawazao mema kuanzia nafsini mwao hadi kwenye jamii yao, hawa huitwa wenye hekima
kuna wale wawazao njama, visa,chuki, machafuko na hata vita,hawa tunawaita washenzi
''

CONCLUSION: ZITTO : MWENYE HEKIMA
DR.SLAA: MSHENZI

LOGICALLY PROVED.

ww unasemaje????????????????????????????

Hapo kwenye RED amekukosea nini?Wakati mwingine tunajichumia dhambi zisizo za msingi ndugu.
 
Katika gazeti la Mtanzania toleo na. 7269 la Jumatano Machi 27, 2013 kuna habari yenye kichwa chenye maneno ‘SIRI YA KUUWAWA ZITTO YAFICHUKA’ na vichwa vidogo ‘yadaiwa ilipangwa anyweshwe sumu hotelini’ dk. Slaa atajwa kumtuma Saanane kummaliza’. Habari hii imeniletea usumbufu mkubwa kwani ndugu, jamaa, marafiki na wapiga kura wangu, wamejazwa na wasiwasi mkubwa sana kwamba ninaweza kuuwawa.

Napenda kusema yafuatayo:

Moja, sijawahi katika maisha yangu yote kukutana na mtu anayeitwa Ben Saanane na hivyo hicho kikao ambacho inasemekana nilikuwa naye na akajaribu kunipa sumu hakijawahi kutokea. Imetajwa Hoteli ya Lunch Time ambayo sio tu sijawahi kufika, pia hata siijui ipo wapi. Haijawahi kutokea mimi kufanya kikao cha pamoja na Ben Saanane, Juliana Shonza na Mtela Mwampamba. Hivyo habari iliyoandikwa ni ya kufikirika na hivyo naomba mwandishi ahakikishe kuwa vyanzo vyake vya habari vimempa habari sahihi.

Pili, Siamini kamwe kuwa Katibu Mkuu wa chama changu anaweza kupanga kuniua maana hana sababu ya kufanya hivyo. Napenda kurudia kusema kwamba mimi ninaamini kuwa kila nafsi itaonja mauti. Kila mtu atakufa. Kama nitakufa kwa kuuwawa na mtu mwingine ndio itakuwa nimeandikiwa hivyo na Mungu. Ndio maana hata siku moja silalamiki kuhusu vitisho vya kuuwawa nk. Kama kuna mtu anafikiria kuwa kumuua Zitto ndio furaha ya maisha yake atakuwa anajidanganya tu maana Zitto anaweza kufa kimwili lakini mawazo, fikra na maono ya Zitto yataishi tu. Siogopi kufa maana maisha niliyoyachagua ndio haya ambayo yamejaa vitisho. Muhimu kwangu ni kufanya kazi zangu kwa bidii, uhodari na uaminifu. Siku zote nitasimamia ukweli bila kujali uchungu wa ukweli huo.

Tatu, nawashauri watu ambao wamehama CHADEMA na kuhamia vyama vingine watumie muda wao kujenga vyama vyao badala ya kila siku kuzungumzia masuala ya chama ambacho wao sio wanachama tena. Kama mtu kaamua kuhama CHADEMA anapoteza haki ya kujadili masuala ya CHADEMA maana kama angekuwa anapenda kuyajadili asingehama. Naonya mtu yeyote ambaye anatumia jina langu ili kufanikisha malengo yake ya kisiasa. CHADEMA sio pango la watesaji wala wauaji. Kama kuna mwanachama wa chama kingine cha siasa anayedhani kuna mtu ndani ya CHADEMA anapanga mipango ovu aende kwenye vyombo vya sheria kumshtaki. Matendo ya mtu mmoja yasifanyiwe propaganda kama ni malengo ya taasisi.

Nne, Nawashauri viongozi wenzangu wa CHADEMA na hasa wanachama tutumie muda wetu kujenga mshikamano ndani ya chama. Fitna, majungu, uongo, uzandiki nk kamwe havijengi chama. Chama chetu lazima kiwe mfano bora wa kuheshimu demokrasia na haki za binaadamu. Wananchi hawawezi kutoa dola kwa chama chenye mifarakano. Tusiruhusu kugawanywa kwa matakwa ya watu wachache. Tusimamie misingi ya kuanzishwa chama chetu.

=============

Thread inayoongelea kilichoandikwa na Mtanzania hii hapa - https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ajwa-kumtuma-ben-saanane-kummaliza-zitto.html

Siasa kweli ngumu. Naona mkuu Zitto umekanusha lakini pia umetuma ujumbe Mzitto.
 
CCM mpango wao wa kuwatumia vijana {Juliana Shonza, Mwampamba na wengine wengi} pamona na idara ya Usalama ktk harakati za kudhoofisha vyama vya upinzani umeshadhihirika kufikia ukomo wa kuleta matunda wanayo kusudia.

Watanzania wanataka mageuzi CCM imeshindwa kutatua matatizo ya kiuchumi na kijamii yanayoukabili umma wa watanzania. CCM inahitaji chama mbadala kitakacjho watoa Watanzania toka ktk dimbwi hili la Matatizo.
 
Matendo ya Lwakatare yasifanywe ni malengo ya taasisi.
Mkuu sijui kama ni ya Lwakatare ama ya Ben! All in all ni kwamba Zitto ni mwanasiasa aliyeiva. Na mwanasiasa kama huyu tusingetegemea kwamba aseme ni kweli kilichoandikwa kwenye gazeti. Huyo angekuwa ni mwansiasa uchwara. Nadhani asilimia kubwa ya watu hatukumwelewa Zitto watu wamekimbilia tu katika kanusho
 
hahaha..naona mkuu umeshitukia deal..hawa jamaa ben na zito wanapersonal bifu,au huyu ben ni proxy.yaani there is someone behind this guy and he is pulling strings.
Huyu jamaa hana kazi inayotambuliwa na CHADEMA kikatiba lakini unapoona watu kama 'First Lady' wa serikali itakayoundwa na CHADEMA wanampa nguvu na kukubali kwa kile anachokifanya, hapo ndipo unaanza kuelewa kwa nini anakuwa na ubavu wa kurumbana na kukwaruzana Mh. zitto.

Haya chini ni maneno ya 'First Lady'. Sasa sijui kama naye 'First Lady' ni PROXY.
Ben,

Hao wote ndiyo wahusika wa hii move,time will tell.kunawakati nawaza kwanini Mungu amekuwa kmya hivi,Lakini napata jibu,Yeye ni Mungu.

Kama Mungu aishivyo,itajulikana yupo Mungu
Waache waendelee kusema na kuandika.
Pasco ,
upande wangu najua unatetea kula yako.
my brother,kaa mbali na ushabiki,japo najua unaweza kuwa moja ya watu wanaojua haya,kwani si ninyi ndiyo mnahusishwa.

Look here,sikio la Mungu si zito kuzikia.
Haijalishi mtaonga nini,

huu si mda wa kupepesa maneno.
mtaongea yote,ila nimeeleweka.
Josephine ni Josephine, nitasimamia nachoamini.
No matter what,.

This time sitakaa kimya,mnawatesa watu kwa upuuzi wenu,bado nasema,unahusika.
Hakuna anayezaliwa huku akijua atakuwa nani,look here,nitasimamia nachokiamini nasisitiza.
maneno yenu hayatazuia mpango wa Mungu kwenye maisha yangu,what do i mean,what you spoke are the results.

hapa issue nani muhusika,umenisoma umenielewa,huu si wakati wa kumungunya maneno.
lastly,time is over the bell is ringing,everything ,i mean everything shall be out.
Sikiliza Maandalizi ya moyo ni ya mwanadamu,lakini jawabu la ulimi ni la Mungu.

kutoka kwenye thread hii,
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...nza-nape-mchange-na-mwampamba-wahojiwe-6.html
 
asante sana mkuu Zitto kwa ufafanuzi wako haya magazeti ya udaku part II yanapotosha sana umma wa watz
 
Kamanda umepanic,ila nshakusoma wewe nani mbona unapanic hiv.utajitaja muda si mrefu shauri yako.
Kumbe tuko wengi. Wewe pia umeunganisha Dots.

Hakuna kitu kibaya kama kupambana na ukweli. Mwishowe atasahau hata mwelekeo na kujikuta anamwaga mchele kwenye kuku wa hapa JF.
 
Umefanya mambo mazuri ZITTO hongera sana kiongozi,umewaumbua sana akina shonza,mwampamba na akina saanane utazani saa ya ukutani.
 
Kumbe tuko wengi. Wewe pia umeunganisha Dots.

Hakuna kitu kibaya kama kupambana na ukweli. Mwishowe atasahau hata mwelekeo na kujikuta anamwaga mchele kwenye kuku wa hapa JF.
Nilimwambia yeye na first lady wake kunakaribia kukucha na watajita wenywe bila hata kuulizwa.
 
Matendo ya Lwakatare yasifanywe ni malengo ya taasisi.
Chama kilikuwa na muda wa kujiondoa kwenye matendo ya Lwakatare lakini kwa sasa ni vigumu kutofautisha kwa sababu CHADEMA kwa sasa kinatumia resources zake kumtetea mahakamani, kwa maana kuwa, matendo yake bila kujalisha kama mazuri au mabaya, yanaihusu CHADEMA.
 
Heshma yako mkuu zitto.Nakutakia kila la khery katika ujenzi wa chama chetu. Ila nakuomba zingatia ushauri mzuri waliokupatia wanajukwaa,kazi kwako kuchuja upi mzuri na unaofaa kwa chama chako na viongozi wenzio katika ujenzi imara wa chama chetu cha CHADEMA. Pia jaribu kujiweka wazi u pande gani katika chama kuliko unavyofanya sasa kuacha mambo yanafika mbali mbaka yanafikia atua ya kuchafua chama. Kwa style iyo ndio maana wanajamiiforums wanakuona wewe msaliti dhidi ya chama na viongozi wenzio. Pls jitahidi kuwa mkali pale unapoona kuna mambo yanayokuchafua wewe na chama chetu. Pia waangalie kwa makini wanaokupamba.
 
Bravo ZittO!!!!
Katika gazeti la Mtanzania toleo na. 7269 la Jumatano Machi 27, 2013 kuna habari yenye kichwa chenye maneno ‘SIRI YA KUUWAWA ZITTO YAFICHUKA’ na vichwa vidogo ‘yadaiwa ilipangwa anyweshwe sumu hotelini’ dk. Slaa atajwa kumtuma Saanane kummaliza’. Habari hii imeniletea usumbufu mkubwa kwani ndugu, jamaa, marafiki na wapiga kura wangu, wamejazwa na wasiwasi mkubwa sana kwamba ninaweza kuuwawa.

Napenda kusema yafuatayo:

Moja, sijawahi katika maisha yangu yote kukutana na mtu anayeitwa Ben Saanane na hivyo hicho kikao ambacho inasemekana nilikuwa naye na akajaribu kunipa sumu hakijawahi kutokea. Imetajwa Hoteli ya Lunch Time ambayo sio tu sijawahi kufika, pia hata siijui ipo wapi. Haijawahi kutokea mimi kufanya kikao cha pamoja na Ben Saanane, Juliana Shonza na Mtela Mwampamba. Hivyo habari iliyoandikwa ni ya kufikirika na hivyo naomba mwandishi ahakikishe kuwa vyanzo vyake vya habari vimempa habari sahihi.

Pili, Siamini kamwe kuwa Katibu Mkuu wa chama changu anaweza kupanga kuniua maana hana sababu ya kufanya hivyo. Napenda kurudia kusema kwamba mimi ninaamini kuwa kila nafsi itaonja mauti. Kila mtu atakufa. Kama nitakufa kwa kuuwawa na mtu mwingine ndio itakuwa nimeandikiwa hivyo na Mungu. Ndio maana hata siku moja silalamiki kuhusu vitisho vya kuuwawa nk. Kama kuna mtu anafikiria kuwa kumuua Zitto ndio furaha ya maisha yake atakuwa anajidanganya tu maana Zitto anaweza kufa kimwili lakini mawazo, fikra na maono ya Zitto yataishi tu. Siogopi kufa maana maisha niliyoyachagua ndio haya ambayo yamejaa vitisho. Muhimu kwangu ni kufanya kazi zangu kwa bidii, uhodari na uaminifu. Siku zote nitasimamia ukweli bila kujali uchungu wa ukweli huo.

Tatu, nawashauri watu ambao wamehama CHADEMA na kuhamia vyama vingine watumie muda wao kujenga vyama vyao badala ya kila siku kuzungumzia masuala ya chama ambacho wao sio wanachama tena. Kama mtu kaamua kuhama CHADEMA anapoteza haki ya kujadili masuala ya CHADEMA maana kama angekuwa anapenda kuyajadili asingehama. Naonya mtu yeyote ambaye anatumia jina langu ili kufanikisha malengo yake ya kisiasa. CHADEMA sio pango la watesaji wala wauaji. Kama kuna mwanachama wa chama kingine cha siasa anayedhani kuna mtu ndani ya CHADEMA anapanga mipango ovu aende kwenye vyombo vya sheria kumshtaki. Matendo ya mtu mmoja yasifanyiwe propaganda kama ni malengo ya taasisi.

Nne, Nawashauri viongozi wenzangu wa CHADEMA na hasa wanachama tutumie muda wetu kujenga mshikamano ndani ya chama. Fitna, majungu, uongo, uzandiki nk kamwe havijengi chama. Chama chetu lazima kiwe mfano bora wa kuheshimu demokrasia na haki za binaadamu. Wananchi hawawezi kutoa dola kwa chama chenye mifarakano. Tusiruhusu kugawanywa kwa matakwa ya watu wachache. Tusimamie misingi ya kuanzishwa chama chetu.

=============

Thread inayoongelea kilichoandikwa na Mtanzania hii hapa - https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ajwa-kumtuma-ben-saanane-kummaliza-zitto.html
 
Huyu jamaa hana kazi inayotambuliwa na CHADEMA kikatiba lakini unapoona watu kama 'First Lady' wa serikali itakayoundwa na CHADEMA wanampa nguvu na kukubali kwa kile anachokifanya, hapo ndipo unaanza kuelewa kwa nini anakuwa na ubavu wa kurumbana na kukwaruzana Mh. zitto.

Haya chini ni maneno ya 'First Lady'

kutoka kwenye thread hii,
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...nza-nape-mchange-na-mwampamba-wahojiwe-6.html

Sasa si unaona ile thread ilivyozaa matunda?
 
Hizi sarakasi za sijui zitaisha lini hasa.......

Inaonekana kuna mambo mengi sana yamejificha nyuma ya pazia....

Hebu tujikumbushe japo kwa ufupi....

Ninasikitika sana kuona wanachama wa CHADEMA wanavyoweza kutumika kwa maslahi ya kundi fulani kuharibu heshima ya viongozi wao mbele ya jamii.

Ninaomba ndugu Ben Saanane aje hapa jukwaani kuthibitisha maelezo haya ya Bwana Mamuya kutoka Arusha. Mimi binafsi nikikutana na Ben Saanane leo naweza kupishana naye maana sijawi kumwona, wala kukutana naye. Ndugu Ben Saanane nimewasiliana naye kwenye simu mara mbili au tatu kuhusu masuala yake ya kitaaluma au pale alipohisi kuonewa ndani ya chama. Sijawahi kukutana naye hata siku moja. Kama nasema uwongo yeye binafsi aje hapa kukanusha.

Mimi pamoja na wenzangu tumejenga chama hiki mpaka hapa tulipofika. Tumeingiza watu kwenye chama hiki ili kwa pamoja tuweze kujenga asasi imara kabisa ya kidemokrasia. Chama hiki kina damu yangu. Chama hiki kina muda wangu. Chama hiki kina jasho langu. Nitakuwa mtu wa mwisho kusaliti chama hiki. Sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa tofauti na CHADEMA. Sitarajii kuwa mwanachama wa chama zaidi ya CHADEMA.

Ninawasihi wana CHADEMA tuache propaganda za kuchafuana. Nguvu kubwa inayotumika kumchafua Zitto ielekezwe kwenye kujenga taasisi imara ya CHADEMA, chama chenye demokrasia, kisicho na upendeleo, chenye uwakilishi wa kitaifa na chenye kuthamini nafasi ya kila mwanachama.

Mamuya, mara kadhaa umetaka kuniona kwa sbaabu nisizozijua na imekuwa ikishindikana. Unapata dhambi kubwa sana kumwaga sumu unayomwaga kwa mtu usiyemjua wala hujawahi kukutana naye.Acha kutumika. Jisimamie. Simamia chama.

Vijana, wote wa vyama vyote, siku zote simamieni misingi (principles) na sio kusimamia watu. Watu sio mawe. Mtaja juta. Misingi inadumu. Watu hawadumu. Acheni kuramba miguu ya watu. Simamieni misingi ya chama. Misingi ya nchi yetu. Misingi ya demokrasia. Kataeni kutumika.

Angalieni, wanaozungumzia sana usaliti waweza kuta ndio wasaliti wakubwa. wanazungumzia usaliti kama 'defensive mechanism'.

Tuacheni ujinga huu. Tufanye kazi. Kazi tu ndio kipimo cha ukamanda na sio kurambaramba visigino vya watu.

Mwisho, nasikia sikia sana habari za kuchinjana. Kuuana nk. Nasikia habari hizi kwa watu wale wale wa kikundi kile kile. Moja, natoka Kigoma. Nimeaga kwetu. Nitakufa kwa amri ya Mungu. Siogopi kufa. Iwapo kifo changu kitatokana na mkono wa mtu, sidhani kama kwa mtu huyo kama hata panya atabaki nyumbani kwao. Underline this.

Pili, revolutioneries don't talk about deaths. Only cowards do.

Ndugu Zitto na Wanabodi,

Kama nilivyosema awali, sikutaka kuchangia mjadala huo tangu jana kwakuwa niliamini mambo nyeti yaliyopo yataelekezwa kwenye vikao ndani ya Chama.

Ingawa hawezi kuwa sahihi kwa asilimia 100 kwa alichoandika, lakini Exaud Mamuya amekuwa na haraka kidogo kutokana na kushindwa kuvumilia yeye alichoona kama ‘uchafu na hujuma' vinayoendelea dhidi ya CHADEMA na viongozi wake.

Katika kundi hili alilolitaja Mamuya karibia wote tumeshakaa nao na mara ya kwanza Mamuya alishtuka sana aliposikia kilichokuwa kikijadiliwa kwenye kundi hilo. Pamoja na kushtuka lakini hakushangazwa sana maana hata kwenye sakata la madiwani wa Arusha anajua jinsi Mhe. Zitto alivyohusika na kumuahidi kwamba utamuunga mkono. Tulipotoka kwenye kikao kile alisononeka sana na aliniuliza mambo mengi sana kuhusu kundi hili na mengine nilipanga kuyasema ndani ya vikao hasa yale mambo ambayo ni very very sensitive.

Sasa kwa sababu kiongozi wangu Zitto Kabwe ameibuka na kujaribu kukanusha na kupotosha imebidi nije niweke sawa upotoshaji huu japo kwa kifupi:

Ndugu Zitto,

Mosi:
Sishangazwi na kauli yako kwamba hunifahamu. Ni muendelezo wa siasa zile zile za kutosimamia ukweli na kuendekeza siasa za uongo na upotoshaji. Nimemkumbuka Mwanasiasa Mzee Stephen Wassira (Aliyekitabiria CHADEMA kwamba kitasambaratika) aliposimama na kumkana Mwanafamilia wake mbele ya vyombo vya habari kwa sababu ya siasa na katika mkakati wa kuendeleza ghiliba. Kama mwanasiasa wa Tanzania anaweza kumkana hata mwanafamilia au kusema chochote hakuna la kushangaza.

Sasa, kwa kuwa ushahidi ninao wa jinsi tunavyofahamina na jinsi tulivyoshirikiana kuwashughulikia viongozi wa juu wa chama pamoja na uhusika wetu katika hujuma dhidi ya chama nitaomba chama changu sasa kiitishe kikao cha dharura ili nimwage mambo yote nyeti na ushahidi nilio nao ndani ya vikao. Naamini katika vikao kwa kuwa napenda kuona CHADEMA kikikua kama Taasisi imara ya mabadiliko.

Jana nilimwambia Dr. Kitila haya mambo baada ya wewe kuongea nae na kunitaka mimi niingie JF nikanushe thread hii iliyoanzishwa na Mamuya. Kumbe shinikizo lote ulitaka nikusafishe tu, kitu ambacho sikuwa tayari kufanya. Ushahidi nianao pia! Ulipoona imeshindikana mimi kumkanaExaud Mamuya, wewe ukaamua kuja huku kuja kunikana. Hizo rhetorics unazotumia katika dhana ya kujenga ukabila kwa kufanya ulinganisho wa Mamuya na Ben Saanane ni muendelezo wa propaganda chafu dhidi ya chama ambazo mimi na wewe tulikuwa tukizitumia kuhalalisha kazi yetu hii ambayo kimsingi niliamua kuachana nayo na sikuwa tayari kuendelea kuishiriki.

Pili:

Nigusie kidogo hizi tuhuma za ‘kuuana na kuchinjana'. Tafadhali sana naomba uwe mkweli na usimamie kauli yako ya ‘siasa za ukweli na uwazi'. Hizi siasa za uzandiki hazitufikishi popote. Hizi ni tuhuma ambazo zimekuwa zikisambazwa na kundi la akina ‘TUNTEMEKE' ambao sote tunawajua yaani mimi na wewe. Hawa tumefanya nao kazi kubwa tangu uchaguzi wa BAVICHA. Madai haya yamekua yakitolewa na Habibu Mchange na Mtela Mwampamba wakishirikiana na Gwakisa baada ya kuona mimi sitaki kushiriki hujuma kwa chama changu.

Wamekuwa wakiandika haya hapa JamiiForums kwamba nimetumwa kukuua. Wamekuwa wakiandika walinikamata na sumu ya kutaka kukuua wewe. Leo unaleta mambo haya hapa! Pia wamekuwa wakinipigia na kunitumia message za kunituhumu kwa haya na kunitisha. Hii ni 'pre-emptive attack'.

Mmekuwa frustrated baada ya kuona jitihada zenu za kunitumia kufikia malengo yenu kwa kutumia mwanya mlioupata baada ya mimi kutoridhishwa na mchakato ule wa BAVICHA zinagonga mwamba. Chama hiki watu wamekifia. Kama kuna damu yako hata mimi na wengine tuna damu yetu hapo pia!

Kazi hii ya kuzusha tuhuma kwa mtu ambaye tunaona anatuvurugia malengo yetu tuliifanya sana na ninaijua kaka! Mmesahau tumekuwa tukifanya jitihada za kumtenganisha mwenyekiti na Katibu mkuu kwanza ili tuweze kuwashinda kwa pamoja? Hili unalijua moyoni mwako . Sasa naomba kama hutanithibitishia tuhuma hizi nitaomba kwa kuwa wewe ni kiongozi wa chama kikao kiitishwe na nitamwaga yote huko. Kama hutafanya hivyo, mimi nitaandika Barua kwa katibu mkuu ili uje unithibitishie tuhuma hizi pamoja na kundi zima la ‘Masalia'. Sitaogopa chochote na nipo tayari kwa lolote kwa kuusema ukweli. Sikutaka kujibu thread hii lakini tuhuma za kutaka kuuana ni serious allegations kwa kuwa zinahusu maisha ya mtu. Kuliko nifanye siasa za aina hii, ni bora niache siasa kaka.

Pia, vitisho vya kuaga kwenu havinihusu na wala havinitishi. Siamini kama ushirikina una nguvu kwangu na hilo unalijua na kundi lote la masalia linajua ndiyo maana ilishindikana mimi kwenda kula viapo kwa mganga wa kienyeji na unakumbuka vizuri! (Ati kula kiapo kwa kundi la masalia ili tusisalitiane katika kazi ya kukihujuma chama chetu). Afadhali Juliana Shonza na rafiki yangu Emmanuel Mwakajila waliniunga mkono katika kukataa hili. Ninaye Mungu anayenipigania na sitaogopa vitisho vyovyote. Mnanifahamu kwa hili, I dare you to challenge me! Twende kwenye vikao.

Mwisho:

WanaJF,
Mambo mengi sitaweza kuyaweka hapa kwa kuwa ni nyeti sana, nitasubiri vikikao ndani ya chama ili kikao kiitishwe nimwage huko. Nadhani safari hii tutakomesha tabia hii chafu ya baadhi ya wanasiasa kujaribu kuwatumia vijana kwa maslahi binafsi. Naamini itakuwa ni kikomo cha siasa za uzandiki na uongo ndani ya vyama vyetu vya siasa.

Wale wanaosema mimi ni mtu wa kutumika, nitapata fursa ya kuwathibitishia hayo. Sinunuliki na sina price tag. Wanaosema haya, ukweli wanaujua moyoni. Ninajiamini kwa kuwa nina taaluma yangu na miradi yangu na sinunuliki labda bei yangu ni Ukweli ambao nipo tayari pia kuulipia in return kwa gharama ya damu yangu.

Brave people, given the opportunity and even under any oppression or threat to life, stay and defend their comrade in arms and their entity....not run away and abandon it....unless something hinders their dignity and pride. Wanamapinduzi wote hufanya haya!

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...wa-zitto-na-kundi-lake-kutoka-kwa-mamuya.html
 
Back
Top Bottom