Siri ya Kuuwawa Zitto - UWONGO

Komredi,
Poleni sana. Hatimaye mmekanwa. Na bado tutaona na kusikia mengi. Kumbe mlijivika ujasiri na kiherehere cha kusema mliona ungaunga mwekundu? That post was so poor. Nadhani ndo ya kufungia 2012.

Haya, Muha kawachinjieni baharini. Na huko mlipo, muda si mrefu mtatupwa...mtaenda wapi? ADC? CHAUMA? CHAUSTA? NDL?

Ha ha ha watajiju walishauriwa mapema waombe msamaha waeneleze siasa zao kwa kuwa ni vijana wazuri wakadhani ufitini ni dili ona sasa wamejiumbua
 
Safi sana Kamanda! pia Ningemshauri meneja wa Hiyo Hoteli ya Lunch Time kuchukua hatua za kisheria dhidi ya gazeti hilo!
 
Baabda ya kuwa nimepoteza imani na wewe Zitto sana naona kijana upo kwenye mstari. Kimya chako kilinifanya niamini wewe ni msaliti. Ila sitokaa kuamini kama masalia umewachinjia baharini. Kweli siasa ni zaidi ya uijuavyo.
 
Mwampamba ni hatari sana, inavyoonekana ni msaliti wa muda mrefu maana kwa inavyoonekana wote aliowahi kutumiana nao meseji alikuwa hafuti, anazihifadhi..ina maana alikuwa anajua atazihitaji, yaleyale ya ludo.,
vijana mmetuangusha sana
 
Wanazidi kututengenezea njia ya mwaka 2015. Waacheni waangaike zitto ameonyesha alivyokuwa makini.
 
Kwa siasa hizi mnazoendesha vijana wenzangu ni aibu
La kujiuliza ni timing ya hizo kashfa unazosema, inaonyesha hamko strategic na hamjui hata maana ya strategy.. haya maelezo yako na matendo yenu ni dalili za kukurupuka na ina reflect one thing for sure, YOU ALREADY A LOOSER AND YOU DONT CARE SINCE YOU HAVE NOTHING TO LOOSER... AMBACHO HUJAFAHAMU MPAKA SASA NI KWAMBA U MISS THE TARGET.. AND BIG GUY IS ON YOU BACK... hapo ndipo ninaposikitika ni pale kijana mwenye akili zako unakutana na simba katulia zake anajilia vya kwake una risasi moja tuuu unaambua kuitumia kumlenga... sasa umemkosa tafuta mti wa kupanda....

WAZO LANGU NADHANI MKAKAE CHINI MJE NA KASHFA KUBWAAAAA MFANO VIONGOZI WA CHAMA WALIKUWA WANAWAINGILIA KINYUME CHA MAUMBILE AU WALIWAHI KUWASHIKASHIKA SEHEMU ZA SIRIII AU WALIKUWA WANAWALAZIMISHA MZICHEZEE ILI MPATA UONGOZI KITAIFAA........... KASHFA KAMA HIZOO NDIO ZILIIZOBAKI NA SITASHANGAA MKIIBUKA NAZOOOO MAANA MLIVYO NA CHUKIII NA SLAAA NA UKICHUKULIA AINA HIII YA KASHIFA IMEWAHI KUWAKUMBA MAPADRE WENGIIII..... THAT IS PERFECT OPPORTUNITY TO TAKE HIM DOWN ....... AU SIO!!!!!!!!!!!!!!!???? vipi upo CCM lakini vita unavyoendesha ni kama unataka kuiua chadema ili mkose wote au unataka kurudi chadema!!!???? CCM SI CHAM KIKUBWA JAMANIII MBONA HUONYEHSI KURIDHIKA HUKOO ULIKOOO AU KWELI CHADEMA NI ZAIDI YA TUNAVYOIJUA.... KUNA JAMBO KUBWA SANAA HAPA AMBALO NI PERSONAL LIMEJIFICHAA
Mpuuzi na huna adabu hapa ni GF unahamisha dhambi ya Zitto kupeleka kwa DR SLaa kuonyesha ana mfanya vibaya MTela,kama unataka kutueleza Zitto ndio alikuwa anamfanya Mtela ppeleka ujinga wako huko huko ,Mpuuzi sana uhuru wa JF isiwe kukosea adabu watu wazima , wewe ni mwehu Zitto amejiumbua hawezi kuwakana hawa vijana ameandika makala nyingi katika makala mbalimbali akiwasupport,hapa Jf hivyo hivyo kwa hiyo koma kama ulivyokoma kunyonya ziwa la Mama yako kumkosea adabu Dr Slaa namna hiyo
 
Waliokuwa wanajifanya wanamtetea Zitto kawaruka, hawajui, hajwahi kukaa nao na wajadili mambo yanayohusu Vyama vyao. Labda sasa watajadili mambo yanayotukabii kama Taifa, akiwmo yule aliyesema Zitto ni role model wake
 
Last edited by a moderator:
zito anasema matendo ya slaa yasifanywe kuwa ya taasisi

Mkuu ni vyema ukalifahamu hili mapema; Adui wa CCM ni Ufisadi, Ujinga, Maradhi, Umasikini, Rushwa, Huduma duni za afya, Ukosefu wa mitaala ya elimu, Migomo ya walimu, Migomo ya madaktari, Mikataba tata na Rais wa china, Mitandao ya urais ndani ya CCM, mfumuko wa bei na ugumu wa maisha kwa mwananchi wa kawaida na siyo Dr. Slaa kama mnavyotaka kutuaminisha sisi watanzania.
 
Kisaikolojia, mtu akizoea kukudanganya,kisaikolojia ukajenga dhana kuwa huyo mtu ni mwongo,hutamwamini kwa jambo lolote. hata akisema ukweli hutamwamini. ccm walivyo wajinga hawajui kuwa si tu kisaikojia wanawajengea watanzania usugu wa kutoamini jambo lolote watalosema. bali pia wanasaidia kukiua chama chao na kuongeza imani katika akili za watu kwa CHADEMA. mtu akisingiziwa jambo, halafu ikaja kuthibitika kuwa hilo jambo si kweli bali kasingiziwa tu, kisaikolojia watu huvutwa na huruma na imani dhidi ya mtu aliyesingiziwa jambo. propaganda dhidi ya huyo mtu zikiwa nyingi na zote zikathibitika kuwa ni uongo, imani na heshima ya watu huongezeka zaidi kiasi cha watu kuziba hata masikio yao wasiendelee kusikia upuuzi wa wapiga propaganda. hapo ndo hufikia mali wapiga propaganda hata wataposema jambo la kweli,watu hataliamini. kwa hiyo ccm wajue jinsi wanavyozidisha mbinu chafu dhidi ya chadema, ndivyo wanavyokidhoofisha zaidi chama chao kuelekea 2015 kwa watu kuzidi kukipuuza. na ndivyo wanavyosaidia kukiimarisha zaidi chadema kwa ku-win huruma na imani ya watu kuelekea 2015. ccm wasome nyakati. wabadilike na kuacha kuishi kwa mazoea kwa kuangalia nyuma jinsi walivyovifanya cuf, nccr mageuzi na tlp. kizazi cha dot.com si kizazi cha mwaka 47.
 
Chanzo cha habari hiyo kwenye gazeti la Mtanzania ni Juliana Shonza, ambaye amekuwa kipenzi cha wana CCM kwa maneno anayozungumza kuhusu chadema

quote_icon.png
By Juliana Shonza

KUHUSU BEN SAANANE NA KUTUMIKA KUMUUA ZITTO KABWE

Wana jf, Nakili wazi hili swala lilitokea mnamo mwezi wa 5 mwaka 2012 tukiwa Lunch time hotel external kwenye mazungumzo ya kawaida(ambavyo ben saanane anaita ni vikao vya kuhujumu chama). Siku ya tukio tukiwa meza moja na Ben Saanane mkono wake wa kushoto alifunga bandeji akidai ameumia mkono(nakumbuka). Kwa babati mbaya sana katika maongezi yale Ben alilewa pombe (alikuwa anakunywa bia(kilimanjaro). Kulewa kwake pombe alijisahau na kutoa bahasha ya kaki yenye fedha, ndani ya bahasha ile wakati wa kutoa fedha alipe huduma ya chakula na vinywaji alidosha karatasi ya nailoni ndogo ikiwa na unga mwekundu ndani.

Tulimuuliza ni nini hicho akadai ni kuberi,na kuing'ang'ania tusifungue(aliyekiokota ni mwampamba).Lakini Mwampamba aligoma kumpa na kudai lazima ifunguliwe pale pale.

Ben saa nane akiwa katika hali yake ya kulewa alifura kwa hasira kutaka arudishiwe ilekaratasi,haliiliyopelekea uvunjifu wa amani pale lunch time hotel.Mwampamba aliondoka na mzigo ule kwa kukimbia nao, usiku ule Ben alitafutana na mwampamba hadi nyumbani kwake(temeke) akidai huo mzigo(ikumbukwe mwampamba na mm nimeishi kwake na nikaka yangu) . Lakini katika hali ya kusikitisha ben aliomba mzigo ule usiende mbali na kuahidi atasema kweli kile ni nini.

Ben saanane alikili wazi kwamba ile ni sumu lakini anapeleka nyumbani kwa ajili ya kuulia panya, Swala hili halikuishia usiku ule,ben hakufanikiwa kupata mzigo ule kesho yake asubuhi(jumapili) alikwenda kumsihi mwampamba ampatie mzigo.

Sharti lilikuwa aseme ni nini kwasababu huwezi kuwa na sumu eneo la starehe kama pale hotelini huku akisisitiza kuonana na zitto ambaye alisafiri usiku ule kwenda marekani bila kuonana na yeyote kati yetu?

Ndipo Ben saanane akakili ile ni sumu akilenga kumpatia zitto akiwa ametumwa na Dr.slaa.Tulihamaki kusikia kile kitu(hapa tulikua tabata reli stand tukisubiri usafi).Nilimuuliza uthubutu wake wa kufanya kitu kama hicho na kwanini afanye unyama huo,akadai ametumwa Kisa kikiwa ni zitto kumsakama dr.slaa ndani ya vikao vya chama.

Swala hili lilifika mbali kwa kuwekeana mipaka ya kula vyakula mahotelini na kutoshirikiana tena katika ushikaji wetu
kama masalia.
Juliana Shonza: hatutakuamini tena uyasemayo.
 
asante mtani kwa ufafanuzi na kwa vile hii ni kauli yako mwenyewe basi watatumia wino na karatasi zao kuandika mambo ya maana.
Naungana wewe kumshkuru Zitto kwa hayo majibu nafikiri gazeti la Mtanzania linapaswa kuyaandika ukurasa wa mbele kwa uzito uleule walioandika uzushi wa kwanza kama kweli wao ni objecive
 
[QUOTE=Zitto mdogo wangu wewe ni kama swala Kati ya simba (ccm) na chui (cdm)maadui ni wengi pande zote jichunge vijana tupo nyuma yako
 
Mpuuzi na huna adabu hapa ni GF unahamisha dhambi ya Zitto kupeleka kwa DR SLaa kuonyesha ana mfanya vibaya MTela,kama unataka kutueleza Zitto ndio alikuwa anamfanya Mtela ppeleka ujinga wako huko huko ,Mpuuzi sana uhuru wa JF isiwe kukosea adabu watu wazima , wewe ni mwehu Zitto amejiumbua hawezi kuwakana hawa vijana ameandika makala nyingi katika makala mbalimbali akiwasupport,hapa Jf hivyo hivyo kwa hiyo koma kama ulivyokoma kunyonya ziwa la Mama yako kumkosea adabu Dr Slaa namna hiyo

Read between lines utaona tofauti ya nilichoandika na tafsiri yako. Hawa jaamaa ni wapika kashfa wakubwa na nilichofanya ku-preempty kabla hajaingia maabara na kuja na kashfa kubwa na mark my word sintashangaa hawa jamaa walivyo viazi wakibeaba na kuileta siku moja hapa JF... Hawa jaamaaa ni wachumia tumbo wa kufa mtuuuu....

Kashfa za namna hii zipo na zishapikwa Zimbabwe kwa Kanan Banana na Zilimkuta Zuma wa South Africa.... Usikasirike I know I have criminal mind cause I love criminal physcology.... Naweza nisiwe GF kama wewe ila I use my brain too see what other dont usualy seee .... bahati mbaya kama hukupenda lakini I didnt mean no desrespect.... But face it hilo ni moja kati ya mabomu mabaya sanaa ambayoo hawa wachumia tumbooo wako-willing kuyatumia
 
Mama Josephine,

Kama wewe ndiye mke wa Dr. Slaa, nakushauri usiwe una-comment humu, especially kwa masuala yanayomhusu mzee au CDM. Ndiyo, ni haki yako lakini at times nafikiri unafanya kazi ya Daktari inakuwa ngumu sana. You will do more to support the cause by watching from a distance than trying to defend your husband in this forum. I am just saying. I maybe wrong.
Josephine Mushumbusi ID yake ni Josephine. Huyu Josephine03 ni mtu mwingine.
 
Last edited by a moderator:
katika gazeti la mtanzania toleo na. 7269 la jumatano machi 27, 2013 kuna habari yenye kichwa chenye maneno ‘siri ya kuuwawa zitto yafichuka’ na vichwa vidogo ‘yadaiwa ilipangwa anyweshwe sumu hotelini’ dk. Slaa atajwa kumtuma saanane kummaliza’. Habari hii imeniletea usumbufu mkubwa kwani ndugu, jamaa, marafiki na wapiga kura wangu, wamejazwa na wasiwasi mkubwa sana kwamba ninaweza kuuwawa.

Napenda kusema yafuatayo:

Moja, sijawahi katika maisha yangu yote kukutana na mtu anayeitwa ben saanane na hivyo hicho kikao ambacho inasemekana nilikuwa naye na akajaribu kunipa sumu hakijawahi kutokea. Imetajwa hoteli ya lunch time ambayo sio tu sijawahi kufika, pia hata siijui ipo wapi. Haijawahi kutokea mimi kufanya kikao cha pamoja na ben saanane, juliana shonza na mtela mwampamba. Hivyo habari iliyoandikwa ni ya kufikirika na hivyo naomba mwandishi ahakikishe kuwa vyanzo vyake vya habari vimempa habari sahihi.

Pili, siamini kamwe kuwa katibu mkuu wa chama changu anaweza kupanga kuniua maana hana sababu ya kufanya hivyo. napenda kurudia kusema kwamba mimi ninaamini kuwa kila nafsi itaonja mauti. Kila mtu atakufa. Kama nitakufa kwa kuuwawa na mtu mwingine ndio itakuwa nimeandikiwa hivyo na mungu. Ndio maana hata siku moja silalamiki kuhusu vitisho vya kuuwawa nk. Kama kuna mtu anafikiria kuwa kumuua zitto ndio furaha ya maisha yake atakuwa anajidanganya tu maana zitto anaweza kufa kimwili lakini mawazo, fikra na maono ya zitto yataishi tu. Siogopi kufa maana maisha niliyoyachagua ndio haya ambayo yamejaa vitisho. Muhimu kwangu ni kufanya kazi zangu kwa bidii, uhodari na uaminifu. Siku zote nitasimamia ukweli bila kujali uchungu wa ukweli huo.

tatu, nawashauri watu ambao wamehama chadema na kuhamia vyama vingine watumie muda wao kujenga vyama vyao badala ya kila siku kuzungumzia masuala ya chama ambacho wao sio wanachama tena. Kama mtu kaamua kuhama chadema anapoteza haki ya kujadili masuala ya chadema maana kama angekuwa anapenda kuyajadili asingehama. Naonya mtu yeyote ambaye anatumia jina langu ili kufanikisha malengo yake ya kisiasa. Chadema sio pango la watesaji wala wauaji. Kama kuna mwanachama wa chama kingine cha siasa anayedhani kuna mtu ndani ya chadema anapanga mipango ovu aende kwenye vyombo vya sheria kumshtaki. matendo ya mtu mmoja yasifanyiwe propaganda kama ni malengo ya taasisi.

nne, nawashauri viongozi wenzangu wa chadema na hasa wanachama tutumie muda wetu kujenga mshikamano ndani ya chama. fitna, majungu, uongo, uzandiki nk kamwe havijengi chama. Chama chetu lazima kiwe mfano bora wa kuheshimu demokrasia na haki za binaadamu. Wananchi hawawezi kutoa dola kwa chama chenye mifarakano. Tusiruhusu kugawanywa kwa matakwa ya watu wachache. Tusimamie misingi ya kuanzishwa chama chetu.


=============


thread inayoongelea kilichoandikwa na mtanzania hii hapa - https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ajwa-kumtuma-ben-saanane-kummaliza-zitto.html

hivi jamani, hizi kauli kweli zinamaanisha kuwa kilicho andikwa na mtanzania si cha kweli???. Ndugu zito, tunaomba utufafanulie. Nina hakika hao viongozi wenzako wasingependa kuona haya maneno, na nina hakika wewe unalijua hilo, lakini zaidi kabisa nina hakika hayo maneno hujayaandika kwa bahati mbaya, umeyaandika kwa makusudi kabisa pamoja na kujua mambo hayo niliyotangulia kuyasema.
 
Amen
sisi wapiga kura ni observant right wangejua wana ruin wangeacha na kuanza ku settle their mess since back in days ila kwakuwa Mungu yupo wao wapo upande wa Shetani sasa hawaoni na kila siku kila wizara inaboronga

amen
 
Back
Top Bottom