Siri ya Kuuwawa Zitto - UWONGO

Siri ya Kuuwawa Zitto - UWONGO

mh! Mbona hii hatari sasa! Mi nashauri ZZK akae kimya maana hawa watu Mwampamba & co, wanaonekana wana siri mbaya zake, pia nahisi harufu za ukweli wa tuhuma juu yake!

Mh Zitto unachotakiwa kufanya ni kuita waandishi wa habari ukanushe na uwaamishe waTz wanaoamini kila wanachokisikia ktk tv zetu,

Nina maana gani

1. Si watz wote ambao wanaweza kuingia kwa net na ktk mitandao ya kijamii

2. Fanya hivyo wtz wote wakisikia maelezo kutoka ktk kinywa chako

hakoka aibu kubwa sana kwa waliokuwa wanashabikia hii mada especialy media!!

ni maoni yangu tu!

bora akae kimya, otherwise asiwaguse kina mwampamba course inaonekana nao wamechoka kutunza siri.

Zitto, wakati mwingine haya mambo unayataka mwenyewe,(Rejea panya hatapona) Hii story ilikuwepo toka mwaka jana leo ndio unakanusha? Binafsi nazidi Kumpongeza sana kijana Ben Saanane, kwa kulishupalia hili, mpaka umejitokeza, Well done Ben wa saanane..

Kama ulivyosema, Tusonge mbele kujenga CHADEMA

Last edited by a moderator:
Ni kweli kabisa watazidi kumwaga uongo ili wakubalike katika chama cha magamba kwa ajili ya kupata nyadhifa na nafasi za kufanya madili.

Subirini tu, sasa hivi wanafikiria mengine kwa vile lile la Zitto kutaka kuuwawa na akina Dr Slaa li mebackfire baada ya mhusika mkuu (Zitto) kukana kuwepo njama hizo. Yaana baada ya mwaka mzima tangu ‘tukio' ndiyo wanakuja kusema? Tena baada ya kutimuliwa CDM?

Naamini bado watajitahidi kwa mengine. Na hatutashangaa iwapo watakuja kusema kuwa Ulimboka na kibanda walipigwa kutokana na njama za akina Slaa.

Kuna siku CCm watawastukia watu hawa kuwa ni hatari sana!

Ni kweli kabisa watazidi kumwaga uongo ili wakubalike katika chama cha magamba kwa ajili ya kupata nyadhifa na nafasi za kufanya madili.

Subirini tu, sasa hivi wanafikiria mengine kwa vile lile la Zitto kutaka kuuwawa na akina Dr Slaa li mebackfire baada ya mhusika mkuu (Zitto) kukana kuwepo njama hizo. Yaana baada ya mwaka mzima tangu ‘tukio’ ndiyo wanakuja kusema? Tena baada ya kutimuliwa CDM?

Naamini bado watajitahidi kwa mengine. Na hatutashangaa iwapo watakuja kusema kuwa Ulimboka na kibanda walipigwa kutokana na njama za akina Slaa.

Kuna siku CCm watawastukia watu hawa kuwa ni hatari sana!
Hawa hawako pekee yao. Ni GENGE la WAHUNI linaloongozwa na MWIGULU, NAPE na KIGWA. Huenda wako mbioni kuuwa viongozi wa CHADEMA ili asingiziwe Slaa

Wewe ndio kilaza namba moja,unamtetea huyo aliyehongwa suti nne kilimanjaro???Mpaka sasa ni miaka 8 amefikisha 6% ya ahadi zake utamwitaje????Refer kuna uzi ulikuwa hapa jamvini jana(anayeweza kumwekea huyu kilaza bocho huo uzi msaada pliz)

Mimi najua siku nyingi, CHADEMA ni weupe na wingi wa matusi mkiishiwa hoja. Tuthibitishia kwamba ahadi za Kikwete zimetekelezwa kwa 6% kama una akili sawa sawa. Kama hujuwi pia sema ndio uungwana. Inawezekana nikawa kilaza, ila wewe mwerevu hebu tuoneshe namna ulivyoipata hiyo 6%.

Dhana yangu ni kwamba kwa kauli hiyo na huu uzi hapa unaendelea kuuthibitishia ulimwengu kwamba viongozi wa CHADEMA na wafuasi wao ni waongo. Tukiwapa nchi si mtaiuza nyie?

kamanda Zitto umemaliza.

Kazi kwao kufafanua kwa ushahidi madhubuti

Nashukuru sana kwa ufafanuzi huu murua kabisa, ningependa Julina Shoza achangie hapa cause yeye ndiye muasisi wa hili na nadhani Mtanzania wametoa kwake pia sababu uzi kama huu uliwahi kubandikwa humu na hata Ben Saanane amewahi kuu re-call, well, naomba muheshimiwa Zitto nenda mbali zaidi, waandikie pia Mtanzania kuwataka wakanueshe hii habari, sababu kubwa ni hii, sina hakika kama wapiga kura wako wa Mwandiga, Manyovu, Kalinzi, Mkabogo n.k kama hua wanapitia jamvi hili la JF.

kimeo mwenyewe...abdul mohamed alikuwa anatangaza sports na news now anakula bata majuu landani bbc swahili....

kumbe alikuwa... mi naongelea waliopo wewe unaongelea miaka ya 2000....hebu nambie nani aliyepo sasa hivi anafaa kutangaza BBC ama CNN

Mimi najua siku nyingi, CHADEMA ni weupe na wingi wa matusi mkiishiwa hoja. Tuthibitishia kwamba ahadi za Kikwete zimetekelezwa kwa 6% kama una akili sawa sawa. Kama hujuwi pia sema ndio uungwana. Inawezekana nikawa kilaza, ila wewe mwerevu hebu tuoneshe namna ulivyoipata hiyo 6%.

Dhana yangu ni kwamba kwa kauli hiyo na huu uzi hapa unaendelea kuuthibitishia ulimwengu kwamba viongozi wa CHADEMA na wafuasi wao ni waongo. Tukiwapa nchi si mtaiuza nyie?

Mkuu, samahani, nchi iuzwe mara ngapi? mbona ccm wameisha iuza siku nyingi tu, nambie kitu tunacho miliki wenyewe sasa hivi ni nini? Hujui hata bei ya umeme na hata huo umeme wenyewe wanaoa amua tuwe nao au tusiwe nao sio sisi, kama hili hulijui basi we unaishi sayari nyingine na kama unalijua ila unajaribu kupotosha ukweli, tambua Mtanzania wa leo sio mwaka 1947!

bora akae kimya, otherwise asiwaguse kina mwampamba course inaonekana nao wamechoka kutunza siri.

Who is Mwampamba juu ya mustakabali wa maisha ya watanzania bana!!!!binadamu yeyote pua yake
imeelekea chini hawezi kuwa juu ya wengine kwa kuogopwa eti ana siri!?Mwanangu anapenda kutumia neno "RUBISH"
mwenye siri ni Mungu tu anaejua siri ya siku ya kufa mwanadamu awaye yote' No sense'

Mkuu, samahani, nchi iuzwe mara ngapi? mbona ccm wameisha iuza siku nyingi tu, nambie kitu tunacho miliki wenyewe sasa hivi ni nini? Hujui hata bei ya umeme na hata huo umeme wenyewe wanaoa amua tuwe nao au tusiwe nao sio sisi, kama hili hulijui basi we unaishi sayari nyingine na kama unalijua ila unajaribu kupotosha ukweli, tambua Mtanzania wa leo sio mwaka 1947!

Umeanza porojo ee? Swali la msingi nchi ni nini? Na katika hizo components utakazozitaja useme ameuziwa nani?

Vyama vingi sio kupinga kila kitu cha chama kilichopo madarakani ila ni kuonesha mbadala wa mawazo kupata ufanisi zaidi.

Zitto umefanya jambo la maana sana kuujulisha umma kuhusu suala hili hatari ambalo limekuwepo kwa mda mrefu vichwani mwa watu na kusababishwa lundo la maswali ambayo hata hivyo hayakuwa na majibu.Kama kichwa changu hakijapoteza kumbukumbu hili suala limeanza kabla akina mwampamba na mwenzake hawajavuliwa magwanda na kwenda kujisitili magamba kuficha utupu wao,walipotoa tuhuma hizo Zitto nawe uliibuka kwa kusema "umetoka kigoma umeaga,hayupo atakaye kudhuru akabaki salama hadi hata panya walioko nyumbani kwake nao hawatasilimika" kauli hii ni nzito sana ilionesha dhahili kuna kitu upande wa pili ambacho yaweza kuwa tu mchezo wa kisiasa au mpango uliopangwa ili kukumaliza kweli.Cha mhimu zaidi chadema kweli kama malengo ni kuliongoza taifa inabidi msilee unafiki,wahenga walisema mficha maradhi kifo humuumbua,tusingependa mfike huko sababu chadema ndio tumaini la pekee kwa mtanzania lililosalia,tofauti ya mawazo katika chama ni kitu chema na chenye kujenga lakini kinapofikia kuleta uadui basi tunatamani kurudi kwenye zidumu fikra za mwenyekiti.

Mimi nashangazwa na kitu kimoja.Waliotuhumiwa kuhusika na tukio kwa upande mmoja (yaani Ben Saanane na Dr. Silaa) wanakana kuhusika na tukio, anayeshutumiwa kuhusika na tukio upande wa pili (yaani mkuu Zitto) naye anakana tukio kuwepo, anasema halifahamu kabisa tukio, na wala hayafahamu kabisa mazingira yanayodaiwa tukio lilitokea, halafu upande wa tatu wako mashahidi (yaani Juliana Shonza na Mtela Mwampamba )wao wanadai walishuhudia tukio kwa macho yao (tukio ambalo wanaotajwa kutaka kudhuriana wote wanalikana), lakini nao mashahidi baada ya kushuhudia tukio hawakuchukua hatua yeyote, na sasa wanafuatilia mjadala hapa kama wageni bila kuchangia chochote. Kama wewe ni Hakimu (jaalia una certificate yako tu ya sheria), umekabidhiwa kesi kama hii unatoa hukumu gani? Nashauri hawa wanaodai ni mashahidi wa tukio hili wakamatwe na kufunguliwa mashitaka ya kufanya uchochezi unaolenga kutengeneza mazingira ya uhasama na wasisiwasi miongoni mwa watanzania.

Last edited by a moderator:
Leo Alhamisi 28 March 2013, nafungua gazeti la Tanzania Daima nakutana na habari kuu isemayo CHADEMA SI PANGO LA WAUAJI. Naingia ndani zaidi na kukutana na habari za press conference ya Zitto na waandishi wa habari akikanusha uvumi wa kuwa Ben Saanane aliwahi kutumwa na Dr Slaa kumuua kwa sumu.

Katika habari hii anaonekana mia kwa mia kumsafisha Dr Slaa kuwa haamini anaweza kupanga njama za kumuua kwa kuwa hakuna sababu zozote za kufanya hivyo. Ninapo pata shida kuelewa ni pale Zitto ambaye ni naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA (Bara) kukili kutomfahamu Ben Saanane kijana mwenzie Mjumbe wa BAVICHA wakati huo huo akisema hajawahi kukutana naye.

Nilipoendelea kusoma habari hii, nakutana na maelezo ya Ben Saanane akieleza kuwa alikwisha kutana mara kadhaa na Zitto, japo kuwa maelezo yao wote yalifanana kwa kutowahi kukutana hotel ya Luch Time kikao kinachodaiwa ilipangwa Zitto akiingia kwenye target azimishwe kwa sumu.

Katika aya ya sita(6) ya gazeti hilo Zitto anasema, "...sijawahi katika maisha yangu yote kukutana na mtu anayeitwa Ben Saanane..." Naye Ben Saanane katika aya ya kumi na nane (18) mwandishi anaandika hivi Aliongeza kuwa mara zote alizokutana na Zitto hajawahi kufika hotel ya Luch time.. Anasema Ben Saanane.

Wana JF, Zitto anasema hajawahi kukutana na Ben Saanane maisha yake yote Ben Saanane anasema. Mara zote alipokutana na ZITTO.... Hii contradiction ya Zitto sijawahi kukutana na Ben naye Ben mara kadhaa nilipokutana na Zitto imekaaje? Naombeni mawazo yenu.

Mponjori ndo maana nilisema Zitto aitishe waandishi na watz nao wajue wote jaman mbona mnafaidi pekee yenu humu;
harafu unasema anyamaze ili hawa watu wasiendelee kutoa siri,

siri ipi tena iliyobaki mkuu si waweke wazi tu kila kitu tu!
ukisema@Zitto akae kimya sawa atakaa kimya lkn tuhuma hazihishi kila siku hili mara hili yote ni kwa CHADEMA, waswahili wanasena kukaa kimya ni jibu la mjinga,
lkn inategemea na huyo mjinga alivyochachamaa kukuangamiza
anatakiwa wakati mwingine ajibiwe ajibiwe sawasawa na ujinga wake
ni kwa sababu gani nilisema Zitto ajitokeze media akanushe aibu iwashke na kama wana siri zingine watoe kwann nasema hivyo ni kuwa leo asubuh natoka home kuna watu walikuwa wanaongelea kuhusu swala la Dr.Slaa kumdhuru Zitto kwa sumu ikabidi niwasomee maelezo ya humu lkn bado hawakunielewa niliwaacha njia panda coz nilikuwa nawahi Job!
sasa naomba tuelezane kuwa mTz huyu aliyeamini chombo cha habar na pia labda na mwanachama atafumbuliwa macho na nani?????

zito mnayemchukia sana ndiyo huyu hapa>>>>>>>>

watanzania wengi ni wanafiki tu

zito atabaki kuwa juu< just imagine hata kama njama hizo ni kweli......mmeingizwa mjini,

Back
Top Bottom