Ben saanane nafaham ni member wa nec ya cdm,na zitto nadhani ni member nec na cc. Katika kikao cha nec kilichofanyika diamond jubilei kilichobariki kutimuliwa kwa mwampamba na shonza wote walikuwemo. Je kulikuwa na uzibe gani kati ya ben na prezo kuonana? Pathetic. Prezo atakuwa ni muongo!
-Majibu yangu nilishayatoa huku.Sioni sababu yoyote ya kuanzisha thread kama hizi
-Badala ya kuniuliza mimi muulize yeye awe mkweli.Sipendi malumbano ya kipuuzi kwa vitu ambavyo ni obvious.
-Kama umesoma gazeti la jambo leo la jana utakutana na maoni ya marafiki zetu wa zamani na utajua ni lipi linaloendelea
-Akina Mwampamba walikana humu mwezi December,kila mtu alinikana lakini baada ya wao kukanwa juzi wameona hakuna dili kuendelea na siasa za kinafiki.Wamechoka na wamesema pamoja na mapungufu na upotoshaji fulani kweny kauli zao
-Hili suala sipendi kulijadili kwa kuwa ni la kipuuzi.Kuna vikao vinakuja ndani ya chama.Anayesema mimi ni muongo nitasema ukweli juu yake hadi atakapoacha kusema uongo juu yangu
-Bernard Membe alituachia fumbo watanzania,tujiulize kwamba ujasiri huu wa kusema uongo kwa kiwango cha kutisha tumeutoa wapi.Nami nawaachia kitendawili hiki hiki mkitegue.
-Majibu yangu nilishayatoa huku.Sioni sababu yoyote ya kuanzisha thread kama hizi
-Badala ya kuniuliza mimi muulize yeye awe mkweli.Sipendi malumbano ya kipuuzi kwa vitu ambavyo ni obvious.
-Kama umesoma gazeti la jambo leo la jana utakutana na maoni ya marafiki zetu wa zamani na utajua ni lipi linaloendelea
-Akina Mwampamba walikana humu mwezi December,kila mtu alinikana lakini baada ya wao kukanwa juzi wameona hakuna dili kuendelea na siasa za kinafiki.Wamechoka na wamesema pamoja na mapungufu na upotoshaji fulani kweny kauli zao
-Hili suala sipendi kulijadili kwa kuwa ni la kipuuzi.Kuna vikao vinakuja ndani ya chama.Anayesema mimi ni muongo nitasema ukweli juu yake hadi atakapoacha kusema uongo juu yangu
-Bernard Membe alituachia fumbo watanzania,tujiulize kwamba ujasiri huu wa kusema uongo kwa kiwango cha kutisha tumeutoa wapi.Nami nawaachia kitendawili hiki hiki mkitegue.
JK: sijui nani mmiliki wa Richmond
Zitto :Sijawahi kukutana na wala simjui Ben Saanane
Dr Shein na Maalim Seif:Hatuwafaham uamsho
Uhuru Kenyatta:sijawahi kuona hata mfuasi mmoja wa MUNGIKI
BADO MZEE WA HAKUNA MGAO WA UMEME,
Ben, Zitto anadai hamjawahi kukutana, na hata wewe unakiri pale Lunch Time hotel Zitto hakuwapo, na inadaiwa ulilalamika kwa nini Zitto anakukwepa, jee, waweza sema mahali gani mliwahi kukutana? hujawahi hata siku moja kusema mlionana hotel fulani, baa fulani au nyumba ya fulani, ila wewe wakazania mlionana, je mlionana wapi?
Katika gazeti la Mtanzania toleo na. 7269 la Jumatano Machi 27, 2013 kuna habari yenye kichwa chenye maneno SIRI YA KUUWAWA ZITTO YAFICHUKA na vichwa vidogo yadaiwa ilipangwa anyweshwe sumu hotelini dk. Slaa atajwa kumtuma Saanane kummaliza. Habari hii imeniletea usumbufu mkubwa kwani ndugu, jamaa, marafiki na wapiga kura wangu, wamejazwa na wasiwasi mkubwa sana kwamba ninaweza kuuwawa.
Napenda kusema yafuatayo:
Moja, sijawahi katika maisha yangu yote kukutana na mtu anayeitwa Ben Saanane na hivyo hicho kikao ambacho inasemekana nilikuwa naye na akajaribu kunipa sumu hakijawahi kutokea. Imetajwa Hoteli ya Lunch Time ambayo sio tu sijawahi kufika, pia hata siijui ipo wapi. Haijawahi kutokea mimi kufanya kikao cha pamoja na Ben Saanane, Juliana Shonza na Mtela Mwampamba. Hivyo habari iliyoandikwa ni ya kufikirika na hivyo naomba mwandishi ahakikishe kuwa vyanzo vyake vya habari vimempa habari sahihi.
Pili, Siamini kamwe kuwa Katibu Mkuu wa chama changu anaweza kupanga kuniua maana hana sababu ya kufanya hivyo. Napenda kurudia kusema kwamba mimi ninaamini kuwa kila nafsi itaonja mauti. Kila mtu atakufa. Kama nitakufa kwa kuuwawa na mtu mwingine ndio itakuwa nimeandikiwa hivyo na Mungu. Ndio maana hata siku moja silalamiki kuhusu vitisho vya kuuwawa nk. Kama kuna mtu anafikiria kuwa kumuua Zitto ndio furaha ya maisha yake atakuwa anajidanganya tu maana Zitto anaweza kufa kimwili lakini mawazo, fikra na maono ya Zitto yataishi tu. Siogopi kufa maana maisha niliyoyachagua ndio haya ambayo yamejaa vitisho. Muhimu kwangu ni kufanya kazi zangu kwa bidii, uhodari na uaminifu. Siku zote nitasimamia ukweli bila kujali uchungu wa ukweli huo.
Tatu, nawashauri watu ambao wamehama CHADEMA na kuhamia vyama vingine watumie muda wao kujenga vyama vyao badala ya kila siku kuzungumzia masuala ya chama ambacho wao sio wanachama tena. Kama mtu kaamua kuhama CHADEMA anapoteza haki ya kujadili masuala ya CHADEMA maana kama angekuwa anapenda kuyajadili asingehama. Naonya mtu yeyote ambaye anatumia jina langu ili kufanikisha malengo yake ya kisiasa. CHADEMA sio pango la watesaji wala wauaji. Kama kuna mwanachama wa chama kingine cha siasa anayedhani kuna mtu ndani ya CHADEMA anapanga mipango ovu aende kwenye vyombo vya sheria kumshtaki. Matendo ya mtu mmoja yasifanyiwe propaganda kama ni malengo ya taasisi.
Nne, Nawashauri viongozi wenzangu wa CHADEMA na hasa wanachama tutumie muda wetu kujenga mshikamano ndani ya chama. Fitna, majungu, uongo, uzandiki nk kamwe havijengi chama. Chama chetu lazima kiwe mfano bora wa kuheshimu demokrasia na haki za binaadamu. Wananchi hawawezi kutoa dola kwa chama chenye mifarakano. Tusiruhusu kugawanywa kwa matakwa ya watu wachache. Tusimamie misingi ya kuanzishwa chama chetu.
=============Thread inayoongelea kilichoandikwa na Mtanzania hii hapa - https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ajwa-kumtuma-ben-saanane-kummaliza-zitto.html
Kaka we tuweke wazi ili tujue nani ni muongo
Chamakh,
Sipendi kujadili suala hili kwa kuwa ni mara nyingi sana tumekutana.Hazihesabiki.Wakati mwingine kwa siri wakati mwingine in public
Mara ya kwanza ilikua kwenye kongamano la CHASO pale Makubiri ambalo Dr.Slaa alikua mgeni Rasmi.
Mchange,Mwakajila,Dr.Kitila na baadhi ya viongozi wa CHASO kipindi kile wanaweza kuthibitisha hili.Hata kuondoka uwanjani tuliondoka pamoja kwenda pamoja kwenye gari yake
-Baada ya uchaguzi wa BAVICHA tumekutana maeneo mengi sana yakiwemo UDASA,Tamal Hotel,Southern Sand, na maeneo mengi
-Wanasiasa tuache uongo.Nawaonea huruma akina Mwampamba kwa kusalitiwa na mtu/watu waliowaamini .
Nimezisikia hizi habari zikishabikiwa na kiredio fulani kama sikosei ni clouds fm wameishabikia hii mada utadhani siyo professionals, as if ni wamama fulani wamekaa kibarazani wanajadiri umbea. Clouds FM inajipotezea sana status yake kushupalia uzushi tena kwa upendeleo, uzushi unaokichafua CCM wanakuwa kimya ila uzushi wa kuichafua CHADEMA utamsikia Geladi Hando, Kibonde na watu wa level hiyo jinsi wanavyo ishupalia kimbea,
Namshukuru Mungu kwa kuniepusha na aibu ya kutumika na wanasiasa.
Simply Zitto ndio muongo. Period.Nami sitaki kuamini kuwa Ben hajawahi kukutana na Zitto. Chadema yote hii na mikutano yote hii kweli? Kuna mmoja anaongopa hapa.