Siri ya Kuuwawa Zitto - UWONGO

Siri ya Kuuwawa Zitto - UWONGO

MHeshimiwa zitto, with all due respect, please do not sell us short, we are educated lots. I am one of your ardent supporter. Na ninajua ya Kuwa u were aware that there has always been A sinister plan to eliminate you anyways possible by some of the high ranking CDM leaders, who could never compete with you and saw you being the only obstacle to their plans. Yes I like the idea of trying to pull together the party, lakini usitufumbe macho, an usijaribu kuficha uchafu china ya carpet. Let the bad elements in Charlemagne be exposed and good riddance of them, Leo unawatetea bure tutu hao majangili, an usipoangalia watakupata tutu, Kama hukai makini. You are a thorn in their throat and there is no love between yourselves.
 
Mkuu siyo waongo tu wako zaidi ya hapo,

Kama kauli hii ya Mh.Zitto na Ben Saanane zinavyotofautiana na kushutumiana, bali pia wanafanya siasa za kuviziana. Mmoja akisinzia anatandikwa kofi la kisiasa. Na hapo harakati za uchaguzi wa viongozi wa chama hazijapamba moto.

Hii statement inaonyesha kuwa CHADEMA kimeondoka nje ya misingi ya uanzishwaji na uendeshaji wake.

quote_icon.png
By zitto
Wananchi hawawezi kutoa dola kwa chama chenye mifarakano. Tusiruhusu kugawanywa kwa matakwa ya watu wachache. Tusimamie misingi ya kuanzishwa chama chetu.

Hiyo kauli ya Zitto inaonesha kuwa kuna mfarakano ndani ya CHADEMA. Kwa vile wewe ni mfuatiliaji wa posts za humu JF utakuwa shuhuda kwamba wengi wa machadema anapozungumzwa Zitto huwa wanamsema vibaya ikiwa ni pamoja na kumtukana. Cha ajabu sijawahi kusikia kiongozi nwingine wa CHADEMA akimtetea Zitto.

Pitia pitia majina ya wachangiaji leo, kuna baadhi ya wanachadema maarufu hawamo kwa ID zao kwa kuogopa aibu!

Yuwapi Mwita Maranya?
 
Kwanza gazeti hujalielewa vizuri. Pili, sijaona bado mtu mwenye ubavu ndani na nje ya CHADEMA wa kumpeleka Mh. Zitto mahakamani zaidi ya kupiga kelele hapa JF kwa IDs ambazo siyo VERIFIED.
Toa boriti kwenye jicho lako kabla hujatoa kibanzi kwenye jicho la mwenzio.

Mbona hata wewe ni verified!?
 
Mh. Zitto, heshima kwako!

Strategy za serikali ya CCM ni devide and rule. Kwa kuwa hapa umekana kauli ile, umepiga adui bomu la maangamizi.

Umefanya jambo la busara mno mkuu. Ninaheshimu pia ujasiri wa Ben Saanane alivyotoa utetezi wake humu JF.
 
Last edited by a moderator:
Lakini hapa sio walipoweka hiyo habari nafikiri publish kabisa hii ili wakome kabisa
 
Kwanza gazeti hujalielewa vizuri. Pili, sijaona bado mtu mwenye ubavu ndani na nje ya CHADEMA wa kumpeleka Mh. Zitto mahakamani zaidi ya kupiga kelele hapa JF kwa IDs ambazo siyo VERIFIED.
Zitto hawezi pelekwa mahakamani na wanachadema ,mahakama ya zitto ni wananchi credibility yake zero hana nyimbo huyo anabebwa na CCM kwa sasa ndio alikoegemea
 
Well said,

Msimamo wa Mheshimiwa huyu toka enzi hizo pale Rev square umebaki vilevile. sijaona mabadiliko. He believes in himself. Kama ni kufa basi DUA NYINGI za wana CDM zingeshamuua. Tuseme Ukweli na wala sio kuwa ni wa CCM tu wanaomchukia. Nadhani katika ratio CDM 7 CCM 3 ambao wangependa Zito afe. Kweli au si kweli???

Lakini kwa taarifa yenu Zitto hatokufa mpaka amri ya Mungu itakapofika.

Big up MZALENDO ZITTO. Dua zangu kwako. Mungu akuepushe na mahasidi na wafitini. Nyota yako ing'are Duniani hata Mbinguni. Alilolipanga Mungu kwako liwe kama ndoto zako zilivyo.
Nafikiri wewe u r among the people who want to see CDM fails in every steps they are making to let the ordinary Mwananchi knows every bad things your party of affiliation is doing in this country. You pretend and you are using Zitto so that he can bring conflict in CDM. But i am sorry to tell that Tanzanians now can distinguish rubbish and real words. Continue with your propaganda and we will see if CDM will die as you wish. Goodluck in your ambition.
 
Je, ulishawahi kukutana na kushirikiana na Bw.Isa Ponda na Bw.Lipumba mahali popote? Natanguliza shukrani zangu!
 
kwa hiyo unakubali kuwa jamaa alitaka kumwua Zitto,maana unalazimisha kuwa wanafahamiana na kumbuka zitto alisema haya kitambo sana kuwa yawezekana kwa sura hawajawahi onana,ukiacha mawasiliano ya kupigiana simu
Ninachofahamu ni kuwa serikali ya masalia iliyokuwa inaongozwa na ZZK ilipinduliwa na Ben Saanane kama ambavyo Serikali ya JK ilivyopinduliwa na RICHMOND/DOWANS ya Rostam. Kama ambavyo haiingii akilini JK anaposema hamfahamu Rostam ndivyo hivyohivyo haiingii akilini ZZK anaposema hamfahamu aliyepindua kikundi chake cha Masalia.
 
JKT ya wiki tatu akiwa huko Rafiki yake kipenzi Denis Msacky akaamulu video aka buma ugaidi itoke,siku ambayo wanamaliza anaamwamulu rafiki yake Kipenzi kuweka front line na mapicha ya akina Dr Slaa,Ben na yeye ,Zitto he will rip what he sow, ni mwanaume wa ajabu asiye waza mbele naona yeye contract yake ya kuishi ni miaka 35 vinginevyo angekuwa makini na mchezo anaocheza hautamfikisha popote hakuna anayetumia jina lake yeye anashiriki musilete damage control hapa
Mimi naamini wachangiaji ndani ya mtandao huu ni waelewa kwa maana ya kwamba ni Watanzania walioenda Shule hivyo utambuzi wao wa mambo ni tofauti na Babu yangu aliyeishia kuangalia Mifugo yake katika maisha yake yote.Inashangaza na kutia wasiwasi pale Watu wasomi wanapojitia ujinga eti tu kwa vile Mtu fulani kaamua kuwapa vihela vya kupata chai na Andazi asubuhi hivyo kuamua kumpamba na kuandika kile atakacho dhidi ya Watu wengine.Habari hii ya Zitto kudawia kupewa sumu haikuandikwa na kuhariri na watu Mbumbu bali ni Wasomi na wanaojua miiko na maadili ya kazi yao kwa jamii wanayoiandikia.Wameamua kwa makusudi kuipa taaluma na wao wenyewe bei ya Mafungu ya Dagaa hivyo kuandika huu uchochezi ndani ya jamii ya Watanzania.
 
Napenda kusema yafuatayo:

Moja, sijawahi katika maisha yangu yote kukutana na mtu anayeitwa Ben Saanane na hivyo hicho kikao ambacho inasemekana nilikuwa naye na akajaribu kunipa sumu hakijawahi kutokea. Imetajwa Hoteli ya Lunch Time ambayo sio tu sijawahi kufika, pia hata siijui ipo wapi. Haijawahi kutokea mimi kufanya kikao cha pamoja na Ben Saanane, Juliana Shonza na Mtela Mwampamba. Hivyo habari iliyoandikwa ni ya kufikirika na hivyo naomba mwandishi ahakikishe kuwa vyanzo vyake vya habari vimempa habari sahihi.

Pili, Siamini kamwe kuwa Katibu Mkuu wa chama changu anaweza kupanga kuniua maana hana sababu ya kufanya hivyo. Napenda kurudia kusema kwamba mimi ninaamini kuwa kila nafsi itaonja mauti. Kila mtu atakufa. Kama nitakufa kwa kuuwawa na mtu mwingine ndio itakuwa nimeandikiwa hivyo na Mungu. Ndio maana hata siku moja silalamiki kuhusu vitisho vya kuuwawa nk. Kama kuna mtu anafikiria kuwa kumuua Zitto ndio furaha ya maisha yake atakuwa anajidanganya tu maana Zitto anaweza kufa kimwili lakini mawazo, fikra na maono ya Zitto yataishi tu. Siogopi kufa maana maisha niliyoyachagua ndio haya ambayo yamejaa vitisho. Muhimu kwangu ni kufanya kazi zangu kwa bidii, uhodari na uaminifu. Siku zote nitasimamia ukweli bila kujali uchungu wa ukweli huo.
You are precise and clear kwamba habari za kuuawa ni uongo uliopindukia, well done Zitto....sasa mbona bado unaendeleza madai ya vitish vya kuuawa?! Kauli kwamba "silalamiki kuhusu vitisho vya kuuawa nk. Kama kuna mtu anafikiria kuwa kumuua Zitto ndio furaha ya maisha yake atakuwa anajidanganya tu maana Zitto anaweza kufa kimwili lakini mawazo" ni kauli inayotia shaka dhamira yako ya kukanusha taarifa za kutaka kuuawa kwako!! Kama ulikuwa na lengo la kukanusha kwa dhati, usingeleta tena hapa habari za vitisho vya kutaka kuuawa kwani kauli hii inatoa tafsiri moja tu, kwamba kumbe kweli unawindwa ama umekuwa ukitumiwa vitisho vya kutaka kuuawa!! Kwa bahati mbaya kabisa, hata JF members wanaamini wazi kwamba hauna tatizo na CCM au wana-CCM lakini huenda una tatizo na Chama chako au watu wa chama chako! So, kutuletea hapa habari za vitisho ni kutufungua macho kwamba ama chama chako au watu ndani ya chama chako wamekuwa wakikutumia taarifa za vitisho! Ni very unfortunate kwamba, endapo siasa za Kimafia zitaendelea TZ basi ni rahisi hata watu wa chama kingine wakakufanyia umafia kwavile inafahamika tuhuma zitakuwa dhidi ya chama chako......kauli yako niliyoi-quote inaonesha kwamba HAMKANI HALI SI SHWARI, umekuwa ukitishiwa kifo!! Kauli ya ajabu kabisa kati kati ya kauli ya kukanusha kutaka kuuawa!
 
Last edited by a moderator:
Hajamchnijia mbali yeyeote sema akaumbuliwa hana ujanja ,Juliana Shonza anathibitisha kwamba bado wako kwenye misssion moja kuchafua chama,Zitto wakumpa pole kila siku nasema hawezi kuwa juu ya Mungu ,na aendelee na fitina majibu yake ni hapa duniani


...aisee huyu mtu pressure yake ipo juu sana, tafadhari mlie karibu nae msimwache awe peke yake, anaweza jitundika huyu, ebu jifariji dogo kwa hekima ya Wahenga, walisema "machozi ya samaki...."
 
Rafiki yako amerikoroga ujuaji mwingi hili limemvua nguo imethibitisha yeye ni kichwa cha masalia alionywa na Ben kwamba Juliana Shonza na Mtera Mwampamba huwa hawafikiri kabla ya kutenda kitu kinachowekwa kwenye gazeti ni maandishi ni ushahidi utakao kaa milele,bila kuwa na strategy nzuri ya kutengeneza propaganda wengine wanaweza kuishia jela,Zitto ni master minder hii article wiki iliyopita na mwanzoni mwa wiki hii kundi lao lote la masalia kwa ID mia walizonazo ukiwemo wewe mulimsakama sana Ben, na mwishowe mumeamua kupeleka Mtanzania mwandishi bila ajizi amewauumbua amewauliza wahusika wamesema ya kwao sasa ni kazi ya Zitto Kuwaambia Watanzania kwamba hakuwatuma hao masalia wake,nani atamwamini tena ,sterling wa kuchafua chama kwa manufaa yake mwenyewe soma message yake anasema chama hakiwezi kushinda kikiwa na mifarakano ipi wakati yeye ndie anavuruga chama baada ya pindua mbowe kushindwa sas target ni Dr Slaa hembu niambie anafanya nini na hawa baada ya kuwa kila siku wanatukana viongozi wote wa Chadema kasoro Zitto ana lugha gani sahihi atakayotuambia wananchi kuwa si sehemu ya waliopeleka mada gazetini,Kuchamba kwingi mwisho utatoka na mavi ndivyo gazeti la Mtanzania lilivyomtenda Zitto,kumdharilisha beyond uwezo wake wa kujijitetea ,Denis Msaky best friend wake yuko kwenye centre ya Lwakatare ukijumlisha moja na moja huwa mbili

Tafadhalini,nimemfahamu zitto na shonza,hao wengine ni kina nani?
 
Hiyo kauli ya Zitto inaonesha kuwa kuna mfarakano ndani ya CHADEMA. Kwa vile wewe ni mfuatiliaji wa posts za humu JF utakuwa shuhuda kwamba wengi wa machadema anapozungumzwa Zitto huwa wanamsema vibaya ikiwa ni pamoja na kumtukana. Cha ajabu sijawahi kusikia kiongozi nwingine wa CHADEMA akimtetea Zitto.

Pitia pitia majina ya wachangiaji leo, kuna baadhi ya wanachadema maarufu hawamo kwa ID zao kwa kuogopa aibu!

Yuwapi Mwita Maranya?

Kama ulivyosema, kuna baadhi ya watu huwa wako hapa 24/7 kujibu kila bandiko linalohusu CHADEMA na baadhi ya viongozi. Huwezi kuwaona wanamtetea Mh. Zitto na ndiyo maana kwa sasa hawaonekani na hata wale ambao wanaonekana, kwa sasa wako mstari wa mbele kumpongeza Mh. Zitto kwa pongezi za kejeli. Hii ni ishara tosha kuonyesha kuwa CHADEMA kumejaa vijana vinyonga na maslahi tumbo. Hawako kwa maslahi ya CHADEMA bali kwa maslahi ya viongozi wachache ndani ya CHADEMA.
 
Tatu, nawashauri watu ambao wamehama CHADEMA na kuhamia vyama vingine watumie muda wao kujenga vyama vyao badala ya kila siku kuzungumzia masuala ya chama ambacho wao sio wanachama tena. Kama mtu kaamua kuhama CHADEMA anapoteza haki ya kujadili masuala ya CHADEMA maana kama angekuwa anapenda kuyajadili asingehama. Naonya mtu yeyote ambaye anatumia jina langu ili kufanikisha malengo yake ya kisiasa. CHADEMA sio pango la watesaji wala wauaji. Kama kuna mwanachama wa chama kingine cha siasa anayedhani kuna mtu ndani ya CHADEMA anapanga mipango ovu aende kwenye vyombo vya sheria kumshtaki. Matendo ya mtu mmoja yasifanyiwe propaganda kama ni malengo ya taasisi.

Wambie na wenzako muache kuijadili ccm na viongozi wake kwakuwa ninyi siyo wanaccm na vile vile mtudokeze huyo mwenye mipango ya pekeake ambayo inahusishwa na chama ni nani?
 
Ameweka press release kwenye blog yake na facebook na twitter for information. Media are free to publish or ignore it. Yeye anasema pale anapoweza kusema. Huko mtanzania hana mamlaka napo.
You might be right, but my point is, hizi habari alitakiwa kuzikabnusha tangu mara ya kwanza hapa JF badala ya kuziacha!! Hainiingii akilini kwamba habari ile ilitolewa hapa JF na akaiacha watu wa-swalllow kama ilivyo lakini miezi kadhaa baadae anakuja kuikanusha hapa hapa JF lakini baada ya kutoka gazetini! Suala la Zitto kuiacha ile habari hapa JF ilikuwa ni kama aliona haikufaa kukanushwa na si ajabu ndio maana watu wakaiendeleza!
 
Kama Benn akiwa ni kijakazi sasa jiulize we si ndo utakuwa umefunga ndoa na Mwigulu kabisa maana naona unajitahidi kusafisha nyota za bundi ambazo hazisafishiiki kwa kutegemea ujira wa lumumba.

Pole kwa utumwa wa fikra unapiga kelele tu hapa kwa akili za kuazima.
 
Ben Saanane u wp? Utuambie ukweli wa jambo hili na uhusika wa zitto ktk kundi la masalia.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom