Siri ya Kuuwawa Zitto - UWONGO

Siri ya Kuuwawa Zitto - UWONGO

This is what i callTalk firstTalk fast Talk truthBravo Zitto.
 
Heshima ya Upande mmoja! Hapa Zitto utapongezwa kwakuwa tu 'umem-save' 'nabii' SLAA. Hawa hawa ndio wanaokuporomoshea matusi kila siku! Lengo lao wakutumie tu kama 'kile kifaa' kisha waku-dump! Sijui kama hulijui hili!

Ndugu acha kuwewezeka Mh. Zitto amesema yote. Fahamu kuwa CDM wana udhubutu wa hali ya juu wa kukemea mabaya ya mtu ye yote bila kificho. Kigezo hiki cha kupendaukweli na uwazi kinaongeza zaidi nafasi ya CDM kushinda uchaguzi 2015.Elewa kama unasubiri Dr. Slaa na Zitto wagombane utasubiri sana,
 
Last edited by a moderator:
Katika gazeti la Mtanzania toleo na. 7269 la Jumatano Machi 27, 2013 kuna habari yenye kichwa chenye maneno ‘SIRI YA KUUWAWA ZITTO YAFICHUKA’ na vichwa vidogo ‘yadaiwa ilipangwa anyweshwe sumu hotelini’ dk. Slaa atajwa kumtuma Saanane kummaliza’. Habari hii imeniletea usumbufu mkubwa kwani ndugu, jamaa, marafiki na wapiga kura wangu, wamejazwa na wasiwasi mkubwa sana kwamba ninaweza kuuwawa.

Napenda kusema yafuatayo:

Moja, sijawahi katika maisha yangu yote kukutana na mtu anayeitwa Ben Saanane na hivyo hicho kikao ambacho inasemekana nilikuwa naye na akajaribu kunipa sumu hakijawahi kutokea. Imetajwa Hoteli ya Lunch Time ambayo sio tu sijawahi kufika, pia hata siijui ipo wapi. Haijawahi kutokea mimi kufanya kikao cha pamoja na Ben Saanane, Juliana Shonza na Mtela Mwampamba. Hivyo habari iliyoandikwa ni ya kufikirika na hivyo naomba mwandishi ahakikishe kuwa vyanzo vyake vya habari vimempa habari sahihi.

Pili, Siamini kamwe kuwa Katibu Mkuu wa chama changu anaweza kupanga kuniua maana hana sababu ya kufanya hivyo. Napenda kurudia kusema kwamba mimi ninaamini kuwa kila nafsi itaonja mauti. Kila mtu atakufa. Kama nitakufa kwa kuuwawa na mtu mwingine ndio itakuwa nimeandikiwa hivyo na Mungu. Ndio maana hata siku moja silalamiki kuhusu vitisho vya kuuwawa nk. Kama kuna mtu anafikiria kuwa kumuua Zitto ndio furaha ya maisha yake atakuwa anajidanganya tu maana Zitto anaweza kufa kimwili lakini mawazo, fikra na maono ya Zitto yataishi tu. Siogopi kufa maana maisha niliyoyachagua ndio haya ambayo yamejaa vitisho. Muhimu kwangu ni kufanya kazi zangu kwa bidii, uhodari na uaminifu. Siku zote nitasimamia ukweli bila kujali uchungu wa ukweli huo.

Tatu, nawashauri watu ambao wamehama CHADEMA na kuhamia vyama vingine watumie muda wao kujenga vyama vyao badala ya kila siku kuzungumzia masuala ya chama ambacho wao sio wanachama tena. Kama mtu kaamua kuhama CHADEMA anapoteza haki ya kujadili masuala ya CHADEMA maana kama angekuwa anapenda kuyajadili asingehama. Naonya mtu yeyote ambaye anatumia jina langu ili kufanikisha malengo yake ya kisiasa. CHADEMA sio pango la watesaji wala wauaji. Kama kuna mwanachama wa chama kingine cha siasa anayedhani kuna mtu ndani ya CHADEMA anapanga mipango ovu aende kwenye vyombo vya sheria kumshtaki. Matendo ya mtu mmoja yasifanyiwe propaganda kama ni malengo ya taasisi.

Nne, Nawashauri viongozi wenzangu wa CHADEMA na hasa wanachama tutumie muda wetu kujenga mshikamano ndani ya chama. Fitna, majungu, uongo, uzandiki nk kamwe havijengi chama. Chama chetu lazima kiwe mfano bora wa kuheshimu demokrasia na haki za binaadamu. Wananchi hawawezi kutoa dola kwa chama chenye mifarakano. Tusiruhusu kugawanywa kwa matakwa ya watu wachache. Tusimamie misingi ya kuanzishwa chama chetu.

Mkuu Zitto yaani umenusuru Moyo wangu na msongo wa mawazo maana kwa hakika mimi huwa napendelea kusoma magazeti na kusikiliza radioni ila ya leo asubuhi yameniharibia siku baada ya kusikia habari hii japokuwa kwa hakina nilikuwa naamini kuwa si ya kweli ila uongo ni dhambi sikuweza kujizuia NIMEHUZUNIKA SANA na nkawa najiuliza nani wa kuniondolea tongo tongo hili kichwani mwangu...yaani mh zitto umenisafisha akili yangu na ule msongo umepotea ghafla...
ahsante zitto..
chadema oyeeeeeeeeeeeeeee....
hekima zako zitto ni nzitto sana regardless of your shortcomings as human being....
Chama kinakutegemea sana zitto na busara zako na promptness kama hii ya ku pre-empt njama za wabaya wa chama kama hawa watu wanaokichafua chama kwa mbinu mbali mbali.
Endelezeni mshikamano baina yenu wakubwa wa chama wekeni tofauti zenu za kibinadamu pembeni,jengeni chama ili wabaya wa chadema waumie matumbo yao..
maana wabaya wa chadema wanafurahia sana habari kama za gazeti la mtanzania la leo ziwe za ukweli ama za uongo wao hawajalishi...

asalaaaam....
 
katika gazeti la mtanzania toleo na. 7269 la jumatano machi 27, 2013 kuna habari yenye kichwa chenye maneno ‘siri ya kuuwawa zitto yafichuka’ na vichwa vidogo ‘yadaiwa ilipangwa anyweshwe sumu hotelini’ dk. Slaa atajwa kumtuma saanane kummaliza’. Habari hii imeniletea usumbufu mkubwa kwani ndugu, jamaa, marafiki na wapiga kura wangu, wamejazwa na wasiwasi mkubwa sana kwamba ninaweza kuuwawa.

Napenda kusema yafuatayo:

Moja, sijawahi katika maisha yangu yote kukutana na mtu anayeitwa ben saanane na hivyo hicho kikao ambacho inasemekana nilikuwa naye na akajaribu kunipa sumu hakijawahi kutokea. Imetajwa hoteli ya lunch time ambayo sio tu sijawahi kufika, pia hata siijui ipo wapi. Haijawahi kutokea mimi kufanya kikao cha pamoja na ben saanane, juliana shonza na mtela mwampamba. Hivyo habari iliyoandikwa ni ya kufikirika na hivyo naomba mwandishi ahakikishe kuwa vyanzo vyake vya habari vimempa habari sahihi.

Pili, siamini kamwe kuwa katibu mkuu wa chama changu anaweza kupanga kuniua maana hana sababu ya kufanya hivyo. Napenda kurudia kusema kwamba mimi ninaamini kuwa kila nafsi itaonja mauti. Kila mtu atakufa. Kama nitakufa kwa kuuwawa na mtu mwingine ndio itakuwa nimeandikiwa hivyo na mungu. Ndio maana hata siku moja silalamiki kuhusu vitisho vya kuuwawa nk. Kama kuna mtu anafikiria kuwa kumuua zitto ndio furaha ya maisha yake atakuwa anajidanganya tu maana zitto anaweza kufa kimwili lakini mawazo, fikra na maono ya zitto yataishi tu. Siogopi kufa maana maisha niliyoyachagua ndio haya ambayo yamejaa vitisho. Muhimu kwangu ni kufanya kazi zangu kwa bidii, uhodari na uaminifu. Siku zote nitasimamia ukweli bila kujali uchungu wa ukweli huo.

Tatu, nawashauri watu ambao wamehama chadema na kuhamia vyama vingine watumie muda wao kujenga vyama vyao badala ya kila siku kuzungumzia masuala ya chama ambacho wao sio wanachama tena. Kama mtu kaamua kuhama chadema anapoteza haki ya kujadili masuala ya chadema maana kama angekuwa anapenda kuyajadili asingehama. Naonya mtu yeyote ambaye anatumia jina langu ili kufanikisha malengo yake ya kisiasa. Chadema sio pango la watesaji wala wauaji. Kama kuna mwanachama wa chama kingine cha siasa anayedhani kuna mtu ndani ya chadema anapanga mipango ovu aende kwenye vyombo vya sheria kumshtaki. Matendo ya mtu mmoja yasifanyiwe propaganda kama ni malengo ya taasisi.

nne, nawashauri viongozi wenzangu wa chadema na hasa wanachama tutumie muda wetu kujenga mshikamano ndani ya chama. Fitna, majungu, uongo, uzandiki nk kamwe havijengi chama. Chama chetu lazima kiwe mfano bora wa kuheshimu demokrasia na haki za binaadamu. Wananchi hawawezi kutoa dola kwa chama chenye mifarakano. Tusiruhusu kugawanywa kwa matakwa ya watu wachache. Tusimamie misingi ya kuanzishwa chama chetu.
mjomba life is not a rehersal is a performance nimefurahishwa sana na hii paragraph ya nne!!!!!!!umemaliza kila kitu ccm mijinga mijinga tu.
 
Nilipoiona habari ile katika gazeti, kwanza nilicheka, kisha nikapandwa na hasira, nakisha zaidi nikazama katika tafakuri pana,

Nilifanya hivyo kwa dhana ileile ya hakuna upuuzi ulio upuuzi mtupu,


Nilisubiri kauli ya ndugu yangu Zitto kwakuwa niliamini fika kuwa ni lazima ajibu, tena mapema na jibu lake ndio hili.

Kwanza kabisa dhana yakujibu namsifu kwa asilimia mia, Pili mizani ya majibu yake inahitaji tafakuri pana na ya nera zaidi.
 
Hivi ni nani yule aliimba: kumbe CCM waongo, au nilikuwa naota? Nayachukia haya maCCM.
 
Well said,

Msimamo wa Mheshimiwa huyu toka enzi hizo pale Rev square umebaki vilevile. sijaona mabadiliko. He believes in himself. Kama ni kufa basi DUA NYINGI za wana CDM zingeshamuua. Tuseme Ukweli na wala sio kuwa ni wa CCM tu wanaomchukia. Nadhani katika ratio CDM 7 CCM 3 ambao wangependa Zito afe. Kweli au si kweli???

Lakini kwa taarifa yenu Zitto hatokufa mpaka amri ya Mungu itakapofika.

Big up MZALENDO ZITTO. Dua zangu kwako. Mungu akuepushe na mahasidi na wafitini. Nyota yako ing'are Duniani hata Mbinguni. Alilolipanga Mungu kwako liwe kama ndoto zako zilivyo.
Hakuna mwana chadema anayependa zitto afe ila wanataka mikono ya ccm inayomuelekea zitto ikatiliwe mbali ..
zitto ni kipenzi cha wana chadema hilo halina ubishi..wanachadema huwa wanasikitika sana wasiojua mienendo ya zitto....
wanataka kumuona zitto wao majukwaani,kwenye kila matukio ya chadema wanataka kumuona yupo ...hivyo ndo ilivyo mkuu...
zitto ni chadema na chadema ni zitto...
zitto + mbowe +dr.slaa == ushindi wa chadema 2015...

zitto + mbowe +dr.slaa== maumivu,kuchanganyikiwa kwa ccm
mbowe +dr.slaa - zitto == furaha na ahueni kwa ccm na mafisadi wote...
 
Bwana Mtela, Saanane na Shonza njooni huku mmevuliwa nguo hadharani na kila mtu anatazama viungo vyenu vya uzazi bila hata malipo!! Hongera kamanda Zitto kwa kuusema mtazamo wako hadharani, wengine wangefukia chini ya kapu.
 
Kuna kauli moja ya kifalsafa inasema hivi; ''wapo wale wawazao mema kuanzia nafsini mwao hadi kwenye jamii yao, hawa huitwa wenye hekima ila kuna wale wawazao njama, visa,chuki, machafuko na hata vita,hawa tunawaita washenzi''. Mh. ZZK umeonesha nia ya dhati kuanzia nafsini mwako kwamba we si mtu wa kuyumbishwa na political assassination propaganda tunakuombea uendelee na moto huo ili maadui tuwaone kama rafiki japo tunaijua tahadhari ya unafki wao. Big up.

LOGIC
wapo wale wawazao mema kuanzia nafsini mwao hadi kwenye jamii yao, hawa huitwa wenye hekima
kuna wale wawazao njama, visa,chuki, machafuko na hata vita,hawa tunawaita washenzi
''

CONCLUSION: ZITTO : MWENYE HEKIMA
DR.SLAA: MSHENZI

LOGICALLY PROVED.

ww unasemaje????????????????????????????
 
Mkuu Zitto,

Unaonanaje ungewaomba Mtanzania wakuombe radhi kwa kuandika habari nzito kama hiyo bila ridhaa yako?
Tena , unaonaje ukaitisha Press conference uwakane hao akina Shona & Co. kwamba huhusiani nao? Maana huko nyuma hujwahi kuwakana na mpaka leo wanakutetea kwa hali zote. Mie nadhani, badala ya kukanusha kijuu juu hivi uonyeshe kuchukizwa kwako na hilo kundi kwa matendo
 

Juliana na kundi lako umesikia wosia wa Zitto kabwe? maana nyie kutwa nzima mpo JK kuchafua hali ya hewa hivi mnapata muda hata wa kupitia ilani yenu ya CCM na kuielewa? hivi hiyo mlivyofundishwa kwamba kwenye siasa mchafue mwenzako? tumewachoka.

Yaani ni sawa Unampa taraka mkeo au mumeo lakini kutwa kucha unaongelea ubaya wake, mwenye akili timamu lazima atagundua kuwa wewe u zuzu.

Asante Zitto kutuweka sawa kwa hili, ila umeniacha njia panda kwenye sentensi hii "
Matendo ya mtu mmoja yasifanyiwe propaganda kama ni malengo ya taasisi." nitaomba ufafanuzi wako kama una muda.

Otherwise nakubaliana na wewe kwamba
CDM kipo imara na kitavuka hiki kikwazo cha mwisho kuelekea ukombozi wa kweli wa taifa hili.

Jamani wabongo tu wagumu kuelewa hata Kiswahili rahisi ama mantiki sahili kama hii! Chama ni taasisi au asasi ambayo inakamilishwa na ujumla wa mtu mmoja mmoja wawe viongozi au wanachama hata washabiki. Mimi ninafikiri ametaka kusisitiza kuwa huyo mtu mmoja mmoja ni binadamu ambaye anaweza kutenda makosa yake binafsi (hakutumwa na chama) kama walivyo binadamu wanachama wa CCM au CUF au hata wafanyakazi wa kampuni. Makosa binafsi ya mwanachama, kiongozi, mfanyakazi, nk yasichukuliwe kuwa ni makosa ya kitaasisi kama ambavyo inaelekea kuwa utamaduni wa kisiasa (siasa za majitaka) unaoibukia nchini bongoland!!
Pokea pongezi zangu Mhe Zitto kwa kulitolea suala hili ufafanuzi wa kuridhisha. Wewe ni mfano kwa vijana wanaowania kuingia katika siasa jinsi ulivyoanza, na unavyoendelea kukua na kuelekea kukomaa!
 
Ben saanane is typing.............

Ndugu jaribu kuficha husuda yako kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu. Kamanda Zitto keshatoa tamko,chapa kazi za kujenga taifa. BenSaanane anafahamu Zitto ni kiongozi wake hivyo anaelewa nini kifanyike kwa ajili ya kuimarisha afya ya chama. Time is money and remember 2014/2015 is around the corner,
 
Last edited by a moderator:
Hajamsfundisha bali amemshauri. Hakuna mtu asiyeshauriwa, huenda wewe utakuwa wa kwanza. Hata rais ana rundo la washauri.
Mkuu ni kweli hakuna mtu asiyeshauriwa lakini ushauri unatolewa pale mtu anapotaka ushauri, halafu pia kuna taratibu zake. sidhani kama Invisible ametaka huo ushauri.

Ni wazo langu tu.
 
Last edited by a moderator:
Matendo ya Lwakatare yasifanywe ni malengo ya taasisi.
 
Ben: 'Nimeshawahi kuonana na Zitto'
Zitto: '
Sijawahi kuonana na Ben'


Integrity: Sifa kuu ya kiongozi


Ukweli ndio msingi wa uaminifu kwa kiongozi. Kiongozi ni Yule anayesema ukweli siku zote na sehemu yoyote.


Nimegundua kitu kimoja ndani ya CHADEMA: Baadhi ya viongozi si wa kweli.

Ni nani mkweli kati ya Zitto na Ben Saanane?

Kwa vile wote hawawezi kuwa wakweli, what is the future of politics in our country and CHADEMA in particular?

Ikiwa mmeanza kuwa waongo ndani ya chama chenu, mtakuwa wakweli kwa taifa?
Kwa vile wote hawawezi kuwa wakweli, what is the future of politics in our country and CHADEMA in particular?

Ikiwa mmeanza kuwa waongo ndani ya chama chenu, mtakuwa wakweli kwa taifa?



 
Back
Top Bottom