Siri ya Kuuwawa Zitto - UWONGO

Siri ya Kuuwawa Zitto - UWONGO

Ndugu yangu Zitto napenda kukushukuru kwa kujibu gazeti hilo la Mtanzania. Maneno uliyoyaandika hapa haina unafiki hata mmoja. Haya maneno ni maneno ya busara na maneno ya Mungu. Sitokusahau siku ile uliposimama pale Revolution square pale mlimani na kuonyesha msimamo wako. Ninaamimi sana katika msimamo na hautatuangusha sisi vijana wenzako katika kupigania haki na ukweli katika nchi hii, hata kama ina uchungu. Ninakuombea kwa Mungu akubariki utujengee chama chetu cha chadema. Najua watu wengi wamo humo wanatumiwa na CCM ili CDM kife. Angalia walivyoiuwa CUF kwa kutumia mbinu zile zile wanazotumia sasa. Mungu akubariki mheshimiwa.
 
Ili kuonyesha kwamba hauko na masalia mwampamba na shonza,peleka mahakamani wakulipe mabilioni au waombe msamaha hadharani
 
Before I was like; if Zitto is as bright as many think he is,he shld say something about what Mtanzania wrotte....there you go.
Respect.
 
Umeambiwa utumie muda kuimarisha chama chako
Jadilini yote, Toeni pongezi zote lakin hii tamko la Zitto halitakuwa na maana endapo tu hataitisha press conference ili jamii ya nje ambayo idadi kubwa iweze kujua ukweli huu, Pia Zitto uache lugha tata katika maelezo yako kwan unazidi kuchanganya watu na kuwapa binamu zako wa damu CCM cha kupigia propaganda mfano unaposema sijui "malengo ya mtu mmoja yasifanywe kuwa ni ya taasisi"

Pia cha mwisho uache vita yako kwa Ben Saanane kwan unajishushia hadhi mwenyewe kwan Ben si mjinga kama unavyofikiri ww, kwani unapotumia masalia kumchafua usifikiri taarifa hazimfikii,

All in all Bravo Zitto kwa kuonesha uthubutu.
 
Mkuu nadhani unafurahia sana utengano, Kamanda kesha sema na inaeleweka sasa wewe hukatazwi kutoa maoni lakini siyo ya kuendeleza utengano, after all mwenyewe ndio kasema hivyo na hatakiwi kulazimishwa kusema tunavyofikiri.
Nisome vizuri mkuu.
 
Yeyote atoae kauli hasi dhidi ya mwenzie anatengeneza sumu kali ndani ya roho yake na uadui mkubwa kwa wanaomzunguka..Jiepusheni na watu wa aina hii.
Kama CLOUDS wameshadidia sioni ajabu maana kipindi chao siku hizi ni kama cha Dida wa Times moreover with people like Kibonde ndani ya Redio wht would you expect..
mwanaume/mwanamke wa kweli husikiliza redio zenye maslahi na nchi na si redio za umbea
Zitto welcome uraiani kamanda..hongera kwa kuhitimu mafunzo. Ila Halima kama amekufunika kaka maana alionekana full kamanda ahahaaaaaaaa
 
Zitto mzito!labda mjaribu tena siku nyingine mje na winchi!kawapangua panguu!mnajaribu sana kumpotezea dira lakini huyu kijana makini!mnajaribu sana kumfarakanisha na viongozi wenzake wa chama chake lakini wapi!..the number you are calling is not reachable,please try again later...!na lile gazeti lililoandika habari hizi lile..bora kina Ulimwengu wangebaki na kampuni yao tu!
 
Hongera sana kijana mwenzangu, mpigania rasmali za taifa letu pia ni mwanamkombozi wa kweli. Hongera kwa kumaliza mafunzo ya JKT na pia nimefurahi leo ulivyotelea ufafanuzi wa haya mabo kwa Undani na maelezo yalinyooka.Sijui watu wanataka kuipeleka nchi yetu wapi..
 
Watakuja kwa njia moja lakini watatawanyika kwa njia saba. Na hizo njia zitaongezeka tu tunapoelekea uchaguzi ujao!
 
Vizuri sana Zitto kwa ufafanuzi mzuri.Gazeti la Mtanzania siku hizi limekuwa kama gagulo la kuandika uchochezi,chuki,fitina,majungu na uzandiki dhidi ya Chadema hasa likimuandama Dr Slaa.

Sijui kwanini Hussein Bashe anaruhusu gazeti hili kuandika upuuzi kama huu.

Again Thankyou Zitto you have made my day.

Gazeti hili liliwahi kuandika habari za Kituo kimoja cha Kiislam Ukerewe kuwa kinafunza magaidi wa alshabaab na alqaeda na kwamba kinaingiza makontena ya Silaha huku kamanda wa mkoa akishangaa uzushi huo mkashangilia. Leo hii mnaliona halina maana na limejaa fitina na uzushi.
Huwa napenda tuwe wazalendo katika kila jambo hata kama hulipendi au huwapendi wasemwaji na tuache unafiki.

Wakati mwengine waandishi hujitakia wenyewe. ndio maana akina Lwakatare wanapata mwanya wa kufanya UGAIDI.

Je, unaonaje kama ukimpata mwandishi wa habari hii na una ruhusa ya kufanya chochote utafanyaje??

Basi wewe ni GAIDI # 3.
 
Nakadiria kati ya siku 12-15 zijazo tutakuwa tena na kazi ya kusoma hapa thread ya "kiuchuzi" au "kiuchambuzi" ambayo itakuwa inapata sapoti toka kwa mwanzilishi akitumia IDs zake zaidi ya tano ikijitahidi sana kumchonganisha Zitto na wanachadema. Niwaambie tu watu wanaodhani kuwa CDM itasambaratishwa kwa kumchonganisha Zitto hamna tofauti na fisi anayedhani atapatanyama kwa mkono wa binadamu kudondoka, pale anapoona ukitikisika,
...
 
Mh.zitto haya magazeti yetu na vyombo mbalimbali vya serekali vinaendeshwa na skendo/mawazo ya watu humu jamii forums
1)TCRA ilivifungia vyombo kadhaa vya habari baada ya thread kuanzishwa humu
2)gazeti hilo la mtanzania na magazeti mengine yanaendeshwa na habari wanazoziona huku
3)hata kukamatwa kwa lwakatare walipata hiyo clip hukuhuku jamii forums
Kwaiyo nadhani wasikupe shida sana na pili washauri wabadilike kama nchi inaendeshwa na mawazo ya watu hapa jf inasikitisha

Kikubwa mheshimiwa zitto nakushauri hama chadema na utengeneze chama chenye malengo ya kumkomboa mtanzania
Chadema imeshaoza sana .........Take this from me

sio lazima kuchangia kila mada.
 
safi kiongozi kwa kuweka uwazi uhuisano wako na katibu
 
Mara nyingi sana hapa jukwaani ben amekuwa akimsakama zitto kwa tuhuma za kuhujumu chama lakini zitto kwa busara zake hataki kabisa kulumbana na ben.. Hii ndio sifa ya kiongozi na tofauti kubwa iliyopo kati ya zitto na ben
[MENTION]ben sanane[/MENTION]salamaa
 
Kazi kwa stella mwampamba a.k.a mtela mwampamba na mwenzie sasa kutengeneza story za kesho ili maboss wake wa lumumba wampe token ya pasaka,toto kubwa linakuwa jingajinga tu utanisababishia ban bure pasaka yote hii,tupo pamoja kamanda zitto.fresh from jkt.
 
Kwa hili Zitto umetumia hekima sana, nakupongeza kwa dhati pia kwa maneno yako ya busara. Ni kweli muda huu ni wa kujenga chama siyo kurumbana. Endelea hivo hivo na usiwape nafasi wanao jitahidi kutumia jina lako kuleta mfarakano ndani ya CHADEMA.
 
Ndugu yangu Zitto napenda kukushukuru kwa kujibu gazeti hilo la Mtanzania. Maneno uliyoyaandika hapa haina unafiki hata mmoja. Haya maneno ni maneno ya busara na maneno ya Mungu. Sitokusahau siku ile uliposimama pale Revolution square pale mlimani na kuonyesha msimamo wako. Ninaamimi sana katika msimamo na hautatuangusha sisi vijana wenzako katika kupigania haki na ukweli katika nchi hii, hata kama ina uchungu. Ninakuombea kwa Mungu akubariki utujengee chama chetu cha chadema. Najua watu wengi wamo humo wanatumiwa na CCM ili CDM kife. Angalia walivyoiuwa CUF kwa kutumia mbinu zile zile wanazotumia sasa. Mungu akubariki mheshimiwa.

Well said,

Msimamo wa Mheshimiwa huyu toka enzi hizo pale Rev square umebaki vilevile. sijaona mabadiliko. He believes in himself. Kama ni kufa basi DUA NYINGI za wana CDM zingeshamuua. Tuseme Ukweli na wala sio kuwa ni wa CCM tu wanaomchukia. Nadhani katika ratio CDM 7 CCM 3 ambao wangependa Zito afe. Kweli au si kweli???

Lakini kwa taarifa yenu Zitto hatokufa mpaka amri ya Mungu itakapofika.

Big up MZALENDO ZITTO. Dua zangu kwako. Mungu akuepushe na mahasidi na wafitini. Nyota yako ing'are Duniani hata Mbinguni. Alilolipanga Mungu kwako liwe kama ndoto zako zilivyo.
 
Back
Top Bottom