SoC02 Siri kuu saba zilizonifanya kufungua kiwanda baada ya kufukuzwa Chuo

Stories of Change - 2022 Competition

tenachew

Member
May 27, 2021
10
10
Siri kuu saba zilizonifanya kuanzisha kiwanda baada ta kufukuzwa chuo.

Moja kati ya shughuli za kiuchumi zenye kuleta mageuzi makubwa Kwa uchumi wa nchi yoyote ni kuanzisha viwanda. Kuanzisha na kuendesha viwanda ni rahisi sana kwa mtu binafsi hasa ukipewa Siri yake. Hapa kuna siri kuu saba ambazo Heri Aloyce Mtanga, ambae ni mmiliki na mwanzilishi wa kiwanda Cha Mtanga polymachinery industry kilichopo picha ya ndege, kibaha mkoani pwani kinachojihusisha na utengenezaji vinu,mitambo na mashine mbalimbali amekiri kuzitumia na kupata mafanikio makubwa baada ya kuwa amefukuzwa chuo (kudisco) tembelea Mtanga Polymachinery .

Leo napenda kukupa Siri kuu saba za kufanikiwa kuanzisha na kuendesha kiwanda au viwanda. Hapa Nazungumzia kiwanda kinachohusisha Utengenezaji au uundaji wa bidhaa Kama vile Utengenezaji bidhaa za chuma kama mashine aina mbalimbali, gari, Vinu vya kuendesha mitambo, viwanda vya kugeuza malighafi za asili kuwa bidhaa , vifaa vya tiba Kama hadubini,uchakataji bidhaa za vyakula, vipodozi na bidhaa zingine anuai.Kama una ndoto ya kuanzisha kiwanda Chochote hizi hapa Siri kuu sita za kuanzisha kiwanda.

Siri ya kwanza ni kuanza Kuanza hapa inamaanisha kuchukua hatua za kutekeleza wazo Kwa vitendo bila kujali una ujuzi, una mtaji, una vitendea kazi ,umesajiri biashara yako, una eneo la kiwanda au pa kuanzia. Hii siri ya kuanza imekwamisha wengi Kwa kujiwekea vikwazo vya nitaanzaje, sijui , mtaji sina au kuogopa na kudhania huenda Kuna mambo ya kujua kwanza . Heri Mtanga Alianza Kwa kuning'ing'iniza kipande cha chuma juu ya mti na alipoanza kuunganisha chuma aligundua mambo mengi yaliyomtia moyo kukundua zaidi .

Siri ya pili ni kujaribu Hii ni siri ya pili ambayo pia Heri Mtanga aliitumia na anaendelea kuitumia ni kujaribu asichokijua. Alipotengeneza incubator Kwa Mara ya kwanza aligundua pia anaweza kutengeneza friji na alipotengeneza friji aligundua na akajaribu pia kutengeneza oven ya kuoka mikate, mashine ya kutengenezea vipodozi, kusaga unga, kuvuna mpunga na mengine mengi. Anza na ukianza jaribu pia usichokijua utagundua siri ya ubunifu ulionao maradufu.​

Siri ya tatu ni uzalendo
Kuwa mzalendo namaanisha kutanguliza mbele masirahi ya taifa lako . Kwa mtanzania yeyote hapa inampasa atambue ni ukweli usiopingika kuwa mafanikio ya viwanda inahitaji ujitoe kushirikiana na watanzania , ukiwapa nafasi na kusikiliza mawazo yao,kuwa mtii ya sheria za nchi na kuzingatia kanuni zote za uendeshaji shughuli. Hapa namaanisha ukishaanzisha kiwanda chako, kisajili, rasimisha shughuli zake, lipa Kodi na fuata taratibu zote za uendeshaji biashara. Nakuhakikishia ukizingatia uaminifu wa kufuata sheria za nchi utaona watu wenye hela wakikufuata na utaona mafanikio makubwa ya kiwanda chako , alieleza Mtanga.

Siri ya nne ni kuiba teknolojia ya kigeni
Hii Siri ndio inawezesha kuimarisha na kukiendeleza kiwanda chako. Hii nimekuwa shahidi mwenyewe kwani imepelekea ukuaji na pia kiwanda changu kuwa imara na mfano wa kuigwa Kwa viwanda vyote vya wazawa Kwa Tanzania. Kiukweli Hii ndio maana ya ubunifu , unachukua alichonacho mwenzako Kisha unaongeza ubora na kukifanyia mfumo mpya na wa kisasa zaidi. Nimejifunza Mengi sana nikitumia teknolojia ya machina ambayo ni rahisi kuigwa na kuitumia kubuni na kuanzisha mifumo mingine inayofanana kiutendaji.Hivyo Kwa watanzania nawasihi tutumie teknolojia za nje kuboresha bunifu zetu .​

Siri ya tano ni kujifunza Kila siku
Kwa upande wangu nilijawa na hamasa ya kujifunza Kwa kutembelea viwanda mbalimbali vilivyokuwa karibu nami katika wilaya ya kibaha mkoani pwani. Nilitembelea ofisi za TBS, TMDA na SIDO na sehemu mbalimbali na nilitoka nimehamasika Sana na kujiona nimebarikiwa Sana na kuwa nina ujuzi mwingi nimechelewa kuanza.anaendelea kueleza Mtanga kuwa, hii imekuwa ni Siri kwangu iliyonifanya kuanzisha kiwanda na ni kweli haikuwa rahisi Ila badae niliona mafanikio makubwa ambayo sikuyategemea. Moja ya mafanikio yangu ni kuweza kutengeneza mashine mbalimbali zaidi ya aina 50 za mitambo na Vinu, nimeweza pia kuajiri watanzania wengi na ukifika utajionea mwenyewe kina wahitimu wa chuo wenye GPA kali wapo hapo.

Siri ya sita ni kurasimisha biashara yangu
Kurasimisha biashara ni kuifanya au kuiingiza biashara yako katika mfumo wa kiutendaji unaokubalika kisheria. Kurasimisha biashara kunaifanya biashara kuaminika na watu hasa wahisani ambao watakupatia nguvu kifedha kwa njia ya mkopo, ruzuku au hata kuwekeza mitaji yako kwenye biashara yako. Niwape siri moja ya mafanikio ya kibiashara kwenye Karne hii ni kuwa , tasisi nyingi, makampuni na hata watu binafsi siku hizi hawatoi fedha zao Kwa mtu binafsi badala yake watatoa Kwa kikundi kinachoaminika Kama vile kampuni,SACCOS , NGOs na kadhalika. Kwa hiyo ukitaka msaada kifedha basi rasimisha biashara yako kwa kusajiri kampuni au mfumo wowote unaoaminika.

Siri ya saba ni kujitangaza
Kujitangaza ni kujiweka katika hali ya kujulikana na kufikiwa na wengi. Hii ni njia rahisi Sana iliyonipatia mafanikio katika kukuza kiwanda changu na kikiendeleza. Nimetumia sana sana mitandao ya kijamii,nimetumia tv na radio kutoa elimu juu ya umuhimu wa kujiajiri na kuepuka utegemezi.Kwa wanaofatilia watakuwa mashahidi kupitia morning star radio na Hope channel Tanzania ambapo hutoa elimu na kuhamasisha vijana kuwa wabunifu.Njia nyingine ambayo imenipa mafanikio Sana ni kupitia maonyesho ya kitaifa Kama vile maonyesho ya sabasaba na nanenane.Yote hayo kwangu yawekuwa mchango mkubwa Kwa kujitangaza na kuitangaza biashara na bidhaa zangu.Hivyo Kwa watanzania hasa vijana nawasihi mwekeze katika Siri hizi hakika Kuna mafanikio, Akieleza Mtanga.

Siri hizi Kwa mtanzania yeyote akidhamilia kuanzisha kiwanda atafanikiwa. Tatizo kubwa ni kutojua Cha kufanyaikiwa hujaanza . Ukichukua hatua na kuanza Mara moja hakika utafungua mlango wa milango mingine mingi iliyofunguliwa. Anza na kile ulichonacho na ujue unapoanza basi unaanzisha na hatua zingine ulizowahi kuzifikria. Anza sasa utaona jinsi usivyojijua ilivyo unaweza.

1662050386398.jpg

Chanzo: picha toka kiwandani kibaha ,Pwani.
Call +255621282979
 
View attachment 2342361

Chanzo: picha toka kiwandani kibaha ,Pwani.
Call +255621282979
Ndoto yangu hii
 
Back
Top Bottom