Moja ya tatizo kubwa linaloiuwa CHADEMA ni wao kudhani adui yao mkubwa ni CCM pekee. Yes, CCM ni adui wa CHADEMA na wanataka leo hata kesho chama hiko kife. Lakini hata hivyo, CHADEMA pia ni adui wa CCM na wao wangependa kuiona CCM ikifa leo hata kesho. Na hii ndo tunaita SIASA, kila chama lengo lake ni kushika dola kwa gharama yoyote Ile. Kwahiyo, CCM kuitakia CHADEMA mabaya siyo DHAMBI bali ni SIASA. CHADEMA kikifa leo, kitakuja chama kingine kwani upinzani ni fikra na mitazamo ya watu siyo chama. Ndo maana tulikua na vyama vyenye nguvu kama NCCR, CUF na leo tuna CHADEMA. Kwahiyo, CCM hata ifanyaje haiwezi kuua Upinzani.
Lakini hebu tuangalie kwa undani zaidi bila kuleta ushabiki wowote wa kivyama. Hivi haya yanayotekea CHADEMA leo CCM haikuwahi kuyapitia? CCM haikuwahi kukimbiwa na wabunge wake? CCM haikuwahi kukimbiwa na Madiwani wake? CCM haikuwahi kushindwa kwenye chaguzi ndogo za ubunge? CCM haikuwahi kukimbiwa na Wanachama wake waandamizi wenye ushawishi kwa Jamii? Jibu ni NDIO. Tena vizuri umetolea mfano mpaka wa kina Mrema hapa sijataka kuyataja yaliyotokea 2015 kila mtu anajua kilichotokea CCM. Lakini bado chama hicho kiliendelea kuwepo na kushika dola.
Jambo kubwa ambalo CCM inavishinda vyama vingine vya Upinzani inapopitia kwenye migogoro ni uwezo wake wa kuweza kujibadilisha kulingana na wakati. CCM ya nyerere siyo sawa na CCM ya Mwinyi wala Mkapa. CCM ya Kikwete ni mbingu na ardhi na CCM hii ya Magufuli tunayoiona sasa. Lakini kwa vyama vya Upinzani ni tofauti kabisa, Viongozi tulio nao ni wale wale, mbinu wanazotumia kupambana na CCM ni zile zile. Huwezi kupambana na CCM ya Magufuli kwa kutumia mbinu ulizokua unatumia kwa Kikwete lazima utafeli. Ili Vyama vya Upinzani viweze kuwa imara muda wote ni lazima na vyenyewe viwe na uwezo wa kujibadilisha kimfumo na kiungozi kama ilivyo CCM ili kuweza kupambana nayo.
Kinachoendelea kwa sasa CHADEMA, kwa kiasi kikubwa kinasababishwa na migogoro ya ndani ya chama hicho tena ya muda mrefu. Hivyo, CCM inachofanya ni kutumia mwanya huo kuhakikisha chama hicho kinasambaratika jambo ambalo siyo DHAMBI bali ni SIASA. Migogoro ya ndani ya CHADEMA ilipaswa kutatuliwa kwa busara na hekima za kiuongozi badala ya kutumia mihemko na ubinafsi. Na hiki ndicho kinachoiua CHADEMA kwasasa.
Sasa kama tunakubali chama kina mapungufu katika uongozi wake, lakini badala ya kuona ni namna gani ya kuondoa mapungufu hayo, Sisi tunasema eti mapungufu hayo waliyonayo viongozi wetu ni ya kibinadamu hivyo yapaswa tuwavumilie kwasabbu wamekifanyia mambo mengi mazuri chama chetu. Tunasahau kwamba, mapungufu haya waliyonayo viongozi wetu ndiyo yanayotumiwa na CCM kuvibomoa vyama vya upinzani. Hata Nyerere aliifanyia mengi mazuri nchi yetu, lakini ilipofika wakati changamoto za nchi zilivyozidi ilibidi ang'atuke kupisha fikra nyingine ili nchi iweze kuendelea.
Tutaendelea kuilaumu CCM inayofanya SIASA zake ili kuendelea kushika dola, tukidhani ni DHAMBI kubwa kutaka CHADEMA ife kumbe CHADEMA inajimaliza yenyewe.
Alamsiki.
Sent from my SM-A730F using
JamiiForums mobile app