Mkuu DenooJ, kwanza nikupongeze una kupaji cha uandishi na una uwezo wa kuandika maana umeshuka na para 7 aa nguvu.
Nakushauri tuu, ili kukilinda kipaji chako na kiandika kitu cha maana kwa kirefu,
- Jifunze kusoma, penda kusoma mada, ukikuta link fungua link ili ujue kitu kinachozungumzwa, ndipo uchangie kwa kirefu.
- Unaruhusiwa kumjua mtu, information is power hivyo ni kweli unamjua sana Pasco na umewasaidia wengine kujua.
- Jee unaijua Katiba ya Chadema na taratibu za kumfukuza mwanachama kwa makosa ya nidhamu?. Jee utaratibu huo zilifuatwa?.
- Kwenye bandiko nilizungunzia video, kumbe ni video ya kutekwa kwa Lwakatare!, Duh...!. Kumbe Lwakatare aliwahi kutekwa?!.
- Kumbe ni Mwigulu Nchemba alijitokeza hadharani akasema anayo video ya Lwakatare kutekwa, na Mwigulu alisema hivyo makusudi kwasababu za kisiasa, but mpaka leo hii, Mwigulu Nchemba hakuwahi kuonesha umma wa watanzania hiyo video?!.
- Umejuaje mimi naujua ukweli? ukweli gani?, wa kutekwa kwa Lwakatare au video ya kutekwa kwa Lwakatare?.
- Nitauzingatia ushauri wako.
La mwisho, kama ukisoma kitu na hukuelewe, usijibu kwa kirefu ili kuonyeshea kuwa wewe ni mwelewa, unajua watu kama unamjua Pasco, na unajua vitu, kama unavyojua kuhusu kutekwa kwa Lwakatare, sasa wanaojua video ni ya nini na nani ndio alikuwa atekwe, watakuona mjinga!.
P