Sio wakati wa kuitabiria mabaya CHADEMA

Sio wakati wa kuitabiria mabaya CHADEMA

Ukiachana na kile kitengo cha propaganda cha CCM na ile praise team. Wengine wote hatupaswi kuwa na muono kimo cha mbilikimo. Ni lazima tuwaze zaidi ya mwisho wa uono wa macho yetu.

Nimemuona P kwenye mada za CHADEMA. Utabiri wa mabaya. P ulituasa tuepuke prophecy of doom. Tusiwaase wengine huku sisi tunatenda.

Natambua mgongano wa mawazo na hoja. Natambua tofauti za kimtazamo kati yetu lakini haya yasitufanye tukafika mahali tukawa na mitazamo finyu. Tunaihitaji CHADEMA kama taasisi imara ili CCM isijisahau sana. Miaka ile ya 1995-2005. Wakati huo NCCR kikiwa chama chenye nguvu na ushawishi, kuna mengi yaliyotokea lakini pengine hayakumbukwi sana.

Alitokea Augustine Mrema, waziri machachari wa CCM aliyebwaga manyanga na kujiunga na NCCR Mageuzi. Wengi bado tunakumbuka kilichotokea pale, kukawa na vichwa hasa.

Baadae NCCR ikafitinishwa na kumgeuka. Kukawa na NCCR mbili. Huo ndio ukawa mwisho wa kile chama. Kuna mtu pale NCCR mmojawapo wa viongozi mahiri akiitwa Prince Bangeda. Mpaka leo sijui alitofautiana nini na Mrema. Alimuandika vibaya na kumchambua Mrema kwenye safu yake ndani ya gazeti la Rai kila Jumatano kwa makala ndefu ndefu kwa miezi kadhaa. Nadhani hakuna mwanasiasa alichambuliwa na kuandikwa vibaya mpaka leo hii kama alivyofanya Bangeda kwa Mrema.

Leo hii Bangeda yuko wapi na Mrema yuko wapi? Unapotumika angalia unatumikaje. Usipojiongeza, wanaweza kukufanya kama toilet paper.

CHADEMA inapigwa vita sana kwakuwa ni mwiba mchungu kwa CCM. Project za kukiangamiza hiki chama ni nyingi mno. Watu wanaotumika ni wengi mno. Pesa iliyokwisha tumika ni nyingi mno. Hakuna chama cha siasa kimepitia mapigo mengi kama CHADEMA, lakini mpaka leo kipo hai na kinadunda. Kukiombea kife ni:

Kupoteza matumaini ya vijana wasomi wengi
Ni kupoteza viongozi wazuri wa kesho
Ni kupoteza matumaini na furaha wa wapiga kura milioni 7
Ni kupoteza matumaini na furaha ya wapenzi, washabiki na wafurukutwa zaidi ya milioni kumi

Hakuna kosa kubwa tutalifanya kama kuombea CHADEMA ife. Hiyo laana haitakaa ituache, itakula nasi sahani moja. Kama tulikubali NCCR na CUF vinyongwe, tusikubali haya kwa CHADEMA.

Viongozi walioko CHADEMA ni binadamu kama wewe na mimi wana mapungufu yao, lakini kwenye mizania ya haki wana mengi mazuri ya kukumbukwa vizazi na vizazi. Wanahitaji tuwatie moyo, tuwasaidie na kuwapa faraja kwenye kila hatua wanayopitia. Tusiwakatishe tamaa. CCM iliyokuwa na upendo wa kweli kwa Watanzania ni ile ya Mwalimu Nyerere tu. Baada ya hapo ni vurugu mechi kwa kwenda mbele.

Makala nyingi za kuiponda CHADEMA na kukiombea mabaya hata kama sio sehemu ya zile project zina ukakasi na kuacha maswali mengi kuliko majibu.

Je, kuna personal issues nje ya politik?

Jr[emoji769]
Ubarikiwe sana mkuu maana uneongea ukweli mtupu.
Japo kuna watu kazi yao ni kuisema vibaya CHADEMA pasipo kujua kuwa bila kuwepo na upinzani hali ingekuwa mbaya zaidi ya hapa!
Ukiwaangalia viongozi wengi wa upinzani wanapigania zaidi haki na usawa kwa maslahi ya Taifa zima bila kujali tofauti zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji120][emoji120][emoji120]

Jr[emoji769]
 
Kwahiyo CHADEMA kimezuiwa kufanya shughuli za kisiasa za majukwaani na mivutano ya ndani ya chama ?

Zile kesi za kubambikiwa zinazowakabili viongozi wa CHADEMA nazo zinatokana na movutano ya ndani ?

By the way mivutano ya ndani ya CHADEMA si ingekuwa nafuu ya ccm mbona bado kinatumia mpaka vyombo vya dola kuikandamiza CHADEMA?

Hivi unadhani kama kusingekuwa na mbeleko ya vyombo vya dola ccm kingekuwa bado hakijatolewa madarakani ?

Itikadi zetu zisituzibe macho tukashindwa kuiona hali halisi ya kisiasa nchini tutakuwa tumepotoka mno kama taifa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Wewe unaweza kusema kesi za kubambikwa, lakini mtu akisema anafanya maandamano nchi nzima na kuhatarisha usalama wa watu wengine utasema huyo amebambikiwa kesi? Ndio maana nikasema kwenye post yangu ya kwanza, Chadema ina wafundisha vibaya viongozi vijana mbao ndio wangekuwa viongozi bora wa kesho. Mtoto umleavyo ndivyo akuwavyo, ukimfundisha kijana kuvunja sheria usitegemee ataenda kutenda mema huko uraiani. And then yakivurugika, watu wanasema CCM inashirikiana na dola. Chukulia kina Mdee walivyokwenda gerezani na kulazimisha kuingia maeneo maalum bila vibali, kama waliona hawakutendewa haki, walishindwa vipi kumhoji kamishna kupitia vyombo husika? na wao ni wabunge ambao walitakiwa wajuwe utaratibu wa kutoa malalamiko yao.
 
Wewe unasema CHADEMA kinawalea vijana vibaya ccm inatumia mpaka pesa za umma kuwalipa wahamie huko ili iwape uongozi mifano hai iko mingi sina hata muda wa kukuorodheshea hapa.

Serikali ya ccm imezuia shughuli za kisiasa kwa vyama vingine huku wenyewe wakitamba nchi nzima huoni kuwa huku nikupigana na mtu aliyefungwa kamba ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu #Mshana acha haya yatokee ili neno litimie ccm wanaamini kubambikia kesi viongozi wa Chadema no ushindi kumbe ni kushindwa vibaya walijua yakua wakilazimisha TV na Radio zikiwatangaza wao pekee ndio watapendwa kumbe wapi chadema imeendelea kupenya hivyo hivyo sasa wanakosa wakumlaumu kwa sababu mpanga mikakati ndio Hugo polepole utategemea jipya zaidi ya mbinu za kijuha za kununua wabunge na madiwani kitu ambacho hata SADAM HUSEIN NA OSAMA BN RADENI WANATUSHANGAA MNOOO.
 
Upinzani ni haki ya kisheria ya chama chochote cha upinzani, wanalipwa ili watoe njia mbadala ya suluhisho ya matatizo nchi yetu. Ikifikia mahala wanapinga hata maswala muhimu kwenye ustawi wa nchi kama elimu, afya nk. Hapo unajiuliza kama ni kweli hawa wanania njema au ndio tamaa ya uwongozi. Ikifikia mahala chama kinaweka mikakati ya kushawishi wabia wetu wa maendeleo wasitishe misaada au mikopo ambayo ingesaidia hata wana Chadema. Kwangu mimi huo sio upinzani.

Unakosea kusema fedha ya walipa kodi sio fedha ya serikali, serikali imewekwa na wananchi kusimamia mambo yote yanayoihusu nchi, kodi ikiwa ni mojawapo ya mambo iliyokabidhiwa kuiangalia. Kumbuka hakuna anayeilaumu Chadema jinsi inavyotumia pesa zake, hilo ni swala la wana CDM wenyewe kulisema. Lakini kama kweli unataka kwenda na uhalisia wa nchi ilivyo, huwezi kutumia pesa ukidhani kama walipa kodi hawaoni. Walipa kodi sio CDM peke yao, hata vyama vingine navyo vinachangia kodi na wanahaki ya kujiuliza kama kweli mchango wetu kwa chama fulani inatumika ipasavyo?

Wala sina haja ya kuingilia kununua viongozi maana ni hoja isiyo kuwa na ushahidi wa aina yoyote.
Unaposema wanapinga masuala mujimu kama elimu, afya naona hujui unachoongelea.

Hilo suala la elimu mkopo wa world bank seeikali ilipewa masharti iyafuate, ikishindwa mkopo hakuna, wamefuata masharti wamepewa mkopo, wewe ulitaka waachwe tu bila kujali athari ambazo wangesababisha kwa watoto ambao walipata ujauzito?

Suala la kununuliwa wapinzani huna ushahidi, kwamba hata kile kilichomkuta meya wa Iringa mjini hukuona mil. 200 alizoahidiwa akazikataa?!

Unavyosema hakuna mtu anaeilaumu Chadema kutumia pesa zake wakati wewe mwenyewe mwanzo ulionesha kuwalaumu kwa matumizi mabaya ya fedha hata sikuelewi, naona hujui unachosimamia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini sasa kwa mtazamo wako yule aliyeishia la saba na anataka uwanachama au uongozi, anayajua hayo ya mrengo upi CHADEMA inasimamia? Sio kila mwanachama ana degree in political science.

Ukiachana na CCM survival, CHADEMA ina banwa na mivutano ya ndani kuliko ya nje. Mivutano ya matumizi ya fedha, mivutano ya uwongozi, hata mivutano ya fursa za kuwania nafasi za kiutawala kwenye jamii ubunge udiwani nk. Ukisema CCM ndio inaikwanisha CDM unakuwa umechukuwa njia fupi ya kutafuta mchawi wa mbali wakati kumbe mchawi yuko ndani ya nyumba yako.
Haya unayoyaandika nitaanza kukushangaa, maana kama una civic education kidoogo utaelewa maana ya propaganda, ushuzi na uchafu wa Siasa chafu haswahaswa za watu waliokosa hoja.

Nimeandika hapo juu kuwa CCM ni chama laghai, NI CHAMA KINACHOFUATA ITIKADI YA KIJAMAA kikiwa hakina mwanachama mjamaa Hata mmoja!

Sasa kama chama ni laghai ukiwa vizuri kichwani utafuataje chama laghai, nilikuomba unisahihishe kwa kunitajia mjamaa mmoja tuu wala si wawili waliopo CCM! kama hamna jitafakali akili yako mwenyewe au laa you are the elite na ni mlaghai mwingine, na kama ni mlaghai jilie nchi usiingie humu kutetea chochote endelea kuwalaghai mahamnazo!!
 
Mtu akiniambia CHADEMA ni chama bora, nashindwa kuelewa ubora uko wapi. Ikiwa miaka yote hii kimeshindwa kuwaandaa vijana wasomi kuchukuwa nafasi za uwongozi, sijui huo ubora unatoka wapi? Kijana anachukuliwa chuo kikuu, akiingia CHADEMA anafundisha kupinga kila kitu na kukimbizana na dola. You can't create tomorrow's leader by disobeying the rule of law.

Ukiwa CHADEMA lazima uwe tayari kutafuna pesa ya umma bila woga wala ukakasi, mikutano kwenye mahoteli makubwa, safari za nje zisizo za lazima, magari ya kifahari hata mmiliki hajulikani ni nani kusema hicho ndio chama cha mfano, sio kwa mfumo uliopo.

Hata itikadi, CHADEMA imeshindwa kuwa hata na kachuo kadogo kutowa somo la itikadi kwa viongozi watarajiwa ili kuwe na muongozo hawa wajuwe CHADEMA inasimamia kitu gani. Halafu watu wanashangaa kuona wanachama wanakihama chama, ni kwasababu wanafikiri CHADEMA na CCM wote wako sawa lakini ni vyama vyenye misimamo tofauti.
Huwezi kuwa ccm ukaisifia chadema kwamba wako vizuri hata siku 1 Leo hii ukiuliza Mwana ccm kati ya cdm na cuf bora chama kipi lazima aseme cuf hapo jua tayari cuf ni dhaifu mm naugana na mtoa mada bila kuwa na upinzani imala hakuna ccm imala Leo hii tunaona mabadiliko ndani ya ccm yote haya sababu ya cdm mm naungana na mtoa mada tuwape moyo hawa viongozi Wa cdm ili tuweze kupata maendeleo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mshana Jr,

Ingawa hujazungumzia harakati na nimekuwa nikiona wengi wakisema siasa zimebadilika kwamba siasa za sasa hazijitaji hatakati lakini aise Mimi Nina mtazamo tofauti kabisa!

Nikikumbuka miaka ya nyuma wkt wa siasa za harakati kuanzia mtaani, vyouni mpk makazini ilikuwa moto na ilitishia sana sisiemu sielewi kwann siasa za harakati zinapigwa kwasasa mpaka upinzani hawazitumii pamoja na kwamba nyakati zimebadilika

Sent using kidole gumba
Ukiongelea neno harakati sio kila mtu anajua maana Yake. Kwa maslahi mapana ya watumiaji wa JamiiForums, wanachama na wasio wanachama, tunaomba ufafanue Nini maana ya neno "HARAKATI ZA KISIASA"
 
Nimemuona P kwenye mada za CHADEMA. Utabiri wa mabaya. P ulituasa tuepuke prophecy of doom. Tusiwaase wengine huku sisi tunatenda.

Hakuna kosa kubwa tutalifanya kama kuombea CHADEMA ife. Hiyo laana haitakaa ituache, itakula nasi sahani moja. Kama tulikubali NCCR na CUF vinyongwe, tusikubali haya kwa CHADEMA.

Makala nyingi za kuiponda CHADEMA na kukiombea mabaya hata kama sio sehemu ya zile project zina ukakasi na kuacha maswali mengi kuliko majibu.

Je, kuna personal issues nje ya politik?

Jr[emoji769]
Mkuu Mshana Jr, kwanza heshima mbele, hakuna mtu yoyote anayeiombea Chadema ife, kosa langu ni kuwa mkweli too much.

Humu jf tuna members wa aina 3, tuna
  1. Simple minds, discuss people, wao badala ya kujadili hoja iliyo mezani, hawa watamjadili mtoa hoja.
  2. Ordinary minds, discuss events, hawa watadili matukio, nini kimetokea etc
  3. Great minds discuss ideas, hawa watajadili hoja iliyo mezani.
Hivyo naomba keep on being free, kujadili watu, matukio na hoja, katika mabandiko yangu, ukiweza kujibu hoja, nitashukuru, ila hata ukinijadili, sikulaumu na likes nakutwangia.
Ukipata muda karibu ujibu hoja za bandiko hili.

Asante
P
 
P heshima kwako pia isionekane nataka kuanzisha vita na wewe la hasha.. Hatuwezi kufanana kwa kila kitu.. Kuna mahali lazima tutofautiane hoja na mitazamo.. Na hili wala sio kosa hata kidogo...
Mwelekeo wa mada ndio hutoa tafsiri tofauti kulingana na wachangiaji.... Natambua hulka yako ya kuwa mkweli sana... Bado hili pia sio dhambi.... Mimi mtazamo wangu sio kuwa mkweli sana bali huwa naamini katika uhalisia zaidi kuliko ukweli kwakuwa ukweli hubadilika kulingana na mazingira na nyakati lakini uhalisia hubaki kuwa uhalisia
Tuko pamoja [emoji120]

Jr[emoji769]
 
Huwezi kuwa ccm ukaisifia chadema kwamba wako vizuri hata siku 1 Leo hii ukiuliza Mwana ccm kati ya cdm na cuf bora chama kipi lazima aseme cuf hapo jua tayari cuf ni dhaifu mm naugana na mtoa mada bila kuwa na upinzani imala hakuna ccm imala Leo hii tunaona mabadiliko ndani ya ccm yote haya sababu ya cdm mm naungana na mtoa mada tuwape moyo hawa viongozi Wa cdm ili tuweze kupata maendeleo

Sent using Jamii Forums mobile app
Sikatai kama kuna wana CCM ambao hawawezi kufurahia lolote kuhusu Chadema. Mimi sina kinyongo na Chadema, naichukulia kama taasisi. Lakini kwa mtazamo wangu Chadema ya sasa imetekwa na wachache ambao wanaipa jina baya.

Itaniuma sana kama Chadema ikuchukuwa dola na viongozi wasio wazalendo, wale ambao wanafurahia nchi ikipata majanga badala kujenga umoja ili kupata suluhisho la matatizo ya nchi.
 
Haya unayoyaandika nitaanza kukushangaa, maana kama una civic education kidoogo utaelewa maana ya propaganda, ushuzi na uchafu wa Siasa chafu haswahaswa za watu waliokosa hoja.

Nimeandika hapo juu kuwa CCM ni chama laghai, NI CHAMA KINACHOFUATA ITIKADI YA KIJAMAA kikiwa hakina mwanachama mjamaa Hata mmoja!

Sasa kama chama ni laghai ukiwa vizuri kichwani utafuataje chama laghai, nilikuomba unisahihishe kwa kunitajia mjamaa mmoja tuu wala si wawili waliopo CCM! kama hamna jitafakali akili yako mwenyewe au laa you are the elite na ni mlaghai mwingine, na kama ni mlaghai jilie nchi usiingie humu kutetea chochote endelea kuwalaghai mahamnazo!!
Labda nikuulize kidogo ujamaa kwako ni nini, ni mtu kuwa masikini au ni kugawana kwa usawa kile kidogo kilicho kuwepo. Imani yako ni kuwa mtu akiwa mjamaa hatakiwi kumiliki mali ya aina yoyote. Huo ni uwongo, nchi nyingi za Scandinavia zinaongozwa na vyama vya kijamaa, na mgao wa pato la taifa uko karibia na sawa kwa kila raia kupitia elimu bure, matibabu bure kupitia bima ya taifa nk. Itikadi ya Chadema kama ulivyosema ni kutowa fursa kwa wafanyabishara, na watu binafsi kushiriki kiuchumi, lakini vyote hivyo vinaweza ndani ya mfumo wa kijamaa pia. Mfano mzuri ni za China na Urusi ambazo zinaongoza kwa kuwa na mabilionea wengi huku serikali zao zikiongozwa na vyama vya kijamaa. Pato la taifa linatumika kusaidia wale walio na kipato cha chini pamoja na kusomesha watoto wao na kuwajengea miundo mbinu kama hospitali nk
 
Mbona mfano mzuri umetoa China na Russia badala ya kuitumia Tanzania inayoongozwa na chama cha kijamaa toka ipate uhuru ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Mshana Jr, kwanza heshima mbele, hakuna mtu yoyote anayeiombea Chadema ife, kosa langu ni kuwa mkweli too much.

Humu jf tuna members wa aina 3, tuna
  1. Simple minds, discuss people, wao badala ya kujadili hoja iliyo mezani, hawa watamjadili mtoa hoja.
  2. Ordinary minds, discuss events, hawa watadili matukio, nini kimetokea etc
  3. Great minds discuss ideas, hawa watajadili hoja iliyo mezani.
Hivyo naomba keep on being free, kujadili watu, matukio na hoja, katika mabandiko yangu, ukiweza kujibu hoja, nitashukuru, ila hata ukinijadili, sikulaumu na likes nakutwangia.
Ukipata muda karibu ujibu hoja za bandiko hili.

Asante
P
Ume panic.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pascal Mayalla kuya pande hii ujionee waandishi waliobobea
Asanti Mshana Jr

Back
Top Bottom