Sio wakati wa kuitabiria mabaya CHADEMA

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,638
697,929
Ukiachana na kile kitengo cha propaganda cha CCM na ile praise team. Wengine wote hatupaswi kuwa na muono kimo cha mbilikimo. Ni lazima tuwaze zaidi ya mwisho wa uono wa macho yetu.

Nimemuona P kwenye mada za CHADEMA. Utabiri wa mabaya. P ulituasa tuepuke prophecy of doom. Tusiwaase wengine huku sisi tunatenda.

Natambua mgongano wa mawazo na hoja. Natambua tofauti za kimtazamo kati yetu lakini haya yasitufanye tukafika mahali tukawa na mitazamo finyu. Tunaihitaji CHADEMA kama taasisi imara ili CCM isijisahau sana. Miaka ile ya 1995-2005. Wakati huo NCCR kikiwa chama chenye nguvu na ushawishi, kuna mengi yaliyotokea lakini pengine hayakumbukwi sana.

Alitokea Augustine Mrema, waziri machachari wa CCM aliyebwaga manyanga na kujiunga na NCCR Mageuzi. Wengi bado tunakumbuka kilichotokea pale, kukawa na vichwa hasa.

Baadae NCCR ikafitinishwa na kumgeuka. Kukawa na NCCR mbili. Huo ndio ukawa mwisho wa kile chama. Kuna mtu pale NCCR mmojawapo wa viongozi mahiri akiitwa Prince Bangeda. Mpaka leo sijui alitofautiana nini na Mrema. Alimuandika vibaya na kumchambua Mrema kwenye safu yake ndani ya gazeti la Rai kila Jumatano kwa makala ndefu ndefu kwa miezi kadhaa. Nadhani hakuna mwanasiasa alichambuliwa na kuandikwa vibaya mpaka leo hii kama alivyofanya Bangeda kwa Mrema.

Leo hii Bangeda yuko wapi na Mrema yuko wapi? Unapotumika angalia unatumikaje. Usipojiongeza, wanaweza kukufanya kama toilet paper.

CHADEMA inapigwa vita sana kwakuwa ni mwiba mchungu kwa CCM. Project za kukiangamiza hiki chama ni nyingi mno. Watu wanaotumika ni wengi mno. Pesa iliyokwisha tumika ni nyingi mno. Hakuna chama cha siasa kimepitia mapigo mengi kama CHADEMA, lakini mpaka leo kipo hai na kinadunda. Kukiombea kife ni:

Kupoteza matumaini ya vijana wasomi wengi
Ni kupoteza viongozi wazuri wa kesho
Ni kupoteza matumaini na furaha wa wapiga kura milioni 7
Ni kupoteza matumaini na furaha ya wapenzi, washabiki na wafurukutwa zaidi ya milioni kumi

Hakuna kosa kubwa tutalifanya kama kuombea CHADEMA ife. Hiyo laana haitakaa ituache, itakula nasi sahani moja. Kama tulikubali NCCR na CUF vinyongwe, tusikubali haya kwa CHADEMA.

Viongozi walioko CHADEMA ni binadamu kama wewe na mimi wana mapungufu yao, lakini kwenye mizania ya haki wana mengi mazuri ya kukumbukwa vizazi na vizazi. Wanahitaji tuwatie moyo, tuwasaidie na kuwapa faraja kwenye kila hatua wanayopitia. Tusiwakatishe tamaa. CCM iliyokuwa na upendo wa kweli kwa Watanzania ni ile ya Mwalimu Nyerere tu. Baada ya hapo ni vurugu mechi kwa kwenda mbele.

Makala nyingi za kuiponda CHADEMA na kukiombea mabaya hata kama sio sehemu ya zile project zina ukakasi na kuacha maswali mengi kuliko majibu.

Je, kuna personal issues nje ya politik?

Jr
 
Huu uzi wako umetulia sana. Pamoja na mapungufu ya kibinadamu na kiuongozi Chadema ni chama bora sana mara elfu ukilinganisha na ccm na hata ccm wanajua hivyo na ndiyo sababu kubwa hawataki tuwe na Tume Huru itakayosimamia uchaguzi HURU na wa HAKI kwani ndiyo itakuwa Kiama chao hapa Tanzania.

Wanajua wazi bila uchaguzi uliojaa udhalimu, vitisho, wizi na dhuluma wanaweza kubaki na majimbo machache sana nchini na Urais watausikia kwenye bomba.
 
Mshana Jr,

Mshana asante kwa bandiko hili. Sidhani kama kuna mtu wa ku- comprehend such a big mind post.

Ukiona mtu mzima, ana mke na watoto anajiita wa Jalalani ili apendelewe na mwanadamu mwenzake, ujue tuna tatizo kubwa sana.Tunahitaji mageuzi makubwa! A new liberation struggle is needed, tena armed struggle for that matter!
 
Kwa mtazamo wangu changamoto ilianza pale siasa zilippkosa nguvu vyuoni na hiyo kupelekea kukosa vijana wenye nguvu na ushawishi na na ndio maana kwa miaka kama kumi sasa tumekosa vijama wapya wanaoibuka kwenye siasa na kuwa na nguvu yenye ushawishi.

Ukiangalia wanasiasa tuliona nao ni wale walioibuliwa mikama 15 mpaka 20 vyuoni, so kwa mtazamo wangu nguvu iwekezwe kwa vijana na wajengewe Uaminifu na utii hii itaondoa usaliti na kununuana, ingawa sina umri Mkubwa sana lakini kwa miaka 20+ nilishoshuhudia siasa naamini kuwekeza kwa vijana.

Sent using kidole gumba
 
Mshana Jr,

Ingawa hujazungumzia harakati na nimekuwa nikiona wengi wakisema siasa zimebadilika kwamba siasa za sasa hazijitaji hatakati lakini aise Mimi Nina mtazamo tofauti kabisa!

Nikikumbuka miaka ya nyuma wkt wa siasa za harakati kuanzia mtaani, vyouni mpk makazini ilikuwa moto na ilitishia sana sisiemu sielewi kwann siasa za harakati zinapigwa kwasasa mpaka upinzani hawazitumii pamoja na kwamba nyakati zimebadilika

Sent using kidole gumba
 
Mtu akiniambia CHADEMA ni chama bora, nashindwa kuelewa ubora uko wapi. Ikiwa miaka yote hii kimeshindwa kuwaandaa vijana wasomi kuchukuwa nafasi za uwongozi, sijui huo ubora unatoka wapi? Kijana anachukuliwa chuo kikuu, akiingia CHADEMA anafundisha kupinga kila kitu na kukimbizana na dola. You can't create tomorrow's leader by disobeying the rule of law.

Ukiwa CHADEMA lazima uwe tayari kutafuna pesa ya umma bila woga wala ukakasi, mikutano kwenye mahoteli makubwa, safari za nje zisizo za lazima, magari ya kifahari hata mmiliki hajulikani ni nani kusema hicho ndio chama cha mfano, sio kwa mfumo uliopo.

Hata itikadi, CHADEMA imeshindwa kuwa hata na kachuo kadogo kutowa somo la itikadi kwa viongozi watarajiwa ili kuwe na muongozo hawa wajuwe CHADEMA inasimamia kitu gani. Halafu watu wanashangaa kuona wanachama wanakihama chama, ni kwasababu wanafikiri CHADEMA na CCM wote wako sawa lakini ni vyama vyenye misimamo tofauti.
 
Ni ngumu kwa sasa kufanya siasa za kiharakati. Mazingira tuliyonayo hayaruhusu tena. Lakini pia tulianza kuyumba pale tulipoamua kujitoa ufahamu na kuilinda CCM kwa namna yoyote ile.

Jr
 
Nipo ccm lakini nakubaliana na hoja, ila tungependa pia kuona upinzani sio tu unaendelea kuwepo bali upinzani dhabiti, Ili kue na kimbilio kama ccm ikiharibu kma miaka ya nyuma!
Na hata kama ikatokea CCM ikaondoka madarakani kama vyama vingine. Ikae pembeni lakini isife ili iweze bado kuwa na nguvu yake kama mpinzani.

Jr
 
Huu uzi wako umetulia sana. Pamoja na mapungufu ya kibinadamu na kiuongozi Chadema ni chama bora sana mara elfu ukilinganisha na ccm na hata ccm wanajua hivyo na ndiyo sababu kubwa hawataki tuwe na Tume Huru itakayosimamia uchaguzi HURU na wa HAKI kwani ndiyo itakuwa Kiama chao hapa Tanzania.

Wanajua wazi bila uchaguzi uliojaa udhalimu, vitisho, wizi na dhuluma wanaweza kubaki na majimbo machache sana nchini na Urais watausikia kwenye bomba.

Hapa ndipo CCM wanapowapiga bao sasa! Mm npo CCM lakini napenda kue na upinzani tena ikiwezekan hata vyama vingine viongeze nguvu zaidi, yaani Tue ata na vyama vinne vyenye Sera nzito ili CCM wakingua tu bas kazi inakua rahisi kupiga kura chma kingine, sasa chadema hamtaki kwanza kukubali madhaifu yenu hamna mpango wa kuyarekebisha na sidhan ata kama mna huo mpango nyie kikubwa ni kuleta fujo tu, kwa namna hii hatuna namna zaidi ya kukipenda CCM.
 
Mtu akiniambia CHADEMA ni chama bora, nashindwa kuelewa ubora uko wapi. Ikiwa miaka yote hii kimeshindwa kuwaandaa vijana wasomi kuchukuwa nafasi za uwongozi, sijui huo ubora unatoka wapi? Kijana anachukuliwa chuo kikuu, akiingia CHADEMA anafundisha kupinga kila kitu na kukimbizana na dola. You can't create tomorrow's leader by disobeying the rule of law.

Ukiwa CHADEMA lazima uwe tayari kutafuna pesa ya umma bila woga wala ukakasi, mikutano kwenye mahoteli makubwa, safari za nje zisizo za lazima, magari ya kifahari hata mmiliki hajulikani ni nani kusema hicho ndio chama cha mfano, sio kwa mfumo uliopo.

Hata itikadi, CHADEMA imeshindwa kuwa hata na kachuo kadogo kutowa somo la itikadi kwa viongozi watarajiwa ili kuwe na muongozo hawa wajuwe CHADEMA inasimamia kitu gani. Halafu watu wanashangaa kuona wanachama wanakihama chama, ni kwasababu wanafikiri CHADEMA na CCM wote wako sawa lakini ni vyama vyenye misimamo tofauti.
Hupaswi kuilaumu CHADEMA hata chembe... Inaminywa na haipewi nafasi kabisa ilijenge na kustawi... Pamoja na yote haya bado ni chama kinachoogopeka zaidi na watawala wa ccm huku kikiwa ndio chama kinachopendwa zaidi Tanzania na nje ya Afrika

Jr
 
Na hata kama ikatokea CCM ikaondoka madarakani kama vyama vingine.. Ikae pembeni lakini isife ili iweze bado kuwa na nguvu yake kama mpinzani

Jr

Nakubaliana na wewe mkuu, hapa ndipo tutaona ufanisi mkubwa sana wa majukumu, yaani kazi inakua rahisi kwel kwel yawezekaa hata uchama ukatuondoka kama ukabila tulivouruka, wtu wa ccm wanpiga kura kokote na chadema ivo ivo
 
Nakubaliana na wewe mkuu, hapa ndipo tutaona ufanisi mkubwa sana wa majukumu, yaani kazi inakua rahisi kwel kwel yawezekaa hata uchama ukatuondoka kama ukabila tulivouruka, wtu wa CCM wanpiga kura kokote na chadema ivo ivo
I wish this can happen. Natamani mno. Siasa za ushindani wa hoja. Siasa za mijadala yenye kujenga na si kubomoa. Kwakuwa mwisho wa siku Tanzania itabaki hata kama vyama vitakoma kuwa.

Jr
 
Chadema ni sikio la kufa
Alichofanya P ni kushauri sasa yameanza kutimia,unaanza kulia kuwa si wakati wa kutabiria mabaya chadema
Ni faraja kubwa kuona chadema imejizika yenyewe kupitia sultani Mbowe kabla hata ya uchaguzi wa 2020
Haya ndio matokeo ya siasa za chuki zilizoasisiwa na CCM. Huu wako kabombe ni mtazamo finyu mno

Jr
 
Back
Top Bottom