Sio wakati wa kuitabiria mabaya CHADEMA

Sio wakati wa kuitabiria mabaya CHADEMA

Ukiachana na kile kitengo cha propaganda cha CCM na ile praise team. Wengine wote hatupaswi kuwa na muono kimo cha mbilikimo. Ni lazima tuwaze zaidi ya mwisho wa uono wa macho yetu.

Nimemuona P kwenye mada za CHADEMA. Utabiri wa mabaya. P ulituasa tuepuke prophecy of doom. Tusiwaase wengine huku sisi tunatenda.

Natambua mgongano wa mawazo na hoja. Natambua tofauti za kimtazamo kati yetu lakini haya yasitufanye tukafika mahali tukawa na mitazamo finyu. Tunaihitaji CHADEMA kama taasisi imara ili CCM isijisahau sana. Miaka ile ya 1995-2005. Wakati huo NCCR kikiwa chama chenye nguvu na ushawishi, kuna mengi yaliyotokea lakini pengine hayakumbukwi sana.

Alitokea Augustine Mrema, waziri machachari wa CCM aliyebwaga manyanga na kujiunga na NCCR Mageuzi. Wengi bado tunakumbuka kilichotokea pale, kukawa na vichwa hasa.

Baadae NCCR ikafitinishwa na kumgeuka. Kukawa na NCCR mbili. Huo ndio ukawa mwisho wa kile chama. Kuna mtu pale NCCR mmojawapo wa viongozi mahiri akiitwa Prince Bangeda. Mpaka leo sijui alitofautiana nini na Mrema. Alimuandika vibaya na kumchambua Mrema kwenye safu yake ndani ya gazeti la Rai kila Jumatano kwa makala ndefu ndefu kwa miezi kadhaa. Nadhani hakuna mwanasiasa alichambuliwa na kuandikwa vibaya mpaka leo hii kama alivyofanya Bangeda kwa Mrema.

Leo hii Bangeda yuko wapi na Mrema yuko wapi? Unapotumika angalia unatumikaje. Usipojiongeza, wanaweza kukufanya kama toilet paper.

CHADEMA inapigwa vita sana kwakuwa ni mwiba mchungu kwa CCM. Project za kukiangamiza hiki chama ni nyingi mno. Watu wanaotumika ni wengi mno. Pesa iliyokwisha tumika ni nyingi mno. Hakuna chama cha siasa kimepitia mapigo mengi kama CHADEMA, lakini mpaka leo kipo hai na kinadunda. Kukiombea kife ni:

Kupoteza matumaini ya vijana wasomi wengi
Ni kupoteza viongozi wazuri wa kesho
Ni kupoteza matumaini na furaha wa wapiga kura milioni 7
Ni kupoteza matumaini na furaha ya wapenzi, washabiki na wafurukutwa zaidi ya milioni kumi

Hakuna kosa kubwa tutalifanya kama kuombea CHADEMA ife. Hiyo laana haitakaa ituache, itakula nasi sahani moja. Kama tulikubali NCCR na CUF vinyongwe, tusikubali haya kwa CHADEMA.

Viongozi walioko CHADEMA ni binadamu kama wewe na mimi wana mapungufu yao, lakini kwenye mizania ya haki wana mengi mazuri ya kukumbukwa vizazi na vizazi. Wanahitaji tuwatie moyo, tuwasaidie na kuwapa faraja kwenye kila hatua wanayopitia. Tusiwakatishe tamaa. CCM iliyokuwa na upendo wa kweli kwa Watanzania ni ile ya Mwalimu Nyerere tu. Baada ya hapo ni vurugu mechi kwa kwenda mbele.

Makala nyingi za kuiponda CHADEMA na kukiombea mabaya hata kama sio sehemu ya zile project zina ukakasi na kuacha maswali mengi kuliko majibu.

Je, kuna personal issues nje ya politik?

Jr[emoji769]
Free and Fair Election ni mwiba mchungu kwa CCM na kama hawana shaka na hilo waruhusu tume ifanye kazi yake kwa ufanisi nadhani hata kaka Pascal atabadili mawazo yake kugombea CCM au atakua anatambua fika anaenda kugombea. Ila kwa udhalimu wa CCM wa sasa wengi wanaenda kuchukua nafasi na si kuchaguliwa.
CCM hii nchi wameifanya kama shamba la bibi kiasi ambacho ugumu si kuchaguliwa na wananchi ila kupita ndani ya chama na kua mgombea.
 
Mshana Jr,

Mshana asante kwa bandiko hili. Sidhani kama kuna mtu wa ku- comprehend such a big mind post.
Ukiona mtu mzima, ana mke na watoto anajiita wa Jalalani ili apendelewe na mwanadamu mwenzake, ujue tuna tatizo kubwa sana.Tunahitaji mageuzi makubwa! A new liberation struggle is needed, tena armed struggle for that matter!
[emoji123][emoji120][emoji120][emoji120][emoji109]

Jr[emoji769]
 
Ni haki yako kunijibu hivyo,lakini kwenu nyie chadema ndio mabingwa wa siasa za chuki za wazi wazi
Mbowe alishatoa waraka rasmi kuelekeza,wabunge na madiwani wasitoe ushirikiano kwenye ziara za viongozi wa kitaifa
Mlishakubaliana bungeni msiwasalimie wala kuongea na wabunge wa ccm
Ungekuwa wewe ungeshirikiana na watu wanaokuwinda na bunduki usiku, mchana wanakuwinda kwa sumu ?

Tuweni wakweli ccm kimeshindwa kufanya siasa kinafanya vurugu za kipuuzi sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtu akiniambia CHADEMA ni chama bora, nashindwa kuelewa ubora uko wapi. Ikiwa miaka yote hii kimeshindwa kuwaandaa vijana wasomi kuchukuwa nafasi za uwongozi, sijui huo ubora unatoka wapi? Kijana anachukuliwa chuo kikuu, akiingia CHADEMA anafundisha kupinga kila kitu na kukimbizana na dola. You can't create tomorrow's leader by disobeying the rule of law.

Ukiwa CHADEMA lazima uwe tayari kutafuna pesa ya umma bila woga wala ukakasi, mikutano kwenye mahoteli makubwa, safari za nje zisizo za lazima, magari ya kifahari hata mmiliki hajulikani ni nani kusema hicho ndio chama cha mfano, sio kwa mfumo uliopo.

Hata itikadi, CHADEMA imeshindwa kuwa hata na kachuo kadogo kutowa somo la itikadi kwa viongozi watarajiwa ili kuwe na muongozo hawa wajuwe CHADEMA inasimamia kitu gani. Halafu watu wanashangaa kuona wanachama wanakihama chama, ni kwasababu wanafikiri CHADEMA na CCM wote wako sawa lakini ni vyama vyenye misimamo tofauti.
Kwani ni lazima kubadilisha kiongozi hata kama aliyepo bado anaonekana anafaa? tena kwenye kipindi kama hiki tulichopo?

Unavyosema kupinga kila kitu maana yake nini, so unataka wakubali kila kitu, au wakubali 50% ili wakuridhishe wewe?!

Kama mpinzani anasema hili haliko sawa kwasababu hii, kwanini wewe usiseme liko sawa kwasababu hii, badala yake unaamua kumuadhibu kwa risasi na kumlaza rumande kwa kesi za uongo?

Unataka wapinzani wageuke washangiliaji wa chama tawala, ikiwa hivyo kazi ya upinzani ataifanya nani? mnachotwa akili kirahisi sana.

Kama CCM wanataka kusifiwa kwa kile wanachofanya, then nao wawasifie Chadema kwasababu ndio wanawasukuma CCM kufanya wanachofanya, but sio wao walazimishe kusifiwa bila kumsifia anaewafanya watake kusifiwa.

Halafu unavyosema kutafuna pesa za serikali, hiyo serikali inatoa wapi pesa? hizo ni kodi za wananchi, sio pesa za serikali.

Kama unataka Chadema wakafanyie mikutano yao chini ya mwembe ndio ujue ni wazalendo huo ni mtazamo wako, Chadema wanastahili kuchagua eneo wanaloona bora wafanyie mambo yao, kuwa masikini au kufanya vitu vya kimasikini sio sifa, na haya mawazo ya kichovu ndio yametawala awamu hii.

Kuwa na chuo nakubaliana nawe wafundishe itikadi za chama chao, japo sidhani kama hicho chuo kitapewa usajili na serikali ya CCM, sidhani; lakini tena nakupinga unaposema wanaohama Chadema wana sababu za msingi, huu nao ni uongo.

Tumeona wengi wanalazimishwa kuhama Chadema kwa kuhongwa na serikali ya CCM, na wengine wamepigwa wakaumizwa kwasababu wamekataa, na wengine hata kuuwawa kwa sababu hizo hizo, hivyo unavyosema wanahama chama sababu ya kufuata itikadi ni uongo.

Mameya wanalazimishwa kujiuzulu bila sababu zozote za msingi, ni utapeli mtupu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu kwan kutolewa jalalan c alitamka mwenyew?au ulikua mtt kipind hcho?
Kitendo cha kumuita mtu mzima ni wa jalalani sio ustaarabu. Hii ni nchi huru na kila mtu anayo haki ya kutoa maoni yake. Kama mtu anaona kiuhalisia hatima ya Chadema ipo mikononi mwa Lwakatare hayo ni maoni yake. Wewe ulipaswa uje ukanushe anachokisema sio kuleta kebehi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eti wahusika kwa hiyo wspiga kura out hawaruhusiwi kutafsiri? Chadema no secret society kuwa kumwachisha uanachama mbunge anayehudhuria vikao vya binge ni kosa?

Mayala yuko right hatima ya chadema iko mikononi mwa KUB Rwakatare sio siri

Mengine siandiki Ilauna watu chadema watakimbia nchi sema tu sasa hivi ndege haziendi nje ya nchi lakini time will tell niishie hapo

Rwakatare na Mashinji mmmmm no watu Wa kuchezea chadema na kufukuza sidhani uwiii mbavu zangu Mimi wacha nicheke
Mna propaganda za kitoto sana, nawaona kama makatuni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unapoongelea kifo cha CHADEMA.. Tambua unaongelea vifo vya Watanzania milioni kumi hivi... Je hili litawezekana?

Jr[emoji769]
Litawezekana sababu hata uchaguzi wa serikali za mitaa uliona kilichotokea wala hapakuwa na uchaguzi isipokuwa ilikuwa ni laana tupu, hatuna tume huru ya uchaguzi wala mahakama huru hivyo wanaweza kufanya chochote watawala bila aibu wala kufanywa chochote. Tuombe uzima October wagombea wa CCM 90% watapitishwa na tume bila kupingwa, rejea chaguzi mbalimbali za marudio ilikuwa ni vita wala siyo uchaguzi. Asante
 
Ni haki yako kunijibu hivyo,lakini kwenu nyie chadema ndio mabingwa wa siasa za chuki za wazi wazi
Mbowe alishatoa waraka rasmi kuelekeza,wabunge na madiwani wasitoe ushirikiano kwenye ziara za viongozi wa kitaifa
Mlishakubaliana bungeni msiwasalimie wala kuongea na wabunge wa ccm
Mkuu, mshana jr amekuacha mbali sana,ni bora ungetulia tu,isije ukaumbuka
 
Ukiachana na kile kitengo cha propaganda cha CCM na ile praise team. Wengine wote hatupaswi kuwa na muono kimo cha mbilikimo. Ni lazima tuwaze zaidi ya mwisho wa uono wa macho yetu.

Nimemuona P kwenye mada za CHADEMA. Utabiri wa mabaya. P ulituasa tuepuke prophecy of doom. Tusiwaase wengine huku sisi tunatenda.

Natambua mgongano wa mawazo na hoja. Natambua tofauti za kimtazamo kati yetu lakini haya yasitufanye tukafika mahali tukawa na mitazamo finyu. Tunaihitaji CHADEMA kama taasisi imara ili CCM isijisahau sana. Miaka ile ya 1995-2005. Wakati huo NCCR kikiwa chama chenye nguvu na ushawishi, kuna mengi yaliyotokea lakini pengine hayakumbukwi sana.

Alitokea Augustine Mrema, waziri machachari wa CCM aliyebwaga manyanga na kujiunga na NCCR Mageuzi. Wengi bado tunakumbuka kilichotokea pale, kukawa na vichwa hasa.

Baadae NCCR ikafitinishwa na kumgeuka. Kukawa na NCCR mbili. Huo ndio ukawa mwisho wa kile chama. Kuna mtu pale NCCR mmojawapo wa viongozi mahiri akiitwa Prince Bangeda. Mpaka leo sijui alitofautiana nini na Mrema. Alimuandika vibaya na kumchambua Mrema kwenye safu yake ndani ya gazeti la Rai kila Jumatano kwa makala ndefu ndefu kwa miezi kadhaa. Nadhani hakuna mwanasiasa alichambuliwa na kuandikwa vibaya mpaka leo hii kama alivyofanya Bangeda kwa Mrema.

Leo hii Bangeda yuko wapi na Mrema yuko wapi? Unapotumika angalia unatumikaje. Usipojiongeza, wanaweza kukufanya kama toilet paper.

CHADEMA inapigwa vita sana kwakuwa ni mwiba mchungu kwa CCM. Project za kukiangamiza hiki chama ni nyingi mno. Watu wanaotumika ni wengi mno. Pesa iliyokwisha tumika ni nyingi mno. Hakuna chama cha siasa kimepitia mapigo mengi kama CHADEMA, lakini mpaka leo kipo hai na kinadunda. Kukiombea kife ni:

Kupoteza matumaini ya vijana wasomi wengi
Ni kupoteza viongozi wazuri wa kesho
Ni kupoteza matumaini na furaha wa wapiga kura milioni 7
Ni kupoteza matumaini na furaha ya wapenzi, washabiki na wafurukutwa zaidi ya milioni kumi

Hakuna kosa kubwa tutalifanya kama kuombea CHADEMA ife. Hiyo laana haitakaa ituache, itakula nasi sahani moja. Kama tulikubali NCCR na CUF vinyongwe, tusikubali haya kwa CHADEMA.

Viongozi walioko CHADEMA ni binadamu kama wewe na mimi wana mapungufu yao, lakini kwenye mizania ya haki wana mengi mazuri ya kukumbukwa vizazi na vizazi. Wanahitaji tuwatie moyo, tuwasaidie na kuwapa faraja kwenye kila hatua wanayopitia. Tusiwakatishe tamaa. CCM iliyokuwa na upendo wa kweli kwa Watanzania ni ile ya Mwalimu Nyerere tu. Baada ya hapo ni vurugu mechi kwa kwenda mbele.

Makala nyingi za kuiponda CHADEMA na kukiombea mabaya hata kama sio sehemu ya zile project zina ukakasi na kuacha maswali mengi kuliko majibu.

Je, kuna personal issues nje ya politik?

Jr[emoji769]
Chadema haiwezi kufa maana hata nuru kidogo tunayoitazama ya haki ni kwasababu ya chadema.
Leo hii kama siyo chadema hata Raisi Magufuli asingeweza kupata Uraisi

Umeongea fact, cdm inashambuliwa mno utadhani ni adui kuliko covid, vyombo vyote vipo na ccm kuhakikisha cdm inakufa, swali cdm ikifutika ndo maisha ya watz yanabadilika? Simple answer is big nooooo there might be something hidden in the carpet with ccm
 
P badala aelekeze nguvu kumuomba mzee amfutie laana ya kumuita ‘mayala maana yake ni mtu mwenye njaa’ kutwa anahangaika na chadema.

namkumbusha: chadema ni mpango wa Mungu.
 
Umeongea fact, cdm inashambuliwa mno utadhani ni adui kuliko covid, vyombo vyote vipo na ccm kuhakikisha cdm inakufa, swali cdm ikifutika ndo maisha ya watz yanabadilika? Simple answer is big nooooo there might be something hidden in the carpet with ccm
ccm walishashindwa kuongoza nchi siku nyingi tu.

Hawana tena hoja za kuwapelekea wananchi ndiyo maana hawataki tena uwanja sawa kwa sababu hawana cha kuuza kwa wananchi.

Njia pekee waliyobakiza ni kuteka na kuua wapinzani eti wanajisifu wameua upinzani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kwa credibility yako hupaswi kuanzisha nyuzi zilizojaa mahaba kiasi hiki

Tambua kwamba lengo letu la pamoja kama watanzania ni kuiona Tanzania kwanza ikifanikiwa katika kila nyanja bila kujali ni nani ama chama gani kinachosimama mbele

Vijana wengi hasa wa kiafrika hufanya kosa hili mahala pengi kwa kuabudu zaidi mihemko yao ya kisiasa kuliko uzalendo na uhalisia, na mabeberu hutumia mwanya huu kupandikiza "harakati uchwara" na chuki dhidi ya wenyewe kwa wenyewe

Naomba utambue bwana Jr. Tunachohitaji watanzania ni kuliona taifa linaelekea kwenye maendeleo endelevu bila kujali chama kipi kimeshika dola kwani hivi vyama vyote ni sawa tu na viongozi wake ni sawa tu tofauti ni majina tu kwa kua isingekuepo CCM na Chadema nchi ingekuepo na vingekuepo vyama vingine ambavyo si magufuli wala mbowe angeongoza vyama hivyo!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna kosa kubwa tutalifanya kama kuombea CHADEMA ife. Hiyo laana haitakaa ituache, itakula nasi sahani moja. Kama tulikubali NCCR na CUF vinyongwe, tusikubali haya kwa CHADEMA.
Naam. Tutalia na kusaga meno CHADEMA itakapokufa!
 
Back
Top Bottom