Bora Mshana umeleta huu uzi.
Huyo P unayemzungumzia ni vyema ukamtambua kwasasa kama mtu muoga, asiejiamini, anajaribu kuandika story zake akiwa fika anaujua ukweli, ila kwa sababu nilizoweka hapo juu, anaamua makusudi kuzunguka mbuyu kwa kuogopa yasije mkuta yaliyowahi kumkuta.
Ngoja nielezee kidogo kitu umjue vizuri huyo P wa siku hizi yukoje, na ni kwa jinsi gani ameamua kujivisha kilemba cha upotoshaji ili kuwadanganya wasiojua ukweli, na kuwaremba watawala kwasababu ya kuwahofia.
Jana kaja na uzi wa Lwakatare, anasema Lwakatare kaficha mboga Chadema wameshamwaga ugali hivyo anajaribu kuwatisha wasiojua ukweli waamini kwamba Chadema ilikosea kumfukuza uanachama Lwakatare.
Kipindi Lwakatare kapotea/kutekwa ni Mwigulu Nchemba ambaye sasa ni waziri wa Sheria aliejitokeza hadharani akasema anayo video inayoonesha tukio zima la Lwakatare kutekwa, na Mwigulu alisema hivyo makusudi kwasababu za kisiasa, but mpaka leo hii, Mwigulu Nchemba hakuwahi kuonesha umma wa watanzania hiyo video.
Sasa P kwa kile alichoandika jana, ameamua wazi kuudanganya umma uamini kwamba Chadema ndio wanaohusika kumteka Lwakatare, sasa jiulize; kama kweli Chadema walimteka Lwakatare na Mwigulu anao ushahidi, kwanini wasiupeleke mahakamani?!
Kimsingi utaona P ameamua kuwa agent wa shetani, kwasababu licha ya kuujua ukweli dhahiri, ameamua kupotosha makusudi ili kuwalinda watawala anaowaogopa, na kuamua kuwaponda Chadema makusudi kwasababu anaamini hawana cha kumfanya wakati akijua fika Chadema hawahusiki kwa lolote.
Ningemshauri tu, badala ya kuendelea kuandika nyuzi zake za mafumbo ambazo zinaweza kugeuka kuwapotosha wasiojua ukweli kwasababu anawaogopa watawala, bora akae kimya tu, au anaweza kuamua kuanza kusifia ujenzi wa SGR, ununuzi wa Bombadier, na Stieglers, ila asijaribu kuwa mpotoshaji kwasababu hii ni sawa na dhambi ya kusema uongo ili kuwafurahisha watawala anaowaogopa.
Sent using
Jamii Forums mobile app