Sio siri tena: Polisi wanawaonea CHADEMA,wanapendelea CCM

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Nimetafakari sana kauli ya Waziri wa mambo ya ndani, Nchimbi, alipoulizwa na waandishi wa habari iweje mikutano ya CCM haikuingiliwa na polisi siku hiyo hiyo Chadema walipopigwa Iringa na mwandishi kuuwawa, akasema alimuuliza Mukama akaambiwa ile ya CCM ilikuwa mikutano ya ndani. (Angalia picha uone mkutano mmojawapo "wa ndani" wa CCM ulivyokuwa, na watu wengi zaidi ya ule wa CHADEMA Iringa)

Ukiangalia picha za tukio la Iringa (angalia picha nimeambatanisha), utaona waziwazi kwamba CHADEMA wamepigwa na mwandishi kuuwawa katika eneo la ofisi ya CHADEMA, na bendera ya CHADEMA ikipepea katika mojawapo ya majengo ya hilo eneo. Taarifa zinasema polisi walikuwa wanatupa mambomu ndani ya ofisi ya CHADEMA, dhidi ya watu waliokuwa ofisini.

Sasa je, hili suala la kuzuia "maandamano ya CHADEMA", na kuruhusu "mikutano ya ndani ya CCM" siku hiyo hiyo moja linakujaje?

Na iweje Waziri Nchimbi anamuuliza Mukama badala ya kuwauliza polisi kwa nini hawakuzuia mkutano wa CCM? Alitegemea jibu gani toka kwa Mukama?

Mie si mwanachama wa CCM wala CHADEMA, lakini nasema wazi, SIO SIRI, POLISI WANAWAONEA CHADEMA, WANAWAPENDELEA

CCM
attachment.php
attachment.php
 
Attachments

  • Iringa.jpg
    Iringa.jpg
    84.9 KB · Views: 1,945
  • Bububu.png
    Bububu.png
    287.9 KB · Views: 442
Sawa hata kama ni mikutano ya ndani, sababu waliyotopa polisi ni kuwa hiyo mikutano itavuruga zoezi la sensa ndio maana wakasema kuwa mikutano hiyo ina weza kuendelea kuanzia tarehe 9 wezi huu! sasa swali la msingi la kujiuliza ni kuwa hivi hii imekutano ya ndani haihusisi mikusanyiko ya watu, na kama inahusisha je haiwezi kuvuruga hilo zoezi la sensa!?
 
Wale wajinga polisi wanasahau wajibu wao wa kulinda wananchi na kufuata amri za hao wahuni wa ccm ndo maana wanaua watu wasiokuwa na hatia
 
Aisee nauli ya KLM mpaka the Hague ni kiasi gani?

attachment.php

Huyo mwenye bunduki ndiyo alifanya mauaji ya kinyama.anafurahisha watawala huku akijitengenezea maadui yeye na familia yake.anafurahiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii kupewa mtutu
 
Aisee nauli ya KLM mpaka the Hague ni kiasi gani?

attachment.php

Namsifu sana huyo mwandishi anayechukua picha.
Lakini namshangaa sana huyo policcm anayefytulia bomu la machozi nyumba, hivi huyu ana akili sawasaw kweli.Ndhani police wetu inabidi wapimwe akili, kwani haingii akilini kupoteza kodi zetu zilizotumika kununua hilo bomu halafu huyu mjinga anapiga nyumba bomu la machozi!!!!!!!!!!!!!!!!!!.
Lakini pia tumepewa taarifa kuwa CDM waliruhusiwa kufanya mikutano ya ndani, kwa kuangalia hiyo picha tafsiri ni kwamba hata hiyo ya ndani wao polisi hawakubaliani nayo???????????
 
Mi nlishaacha hata kuishabikia yanga coz of colour...jumapili tuna mkutano ktk ofisi yetu ya chadema hapa arusha,2najifua kwa lolote.
 
Aisee nauli ya KLM mpaka the Hague ni kiasi gani?
attachment.php
Mara zote Mabomu ya mAchozi huwa yanalipuliwa kwenye mkusanyiko wa watu ili kuwatawanya, sasa hapo haonekani mtu wala kikundi chochote, hayo mabomu yalikuwa yanafyatuliwa kwa kwa minajili gani?
 
du?polisi mna matatizo coz kwa mtu mwenye akili hawezi kupiga bomu kwenye nyumba ya mtu.:A S 465:
 
Namsifu sana huyo mwandishi anayechukua picha.
Lakini namshangaa sana huyo policcm anayefytulia bomu la machozi nyumba, hivi huyu ana akili sawasaw kweli.Ndhani police wetu inabidi wapimwe akili, kwani haingii akilini kupoteza kodi zetu zilizotumika kununua hilo bomu halafu huyu mjinga anapiga nyumba bomu la machozi!!!!!!!!!!!!!!!!!!.
Lakini pia tumepewa taarifa kuwa CDM waliruhusiwa kufanya mikutano ya ndani, kwa kuangalia hiyo picha tafsiri ni kwamba hata hiyo ya ndani wao polisi hawakubaliani nayo???????????
Mkuu hawa polisi nadhani watakuwa wamechaguliwa kwa sababu inaonyesha wazi kabisa hata wenyewe wana chuki na CHADEMA. Sijawahi kuona polisi wanawatawanya watu kwa kupiga bomu ndani ya ofisi...
 
Mara zote Mabomu ya mAchozi huwa yanalipuliwa kwenye mkusanyiko wa watu ili kuwatawanya, sasa hapo haonekani mtu wala kikundi chochote, hayo mabomu yalikuwa yanafyatuliwa kwa kwa minajili gani?
Labda watu wameshakimbia baada ya kulipuliwa la machozi??
 
Nimetafakari sana kauli ya Waziri wa mambo ya ndani, Nchimbi, alipoulizwa na waandishi wa habari iweje mikutano ya CCM haikuingiliwa na polisi siku hiyo hiyo Chadema walipopigwa Iringa na mwandishi kuuwawa, akasema alimuuliza Mukama akaambiwa ile ya CCM ilikuwa mikutano ya ndani. (Angalia picha uone mkutano mmojawapo "wa ndani" wa CCM ulivyokuwa, na watu wengi zaidi ya ule wa CHADEMA Iringa)

Ukiangalia picha za tukio la Iringa (angalia picha nimeambatanisha), utaona waziwazi kwamba CHADEMA wamepigwa na mwandishi kuuwawa katika eneo la ofisi ya CHADEMA, na bendera ya CHADEMA ikipepea katika mojawapo ya majengo ya hilo eneo. Taarifa zinasema polisi walikuwa wanatupa mambomu ndani ya ofisi ya CHADEMA, dhidi ya watu waliokuwa ofisini.

Sasa je, hili suala la kuzuia maandamano ya CHADEMA, na kuruhusu mikutano ya ndani ya CCM siku hiyo hiyo moja linakujaje?

Na iweje Waziri Nchimbi anamuuliza Mukama badala ya kuwauliza polisi kwa nini hawakuzuia mkutano wa CCM? Alitegemea jibu gani toka kwa Mukama?

Mie si mwanachama wa CCM wala CHADEMA, lakini nasema wazi, SIO SIRI, POLISI WANAWAONEA CHADEMA, WANAWAPENDELEA CCMView attachment 63963View attachment 63965

Analysis imetulia. $1million dollar question!!
 
Dhamiri ya polisi kuandama CDM ni kuwinda na kuua baadhi ya watu kama swala.

Mmoja wa target yao ni huyo mwandishi. Bado wana mission hawajakamilisha wale wanaotaka kuwa ua.

Anachfanya Nchimbi ni kupuliza kama panya vile.

Namuuliza kikwete, utawawinda hawa mpaka lini? Unao wangapi kwenye listi?
 
Namsifu sana huyo mwandishi anayechukua picha.
Lakini namshangaa sana huyo policcm anayefytulia bomu la machozi nyumba, hivi huyu ana akili sawasaw kweli.Ndhani police wetu inabidi wapimwe akili, kwani haingii akilini kupoteza kodi zetu zilizotumika kununua hilo bomu halafu huyu mjinga anapiga nyumba bomu la machozi!!!!!!!!!!!!!!!!!!.
Lakini pia tumepewa taarifa kuwa CDM waliruhusiwa kufanya mikutano ya ndani, kwa kuangalia hiyo picha tafsiri ni kwamba hata hiyo ya ndani wao polisi hawakubaliani nayo???????????

Mkuu bila kupimwa na kuonekana una akili za kijinga kijinga huwezi ingia jeshi la polisi.
Watu wenyewe vimshahara wanavyopewa ni chenji ya sokoni. Mbuzi kabisa hawa.
Huyo Nchimbi ka prove kuwa jeshi la polisi ni idara ya CCM ndo maana alimuuliza bosi wake Mukama.
Kwa nini hakumuuliza Dr Slaa kama vile ni vikao vya nje au ndani?
Ndo shida ya minyoo kushambulia ubongo.
 
Back
Top Bottom