Katibu Mkuu wa CCM na Katibu Mwenezi wasiposoma Mwenyekiti wao anataka na kuwaza nini wataishia kuijadili CHADEMA badala ya kusukuma agenda za CCM

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
873
4,065
Tumeona namna viongozi wa CCM waivyotofautiana kwenye majukwaa kuhusu maandamano. Finally Chadema wamefanikiwa lengo lao na hivyo yawezekana kabisa kamati Kuu ya chadema ina mikakati mingi isiyo wazi katika kutekeleza siasa na viongozi wake wanasomana.

Ukija CCM utaona Mkuu wa Mkoa,, Katibu Mkuu Nchimbi na Makonda wao ni kama awakuguatilia msimamo wa chama cha mapinduzi baada ya kauli ya chadema kutolewa hapo awali.

Badala yake wao pia walikimbilia kuandaa maandamano yao yasiyo rasmi ambayo yalilenga kufanya usafi kwa kutumia dola, kufanya mikutano mikoani ambapo Makonda anachofanya kupita kando ya barabara ya lami na siyo kwenda kwa wananchi, huku katibu mkuu akifanya kosa lilelile la JPM lakuangaika kuwashawishi akina Peneza wajiunge CCM na hivyo kuwafanya wana CCM wajione wakiwa na wasio na thamani kwani kwa miaka sasa wana chadema waliopewa ajira wanakaribia kulingana na wana CCM wenye ajira kwenye nafasi za juu mikoaoni na wilayani

Kama hali hii ya kila kiongozi kujibrand kivyake itaendelea ndani ya CCM sidhani kama kuna uhai wa fikra na utawala utazaliwa. Haiwezekani ukawa na chama ambacho wote mnaonyesha kumwamini mwenyekiti pekee huku wengine mkiona siyo watu. Hakuna mwenyekiti pasipo kuwa na team work from ground. One man show will take you no where, bebeni maono ya chama siyo fikra na utashi wenu.....mtakachofanikiwa tu nikiwafanya wenzenu watumbuliwe na mtaendelea kuzalisha mpasuko
 
M/Taifa kaenda zake ziarani nje ya nchi bila ya kumkaimisha mbadala wake katika kiti chake. Waliobakia wamebakia wakikanyagana kama mgambo.

Makamu wake kauchuna kwa kuletewa mtu kutoka timu Lowasa kama KM, na mtu kutoka Sukuma Gang kama muenezi wa chama. Yeye ni muumini mwaminifu wa timu Msoga, hivyo ana mashaka tele kwa wasaidizi ambao amepewa kufanya nao kazi kwa ukaribu.

Mkuu wa Sekreteriereti ya chama ni mgeni ofisini, na hata hajui bosi wake anataka nini kifanyike kwa muda huu. Muenezi naye anaupyanga barabarani na misururu mirefu ya magari ili kujijengea ujiko wake binafsi na kupiga fedha za chama.

Kunani pale CCM - HQ!?
 
Tumeona namna viongozi wa CCM waivyotofautiana kwenye majukwaa kuhusu maandamano. Finally Chadema wamefanikiwa lengo lao na hivyo yawezekana kabisa kamati Kuu ya chadema ina mikakati mingi isiyo wazi katika kutekeleza siasa na viongozi wake wanasomana.

Ukija CCM utaona Mkuu wa Mkoa,, Katibu Mkuu Nchimbi na Makonda wao ni kama awakuguatilia msimamo wa chama cha mapinduzi baada ya kauli ya chadema kutolewa hapo awali.

Badala yake wao pia walikimbilia kuandaa maandamano yao yasiyo rasmi ambayo yalilenga kufanya usafi kwa kutumia dola, kufanya mikutano mikoani ambapo Makonda anachofanya kupita kando ya barabara ya lami na siyo kwenda kwa wananchi, huku katibu mkuu akifanya kosa lilelile la JPM lakuangaika kuwashawishi akina Peneza wajiunge CCM na hivyo kuwafanya wana CCM wajione wakiwa na wasio na thamani kwani kwa miaka sasa wana chadema waliopewa ajira wanakaribia kulingana na wana CCM wenye ajira kwenye nafasi za juu mikoaoni na wilayani

Kama hali hii ya kila kiongozi kujibrand kivyake itaendelea ndani ya CCM sidhani kama kuna uhai wa fikra na utawala utazaliwa. Haiwezekani ukawa na chama ambacho wote mnaonyesha kumwamini mwenyekiti pekee huku wengine mkiona siyo watu. Hakuna mwenyekiti pasipo kuwa na team work from ground. One man show will take you no where, bebeni maono ya chama siyo fikra na utashi wenu.....mtakachofanikiwa tu nikiwafanya wenzenu watumbuliwe na mtaendelea kuzalisha mpasuko
wao wanaizungumzia chadema huko mikoani,
huku wewe bandiko lako mwanzo hadi mwisho unaizungumzia na kusheheni ccm na viongozi wake :D
 
Back
Top Bottom