Sio siri tena: Polisi wanawaonea CHADEMA,wanapendelea CCM

Nikijiweka kwa mbaaaliiii. Naona kuwa hawa jamaa walipania kupiga/kuumiza hata kuua watu siku hiyo no matter what. Unfortunately walikuwa too reckless to know what was happening on to their mother party (CCM) kule Bububu. Wakisema CCM ulikuwa mkutano wa ndani picha zinawaumbua, na wakisema CHADEMA walikuwa wanafanya mkutano wa hadhara/maandamano or whatever sasa swali ni mabomu waliyorusha ndani ya ofisi walikuwa wanaua mbu?

Conclusion: Hawa watu walipania mno kupita kiasi hata wakashindwa kujipanga. Sasa hata wakisema uongo wa kitaalamu kiasi gani ni bure kwani ukweli umeshawatangulia
 
KWELI HILI LINCHI HILI!!!!! sasa kazi ya police ninin kuua watu au kulinda watu?? mi namuunga mkono mtoa mada!!!
 
Wasiwasi wangu ni kwa Dr. Slaa kipenzi cha watanzania, inabidi CDM iongeze intellingensia kuepukana na hali ya hatari huko mbeleni!!
 
Sawa hata kama ni mikutano ya ndani, sababu waliyotopa polisi ni kuwa hiyo mikutano itavuruga zoezi la sensa ndio maana wakasema kuwa mikutano hiyo ina weza kuendelea kuanzia tarehe 9 wezi huu! sasa swali la msingi la kujiuliza ni kuwa hivi hii imekutano ya ndani haihusisi mikusanyiko ya watu, na kama inahusisha je haiwezi kuvuruga hilo zoezi la sensa!?

Mkuu, mkutano wa ndani ni sawa na shirika/kampuni au taasisi yoyote ikifanya mkutano wa kiofisi.

Ukweli ni kwamba hii ishu ilipangwa na ccm pamoja na msajili na jeshi la polisi. Nia hasa ni kukifanya CDM ionekane chama cha fujo na mwisho kifutwe. Ila Mungu yupo, wamekuja kuumbuka kwenye picha. Ndio maana ripoti ya kwanza ya polisi ilisema Daudi alikuwa anawakimbilia polisi kujiokoa kutoka wafuasi wa chadema na ndipo akarushiwa bomu lililotoka upande wa wafuasi wa cdm.

Bila zile picha CDM ilikuwa inapotezwa kwenye ulingo wa siasa.

Ccm wanachofanya ni kuzuia jua lisiangaze wakati kumeshakucha.
 
Huyo mwenye bunduki ndiyo alifanya mauaji ya kinyama.anafurahisha watawala huku akijitengenezea maadui yeye na familia yake.anafurahiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii kupewa mtutu

serikali ikimsamehe wananchi kwa umoja wetu tutamsaka
 
Kwa ushahidi huu mkuu, polisi walitumwa wakaue. Kwanza watu wako ndani ya endeo la ofisi si uwanja wa mkutano halafu unawafetulia mabomu. Sipati picha.
 
du?polisi mna matatizo coz kwa mtu mwenye akili hawezi kupiga bomu kwenye nyumba ya mtu.:A S 465:

Hapa Morogoro maeneo ya kwa Mtawala siku aliye kufa Bwana Ally Mabomu yalikuwa yanapigwa mpaka kwenye nyumba za watu .....wakati waandamaji walikuwa barabarani. Kwahiyo hiyo ni kawaida yao polisi
 
Nimemsikiliza Waziri Nchimbi akiongea na waandishi wa habari Iringa. Anasema wakati Mwalimu Nyerere akidai Uhuru kutoka kwa wakoloni (waingereza) hakuna mtu alipoteza maisha. Anataka kujenga hoja kuwa Mwalimu Nyerere kwa njia ya kistaarabu zaidi kuliko Dr. Slaa.

Nitumie njia ileile ya kuuliza maswali kama alivyofanya yeye. Je; polisi wa wakoloni walipiga watu risasi au mabomu kama polisi wa sasa na Mwalimu Nyerere aliwazuia?

Kama watanzania walidai haki yao kwa wakoloni kupitia TANU serikali ya kikoloni iliwavumilia Serikali ya CCM imeshindwaje kuvumilia. Je; wakoloni walikuwa na busara kuliko serikali ya CCM?
 
Je; polisi wa wakoloni walipiga watu risasi au mabomu kama polisi wa sasa na Mwalimu Nyerere aliwazuia? Kama watanzania walidai haki yao kwa wakoloni kupitia TANU serikali ya kikoloni iliwavumilia Serikali ya CCM imeshindwaje kuvumilia. Je; wakoloni walikuwa na busara kuliko serikali ya CCM?

Mkuu, Mwaifunga bora hata serikali ya mkoloni

Inasemekana Carl Peters alirudishwa kwao Ujerumani baada ya taarifa kwamba anawatesa wananchi na kupachikwa jina la mkono wa damu

Wakoloni walikuwa na maadili, ndugu yangu. Mwaka 1895, fikiria, kabla hata ya azimio la haki za binadamu,Serikali ya Ujerumani iliamua kumuachisha kazi Carl Peters akiwa Commissioner katika koloni hili

Alirudishwa kwao na hukumu ilipotoka mwaka 1897 akafutwa ajira serikalini pamoja na umuhimu wake katika kuisadia Ujerumani kulitafuta hili koloni
 
Back
Top Bottom